Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Ngoja nikupuuze kimada wa Deusdedit Kakoko coz' hauelekei kuwa na uwezo wa ku-argue!
Ujinga wa kuwapa nchi nyingine sehemu nyeti kama bandari eti waijenge na kuindesha haiwezi kukubalika. Kama ni viwanda wajenge lakini kwa nini wang'ang'anie bandari? Magufuli alipokataa huu ulaghai mlisema tumepoteza fursa kubwa sana na inakwenda kwingine 🤣 🤣 🤣 🤣. Nashangaa mpaka sasa hawajaanza huko kwingine ila bado wanawatumia nyie vibaraka kuanzisha thread za kuuza nchi hapa. Mradi wao si ni mzuri? Ina maana muda wote hawakupata sehemu ya kuupeleka?
 
Shida ya vipi wakati nimekuambia hapo kabla hapakuwa na mkataba as mkataba bali makubaliano tu?! Yale makubaliano yalikuwa ya mpito na yalikuwa yana 1 year expiration period!

Kimsingi ilikuwa ni kama proposal tu ambayo baada ya huo mwaka 1 kupita, ndipo Merchant Group na Serikali wangekaa pamoja kujadiliana yale ambayo kila mmoja anaona yanamfaa kwake!!!

Hivi ingekuwa mkataba ulishasainiwa, mngekosa kusikia kwamba "serikali yavunja mkataba na China"! Umeshawahi kusikia jambo kama hilo zaidi ya kusikia mazungumzo yanaendelea?

Tatizo lenu nyie watu ni moja! Allegiance yenu ipo kwa JPM na sio kwa taifa! Matokeo yake, mkiona jambo lolote mnalohisi linalenga kumsemanga JPM, basi mtakuja juu!!
Wanaamini mwendazake hakukosea wala kupotoshwa!!!
 
Sri-Lanka imefanya nini wakati nimeshailezea kwenye thread?

Dah... we jamaa wewe! Hivi umesoma nilichoandika, au umekurupuka tu kuchangia?!

Ungesoma ungeona nimesema Hambantota ilikuwa ni loss-making port! Hizo tata unazosema wewe hazikuwa biashara mpya kwa Sri Lanka! Ambacho walifanya, meli ambazo hapo kabla zilikuwa zinashusha magari Colombo, baada zikawa zinapelekwa Hambantota ili kuipa unafuu!

Still ikaendelea kuwa loss making huku deni likiongezeka na ndipo walipoamua kuibinafsisha!

Hoja ya kwamba eti ni ujinga kujenga B'moyo bila kuanza ku-create demand for port, nimeshaisema sana, kwenye posts hadi kwenye thread!

Lakini kwavile umekimbilia ku-argue bila kusoma, ndo matatizo yote haya!

Narudia, YOTE HAYO NIMEYAJADILI! The problem thread ni ndefu na watu mmeona uvivu kusoma!!
Issues sio Biashara mpya n.k issue ni uwepo wa mizigo utakayoweza kuihudumia
 
Wanaamini mwendazake hakukosea wala kupotoshwa!!!

..mwendazake alikuwa MUONGO wa kupindukia.

..alikuwa akidanganya hata mahali pasipohitaji kudanganya.

..kwa mfano, aliwahi kwenda bandarini halafu akadai amekuta vichwa vya treni vimetelekezwa na mwenye mali hajulikani.
 
Unajua nini?!

Hawa jamaa hapa JF wanatoka povu bure tu!! Kwanza, ambacho kilikuwepo wakati wa JK sio mkataba bali agreement ambayo ili-expire tangu 2017 kama sikosei!!

Kwenye agreement ile ambayo hata hivyo hatukuoneshwa, serikali na China Merchant walikubaliana iwe kama model, itakayowaongoza katika kufanya majadiliano rasmi, na hatimae kuwekeana mkataba rasmi!!

Majadiliano hayo yamefanyika wakati wa JPM, na vipengele vingi walikubaliana vikabaki vichache ambavyo hata hivyo waligoma kuviweka wazi!!

Hata hivyo, tulipata taarifa zisizo rasmi kwamba moja ya vipengele vilivyoleta taabu ni suala la ardhi ambapo Mchina anataka amilikishwe kwa miaka 99.

