Mabadiliko ya kweli yana gharama kubwa, yanahitaji mtu jasiri na mzalendo kweli kweli

Mabadiliko ya kweli yana gharama kubwa, yanahitaji mtu jasiri na mzalendo kweli kweli

Watanzania siyo watoto wa masikini.
Tumeambiwa "Nchi yetu ni tajiri"
Lakini pia umasikini hauhalalishi udikteta au ukoloni karne hii.

Sent from my XT1097 using JamiiForums mobile app
Rasilimali bila kusimamiwa vizuri haziwezi kuleta tija yoyote ( in abundance of water a fool is thirsty).

Utajiri wa rasilimali ni jambo moja na matumizi stahiki ya rasilimali hizo ili ziweze kuinua maisha ya wananchi ni jambo lingine.

Rais Magufuli amelisimamia hili vizuri na rasilimali zetu sasa zinatumika ipasavyo kutusaidia Watanzania. Mfano mzuri upo kwenye madini. Matokeo yameonekana haraka Sana, uchumi wa kati tushaingia. Unaachaje kwa mfano kumpa kura kiongozi wa mtindo huo?

#2020 kura kwa John
 
Mjomba siku zote iko hivi.ukiona kitu kinapambwa sana jiulize kulikoni.
Kamwe, narudia tena kamwe hatuwezi kuacha uongo utamalaki eti kwasababu ukweli utaonekana tuu. Hili sisi wazalendo wa kweli hatuwezi kuliacha lipite tuu. Ukweli utasemwa daima na fitina kwetu ni mwiko, daima tutaipinga.
 
W
Acheni habari za kuokoteza na kumpamba mtu kwa mafanikio kidogo sana.

Mafanikio makubwa ya pekee ya Magufuli yapo katika nini?

1) Ukuaji wa sejta ya kilimo umeanguka
2) Ukuaji wa uwekezaji umeanguka
3) Ukuaji wa sekta ya utalii umeanguka
4) Ukuaji wa soko la ajira umeanguka
5) Ukuaji wa mauzo ya nje ya mazao ya kilimo umeanguka
6) Ukuaji wa demokrasia umeanguka
7) Idadi ya km za barabara za lami zilizojengwa awamu hii haujafikia hata 40% ya awamu iliyopita
8) Uwekezaji ulifanyika kwenye sekta ya afya, hospitali zote zilizojengwa awamu hii, katika thamani haufikii hata hospitali moja tu kama ile ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, iliyojengwa awamu iliyopita. Hapo ukiachilia nyingine kama za Mloganzila na ya Benjamin Mkapa
9) Ndege - mwalimu Nyerere alinunua 13 ndege mpya za kisasa
10) Bwawa la umeme - huko nyuma yalijengwa mabwawa kama Mtera, Kihansi na Kidatu
11) Reli - mwalimu alijenga reli ya kisasa kwa wakati wake ya TAZARA
12) Viwanda - wakati wa mwalimu tulikuwa na viwanda vya kila aina, mpaka vya kuunganisha malori aina ya Scania pale Kibaha, kiwanda cha kuunganisha matrekta ya kiwango cha juu kabisa aina ya Valmet, tulikuwa na kiwanda cha baiskeli aina ya swala, tikuwa na vituo mbalimbali vya utafiti na sayansi, n.k.

Sasa hayo makubwa ya ajabu ambayo Maguguli amefanya ambayo watangulizi wake hawakuwahi kufanya ni yapi?

Wewe unaweza kuwa mjinga lakini usiwafanye watu wote wajinga.

Magufuli amefanya machache amvayo ameweza kufanya. Na kwa kweli amefanya pungufu sana kuliko aliyofanya Mwalimu Nyerere, Mkapa na Kikwete.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe kumbe ni Lissu! Maana number zinakupita pembeni! Mabwawa ya umeme ya Mtera +....... Unayalinganisha na hili linalojengwa! Reli ya Tazara unailinganisha na SGR? Ndege pia? Hata muda wa mambo haya yalivyo tendeka unaulinganisha na muda wa viongozi waliopita! Mbona kasi ya utekelezaji wa maendeleo wa Magufuli ni zaidi? Nayo huioni? Lissu hapo unachemsha! Vua hiyo miwani na ujifunze hesabu maana kwa fani yako hesabu ni kikwazo!
 
