Ndebile
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 7,745
- 11,267
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alafu ndio utaweka huo wa bandari?Niletee wa Airport ya Chato Kwanza na ununuzi wa ndege
Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Sasa hizi hoja zenu kwamba huo mradi una faida kinyume na selikali inavyotwambia mnatoa wapi kama mkataba wenyewe hamna?Tumeuliza ni mkataba upi mliwahi kuwekewa wazi? Buzwagi? GGM? JNIA? CHATO IA? Ndege za ATC? SGR? SONGAS? ETC... Acheni kujadili mada kinafiki...
Umemaliza yote!! Hawa jamaa walioingia hapa na kuanza kumwaga matusi hakuna hata mmoja ambae amesoma angalau part! Lakini kwavile wanaamini kufeli kwa mradi huu kunatokana na JPM, basi wakiona tu, wanaanza mitusi kwa kile wanachoamini wanalinda legacy ya JPM kumbe ni uzuzu tu!!Mkuu watu wenye roho ya kimaskini wana tabia zinayofanana "KUPENDA UMASKINI, KUCHUKIA WENYE MAFANIKIO, UVIVU WA KUSOMA - KUFIKIRI NA KUJADILI... Hupenda kukurupuka na kuhemkwa hata kwa wasiyoyaelewa!!"
Hakuna hilo sharti!Miongoni mwa masharti ya miradi ya aina hiyo kutoka China ni kwamba iwapo mradi waliowekeza utashindwa kurudisha pesa yao nchi walipowekeza itabidi watafute eneo jingine la kurudisha pesa yao kwa muda mfano kuchimba madini, kupewa uwanja wa ndege, nk
Unasemaje Chige kuhusu hilo!
Kuhujumiwa hapana... Mchina hana uwezo wa kuzuia meli za wengine zisiingie kwenye hizo bandari!! It's strictly business! Kwanza kama ile ya Piraeus Mchina hakuhusika hata kwenye ujenzi wake!Mkuu mimi sipendi siasa ila hili linanishawishi kusema kitu.
Kuna uwezekano mkubwa bandari za piraeus na hambantota zimehujumiwa na mchina ili yeye azikamate kwa maslahi yake.
Hilo linawezekana kabisa, na ndo maana mara kadhaa nimesisitiza issue sio kuwa na uwezo wa kujenga bandari bali uwezo wa kui-utilize hiyo bandari! Mchina kwake inakuwa rahisi ku-utilize kwa sababu ana share kubwa sana ya mizigo inayopita baharini!Kuna uwezekano mkubwa china akijitoa piraeus na hambantota zikarudi kudorora kiufanisi maaana zinaendeshwa kwa influence ya mchina na si umuhimu wao kijiografia.
Miradi mingi kama sio yote ya China inahusisha pia industrial complexes! Tuchukulie Bagamoyo kwa mfano... endapo ile model inafanikiwa kama ilivyokusudiwa, hata Mchina akiondoka baada ya muda kwisha bado bandari itakuwa na mzigo mkubwa sana wa manufactured goods!Endapo miaka ya umiliki wao ikiisha kuna uhakika gani kuwa hawatatengeneza mazingira shindanishi ili bandari ishindwe na wao warudi kuimiliki kama hambantota au kutafuta malisho bora zaidi kwa ajili yao?
Kodi bhana itakusanywa, usisikilize propaganda kwamba hatutachukua kodi!! Kodi ambayo Mchina huwa anataka kusamehewa ni income tax kwa sababu ndiyo anayotakiwa kulipa yeye!!Ni matumaini yangu serikali inatafuta namna bora zaidi ya kuvuna wakati hawa jamaa wakiwa ndio wamiliki wakuu kwa mategemeo kuwa yajayo hayatabiriki ndio maana inakomaa na kodi kuliko kutegemea kuachiwa mradi usiojua mwisho wake.
Tujipemuda tu.
We jamaa heb pumzika utuache tujadili hii mada wenyewe sasa...tangu umeuweka huu uzi upo bze kujibu karibu kila kitu...ume spend the whole day humu ndani.Hakuna hilo sharti!
Sharti linalofanana na hilo ni kutaka kulipwa fidia endapo biashara itaenda ndivyo sivyo lakini sio kutafutiwa eneo lingine!!!
Hili ndio moja ya masuala yanayotakiwa kuangaliwa kwa umakini na watendaji wetu!! Hata hivyo, kwa setup ya mradi ilivyo, sioni ni namna gani mradi unaweza kushindwa kutengeneza biashara ya kutosha!
Biashara inaweza kuwa declared ni ndogo endapo tu mamlaka husika zitashindwa kufuatilia kwa makini kinachoendelea bandarini... ni kama inavyotokea kwenye madini!!
