•Chonde chonde Boss
Maxence Melo ,wekeni option ya kuedit na kudelete message PM.
Kwa sisi wa App.
•Mpangilio wa private messages ni mbaya mno sijapata kuona, hasa pale mtu anaporeply message kwa kuiquote.
•Pia rekebisheni system ya kuquote comments.
App sasahivi haiwezi kuquote comments zaidi ya moja.
Ukitaka ujibu comments zote kwa kuziquote pamoja inagoma.
Hii inakera sana.
Mfano;
Watu 10 wamekupa hongera..
Unataka kuwajibu " Asante" kwa comment moja tu itakayojumuisha comments zao hizo zote;App inagoma kuquote zote kwa pamoja.
Inatulazimu tujibu mojamoja.
•Notifications ni balaa jingine.
Haziji kwa wakati..na hata zikija kwa wakati kuna namna App mmelimit kiasi cha notifications.
Mfano mtu akapita akanimwagia likes 100..App haiwezi kuonyesha zote hizo.
Inaonyesha notifications chache tu!
Mwisho wa siku mtu anashindwa kuona notifications nyingine aidha alikuwa tagged huko nyuzini.
•App iongezewe features za reactions
Kama ilivyo browser...kuna reactions mbalimbali mf;thanks,dislike,Sad nk
Lakini kwenye App kuna like tu.
App pia iongezewe baadhi ya manjonjo ya mwandiko.
Kuwe na miandiko hadi ya milazo kama ilivyo browser.
•Uwekwe mfumo unaotema baadhi ya maneno ya matusi .
Mtu akitaka kuandika tusi, system iteme hilo neno..
Yaani iwe kama system fulani ya ajira portal.. ukitaka apply kazi usiyo na vigezo inakutema yaani inakataa mapema kabisa.
Hii itasaidia kupunguza watu wanaopenda kuropoka matusi hovyo.