Kamwe, narudia tena kamwe hatuwezi kuacha uongo utamalaki eti kwasababu ukweli utaonekana tuu. Hili sisi wazalendo wa kweli hatuwezi kuliacha lipite tuu. Ukweli utasemwa daima na fitina kwetu ni mwiko, daima tutaipinga
Kama unaamini katika ukweli basi nikukumbushe kuwa siku zote ukweli ni mfupi na uongo ni mrefu.Na ukweli unatabia yakujisimamia nakujidhihirisha wenyewe sio hadi uulazimishe au uuseme kwakuupamba.Unachokifanya wewe na wengine mnaounga mkono juhudi ni kutaka kuufundisha ukweli namna yakujiendesha kitu ambacho hakipo. Na wewe sio mzalendo ni mfuasi tu aidha wa mtu au chama cha siasa kimoja wapo.mzalendo wa kweli lazima ajue kanuni Ya Ukweli.
 
Kama unaamini katika ukweli basi nikukumbushe kuwa siku zote ukweli ni mfupi na uongo ni mrefu.Na ukweli unatabia yakujisimamia nakujidhihirisha wenyewe sio hadi uulazimishe au uuseme kwakuupamba.Unachokifanya wewe na wengine mnaounga mkono juhudi ni kutaka kuufundisha ukweli namna yakujiendesha kitu ambacho hakipo.Nawewe sio mzalendo ni mfuasi tu aidha wa mtu au chama cha siasa kimoja wapo.mzalendo wa kweli lazima ajue kanuni Ya Ukweli.
Kama ni hivyo tusingehitaji kujitetea mahakamani na kwingineko tunapoonewa
 
Jitu linaroho mbaya linakataa kuongeza mishahara miaka mitano utafikiri anatoa hela za mfukoni mwake au za baba yake au mama yake ,lakini njiani ni kumwaga hela kwa maigizo yasiyokuwa na kichwa Wala miguu.
 
Jitu linaroho mbaya linakataa kuongeza mishahara miaka mitano utafikiri anatoa hela za mfukoni mwake au za baba yake au mama yake ,lakini njiani ni kumwaga hela kwa maigizo yasiyokuwa na kichwa Wala miguu.
Kauli hizo ni kauli za kifisadi. Ndio mnavyosema, eti pesa hizi sio za baba yako au mama yako.

Halafu utendee haki ubongo wako. Hizo hela unazosema anamwaga ni Kiasi gani kulinganisha na mishahara? Pia kila kiongozi ana staili yake
 
Familia ya chini anawaza kujenga?
Hawali nyama mpaka sikukuu
Kila siku wanatafuta kula, kuvaa, hospitali na madaftar
 
Amani Msumari,

Hii ndo thinking ya masikini aka mnyonge, wengine wanajibana kuongeza uzalishaji (productivity) ,masikini anajibana kuwekeza kwenye dead investments. Now I understand why Americans hupenda kuongozwa na watu wenye fedha zao
 
Magufuli alimtumbua Profesa Assad baada ya report ya Profesa kuonesha mapungufu ya kifedha kwenye serikali ya Magufuli.

Point clear, black n white
Mwanga na giza haiwezekani kukaa kwenye chumba kimoja, Magu ni mwizi,mwongo na mnafiki asingeweza kufanya kazi na Prof Assad
 
Amefanya makubwa katika kipindi cha miaka mitano hii
Yes ameongeza USD 100.00 tu kwenye GNI,amekopa 40T sawa na budget ya nchi ya miaka miwili na sawa na makusanyo ya Kodi ya miaka mitatu na nusu.Amevuruga market systems za mazao ya korosho, kahawa,tumbaku,mbaazi etc.Amejenga barabara ya kilometer 17 Kimara- Kibaha for five years na haijaisha,kweli kapiga kazi
 
Piga picha una familia na kipato chako ni kidogo lakini unataka ujenge nyumba yako. Utaiambia familia tunafunga mkanda, kama mlikuwa mnakula nyama mara nne kwa wiki inaweza kushuka kuwa mara mbili au moja kwa wiki. Utabana matumizi ili lengo litimie.