Ukiweka watumishi wa serikali wasio waaminfu, ni hao hao watumishi wetu ndio wana-collude na investors ili ku-declare uzalishaji mdogo tofauti na uhalisia!
Unajua mkuu 'Ame', haya mambo sasa inafaa kuyasemea waziwazi bila kuyaficha.Kwahakika kama yangekuwa ni maslahi ya taifa kila mtu angepigana kuona yanapatikana, tatizo ni wale wanaousemea mradi hawana moral authority ya kufanya hivyo kutokana na track records zao za nyuma ndiyo sababu ya wengi wetu kuhofu...Kwanini basi kama ni maslahi ya taifa wasiweke wazi kila kitu ili taifa lijue kunani?
Huo ujanjaujanja wa watu hao na background zao ndizo zinazotufanya tuogope...Wengi wao walihusika ku sign mikataba mibovu na dhalili leo hii wanakipi jipya la kutueleza?
Maajabu haya!!!We jamaa heb pumzika utuache tujadili hii mada wenyewe sasa...tangu umeuweka huu uzi upo bze kujibu karibu kila kitu...ume spend the whole day humu ndani.
Unatupa mashaka nguvu na muda ulioiwekeza kwenye huu uzi...
You are all over aisee, ni km mtu alielipwa ashinde siku nzima humu ndani kutetea huu mradi, heb upumzike sasa uwaachie watu wengine nao wadiscuss, au mpo team nzima mnapeana zamu?
Umeandika maneno mengi ambayo hayakusadia kuelewa kujengwa au kutojengwa bandari ya Bagamoyo. Kwanza, hakuna aliyekataa bandari ya Bagamoyo isjengwe. Wananchi pamoja na serkali wanapenda bandari hiyo ijengwe. Ili hiyo bandari kujengwa lazima iwepo pesa. Pesa hiyo inaweza kuwa ya ndani au mkopo. Kwa sasa pesa ya ndani haitoshi kwa sababu inafanya miradi mingine ya kimkakati. Kama itajengwa kwa pesa ya ndani itabidi ingoje kwanza miradi mingine ikamilike.UTANGULIZI
Amini usiamini, wale wale ambao wamekuwa wakijivika uzalendo, linapokuja suala la Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ndiyo hao hao wanaotumikia Mabeberu bila wao kujijua!
Nitajadili mada hii katika sehemu mbili:-
Kwa bahati, binafsi mwaka 2016 nilikuwa “Mbeba Mikoba” wa Researcher mmoja wa Kimarekani (Beberu?) aliyekuwa anafanya utafiti kuhusu Belt and Road Initiative (BRI).
- Kwanini wale wanaoitwa Mabeberu hawawezi kuwa tayari kuona miradi kama ya Bandari ya Bagamoyo inafanikiwa, na
- Hoja zinazotolewa na Wazalendo Kupinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Kazi yangu kubwa ilikuwa Literature Review!
Kwa wanaofahamu mambo ya Resech, ukifanya Literature Reviews, hususani ya wasomi kama huyu bwana, basi unapata fursa ya kufahamu mambo mengi zaidi yaliyopata kutokea hapo kabla kwenye eneo husika!
Kwa wasiofahamu, Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni matokeo ya (BRI) ambayo, Rais wa China, Xi, anailezea BRI kwamba:
Kwa lugha nyepesi, malengo ya China kupitia BRI ni kuiunganisha nchi hiyo na sehemu zingine duniani, hususani Asia, Afrika, na Ulaya! Uunganishaji huo ni kwa ujenzi wa miundombinu, hususani ya bandari, reli, na viwanja vya ndege.
Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA alipata kuchambua kwa undani kabisa suala la Belt and Road Initiative!!
Na hapo sidhani kama mtu anahitaji kuwa na Shahada ya Diplomasia ya Uchumi na Ushikirikiano wa Kimataifa kunusa “threat” ya mpango huo wa China kwa mataifa makubwa, hususani Marekani!
Kutokana na ukweli huo, ndo maana haishangazi mara tu BRI ilipotangazwa, Waandishi na Watafiti mbalimbali kutoka nchi za magharibi wakaanza kulivalia njuga suala hilo.
Makala zikaandikwa, na tafiti zikafanywa kuhusu BRI, lakini makala nyingi kama sio zote zililenga kuyatisha mataifa mengine kuwa makini na BRI!
Watu hawa wakageuka kuwa “Wajomba Zetu” Afrika, huku wakituasa tusije tukaingia kwenye mtego huo hatari wa China!
Ni kupitia hizo tafiti ndipo nami nikajikuta nipo na huyo Mtafiti Msomi kweli kweli wa Kimarekani.