Lingine ni suala la kodi, ambalo ndo hilo nimelisema hapo juu kwamba Kakoko ameamua kutosema ukweli makusudi wakati uhalisia sio kwamba hatutaruhusiwa kukusanya kodi, bali Mchina ana kawaida ya kuomba msamaha wa income tax, na anataka msamaha huo uwe miaka 30.

Sasa kinachogomba hapa ni hiyo miaka 30!!

Na ingawaje nimesema sio taarifa rasmi lakini sio kwamba ni taarifa za kuokoteza barabarani! Ni taarifa kutoka watu wa ndani ambao walizitoa hizo informally, na bila kutaka kuacha evidence ambayo ingetumika kama reference!
Mkuu watu wenye roho ya kimaskini wana tabia zinayofanana "KUPENDA UMASKINI, KUCHUKIA WENYE MAFANIKIO, UVIVU WA KUSOMA - KUFIKIRI NA KUJADILI... Hupenda kukurupuka na kuhemkwa hata kwa wasiyoyaelewa!!"
 
Daah,!! Mkuu umekielewa sasa hata hicho ulichoandika mwenyewe

Ndiyo, JPM alizungukwa na wazandiki, lakini hoja ya msingi mbona unaacha Kwa maksudi kuijadili??

Mwandishi, amejitahidi kutuonyesha uzuri na faida za research aliyoifanya kuhusu mradi huu, ni Jambo jema na kiukweli, Kwa maelezo na umhimu wa mradi huu, ni mzuri na unavutia, lakini sasa, licha ya maelezo matamu yenye viambatanisho vingi Vya msingi, bado kunayo maswali ya kuuliza, na nadhani ameleta hii mada akifahamu fika, itajadiliwa Kwa namna tofauti, na utofauti ni kama huo unaouponda wewe badala ya kutoa maelezo sahaihi ya kile ameuliza

Binafsi, nachotaka kutoka kwenu, imma kwa Mleta mada au kwako ni hiki

JPM, alitudokeza Kwa ufupi kuhusu mapungufu makubwa yaliyo kwenye Mkataba wa mradi wa Bagamoyo, na hata kama ni uwongo!! Ninyi mnaotaka kutuaminisha kwamba haiko hivyo kama alivyodokeza JPM, basi nyinyi mlete huo Mkataba hapa, ama nukuu zenu za Uzi huu, zitawaliwe na nukuu kutoka Kwa Mkataba wenyewe, la sivyo, na nyinyi mnapaswa kutokuwa na mashaka kutoka kwa kina Kakonko

Pili, kuna mtu anaitwa Moasa Mao, ni mchina huyu, yeye, anakataa kila kilichosemwa na JPM kuonyesha jinsi Mkataba usivyo na manufaa kwetu kama nchi na Wala haambatanishi vipengele Vya Mkataba katika kupinga kwake dokezo la JPM kuhusu ubovu wa Mkataba na mashariti yasiyozingatia Uhuru wa nchi yetu na Sheria zetu,

Tunajiuliza, Ikiwa kina Mao ndio wanaotaka waje kuwekeza, nahisi pia huwenda alishiriki kuandaa mkaba ama anaufahamu vema Mkataba huo, Kwa nini asioneshe uwongo wa Kakonko na JPM Kwa kunukuu sehemu za mashariti ya Mkataba huo??

Mpaka sasa Kwa maelezo haya, nadiriki kuwaita kina JPM na Kakonko ni wazalendo wa nchi yetu kwa hichi mnachokitetea, na kama hamtakuja kutuonyesha ukweli unaotoka kwenye Mkataba, muache kuwaita waongo kina Kakonko,

Tatu, Tanzania tumegawika katika sehemu mbili, kuna anayewashuku wenzake kwamba huwenda wamekula chenji ya mchina ili kuupigia Kampeni mradi huu, lkn kuna mwingine anaona ni kama watu hao wanakataa tu bila sababu,

Wanaokataa huu mradi Hadi wajiridhishe Kwa kuusoma Mkataba, mi naona wako Sawa kabisa, Kwa sababu, hili Jambo limeibuka Kwa nguvu na Kwa Kasi ya 4g baada Tu ya JPM kufariki, huoni kwamba kweli hata hizo nukuu za Mao huwenda zimetengenezwa Tu ili kuendelea kuwa sehemu ya Kampeni ya hao tunaodhani wamekula chenji ya mchina? Kampeni nzuri ni Ile inayoonyesha, Sera zako na namna ya kufanya, sasa nyinyi mnakuja hapa bila Sera, Ila mnatuonyesha tu jinsi itakavyokuwa, hii siyo Sawa!!

