Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Sasa hapa tunajadili nini basi kama mkataba wenyewe hatuuoni?

Huoni kama ni ujinga kujadili mada ambayo imeegemea upande mmoja huku mleta mada akiwa kaweka hoja zake kwa hisia tu?
Ukiamua kujigubika uzandiki huwezo ona cha kujadili... aliwahi kuandika Marehemu Shaaban Robert "utu busara, ujinga hasara..." mapenzi yakikithiri moyoni hupofusha ubongo wa mpendaji... Mwalimu ambaye ndio baba wa Taifa mwenyewe alipata kukiri kukosea... iweje wengine? Unadhani alipoandika kitabu TUJISAHIHISHE alikuwa akilenga nini? Tuliandika mara kadhaa humu "Mwendazake alikuwa amezunguukwa na fisi na tai wenye uchu waliokuwa wakimpotosha kwa maslahi yao huku wakimsifu na kumpamba ili kujificha katika sura ya uzalendo..."
ukijivika usafihi na umbumbumbu hata kuvuka barabara tu huwezi jadili bali katisha tu midhali madereva wanakuona...

Halafu wanaboa sana wanavyojiona eti wao ndo wazalendo sana kuliko wengine wakati kimsingi, "uzalendo" wao upo kwa Mwendazake na wala sio kwa taifa!
Tunawaita "wazalendo wachumia tumbo..."
 
MAPENDEKEZO

Reserved for later
Nguvu inayotumika kupigia debe huu mradi inaonyesha pasi na shaka kuwa kuna watu wameahidiwa bakshishi kubwa sana iwapo mradi utapita. Inasikitisha sana Afrika bado ina watu wenye tamaa kama wewe ambao wako tayari kuuza vipande vya nchi ili tu waneemeke. Huu mradi ni bomu kubwa na rais yoyote atakayekubali kuingia kwenye mtego historia itakuja kumhukumu kwa usaliti wake. Katu nchi huru yenye kujitambua haiwezi kuruhusu kuipatia nchi nyingine sehmu nyeti kama bandari imiliki. Wachina ni watu hatari sana na very corrupt. Watatorosha mali za nchi yetu zote kwa kutumia upenyo wa bandari watakayopewa. Baada ya kuona Magufuli amefariki ndiyo mnapata upenyo wa kunadi nchi yetu? Zitto utakufa kwa laana wewe!
 
Pascal unajua hakuna mtu ambae anakataa ujenxi wa Bandari Bagamoyo ila issue hapa wao ikijengwa tutafaidika vipi?

Kati ha Marais wawili waliopota yupo ambae nina hakika alikuwa na uwezo wa kuisoma MOU mwenyewe ata ikiwa na page 200 na yupo ambae kwake alikuwa kazi yake kusaini tu bila ata kusona page moja.
Licha yakumuona Magu anakisirani sijui alidangwanywa lakini nina hakika Magu alikuwa mwepesi kusoma page ata 100 kuliko JK, JK alikuwa ukipeleka document kwake ye anasaini tu hana mda.
Mkuu Mpinzire , hii ni mikataba ya kibiashara, marais hawasaini mikataba ya kibiashara, marais wana sign treaties, by laterals na multilaterals international treaties. Hivyo hii na JK na JPM, ni kuwaonea tuu, kuna wataalamu wa kufanya uchambuzi yakinifu na kushauri.

Ila kiukweli sisi Tanzania ni watu wa ajabu sana!. Mafuta sasa yanachimbwa hapo jirani Uganda, yatapitishwa kwetu na kupakiwa kwenye mi meli kupelekwa ulaya. Mafuta hayo ya Uganda kwetu yatapita tuu, huku sisi tuiendelea kuagiza mafuta kutoka Uarabuni!. Nimesikia mipango tuu ya mradi wa Bomba la mafuta ya Uganda, lakini sijasikia mradi wowote wa sisi kuenga refinery ili na sisi tuache kuagiza mafuta mbali, tunafishe ya Uganda na kuyatumia.

Tunasubiri mzungu, mwekezaji ndio aje atubunie huu mradi!.

P
 
Niyakane kwa nini mkuu wangu!!

Umesema bandiko ni la propaganda kwa sababu tu nina upande!! Na hilo la kuwa na upande sijakataa, na ndo maana nikahoji kwani ni dhambi kuwa na upande?!

Binafsi, nimejaribu kujadili hoja za wapingaji wa mradi.. kwahiyo, there's nothing personal! Ningekuwa ni mwajiriwa wa Merchant Group, ndo pale tungesema nafanya propaganda kwavile nina maslahi! kinyume chake, sio mfanyakazi wa Merchant, na wala sitokei Bagamoyo, wala Mkoa wa Pwani!