Huyu Bwana case studies zake zilikuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Bandari ya Hambantota (Sri-Lanka), pamoja na Bandari ya Piraeus (Ugiriki).
Ukweli ni kwamba, ilinichukua chini ya dakika 3 kugundua Mtafiti huyu ni kama tayari alishakuwa na “matokeo” ya utafiti wake hata kabla kazi haijaanza! Kwa kifupi, alionesha dalili zote za kutounga mkono Mradi wa Bandari ya Bagamoyo!
Hata "beberu" niliyekuwa namtumikia, nae alikuwa pamoja na "Wazalendo" wetu!!
Binafsi, nilikuwa “in favor of” Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, kwahiyo tukaanzisha kimdaharo kisicho rasmi!
Baada ya kuona hoja zake nyingi nazipangua, akaishia kuuliza ikiwa nadhani ni busara kwa taifa maskini kama Tanzania kuwa na bandari kubwa kama ya Bagamoyo!!
Jibu langu kwake lilikuwa rahisi sana, kwamba: Bandari ya Bagamoyo itakuwa ni kubwa mno kwa Tanzania endapo tu unaamini Tanzania na majirani zake wataendelea kuwa maskini kwa miongo kadhaa ijayo, vinginevyo, huwezi kusema ni “kubwa mno”!
Kwa ufupi, Mheshimiwa huyu, kama walivyokuwa wenzake wengine, nyimbo zao zilikuwa ni agenda ya siri ya China kuitumia BRI kama Mtego wa Madeni kwa nchi maskini!
Lilipokuja suala la Bandari ya Hambantota kule Sri-Lanka, propaganda zikasambazwa kwamba China IMEITWAA bandari ya Sri Lanka ili kufidia deni lake!
Wazalendo wetu nao wakazidaka propaganda hizo, na bila kufanya utafiti, wakaanza kutueleza kwamba “tukishindwa kulipa deni, Wachina wataichukua Bandari ya Bagamoyo kama walivyofanya kule Sri-Lanka.”
Kuweka kumbukumbu sawa, habari za Wachina KUITWAA bandari hiyo zilipotoshwa. Nitaeleza hili kinaga ubaga hapo baada kwenye makala hii.
Pamoja na suala la “Debt Trap”, watu hawa tunaowaita Mabeberu ambao kwa hili tunawaona wanajali maslahi yetu, pia wakawa wanatuambia agenda nyingine ya siri ya China ya kuanzisha “military base” kupitia BRI.
Hapa wakawa wanalenga kutuambia, hata mradi kama wa Bandari ya Bagamoyo, lengo lake ni Wachina kutaka kuweka kambi za kijeshi eneo hili la Afrika Mashariki!
Hata hivyo, hawatuambii ukweli kwamba, ni wao wenyewe ndio wanaozihofia hizo “military bases” za China endapo zitawepo!
Kila mfuatiliaji wa mambo duniani, anafahamu Marekani ina kambi za kijeshi sehemu kadhaa duniani, lakini linapokuja suala la China au mataifa mengine kufanya yale yale ambayo yeye keshayafanya kwa miongo kadhaa, hapo inageuka kuwa nongwa!
Waingereza wana msemo “If you can’t beat them, join them.”
Guys, amini usiamini, juzi yule Mtafiti niliyekuwa nae ametoa makala kwenye moja ya majarida maarufu sana duniani! Baada ya kuisoma makala ile, hapo hapo nikajisikia uchungu, na kumhurumia!
Yaani yule yule aliyekuwa anaipinga BRI, kwenye hiyo makala anaulaumu wazi wazi Utawala wa Trump kwa kutumia kete ya Debt Trap kama njia ya kuidhoofisha BRI.
Kwenye makala hiyo, kuna sehemu anahoji “Kama kweli BRI ni kitu kibaya kiasi hicho, ni kwanini basi China inaendelea kutafuta Washirika walio tayari kujiunga na BRI.”
Mwishowe, Mtafiti huyu anaisemanga serikali yake kwamba ”USA haitaweza kumzuia Rais wa China kuwekeza kupitia BRI endapo US haitakuwa na mbadala kwa mataifa yanayoshirikiana na China!
Ufaransa, imeanza kuliona hilo kama ilivyowahi kuripotiwa na France24 kwamba:
Desperation ya Mtafiti huyu bila shaka inatokana na vile anavyoona jinsi ambavyo nchi mbalimbali duniani jzinavyojiunga na BRI, kinyume na matarajio ya USA ambayo ilikuwa ina-lobby nchi zingine, hususani Washirika wake kutojiunga na BRI.