Mradi tunautaka, lakini Kwa sabb umeleta sintofahamu, basi Mkataba upelekwe bungeni Kwa uwazi usomwe, na hapo tutawapuuza vilivyo hao mnaotaka tuwapuuze!! Bila hivyo, basi tunaona ni kama na nyinyi mnataka kuingizwa kwenye shimo moja na speeker!!
Mkuu mbona unajikanganya? Kakonko au kakoko ni sahihi sana au alimpotosha mwendazake? Je kwanini anatuhumiwa ufisadi? Je miradi mingapi imebainika kuwa chini ya kiwango na kwanini CAG atishwe? Mwendazake alifanya alichoona kinafaa kwa upande wake kama watangulizi wake walivyofanya na huyu aliyepo aachwe atekeleze anachoona kinafaa kwa mustakabali wa Taifa. Ikiwa mlimpenda sana kwanini hamkuzikwa nae au ninyi ni wale "mla nawe...?"
 
HITIMISHO

Tukubali tusikubali, fursa ya Bandari ya Bagamoyo ikituponyoka tutakuja kuijutia pale Mchina atakapoamua kurejea tena Lamu, au popote pale kwenye ukanda huu wa Bahari ya Hindi!

Inashangaza sana karne ya 21 bado kuna Watanzania wana mawazo yale yale ya Ujima kwamba, eti “madini hayaozi”, na tutakuja kuchimba wenyewe tukishapata uwezo!

Injinia Kakoko na mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema “…na sisi bandari ile (Bagamoyo), tulifanya feasibility study na TPA. Na TPA kupitia serikali, itawekeza na kuijenga wakati utakapokuwa umefika.

Ni wazo zuri kama serikali itakuwa na uwezo wa kujenga hiyo bandari wao wenyewe haidhuru hata kama tumeshindwa kujenga bandari yoyote ndani ya miaka 60 ya uhuru!

Hata hivyo, Kakoko na wengine wanatakiwa kufahamu kwamba, hoja sio kuwa na uwezo wa kujenga bandari bali uwezo wa ku-utilize bandari husika!

Nimetoa mfano wa Bandari ya Piraeus huko Ugiriki ambayo kabla ya uwekezaji wa China, bandari hiyo ilikuwa haifanyi vizuri. Hata hivyo, baada ya Mchina kuingia, Bandari ya Piraeus imegeuka na kuwa ndiyo bandari kubwa kuliko zote Ukanda wa Mediterranean, huku ikichukua nafasi ya 5 Barani Ulaya!

Na ndivyo hivyo kwa Bandari ya Hambantota ambayo na yenyewe ilikuwa haifanyi vizuri lakini hivi sasa hali imebadilika.

Na sababu kubwa ya China kuwa na uwezo wa kuzifanya bandari anazoendesha kufanya vizuri inatokana na ukweli kwamba China ina-handle biashara kubwa sana duniani. Kwa maana nyingine, China ina uwezo wa ku-utilize bandari zake kupitia mizigo yake tu.

Lakini kwa upande mwingine, Mradi wa Bandari ya Bagamoyo pia unahusisha Industrial Complex kubwa sana! Lengo la Mchina ilikuwa ni kujenga viwanda kwenye eneo la bandari, ili baadhi ya bidhaa zake anazosafirisha kutoka China hadi Afrika ziwe zinazalishwa Bagamoyo.

Ninachotaka kusema ni kwamba, pamoja na suala la kodi, mradi huu endapo ungekamilika, ungekuwa chanzo kikubwa cha ajira kwa wananchi!