Kumbuka katika kufanya hivyo sio kweli kuwa wanafamilia wote watakuelewa. Unaweza kuta hata mkeo hakuelewi. Hapa busara na msimamo vyote vinahitajika.

Tukumbuke kuwa msingi wa taifa unaanzia kwenye familia. Rais Magufuli amechukua njia hii. Wapo watanzania wasiomuelewa. Wanataka kila kitu kiende vilevile, mishahara minono, barabara nzuri, huduma za kiafya Bora na orodha inaendelea. Hawa wanasahau kuwa ni lazima kwanza tufunge mkanda ili tufikie huko.

Sifa moja kubwa ya Rais Magufuli ni kuwa muwazi na mkweli. Yeye hajali itakuwaje ila anasimamia falsafa hiyo ya kunyoosha rula, hapindishi. Katika muda huu ambao kama taifa tumegundua tulikosea wapi na kuamua kwa makust kujirekebisha, Kuna watu wameibuka kutaka kutukwamisha. Wenyewe ni kupinga kila kitu na sasa wameona haitoshi wanaanza kuhubiri chuki na mafarakano. Hawa tuwakatae.

Rais Magufuli amekuwa na msimamo wa kuhakikisha sheria zinafuatwa na maadili na utamaduni wetu vinalindwa. Haya yakifanyika, maadui na wasaliti wanaibua maneno, oooh! serikali inaogopa. Hebu fikirieni mfano mmoja tuu. Watia nia wengi wa nafasi za ubunge walikuwa watumishi wa umma. Karibu wote walitia nia kupitia CCM. Leo tunaona panga la mshahara. Kama kweli kuna upendeleo hawa si wangeachwa? Kama sio kusimamia sheria na kuwa na msimamo haya yangeachwa uchaguzi upite lakini wapi, sheria ni msumeno.

Rais Magufuli amethubutu na ameweza. Tunamuunga mkono.

#2020 kura yangu kwa John
Kwa hio miaka 5 haijamtosha kuijenga nchi Bas apigwe chini waingie visionary leaders
 
Amani Msumari,

Hii ndo thinking ya masikini aka mnyonge, wengine wanajibana kuongeza uzalishaji (productivity) ,masikini anajibana kuwekeza kwenye dead investments. Now I understand why Americans hupenda kuongea na watu wenye fedha zao
Sijijui

Sikia, aki tena utajijua. Nenda kasome uzi wangu wenye kichwa cha habari "je ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?

#2020 kura yangu kwa John
 
Kwa hio miaka 5 haijamtosha kuijenga nchi Bas apigwe chini waingie visionary leaders
Soma uzi wabgu "je ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?
 
Yes ameongeza USD 100.00 tu kwenye GNI,amekopa 40T sawa na budget ya nchi ya miaka miwili na sawa na makusanyo ya Kodi ya miaka mitatu na nusu.Amevuruga market systems za mazao ya korosho, kahawa,tumbaku,mbaazi etc.Amejenga barabara ya kilometer 17 Kimara- Kibaha for five years na haijaisha,kweli kapiga kazi
Kwahayo uliyoandika wewe huishi Tanzania
 
Mwanga na giza haiwezekani kukaa kwenye chumba kimoja, Magu ni mwizi,mwongo na mnafiki asingeweza kufanya kazi na Prof Assad
Kuwa na adabu inayostahili unapomuongelea kiongozi wa nchi. Inashangaza kuona huu ndio Uhuru wa habari mnaoutaka
 
Back
Top Bottom