Kwa bahati mbaya sana, si Afrika, si Asia! Hadi baadhi ya nchi za Ulaya na Carribean zinaingia kwenye BRI. Mbaya zaidi, miradi ya BRI inaonekana kufanya vizuri sana!
Kwa mfano, mwaka 2016 Bandari ya Piraeus ilikuwa ndio ya kwanza barani Ulaya kubinafsishwa chini ya BRI. Bandari hii ndiyo bandari kubwa kuliko zote nchini Ugiriki, na ndio langu kuu la bahari linalounganisha nchi za EU na Asia!
Hapo kabla, bandari hii ilikuwa haifanyi vizuri, na ripoti za nyuma zilikuwa zinaiweka bandari hiyo kama bandari ya 17 barani Ulaya!
Baada ya Wachina kuchukua 51% ya hisa za bandari hiyo, na hatimae hisa hizo kufikia 67%; ripoti ya mwaka huu kupitia Port Economics inasema kwa sasa Bandari ya Piraeus ndiyo bandari kubwa zaidi (kwa kiwango cha makontena) kwenye ukanda wa Bahari ya Mediterranean, na ya 5 Barani Ulaya!!
Sasa haya ndo mambo ambayo watu hawakuyataka! Yaani bandari iliyo kwenye ardhi ya Mzungu, 67% imilikiwe na Mchina, na hapo hapo inaanza kutishia ushawishi wa bandari zingine zinazomilikiwa na Wazungu wenyewe!
JokaKuu
Braza, mimi hapa ntarudi kesho ili tuliweke sawa hili jambo.....Long time no see...
Nilijaribu kutafuta ule uzi wako Belt and Road Initiative lakini nilishindwa kuu-access!! Itakuwa muafaka sana kama utanigea link!
Umenisemea pia mkuu, ubarikiwe sanaWe jamaa heb pumzika utuache tujadili hii mada wenyewe sasa...tangu umeuweka huu uzi upo bze kujibu karibu kila kitu...ume spend the whole day humu ndani.
Unatupa mashaka nguvu na muda ulioiwekeza kwenye huu uzi...
You are all over aisee, ni km mtu alielipwa ashinde siku nzima humu ndani kutetea huu mradi, heb upumzike sasa uwaachie watu wengine nao wadiscuss, au mpo team nzima mnapeana zamu?
Wakati 'ule kimya', wakati 'huu papapapa'Mkuu umelipwa pesa ngapi ili kuupugia chapuo hivi huu mradi?,
Huo mkataba upelekwe bungeni ujadiliwe na wabunge wetu akina musukuma, babu tale . kibajaji, jah people. Na wengine kibaoHatutaki porojo mkataba umesha kuwa na mashaka upelekwe bungeni watu wapewe muda kuusoma then wajadili vinginevyo ni uhujumu uchumi full stop.
Akili ya kawaidatu inakataa kukubali kwamba mchina ataruhusu bandari nyingine zifanye kazi, mchina hataruhusu maana patakuwa na ushindani na itapelekea kuchelewesha kurudisha garamazao za uwekezaji.
Vinginevyo bandari zote zitakufa zenyewe kwakuwa zitakosa mbinu za kushindana na hiyo bandari ya kisasa ya bagamoyo kwenye viwezeshi, pia wanaweza kuzielekeza melizao na nyingine watakazoweza kupitisha mizigo bagamoyo na kuathiri bandarizetu.
Mkataba uwekwe wazi, ujadiliwe.
Kama hatutaweza kupata kodi inayolingana na mapato tunayo pata sasaivi katika bandarizetu na yanayo kuwa kila mwaka, itakuwa ni ujuha wakiwango cha lami kukubali huo mradi.
Shida sio kujengwa au kununua ndege, shida ni je imejengwaje? Au ndege zimenunuliwaje?Kama kufufua ATC, kujenga standard gauge railway ikiwa ni pamoja na kufufua TRC, kujenga bus stand kila mkoa, kununua meli nk ni wizi basi inatakiwa itengenezwe kamusi nyingine ya kiswahili kuelezea maana ya wizi.
Mimi tangu siku ile kasim majaliwa aseme uongo msikitini kuhusu hari ya jpm. Sina hamu nao.Serikali ipi unayotaka iaminike?!
Huyo Kakoko mwenyewe ana tuhuma za wizi, na ndio maana kasimamishwa! Sasa unataka tumwamini mtu mwenye tuhuma za wizi?!
Naongezea hapo Mkuu. Hata jpm na yeye ni wakupuuzwa kwa maana aliukataa mkataba bila ya kutuoesha na sisi tuusome .Kwa vile kakoko hajaweka mkataba akaja na blaa blaa..
Wewe hujaweka mkataba umekuja na blaa blaa..
Wote nyie ni wa kupuuzwa..