Na sidhani kama nina ndugu yeyote anayeishi Bagamoyo... kwahiyo sina sababu ya kufanya propaganda!!
Wewe ni kibaraka wa kuuza nchi. Tunajua kinachoendelea nyuma ya pazia. Wasaliti wauza nchi nyie. Tunajua watu waliyo nyuma ya huu mpango wa kutoa sehemu nyeti kama bandari kwa nchi ya kigeni. Historia itawahukumu ninyi walafi wakubwa. Mnajali matumbo yenu tu. Unataka kumdnganya nani ni mjinga kuwa umejikucha kuandika yote haya bure! Tunajua China imeahidi kutoa fedha nyingi kwa vibaraka watakaofanikisha kupitisha mradi.
 
Kiuhalisia hakuna watanzania tunatamani sana bandari hiyo kubwa na hivyo viwanda vijengwe kwenye huo ukanda wa bagamoyo. Miaka ya nyuma viongozi wetu walikuwa wanaingia kwenye mikataba mibovu na wawekezaji kwa kutosoma/ ama kusoma bila kuyatafakari Masharti ya Mikataba yaliyomo kwenye hiyo mikataba. Mfano mzuri ni mikataba ya madini, kwa kiasi kikubwa imewanufaisha wawekezaji kuliko serikali. Sasa inatubidi tusirudie makosa tuliyoyafanya miaka ya nyuma kwa kudharau kusoma na kuielewa mikataba tunayoingia na wawekezaji, isije tukajutia kugawa ardhi yetu kwa wageni kwa miaka 99 bila kupata matunda ya mkataba huo tukabaki tunalaumiana na wenyewe kwa wenyewe. Kwa uzi huu uliouandika ulifaa sana ungeingiza vipengele kadhaa vya masharti ya mradi maana ikitokea tumekosana nao na tukapelekana mahakamani basi mkataba ndo utaleta suluhu ama ya kutunyonya au kutunufaisha na si maneno matupu.
 
Chige,

..asante kwa mchango wako huu.

..mradi wa bagamoyo unahusisha pia uwekezaji wa viwanda ambao ulikuwa ufanywe na Oman Fund.

..kwa bahati mbaya wachambuzi wengi hawazungumzi chochote kuhusu wawekezaji wa kutoka Oman.

..kwa mfano, kama muwekezaji wa bandari na mbaya kwanini hatukuendeleza majadiliano kuhusu mradi wa viwanda?

..pia kwanini serikali ya Tanzania isichukue hisa ktk mradi wa bandari? Kwanini tusiwe na hisa nyingi ambazo zitazuia hujuma toka kwa Wachina?

..kuna taarifa ziliwahi kutoka kwenye magazeti kwamba serikali ya Tanzania ilikuwa inatakiwa iwalipe fidia wananchi watakaochukuliwa ardhi yao. Na kwa kufanya hivyo, serikali ingepata hisa kadhaa ktk mradi.

..Sasa taarifa za magazeti zilisema serikali imedai kuwa haina fedha na jukumu hilo wameachiwa wawekezaji na kupelekea serikali kupoteza hisa zake ktk mradi huo.

..Binafsi ningependelea serikali yetu / TPA iwe na hisa za kutosha ktk mradi badala ya kuwaachia Wachina mradi wote wa bandari. Tukifanya hivyo naamini tutaweza kuyalinda zaidi maslahi ya nchi yetu na kuzuia uwezekano wa kuhujumiwa na Wachina.

..Again, asante sana kwa mchango wako. Kwa kweli umelipaisha jukwaa letu kwa kutuletea hoja za kisomi.
 
Wewe ni kibaraka wa kuuza nchi. Tunajua kinachoendelea nyuma ya pazia. Wasaliti wauza nchi nyie. Tunajua watu waliyo nyuma ya huu mpango wa kutoa sehemu nyeti kama bandari kwa nchi ya kigeni. Historia itawahukumu ninyi walafi wakubwa. Mnajali matumbo yenu tu. Unataka kumdnganya nani ni mjinga kuwa umejikucha kuandika yote haya bure! Tunajua China imeahidi kutoa fedha nyingi kwa vibaraka watakaofanikisha kupitisha mradi.
Nguvu inayotumika kupigia debe huu mradi inaonyesha pasi na shaka kuwa kuna watu wameahidiwa bakshishi kubwa sana iwapo mradi utapita. Inasikitisha sana Afrika bado ina watu wenye tamaa kama wewe ambao wako tayari kuuza vipande vya nchi ili tu waneemeke. Huu mradi ni bomu kubwa na rais yoyote atakayekubali kuingia kwenye mtego historia itakuja kumhukumu kwa usaliti wake. Katu nchi huru yenye kujitambua haiwezi kuruhusu kuipatia nchi nyingine sehmu nyeti kama bandari imiliki. Wachina ni watu hatari sana na very corrupt. Watatorosha mali za nchi yetu zote kwa kutumia upenyo wa bandari watakayopewa. Baada ya kuona Magufuli amefariki ndiyo mnapata upenyo wa kunadi nchi yetu? Zitto utakufa kwa laana wewe!
NONSENSE! NONSENSE! NONSENSE! NONSENSE!
Badala ya kujadili hoja unajadili mtu... very stupid, and shallow minded!!
 