Bandari ya Bagamoyo sio kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato! Hivyo basi, hata kama tuseme Mzee wa Msoga alilenga kupendelea kwao, hivi kuna mwenye akili timamu anayeweza kuthubutu na kudai kwamba, watakaofaidika na bandari hiyo ni Wakwere na Wazaramo wa Bagamoyo?

Halafu hii nchi ilivyo na viumbe wa ajabu, hao hao wanaosema JK alikuwa anataka kupendelea kwao, kwa kiasi kikubwa ndo hao hao wanaodharau watu wa Pwani kwamba HAWAJASOMA, na kwamba wanaishia kuendekeza madrasa!

Sasa kwavile nyie ndio mliosoma, hamuoni kwamba ni nyinyi wenyewe ndio mtakaofadika na mradi huo huku Wakwere na Wazaramo wakiishia kuwauzia kahawa?

Ukubwa wa mradi ule unaweza kuzalisha Pay As You Earn (PAYE) kutoka kwa wafanyakazi ambayo ni kubwa kuzidi hata thamani ya ukodishaji wa ardhi!

Na hii PAYE ni endelevu kwa miaka na dahari!

Pamoja na yote hayo, katu simaanishi kwamba Mkataba/makubaliano ya Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo upo PERFECT, au ni bora… la hasha!! Tanzania haijawahi kusaini mkataba ulio bora!

Ambacho ningependa kukiona kwenye hili ni Watendaji na Wafanya Maamuzi kuwa “objective”, na pia waache kusambaza habari za uongo ili mradi tu kuhalalisha ajenda zao.

Wengine ajenda zao ni aibu hata kuzitaja hadharani!

Watu hawa wanatakiwa kukaa na wadau, na kuangalia ni kwa namna gani huu mradi unaweza kufanyika huku tukiacha kile kiburi chetu cha Uzalendo Fake Uliopandikizwa na Mfumo wa Ujamaa!

Aidha, wanatakiwa kukaa na wadau kuangalia ni mfumo upi utaweka mbele maslahi mapana ya taifa.

Na kama nilivyosema kwenye utangulizi wangu, Wapinzani wa Bandari ya Bagamoyo wanawatumikia wale wale wanaowaita Mabeberu bila wao kujijua! Mabeberu walianza kuipinga Belt and Road Initiative ya China tangu kuanzishwa kwake!

Kwa bahati mbaya sana, hao hao waliokuwa wanapinga BRI, hivi sasa wanaanza kuingia mmoja mmoja! Kuna dalili zote kwamba Marekani imeanza kusalitiwa na Washirika wake, hata wale wa Jumuiya ya Ulaya.

Kwa mfano, Jarida la The Diplomat la March 23, 2021 linatueleza kwamba:-


Aidha, wakati Marekani ikihangaika na BRI, mwaka juzi tu hapa, huko China ulifanyika mkutano mkuuubwa wa BRI kama ilivyoripotiwa na UNDP-Asia kwamba:-



Na kwa mujibu wa Serikali ya China, kupitia Belt and Road Portal, wanasema kwamba:-

Mzee wa Msoga aliwahi kutujuza kwamba: Akili za Kuambiwa, Changanya na Zako!
Mkuu,ikiwa uyasemayo haya ni true...basi umenifungua macho sana

Shukran Bro
Shukran sana
Unafaa pongezi
 
UTANGULIZI

Amini usiamini, wale wale ambao wamekuwa wakijivika uzalendo, linapokuja suala la Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ndiyo hao hao wanaotumikia Mabeberu bila wao kujijua!

Nitajadili mada hii katika sehemu mbili:-
  • Kwanini wale wanaoitwa Mabeberu hawawezi kuwa tayari kuona miradi kama ya Bandari ya Bagamoyo inafanikiwa, na
  • Hoja zinazotolewa na Wazalendo Kupinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Kwa bahati, binafsi mwaka 2016 nilikuwa “Mbeba Mikoba” wa Researcher mmoja wa Kimarekani (Beberu?) aliyekuwa anafanya utafiti kuhusu Belt and Road Initiative (BRI).

Kazi yangu kubwa ilikuwa Literature Review!

