Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Wakuu,

Tupo kwenye hatua za mwisho kuja na JF yenye mwonekano mpya ambayo inaendana na mabadiliko ya teknolojia. Kwa wanaohitaji kuwa sehemu ya majaribio, mnakaribishwa...

Katika mabadiliko haya, huenda ukakutana na kitu kikakufurahisha, kikakuchanganya, kikakufanya uone kuna haja ya kuongeza au kupunguza n.k - usisite kutujulisha kupitia uzi huu.

Thread hii itatumika kukusanya maoni yenu na yatazingatiwa ajili ya kujenga sehemu bora na salama zaidi kwa ajili ya kila mmoja wetu.

Kwa wale watumiaji wa App, tunashauri kujaribu App Mpya ya JamiiForums: Fuata hatua hizi kwani itaendana vema zaidi na kinachokuja.

Tunawashukuru kwa ushirikiano mnaotupa kila mara kwani hadi toleo hili ni tokana na maoni yenu.

Kutakuwa na features kadhaa hazitakuwa released mapema hadi zikamilike kufanyiwa testing ndipo ziwe applied.

Tunawapenda, tunawajali na tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora.

Asanteni sana!
Mungu ibariki JF
 
Suala la id nyingi itabidi mlitatue, maana kuna watu wanatengeneza Id nyingi sana. Na kila Id una kazi yake utakuta moja ya kukashifu,kutukuza,kupost ujinga n.k inakuwa sio poa, inapaswa user wawe reality na post zao ndio maana mfumo huu ukaitwa jamii forum.
Kudeal na hili mimi napendekeza

Akaunti ifatiliwe kwa kuangalia location ya device, email za mtumiaji Kama zipo kwenye device moja, kulogin mara kwa mara kwa device moja au mbili kwa mda fulani mtakaouset, nahisi mtaweza zuia multiple id kwa user. Inakera jitu linajifanya lijuaji then akaunti nyingine sio lijuaji Kama watoto vile uzuri wengine huumbuka.
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom