Mabadiliko ya maisha yangu baada ya kuoa

Tangu uoe una mda gani sasa?Kama ni hivi karibuni,ungesubiri kwanza ichanganye
 
Kusema kweli ndoa yangu bado changa, ndio kwanza mwaka mmoja. Najua changamoto nyingine zinaweza kuja na nimejiandaa kukabiliana nazo.
Changamoto zitakuja, watoto, mabadiliko yanaokuja na umri.... Ni wewe kuamua kuwa utavuka. Ila all in all, marriage bado ni net positive
 
Hakupi kero kubwa ila anakupa kero, ungekua mwenyewe hizo kero usingezipata. Kukishakua na kero, whether kubwa ama ndogo bado ni hasara.

Unaoa ili iweje hasa?
Kwenye maisha ya kawaida hakukosi kero.
Mzazi wako anaweza akawa anakukera,
Ofisini kuna kero, je inaacha kazi kisa kuna kero za mfanyakazi mwenzio.
Mahusiano ya kawaida, yasiyo na ndoa yana kero zake pia.
Hata ukinunua malaya pia kuna vikero vyake.

Kinachoangaliwa ni positive na negative.
S
Siwezi kuacha mke, kisa tu anapenda kunipigia sana simu kila muda haswa tukiwa mbalimbali nami sio mpenz wa kuzungumza sana na simu(kuongea na simu muda mrefu kwangu ni changamoto, ila kwa sababu ya mke wangu inanibidi niongee dk 10,20 mpaka nusu saa)

Kuna vijikero vya kijinga vinafutwa na mazuri yake.
 
Mi mwenyewe nataka kukimbimbia ubacchela uliwa bachela hata wale magaidi wanashawishika kuja kukushawishi ukajitoe muhanga maana wanajua ni rahisi nyuma yako huna unachowaza hauna mke wala mtoto
Ungekuwa mkristoo aisee ungeshapata mke mwema
 
Ndoa ni nzuri wakikutana wawili wanaoelewana.kila mmoja anatimiza wajibu wake bila kulazimishwa.ama alishindwa anajieleza.
Ila Sasa wakikutana wawili wenye viburi vyao kutoka kwenye makuzi Yao huko🙆
Kingine cha muhimu zaidi,wasipeleke kesi zao nje wala wasisikilize maneno ya watu,
Matatizo yao madogo madogo wayamalize wao wenyewe ndani,kila mmoja amuheshimu mwenzake,asitokee mmoja akajiona yeye ni bora zaidi kuliko mwenzake,hapo ndio ataona kila rangi kwenye hiyo ndoa.
 
Kweli kabisa.hapo kwenye kutoa kesi zao nje wanaweza wakaamua kusameheana na kuganga yajayo lakini wale wa nje walioshirikishwa bado wakayaweka moyoni.
 
Ndoa changa zina raha sana na ni rahisi kuvumiliana.
 
Nunua tv nyingine weka chumban
 
2. Kukosa uhuru wa kufanya ninacho taka nikiwa kwangu kama vile kuweka Chanel ya TV ninayo taka ( sasa hivi nalazikika kuangalia vitu vya kijinga kama juakali)
Mi mwenyewe ndo kinachonikutaga hiki, yani wife anapenda hizi tamthilia balaa. Asa mi napendaga kuchek documentary, yani unataka uweke channel ya documentary, wife kashawahi remote anaweka sinema zetu. Yan sahv natumia pc yangu kuchek ninachotaka, TV nimemwachia wife & mtoto.
 
Kwa hiyo tunachojifunza kwa uzi huu ni kuwa ,timu kataa ndoa ,ni auna ya watu wasioweza kukabili changamoto hasa kuanziq za kimaisha ,hadi za ndoa.

Na huenda ndo timu inayotoa wengi wanaojinyonga
 
Kila mtu anaoa/kuolewa. Ishu ni kudumu kwenye ndoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…