Mabadiliko ya Sheria: Rais, Makamu wake, Jaji Mkuu, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge kutofunguliwa kesi Mahakamani

Mabadiliko ya Sheria: Rais, Makamu wake, Jaji Mkuu, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge kutofunguliwa kesi Mahakamani

Daaah aise hii nchi ni pasua kichwa jitu linafanya makosa alafu linajitungia sheria ya kutokushtakiwa ila tutaelewana tu hakuna kisicho na mwisho.
 
Utawala wa shetani unazidi kujijengea kuta ili usiguswe. Hawa ndio wazalendo uchwara.
 
Mkumbusheni huyo anayejitungia sheria za kishenzi kuwa hizo sheria anaweza kutofaidika nazo kama anavyojidanganya. Hope kiburi chake cha madaraka kitaisha mwaka huu.
 
CCM ni chama kinachoelekea kuiweka nchi katika hali ya sinto fahamu. Vyama vya upinzani vilizuiwa kufanya siasa tangu 2015. Wabunge wengi wa upinzani wamerubuniwa kwa maslahi yao binafsi kurudi CCM na sikuhizi wanachepukia CCM B (NCCR Mageuzi).

Ukizingatia ile kauli ya Rais Magufuli kuwa nikuteue wewe, ni kulipa mshahara na gari la kutembelea alafu umtangaze mpinzani ameshinda. Ni wazi kwamba CCM wamejipanga kuwa na the majority seats katika Bunge lijalo.

Hizo Sheria zitakazopitishwa huko Mungu atusaidie, tunawza kujikuta tunamnunulia Rais oxygen kutoka mawinguni ili tumlinde na magonjwa cams corona, na ni sheria imepitishwa.
Fafanua basi hayo mabadiko ni ya sheria gani? Na yatawaathiri vipi wananchi? Sio kulalama tu sababu umelala peke yako. Muwe mnapiga simu usione aibu. Usiku mrefu mama.
 
Fafanua basi hayo mabadiko ni ya sheria gani? Na yatawaathiri vipi wananchi? Sio kulalama tu sababu umelala peke yako. Muwe mnapiga simu usione aibu. Usiku mrefu mama.
Idugunde
Hivi unadhani hawa jamaa kuupeleka bungeni muswada ambao unasema itakuwa marufuku kumshitaki Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge na Jaji Mkuu, katika masuala yoyote yanayohusu uvunjaji wa Katiba ya nchi, una mwelekeo mwema kweli??

Inashangaza kuona Mkuu wa nchi, ambaye kabla hajakabidhiwa madaraka aliyonayo sasa, anaapa kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi, hivi sasa anaipinga Katiba hiyo, hadi anajiwekea kinga ya kutoshtakiwa iwapo anaivunja Katiba hiyo!

Inaelekea huko tuendako viongozi wa nchi hii, wamepanga kufanya uvunjifu wa Katiba ya nchi wa hali ya juu sana!
 
Hivi unadhani hawa jamaa kuupeleka bungeni muswada ambao unasema itakuwa marufuku kumshitaki Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge na Jaji Mkuu, katika masuala yoyote yanayohusu ucunjaji wa Katika ya nchi, una mwelekeo mwema kweli??

Inashangaza kuona Mkuu wa nchi, ambaye kabla hajakabidhiwa madaraka aliyonayo sasa, anaapa kuitii na kuiheshimu Katika ya nchi, hivi sasa anaipinga Katiba hiyo, had I anajiwekea kinga ya kutishtakiwa iwapo anaivunja Katiba hiyo!

Inaelekea huko tuendako viongizi wa nchi hii, wamepanga kufanya uvunjifu wa Katiba ya nchi wa hali ya huu sana!
Kuna condition zimewekwa ili ufungue kesi. Soma vizuri. Maana watu wanafungua kesi hovyo hovyo tu.
 
Ukweli hata wanaccm ambao sio wachumia tumbo hawazitaki hizi sheria watamfanyia timing pale anapoondoka watachagua mtu tofauti ambaye atakuwa tofauti na yeye
 
Mwamuzi ni Mungu ,wote tunaenda chuoni,na futile sita under grounds zinawahusu tu .Leo nimepata msemo mpya "remove your leg in our neck"otherwise "I can't breath "yanamwisho
 
rais bora wa afrika lakini muda wote anawaza kujificha
Kila kukicha watawala wetu wanafanya juhudi kubwa kupeleka miswada ambayo itaendelea kuwapa kinga kwa vitendo vyao viovu......

Mbona hawataki kuupeleka muswada wenye maslahi mapana kwa Taifa hili wa uundwaji wa Tume ya uchaguzi iliyo huru??
 
