Ni hatari sana,hakuna unafuu hata kidogo,kuna kifurushi Halotel nilikuwa nalipa 1000 napata GB 1 kwa wiki sasa hivi ni MB 400 kwa shilingi 1000.
Tatizo ni pale serikali inapoamini kuwa watumiaji wote Wa internet bundle ni wapiga story mitandaoni so inabidi iwabane kwa kupandisha bei za vifurushi,ukweli sio huo,ikitumika dhana hii utawaathiri watu wengi hasa wale Wa biashara za mtandaoni,pia wapo wanaosoma kwa njia ya mtandao ambao hujiunga kusikiliza madarasa ya mtandaoni,hii ni hatari sana.Ndugulile amefeli mapema sanaa
Kilichofanywa na waziri kujidai kafanya mkutano na wamiliki Wa mitandao juu ya bundle ni ujangili,sikuona maana ya waziri kujitia kimbele front kukaa na wamiliki Wa mitandao eti wapange bei ya vifurushi wakati tuko kwenye ushindani,so mteja ataenda kwenye mtandao anaoona unatoa ofa nzuri.