Ukiamua kujigubika uzandiki huwezo ona cha kujadili... aliwahi kuandika Marehemu Shaaban Robert "utu busara, ujinga hasara..." mapenzi yakikithiri moyoni hupofusha ubongo wa mpendaji... Mwalimu ambaye ndio baba wa Taifa mwenyewe alipata kukiri kukosea... iweje wengine? Unadhani alipoandika kitabu TUJISAHIHISHE alikuwa akilenga nini? Tuliandika mara kadhaa humu "Mwendazake alikuwa amezunguukwa na fisi na tai wenye uchu waliokuwa wakimpotosha kwa maslahi yao huku wakimsifu na kumpamba ili kujificha katika sura ya uzalendo..."
ukijivika usafihi na umbumbumbu hata kuvuka barabara tu huwezi jadili bali katisha tu midhali madereva wanakuona...
Tunawaita "wazalendo wachumia tumbo..."
Daah,!! Mkuu umekielewa sasa hata hicho ulichoandika mwenyewe
Ndiyo, JPM alizungukwa na wazandiki, lakini hoja ya msingi mbona unaacha Kwa maksudi kuijadili??
Mwandishi, amejitahidi kutuonyesha uzuri na faida za research aliyoifanya kuhusu mradi huu, ni Jambo jema na kiukweli, Kwa maelezo na umhimu wa mradi huu, ni mzuri na unavutia, lakini sasa, licha ya maelezo matamu yenye viambatanisho vingi Vya msingi, bado kunayo maswali ya kuuliza, na nadhani ameleta hii mada akifahamu fika, itajadiliwa Kwa namna tofauti, na utofauti ni kama huo unaouponda wewe badala ya kutoa maelezo sahaihi ya kile ameuliza
Binafsi, nachotaka kutoka kwenu, imma kwa Mleta mada au kwako ni hiki
JPM, alitudokeza Kwa ufupi kuhusu mapungufu makubwa yaliyo kwenye Mkataba wa mradi wa Bagamoyo, na hata kama ni uwongo!! Ninyi mnaotaka kutuaminisha kwamba haiko hivyo kama alivyodokeza JPM, basi nyinyi mlete huo Mkataba hapa, ama nukuu zenu za Uzi huu, zitawaliwe na nukuu kutoka Kwa Mkataba wenyewe, la sivyo, na nyinyi mnapaswa kutokuwa na mashaka kutoka kwa kina Kakonko
Pili, kuna mtu anaitwa Moasa Mao, ni mchina huyu, yeye, anakataa kila kilichosemwa na JPM kuonyesha jinsi Mkataba usivyo na manufaa kwetu kama nchi na Wala haambatanishi vipengele Vya Mkataba katika kupinga kwake dokezo la JPM kuhusu ubovu wa Mkataba na mashariti yasiyozingatia Uhuru wa nchi yetu na Sheria zetu,
Tunajiuliza, Ikiwa kina Mao ndio wanaotaka waje kuwekeza, nahisi pia huwenda alishiriki kuandaa mkaba ama anaufahamu vema Mkataba huo, Kwa nini asioneshe uwongo wa Kakonko na JPM Kwa kunukuu sehemu za mashariti ya Mkataba huo??
Mpaka sasa Kwa maelezo haya, nadiriki kuwaita kina JPM na Kakonko ni wazalendo wa nchi yetu kwa hichi mnachokitetea, na kama hamtakuja kutuonyesha ukweli unaotoka kwenye Mkataba, muache kuwaita waongo kina Kakonko,
Tatu, Tanzania tumegawika katika sehemu mbili, kuna anayewashuku wenzake kwamba huwenda wamekula chenji ya mchina ili kuupigia Kampeni mradi huu, lkn kuna mwingine anaona ni kama watu hao wanakataa tu bila sababu,
Wanaokataa huu mradi Hadi wajiridhishe Kwa kuusoma Mkataba, mi naona wako Sawa kabisa, Kwa sababu, hili Jambo limeibuka Kwa nguvu na Kwa Kasi ya 4g baada Tu ya JPM kufariki, huoni kwamba kweli hata hizo nukuu za Mao huwenda zimetengenezwa Tu ili kuendelea kuwa sehemu ya Kampeni ya hao tunaodhani wamekula chenji ya mchina? Kampeni nzuri ni Ile inayoonyesha, Sera zako na namna ya kufanya, sasa nyinyi mnakuja hapa bila Sera, Ila mnatuonyesha tu jinsi itakavyokuwa, hii siyo Sawa!!
Mradi tunautaka, lakini Kwa sabb umeleta sintofahamu, basi Mkataba upelekwe bungeni Kwa uwazi usomwe, na hapo tutawapuuza vilivyo hao mnaotaka tuwapuuze!! Bila hivyo, basi tunaona ni kama na nyinyi mnataka kuingizwa kwenye shimo moja na speeker!!