Kwenye jamii iliyo civilized, mahakama ndio sehemu pekee kwa watu kupumua. Sasa kama wanataka pia na huko wakapige pini, watu watapumulia wapi? Bunge leo Spika anataka hadi hotuba za wapinzani waandike wanachotaka, kesho Serikali inapelekwa mswada kuwalinda hawa viongozi wakuu. Wakae wakijua, wananchi wakichoka, hizi sheria hazitawasaidia c.c Nicolae Ceaușescu
 
Ilianza kama utani kumuona Jaji Mkuu akishindikizwa kufunga watu ili apewe bajeti kubwa.

Sasa Jaji Mkuu anapewa tena hifadhi kama fadhila kwa kutumikia maagizo ya mhimili wa dola.

Tukija kwa Spika tuliona mkuu wa mhimoli wa dola akimshindikiza Spika awashughulikie wapinzani ndani ya Bunge halafu mamlaka ya Mhimili wa dola utawashughulikia wabunge wapinzani nje ya Bunge.

Sasa Spika anapatiwa fadhila ya badiliko la kikatiba kwa kuwa ameifanya vizuri kazi ya kutekeleza maagizo ya Mhimili wa dola.

Tujiulize mpaka sasa mtu pekee aliyekuwa ana kinga ni Rais lakini sasa mabadiliko haya yanagusa mhimili ya Mahakama na mhimili wa Bunge ili kuhakikisha utawala wa mkono wa chuma kuwabana waTanzania.

Je ikifika siku ya kutaka kubadilisha katiba kuongeza mihula ya kutumika kama Rais, je Spika na Bunge lake au Jaji Mkuu na Majaji wake wanaweza kuikataa hoja ya Mhimili wa Dola kuondoa ukomo wa utumishi wa Rais wa miaka 10?
 
Jaji Samatta: Rais Mstaafu anaweza kushitakiwa
By
Mtanzania Digital
-
March 17, 2019

maxresdefault-2-1024x515.jpg

Awaasa wenye siasa za malengo, tamaa Ikulu

NA AZIZA MASOUD-DAR ES SALAAM

JAJI Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 inaonyesha kuwa Rais Mstaafu anaweza kufunguliwa mashtaka mahakamani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kutokana na kile kinachoitwa ‘kinga ya urais’ kuwa na mipaka yake.

Jaji Samatta ambaye amepata kuwa Jaji Mkuu kwa takribani miaka saba kabla hajastaafu mwaka 2007 alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwasilisha mada ya ‘Uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika vyombo vya dola pamoja na utekelezaji wa sheria na utoaji wa haki’ katika kipengele cha wajibu wa Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) na Takukuru kwa wanafunzi wa Shule ya Sheria nchini.

Akiwasilisha mada hiyo katika mkutano wa uwajibikaji ulioandaliwa na taasisi isioyo ya serikali ya Wajibu, Jaji Samatta ambaye amekuwa akisifika kwa misimamo na kusimamia haki alirejea Ibara 46(3) ya Katiba akisema kinga aliyopewa Rais katika ibara hiyo haihusu vitendo Rais alivyovifanya akiwa Rais lakini inahusu vitendo alivyofanya kama Rais.

“Ni ukweli kuwa chini ya Katiba ya nchi hii Rais Mstaafu anaweza kufunguliwa mashtaka Mahakamani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).Ni muhimu sana ukweli huu ukaeleweka.

“Ni sahihi kabisa kusema kuwa chini ya Ibara 46(3) ya sheria mama hiyo rais aliyeacha madaraka ana kinga dhidi ya mashtaka, hata hivyo kinga hiyo ina mipaka. Inahusu tu “jambo …..alilofanya……kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa katiba…..”kinga hii haihusu vitendo alivyofanya Rais akiwa Rais,lakini inahusu vitendo alivyofanya kama Rais,”alisema Samatta.

Alisema kuna tofauti kubwa na iliyo wazi kati ya maneno ya ‘akiwa’ na ‘kama’,kwa mujibu wa kifungu hicho cha Katiba aliyekuwa rais hana kinga dhidi ya mashtaka kuhusu jambo lolote ambalo hakufanya kama Rais.

“Kuhusu jambo la aina hiyo Mkurugenzi wa mashtaka ana mamlaka ya kumfungulia mashtaka na mahakama zina mamlaka ya kusikiliza na kuamua kesi hiyo kama ilivyo kwa kesi za jinai zinazoweza kufunguliwa dhidi ya watu wengine nchini.

“Kwa mfano kama alipokuwa madarakani Rais aliamua siku moja kuendesha gari yeye mwenyewe na akamgonga mtu na kusababisha kifo chake kutoakana na uzembe mkubwa kinga chini ya Ibara 46(3) ya Katiba haitamwokoa kutokana kwenye mashtaka ya kitendo hicho,vitendo vya ufisadi navyo vitakosa kinga hiyo,”.