Kwa wanaofahamu mambo ya Resech, ukifanya Literature Reviews, hususani ya wasomi kama huyu bwana, basi unapata fursa ya kufahamu mambo mengi zaidi yaliyopata kutokea hapo kabla kwenye eneo husika!

Kwa wasiofahamu, Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni matokeo ya (BRI) ambayo, Rais wa China, Xi, anailezea BRI kwamba:


Kwa lugha nyepesi, malengo ya China kupitia BRI ni kuiunganisha nchi hiyo na sehemu zingine duniani, hususani Asia, Afrika, na Ulaya! Uunganishaji huo ni kwa ujenzi wa miundombinu, hususani ya bandari, reli, na viwanja vya ndege.

Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA alipata kuchambua kwa undani kabisa suala la Belt and Road Initiative!!

Na hapo sidhani kama mtu anahitaji kuwa na Shahada ya Diplomasia ya Uchumi na Ushikirikiano wa Kimataifa kunusa “threat” ya mpango huo wa China kwa mataifa makubwa, hususani Marekani!

Kutokana na ukweli huo, ndo maana haishangazi mara tu BRI ilipotangazwa, Waandishi na Watafiti mbalimbali kutoka nchi za magharibi wakaanza kulivalia njuga suala hilo.

Makala zikaandikwa, na tafiti zikafanywa kuhusu BRI, lakini makala nyingi kama sio zote zililenga kuyatisha mataifa mengine kuwa makini na BRI!

Watu hawa wakageuka kuwa “Wajomba Zetu” Afrika, huku wakituasa tusije tukaingia kwenye mtego huo hatari wa China!

Ni kupitia hizo tafiti ndipo nami nikajikuta nipo na huyo Mtafiti Msomi kweli kweli wa Kimarekani.

Huyu Bwana case studies zake zilikuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Bandari ya Hambantota (Sri-Lanka), pamoja na Bandari ya Piraeus (Ugiriki).

Ukweli ni kwamba, ilinichukua chini ya dakika 3 kugundua Mtafiti huyu ni kama tayari alishakuwa na “matokeo” ya utafiti wake hata kabla kazi haijaanza! Kwa kifupi, alionesha dalili zote za kutounga mkono Mradi wa Bandari ya Bagamoyo!

Hata "beberu" niliyekuwa namtumikia, nae alikuwa pamoja na "Wazalendo" wetu!!

Binafsi, nilikuwa “in favor of” Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, kwahiyo tukaanzisha kimdaharo kisicho rasmi!

Baada ya kuona hoja zake nyingi nazipangua, akaishia kuuliza ikiwa nadhani ni busara kwa taifa maskini kama Tanzania kuwa na bandari kubwa kama ya Bagamoyo!!

Jibu langu kwake lilikuwa rahisi sana, kwamba: Bandari ya Bagamoyo itakuwa ni kubwa mno kwa Tanzania endapo tu unaamini Tanzania na majirani zake wataendelea kuwa maskini kwa miongo kadhaa ijayo, vinginevyo, huwezi kusema ni “kubwa mno”!

Kwa ufupi, Mheshimiwa huyu, kama walivyokuwa wenzake wengine, nyimbo zao zilikuwa ni agenda ya siri ya China kuitumia BRI kama Mtego wa Madeni kwa nchi maskini!

Lilipokuja suala la Bandari ya Hambantota kule Sri-Lanka, propaganda zikasambazwa kwamba China IMEITWAA bandari ya Sri Lanka ili kufidia deni lake!

Wazalendo wetu nao wakazidaka propaganda hizo, na bila kufanya utafiti, wakaanza kutueleza kwamba “tukishindwa kulipa deni, Wachina wataichukua Bandari ya Bagamoyo kama walivyofanya kule Sri-Lanka.”

Kuweka kumbukumbu sawa, habari za Wachina KUITWAA bandari hiyo zilipotoshwa. Nitaeleza hili kinaga ubaga hapo baada kwenye makala hii.

Pamoja na suala la “Debt Trap”, watu hawa tunaowaita Mabeberu ambao kwa hili tunawaona wanajali maslahi yetu, pia wakawa wanatuambia agenda nyingine ya siri ya China ya kuanzisha “military base” kupitia BRI.

