Mabasi ya wanafunzi yapewa kibali cha kuwa Daladala kwa muda wa miezi mitatu kukabili uhaba wa usafiri uliosababishwa na " level seat"

Mabasi ya wanafunzi yapewa kibali cha kuwa Daladala kwa muda wa miezi mitatu kukabili uhaba wa usafiri uliosababishwa na " level seat"

Kama vile Corona kuna kitu hakiko sawa
Nimemkumbuka "Profesa Singira" anafanya mazingaombwe hela inatokea wakati huo huo anaweka kiingilio. Kama alikuwa ana uwezo wa kutokeza hela kimazingara ni kwa nini aliweka kiingilio kwenye onesho lake?

Nahisi harufu ya shombo kwenye jambo hili!!
 
nilikua na mipango ya kumaliza chuo mwaka huu...corona imeniwaisha mapema sana kuanza kuhustle na wakati hakuna hata seemu yenyewe ya kuanzia...hakuna hata seemu ya kupigia tuition ningeokota chochote....daah...cha muhimu pumzi wacha nijiunge na waziba pancha kwa hii miezi mitatu tuskume siku
 
Hatua nzuri hiyo. Nakumbuka miaka ya 70 Waziri Mkuu Sokoine aliruhusu kitu kama hicho. Mabasi ya mashirika ya umma na ya serikali (SU na ST) yalikuwa yakimaliza kupeleka wafanyakazi wa taasisi husika yanafanya kazi ya daladala kwa masaa kadhaa. Huu ni utumiaji mzuri wa mali ya umma. Badala ya basi kukaa tu wizarani au kwenye shirika tangu saa mbili asubuhi linapoleta wafanyakazi wa hapo mpaka jioni wakati wa kuwarudisha, linasaidia kupunguza tatizo la usafiri jijini na wakati huohuo linatengeneza hela kidogo za kujiendeshea.

Baada ya hapo nipe mfano wa shirika moja tu au wizara au taasisi ya serikali ambayo ilifanya vizuri na kuonekana ikiwa imepiga hatua ya kwenda mbele ktk muktadha huo, binafsi mradi huo ulifeli 100% na zaidi ulinufaisha baadhi ya watumishi hebu jikumbushe mradi wa mabasi ya umoja wa vijana ambayo yalikuwa yanabeba wanafunzi asubuhi na baadae yakiwa free yalikuwa yanabeba watu wazima yaliishia wapi?
 
Wewe ni mjinga, Danganya wapumbavu wenzako hapa ni JF

Hakuna jiji la Africa Mashariki lililofikisha watu milioni tano

Kenya wamefanya sensa mwaka 2019 kidogo wako sawa na Dar es salaam

Kumbuka Tanzania hatujafanya sensa muda mrefu

You are Gifted fool
Hatua nzuri Lakini uwa najiuliza sana swali nairobi na dar upi mji una popolation kubwa ninapokuwa nairobi sijawahi kuona mtu anasimama kwenye matatu wakati nairobi ina wakazi milion 7 je shida yetu ni uchache wa daladala au ubovu wa miundombinu
 
Nairobi ipi unaongelea wewe?

Kuna sehemu ya hovyo kama Nairobi kwa usafiri wa public

Be serious, Unafahamu mateso wanayopata wanafunzi Kenya hasa Nairobi kwenye usafiri

Achana na upoyoyo mkuu wa kuandika kila ujinga hapa JF

Siju hiyo miezi mitatu itakuwa imemaanisha hata shule ni baada ya miezi mitatu! Hapo tutegemee division sifuli nyingi tena sana maana watoto hata mudi ya kusoma itakuwa imepotea, huku mitaani hata tuition zimepigwa marufuku, eeh Mungu liokoe taifa lako.
 
Acha tu kusimama Nairobi huwezi kuta watu wanagombania kuingia kwenye Daladala
Hatua nzuri Lakini uwa najiuliza sana swali nairobi na dar upi mji una popolation kubwa ninapokuwa nairobi sijawahi kuona mtu anasimama kwenye matatu wakati nairobi ina wakazi milion 7 je shida yetu ni uchache wa daladala au ubovu wa miundombinu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaaa mkuu kule hawana cha Mwanafunzi kulipa nusu, ile ni pure Capitalism, na ndo maana Kenya wana shule chache sana za Day, kwa Secondary, labda shule za Msingi au sijui ndo upili, kule hata Wanajeshi wanalipa nauli au askari police. Kwa kifupi hakuna anaye panda bure au kulipa nusu nauli
Nairobi ipi unaongelea wewe?

Kuna sehemu ya hovyo kama Nairobi kwa usafiri wa public

Be serious, Unafahamu mateso wanayopata wanafunzi Kenya hasa Nairobi kwenye usafiri

Achana na upoyoyo mkuu wa kuandika kila ujinga hapa JF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatua nzuri Lakini uwa najiuliza sana swali nairobi na dar upi mji una popolation kubwa ninapokuwa nairobi sijawahi kuona mtu anasimama kwenye matatu wakati nairobi ina wakazi milion 7 je shida yetu ni uchache wa daladala au ubovu wa miundombinu
Shida yetu ni safari zisizo na mpangilio wala umahususi. Mtu anaweza akatoka nyumbani akapanda bus kwenda mahala kuzungukazunguka tu anakwambia ananyoosha migua ama anasafisha macho. Mwingine anatoka mbezi au kibaha kwenda kununua mchele au mkungu wa ndizi mabibo. Mwingine anatoka tegeta kwenda kununua mtumba karume. Au unakuta watu kumi wako kwenye daladala wote wanakwenda kumuona mgonjwa muhimbili au amana kha!!

Hatujuia kutumia huduma zilizo karibu na maeneo tunayoishi. Idadi ya daladala zilizopo zinakidhi mahitaji kabisa tena kwa bila kusimamisha abiria kama tukijifunza kusafiri kwa sababu zenye umuhimu tu.
 
Back
Top Bottom