Katika hilo hilo, Jaji Samatta alikwenda mbali na hata kuwaasa wale aliowaita wenye siasa za malengo au tamaa ya kuwa mpangaji Ikulu akiwataka watambue fika kwa faida ya nchi,ukweli huo.

Alisema watawala pia wanapaswa kuzingatia kuwa safari yao ya kuelekea huko na wakati wote watakapoongoza nchi kwenye jumba hilo kwamba ukweli ni kuwa Rais aliye madarakani hana mamlaka ya kutoa msamaha kwa mhalifu yeyote kabla hajapatikana na hatia mbele ya mahakama isipokuwa tu kama ibara ya 45(1) ya Katiba itabadilishwa kumpa mamlaka hayo.

Alisema hakuna shaka yeyote kuwa ofisi ya DPP ni moja ya ofisi kuu muhimu ndani ya dola hivyo jinsi Katiba inavyoelekeza ndivyo inavyopaswa kuwa katika nchi yenye kufuata utawala wa sheria.

“Ofisi ya DPP ikiyumba na utawala huo utatereka vibaya, hilo likitokea hakuna mwananchi ambaye hataathirika kwa namna moja au nyingine, moja ya malengo ya sheria ni kumpa DPP uhuru katika kutumia mamkala yake na kuhakikisha hakuna woga, uonevu au upendeleo katika kuamua mshukiwa ashtakiwe au mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya mtu huyo yafutwe au laa,”alisema Jaji Samatta.


Alisema utenganisho huo wa mamlaka hayo pia unalenga kuzuia siasa kuingilia au kutumika katika masuala hayo nyeti na kitaalamu.

Alisisitiza kuwa ofisi ya DPP haipo kwa lengo la kuhakikisha kuwa mshukiwa lazima ashitakiwe au mshitakiwa lazima aonekane na hatia.

Alisema DPP na maafisa walio chini yake ni watumishi wa nchi ambao wajibu wao ni kulinda maslahi ya umma yakiwemo yale yanayohitaji mtu asiye onyeshwa na ushahidi kuhusika na utendaji wa kosa la jinai hashtakiwi na mshitakiwa ambaye ushahidi dhidi yake hauthibitishi kwamba alitenda kosa hatiwi hatiani.

Alisema kutumia njia za uonevu na udanganyifu hakuwezi kuyafanya mapambano dhidi ya uhalifu likiwemo kosa la rushwa yafanikiwe kinyume chake hatua hizo zitafanya mapambano dhidi ya uhalifu kutofanikiwa na chuki dhidi ya watawala kujengeka.

“Mwananchi aliyeshitakiwa na kosa la rushwa na inaonekana na mahakama kuwa haijathibitishwa kutenda kosa hilo ana haki ya kuachiliwa ,kama mshitakiwa aliyeshitakiwa na kosa lingine lolote na ushahidi dhidi yake unaposhindwa kulazimisha atiwe hatiani.

Wakati mwingine siku hizi ninaposikiliza taarifa ya habari kupitia vituo vya televisheni napata picha kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wanateka mamlaka ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, bila shaka yoyote hatua hizo ni kinyume cha Katiba na zinaweza kusababisha viongozi wakahukumiwa kama watafunguliwa kesi za madai mahakamani na kuwalipa wanaonewa,”alisema Jaji Samatta.

Alisema hatua hizo za watawala zinaweza kusababisha kuharibika kwa kesi ambazo vinginevyo zingeweza kuthibitisha hatia za washtakiwa, uovu huo unaweza kutokea hata kwenye kesi za rushwa na mapambano dhidi ya uovu huo lazima yafanyike kisheria na si vinginevyo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa taasisi ya Wajibu ambaye ni Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Ludovick Utouh alisema a alisema lengo la taasisi hiyo ni kuongeza ushirikishwa wa wananchi katika suala zima la uwajibikaji.

Alisema aliamua kumualika Jaji Samatta kwakuwa ni mmoja kati ya viongozi waadilifu ambao wanaongea na kutenda vitu ambavyo wanaviamini na kwamba ni miongoni mwa watu wanaochukia rushwa kutoka moyoni.

Alisema mkutano wa jana ambao ni wa tatu baada ya kufanyika mikutano mingine mwishoni mwa mwaka jana katika Chuo Kikuu Dodoma pamoja na Chuo Kikuu Mzumbe kilichopo Morogoro ni muendelezo wa kutoa elimu kuhusu uwajibikaji kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Mwisho

Source : Jaji Samatta: Rais Mstaafu anaweza kushitakiwa | Mtanzania
 
Back
Top Bottom