Hapa wakawa wanalenga kutuambia, hata mradi kama wa Bandari ya Bagamoyo, lengo lake ni Wachina kutaka kuweka kambi za kijeshi eneo hili la Afrika Mashariki!

Hata hivyo, hawatuambii ukweli kwamba, ni wao wenyewe ndio wanaozihofia hizo “military bases” za China endapo zitawepo!

Kila mfuatiliaji wa mambo duniani, anafahamu Marekani ina kambi za kijeshi sehemu kadhaa duniani, lakini linapokuja suala la China au mataifa mengine kufanya yale yale ambayo yeye keshayafanya kwa miongo kadhaa, hapo inageuka kuwa nongwa!

Waingereza wana msemo “If you can’t beat them, join them.”

Guys, amini usiamini, juzi yule Mtafiti niliyekuwa nae ametoa makala kwenye moja ya majarida maarufu sana duniani! Baada ya kuisoma makala ile, hapo hapo nikajisikia uchungu, na kumhurumia!

Yaani yule yule aliyekuwa anaipinga BRI, kwenye hiyo makala anaulaumu wazi wazi Utawala wa Trump kwa kutumia kete ya Debt Trap kama njia ya kuidhoofisha BRI.

Kwenye makala hiyo, kuna sehemu anahoji “Kama kweli BRI ni kitu kibaya kiasi hicho, ni kwanini basi China inaendelea kutafuta Washirika walio tayari kujiunga na BRI.”

Mwishowe, Mtafiti huyu anaisemanga serikali yake kwamba ”USA haitaweza kumzuia Rais wa China kuwekeza kupitia BRI endapo US haitakuwa na mbadala kwa mataifa yanayoshirikiana na China!

Ufaransa, imeanza kuliona hilo kama ilivyowahi kuripotiwa na France24 kwamba:


Desperation ya Mtafiti huyu bila shaka inatokana na vile anavyoona jinsi ambavyo nchi mbalimbali duniani jzinavyojiunga na BRI, kinyume na matarajio ya USA ambayo ilikuwa ina-lobby nchi zingine, hususani Washirika wake kutojiunga na BRI.

Kwa bahati mbaya sana, si Afrika, si Asia! Hadi baadhi ya nchi za Ulaya na Carribean zinaingia kwenye BRI. Mbaya zaidi, miradi ya BRI inaonekana kufanya vizuri sana!

Kwa mfano, mwaka 2016 Bandari ya Piraeus ilikuwa ndio ya kwanza barani Ulaya kubinafsishwa chini ya BRI. Bandari hii ndiyo bandari kubwa kuliko zote nchini Ugiriki, na ndio langu kuu la bahari linalounganisha nchi za EU na Asia!

Hapo kabla, bandari hii ilikuwa haifanyi vizuri, na ripoti za nyuma zilikuwa zinaiweka bandari hiyo kama bandari ya 17 barani Ulaya!

Baada ya Wachina kuchukua 51% ya hisa za bandari hiyo, na hatimae hisa hizo kufikia 67%; ripoti ya mwaka huu kupitia Port Economics inasema kwa sasa Bandari ya Piraeus ndiyo bandari kubwa zaidi (kwa kiwango cha makontena) kwenye ukanda wa Bahari ya Mediterranean, na ya 5 Barani Ulaya!!

Sasa haya ndo mambo ambayo watu hawakuyataka! Yaani bandari iliyo kwenye ardhi ya Mzungu, 67% imilikiwe na Mchina, na hapo hapo inaanza kutishia ushawishi wa bandari zingine zinazomilikiwa na Wazungu wenyewe!

JokaKuu
Sijasoma hadi mwisho ila hata tukitaka kusingizia wengine, je China katika nchi ilizoenda kuwekeza ni kipi kizuri ambacho tunajifunza zaidi ya mbinu zao za kutawala dunia kama ilivyokuwa Europe enzi zile za karne ya 18? Tofauti ni science tu lakini nia na matunda tunayoyaona kwetu ni yale yale....Sasa utawatetea kwa lipi? Tupe mfano wa nchi iliyopata faida hadi sasa kwenye bara letu ili na sisi tuhamasike...Kwani sisi ndiyo akina nani atupe mteremko kinyume na wengine?

