Mabadiliko ya Sheria: Rais, Makamu wake, Jaji Mkuu, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge kutofunguliwa kesi Mahakamani

Malalamiko yako yako too general. Unalalamikia kitu gani? Sheria gani? Kama ni mswada wa ma mabadiliko ya Basic rights and duties enforcement Act. Sio kwamba haya mabadiliko yanakataza viongozi kama Rais,makamu wake, waziri mkuu,spika na makamu wake wasishitakiwe.
Ila imewekwa taratibu lazima uwe na kiapo kuonyesha namna gani umeathirika wewe unaefungua kesi. Yaani namna gani haki yako imeathirika.
Pili kama unawashitaki wakiwa wanatekeleza majukumu yao atakayekuwa anashitakiwa ni AG. Jambo ambalo ni la kawaida kabisa.
 
Haya marekebisho vipi siku yskiwageuka wakawa wao ndio wapinzani?
 
Nimetoka kusoma kitabu cha state of blood kilichoandikwa na Henry Kyemba aliyekuwa waziri kwenye serikali ya Idd Amini kuna mambo mengi yanayofanana na kinachoendelea sasa.
Mkuu hebu tutajie basi na tena kwa ulinganisho na utawala huu.
 
I guess I am more knowledgeable about the law than you think! All dictators are like that, there is no wonder with that! Time will tell!
 
Makamu rais bendera fuata upepo tumeambiwa hana maamuzi/power sasa hiyo kinga ya nini? Kukaa kimya na kumwakilisha boss wake kwenye misiba na dhifa mbalimbali anahitaji kinga?

Waziri Mkuu pia bendera fuata upepo tumeambiwa hana maamuzi/power ndiyo maana kila anakokwenda anasema nimeagizwa na muheshimiwa, mwishoni lazima amalizie na kale kapambio. Je kumwakilisha rais pia anahitaji kinga. Pinda alikwenda mbali zaidi alilia bungeni akasema angekuwa na maamuzi ... sasa kinga ya nini kwa kuagiza kibaya au ukakubali kuagiza kibaya?

Kinga inamaana kwa mtu wenye maamuzi ya mwisho sio waagizwa baada ya maamuzi.

Tanzania inarudi nyuma!!

Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Afrika.
 
Our freedoms are vanishing. If you do not get active to take a stand now against all that is wrong while we still can, then maybe one of your children may elect to do so in the future, when it will be far more riskier — and much, much harder.
I hear you sister!!!
 
Nimetoka kusoma kitabu cha state of blood kilichoandikwa na Henry Kyemba aliyekuwa waziri kwenye serikali ya Idd Amini kuna mambo mengi yanayofanana na kinachoendelea sasa.
Mkuu hauna pdf ya Hiki kitabu unisaidie? Nmejaribu kukicheki net nimekosa
 
Kwahiyo tunaitafuta Nazi Germany au Korea ya Kim au mseto?
Sikutegemea Tanzania ya Mwl.Nyerere kuna siku itakuwa na sheria katiri na kandamizi huko tuendapo.
Hivi huku ndio kumuenzi Baba wa Taifa?
 
KWANI KINA OLENGURUMWA HAWAJUI KUWA DAWA YA SHERIA NI SHERIA?? ACHA DAWA IWAINGIE
 
Watu wanachukulia masihara sana, hii hali ni ya hatari! Tz bado mimi siichukulii poa! Kama wapo watu wanaojiunga na makundi ya kigaidi mojawapo linalosumbua Msumbiji hii inaonyesha raia wenye uthubutu wapo! Ni suala la muda tu.

Naamini kuna watu wapo kwenye mfumo na ni wazalendo! Kuna wana ulinzi na usalama wa nchi na mipaka bado ni wazalendo. Masihara yao kwenye hii nchi watu watakuja kutafutana humu!
 

Hivi wewe ni Mwanasheria? Kama jibu ni ndiyo basi ulipoteza muda wako bure na iwapo jibu ni hapana waachie Wataalamu wa sheria waongee!

Unajua maana ya SHERIA NI MSUMENO kuwa inakata kotekote?

Rais Magufuli tangu ameingia kwenr Utawala amekuwa ni mwenye kutengeneza sheria kandamizi huku yeye akijihami ili sheria isimshughulikie! Kifupi huyu ni dikteta perce.

Kwa akili ya kawaida tu, haiwezekani afanye makosa Rais Magufuli, Makamu Suluhu Hassan, PM Msjaliwa, Spika Ndugai na Naibu wake Tulia Ackson, lakini ATI atayeshtakiwa ni Mwanasheria Mkuu! Wapi na wapi?

Huu ni uvurugaji mkubwa Sana wa mfumo wa Sheria na Mahakama zetu za Tanzania.
 
Nimekuwa najiuliza kwanini Serikali inapeleka Muswaada wa kuwakinga Viongozi kwani wanataka kufanya nini ili Wakingwe?
 
Kichwa cha habari kinapotosha kabisa. Mabadiliko haya ya sheria hayazuii Rais,makamu wa rais,spika na waziri mkuu kufunguliwa mashitaka. Ila ukitaka kufungua mashitaka lazima uwe Mh Chadema imejaa vilaza. Spika anashitakiwa akiwa anafanya kazi za bunge unataka nani akasimame mahakanani? Hujui hata nini maana ya government liability
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…