Mifano ya hizo bandari ulizotoa ni chambo tu kwa africa, maana China inajua fika haiwezi kuinyonya Europe kirahsi ila inaitumia kuwapa matamanio akina sisi ambao katika equation ya dunia kila mtu katuweka chini ya miguu yake...Ifike sehemu na sisi tufurukute basi....China ianze kuonyesha mifano chanya kwanza ndipo tutakubaliana nao; so far kwa mikataba ile ambayo tumeambiwa mambo wanaotakakufanya ni faida kutofanya mradi huo kwakua ardhi yetu na bahari yetu itatumika hata kwa hicho kidogo kuliko hasara watakayotusababishia ki hali na ki mali watakapotekeleza mradi huo kulingana na mkataba ule tuliohadithiwa na hayati JPM...Wale wenzetu kitumbua chenu kimetiwa mchanga na mwenda zake kwa hakika haiwezekani ni bora kufikiria njia nyingine!
 
Kwanza tupongeze mtoa mada kwa kuleta mada nzuri yenye hoja nzito zinazopaswa kujadiliwa kwa hoja.
Bila kujali hoja ya mtoa mada, tunakubaliana au siyo, niseme tu hizi ndo mada zinapaswa kuletwa kwenye jukwaa hili tuzijadili.
Tumpinge kwa hoja au tumuunge kwa hoja zenye maslahi kwa taifa letu, pia tukubali kwamba tunatofoutiana uono na upeo na uelewa was Jambo fulani fulani , Yale ambayo tunayajua kwa undani na kwa uelewa mpana tunayaeleze kwa faida ya wote Bila kupotosha, lakini Yale ambayo hutuyajui kwà upana tuongeze nguvu kuyajua na kusikiliza wengine , hapo tunaweza kusaidia kuboresha hili jukwaa kujadiliwa hoja, na kuruhusu watu wengine hata viongozi wakubwa was serikali kutoa hoja zao lakini pia kuchukua hoja humu za kusaidia taifa, asanteni tuendelea na mada mezani
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa sana, ingawaje nina mashaka ikiwa tutaijenga wenyewe, halafu kwa ukubwa ule ule aliotaka Mchina, je, tutaweza kui-utilize?

Unajua anachofanikiwa Mchina kwenye miradi mikubwa kama hii ni kwa sababu ana percentage share kubwa sana ya mzigo unaosafiri duniani!

Kuna mamia ya meli kutoka sehemu mbalimbali duniani zinaoingia na kutoka China kila mwezi!! Kutokana na hili, China ana uwezo wa ku-influence bandari zake kuwa busy!!

Sasa assume, sisi tunajenga bandari kuuubwa kama Bagamoyo, na Mchina anajenga bandari kuuubwa Lamu! Hapo ni obvious meli nyingi za China zitaenda Lamu! Hili ndilo liliwakwamisha Bandari ya Hambantota na Piraeus!!

Kuna watu wamekuwa wakihoji kwamba: Hivi huko duniani wakisema "madini yenu hatuyataki tena", hivi tutyayafanyia nini wenyewe kama wenyewe?!

Au ndo itakuwa mwendo wa kuning'iniza vito kwa kwenda mbele?!

Mfano huo wa madini ndo kama bandari! Mchina hamtegemei someone else aje ku-utilize bandari zake bali ni yeye mwenyewe ndie mwenye uwezo wa kufanya hivyo!!!
Mkuu mimi sipendi siasa ila hili linanishawishi kusema kitu.
Kuna uwezekano mkubwa bandari za piraeus na hambantota zimehujumiwa na mchina ili yeye azikamate kwa maslahi yake.
Kuna uwezekano mkubwa china akijitoa piraeus na hambantota zikarudi kudorora kiufanisi maaana zinaendeshwa kwa influence ya mchina na si umuhimu wao kijiografia.

Endapo miaka ya umiliki wao ikiisha kuna uhakika gani kuwa hawatatengeneza mazingira shindanishi ili bandari ishindwe na wao warudi kuimiliki kama hambantota au kutafuta malisho bora zaidi kwa ajili yao?

Ni matumaini yangu serikali inatafuta namna bora zaidi ya kuvuna wakati hawa jamaa wakiwa ndio wamiliki wakuu kwa mategemeo kuwa yajayo hayatabiriki ndio maana inakomaa na kodi kuliko kutegemea kuachiwa mradi usiojua mwisho wake.
Tujipemuda tu.
 
Tutasoma yote hayo huko baadae, lakini kwa sasa nina haya machache:

1. Hakuna nchi yoyote duniani isiyopigania maslahi yake; isipokuwa labda hizi zetu za 'Banana Republic' ambazo maslahi ya viongozi wake ndiyo yanayowekwa mbele zaidi ya yale ya nchi husika.
China wana maslahi, ndiyo maana ya hiyo BRI; kwa hiyo kama nchi inao viongozi wenye akili timamu hawawezi kusubiri mpaka waambiwe na "mabeberu" ni wapi maslahi ya nchi zao yalipo.
Kama wanajua maslahi ya nchi zao yako wapi, basi watafanya uamzi sahihi kuhusu mradi ulio na manufaa kwa nchi zao.

Tuna miaka zaidi ya sitini sasa tukijiamlia mambo yetu. Tunao watu waliosoma vizuri na kuelewa mambo vizuri karibu katika kila fani. Hatuna visingizio tena vya kusema hatuna raslimali watu. Iliyopo sasa ni kutojua tu jinsi ya kuitumia vyema raslimali hiyo.

Acha mchina aje na BRI yake atuonyeshe anataka kufanya nini, na sisi tumueleze mategemeo yetu ni nini, bila ya aibu au woga wowote.
Tujadiliane, tukikubaliana, ajenge kwa makubaliano tuliyofikia pamoja na yeye; kama hatukubaliani juu ya matakwa yake, aende zake, na wala isiwe tena hizi kelele za mabeberu hivi au mabeberu vile. Huu utakuwa ni uamzi wetu.

Na hii haituzuii kuingia kwenye mapatano mengine juu ya mradi huo, eti kwa kuogopa tu "mabeberu".
Tayari Biden na BoJo wanajadili uwezekano wa kuweka $65 Billion mezani kwa kazi hiyo ya kupambana na BRI. Hatuwezi kuwaogopa hawa wala mwingine yeyote, kama tunajua maslahi yetu ni yapi.Hizo enzi za kuyumbishwa na kugawanywa zimepitwa na wakati - ni maslahi yetu pekee ndiyo yaliyo muhimu.

Na si hawa pekee, yaani China na Mabeberu tunaoweza kushirikiana nao kujenga mradi huo, na sio lazima iwe mmoja, wawili au kundi lwa wawekezaji. Huu ni mradi mkubwa, kwa hiyo kila mtu anaweza kushiriki ankoona kunamfaa, na tutakaribisha aje tujadili, tukiafikiana anajiunga.

Tunaweza pia kuanza kujenga sisi wenyewe taratibu, kama Lamu inavyojengwa hivi sasa, baada ya kukosa mwekezaji wa kuuchukua kama huyo BRI na wengine.

2. Ukweli ni kwamba, Tanzania na pwani yake ipo pazuri mno. Wenzetu hapo juu wanahangaika kwelikweli kujiuza bila ya mafanikio yoyote.

Ni viongozi wetu tu watumie akili zao na uzalendo wao ili nchi yetu ifaidike na mahali ilipowekwa kijiografia.

Hakuna lazima ya kujisalimisha kwa mchina kama masharti yake hayana maslahi kwetu.
Kwahakika kama yangekuwa ni maslahi ya taifa kila mtu angepigana kuona yanapatikana, tatizo ni wale wanaousemea mradi hawana moral authority ya kufanya hivyo kutokana na track records zao za nyuma ndiyo sababu ya wengi wetu kuhofu...Kwanini basi kama ni maslahi ya taifa wasiweke wazi kila kitu ili taifa lijue kunani?

Huo ujanjaujanja wa watu hao na background zao ndizo zinazotufanya tuogope...Wengi wao walihusika ku sign mikataba mibovu na dhalili leo hii wanakipi jipya la kutueleza?
 
Back
Top Bottom