NONSENSE! NONSENSE! NONSENSE! NONSENSE!
Mkuu Chige , mkataba wa awali ambao mwendazake aliukataa akiuita wa unyonyaji,tunaruhusiwa kuuweka hapa?
Wewe umeelezea manufaa/faida na hasara za mradi wa Bagamoyo,tatizo watu hawajui tofauti baina ya manufaa/faida na mkataba "hewa" aliousema mwendazake.
Naamini ataamini kweli kama mkataba ulikuwa hivyo alivyokuwa anasema mwendazake,tungeonyeshwa.
Tumeaminishwa kuwa Wachina ndio "rafiki wa kweli", sasa kwa nini hao hao rafiki wa kweli watake kutupiga kwenye mradi huo!!??
Je,huko kwenye miradi mingine ya hao "rafiki wa kweli" Wachina hawatupigi!!?
 
Mkuu big up, umefafanua vizuri Sana. Huu mradi taarifa nyingi Zilifichwa na watu waliaminishwa propaganda.

Kuna kipindi nilikuwa katika mishe mishe nikabahatika kutana na waziri mmoja pale Water Front katika mazungumzo akaongelea Sana madhara endapo China wangejenga Bandari ya Bagamoyo.
 
Chige,

..asante kwa mchango wako huu.

..mradi wa bagamoyo unahusisha pia uwekezaji wa viwanda ambao ulikuwa ufanywe na Oman Fund.

..kwa bahati mbaya wachambuzi wengi hawazungumzi chochote kuhusu wawekezaji wa kutoka Oman.

..kwa mfano, kama muwekezaji wa bandari na mbaya kwanini hatukuendeleza majadiliano kuhusu mradi wa viwanda?

..pia kwanini serikali ya Tanzania isichukue hisa ktk mradi wa bandari? Kwanini tusiwe na hisa nyingi ambazo zitazuia hujuma toka kwa Wachina?

..kuna taarifa ziliwahi kutoka kwenye magazeti kwamba serikali ya Tanzania ilikuwa inatakiwa iwalipe fidia wananchi watakaochukuliwa ardhi yao. Na kwa kufanya hivyo, serikali ingepata hisa kadhaa ktk mradi.

..Sasa taarifa za magazeti zilisema serikali imedai kuwa haina fedha na jukumu hilo wameachiwa wawekezaji na kupelekea serikali kupoteza hisa zake ktk mradi huo.

..Binafsi ningependelea serikali yetu / TPA iwe na hisa za kutosha ktk mradi badala ya kuwaachia Wachina mradi wote wa bandari. Tukifanya hivyo naamini tutaweza kuyalinda zaidi maslahi ya nchi yetu na kuzuia uwezekano wa kuhujumiwa na Wachina.

..Again, asante sana kwa mchango wako. Kwa kweli umelipaisha jukwaa letu kwa kutuletea hoja za kisomi.
Kwanza nakubaliana na wewe kwa 100% kwamba kuna umuhimu wa kuwa na hisa, na suala hilo nililiweka pending kwenye section ya recommendations!

Na hata kwenye hii mada nimesema wazi kinachotakiwa ni kwa watendaji kukaa na wadau ili kuangalia ni mfumo upi utaweka mbele maslahi ya mataifa!!

Kuhusu kwanini serikali isijadiliane basi na Oman ili kuendelea na mpango wa Industrial City!!! Kwa maoni yangu, hiyo itakuwa ngumu sana kuwashawishi Oman, na hata wakikubali, hiyo SEZ itakuwa like any other SEZ... there will be nothing special!

Unajua ingawaje SEZ ilitaka kuwa funded na Oman, bado mwekezaji mkubwa anayetarajiwa kuwa kwenye SEZ ni China, na ndo maana model iliyotaka kutumika ni ile ya Shenzhen!

Yaani the same model iliyoweza kubadili a small fishing town of Shenzhen to industrial city, ndiyo itumike kui-transform a small fishing town of B'moyo to Industrial city!!

Na nilikuwa na video iliyokuwa inaelezea hiyo ndoto ya kuibadili B'moyo to Industrial... it's 100% Chinese stuff, and not Oman stuff!!

On top of that, sio tu viwanda just viwanda bali target ilikuwa ni for export! Ukiangalia ile video ya SEZ Plan, eneo lilitarajiwa kujengwa hadi viwanda vya magari, electronics, chuma, and all that!

Sasa kama hiyo ndo target, basi it's obvious ni uwepo wa bandari itakuwa moja ya factor kubwa itakayowavuta wawekezaji kuwekeza kwenye SEZ!
 
Kuna uwezekano mkubwa sana wakaanza na bandari! Hambantota na Djibouti kote wameanza na uboreshaji wa bandari!!

Watalazimika kuanza na bandari kwa sababu tayari kila mwezi kuna meli kadhaa zinazoenda China kutokea ukanda huu!!! Kwahiyo atahitaji bandari ili kwanza ili ku-handle hiyo cargo!!

Pili, ikiwa mradi wa Industrial City utaenda kama walivyokusudia basi utakuwa mradi mkubwa sana!! Hapa watakuja kuwekeza wafanyabiashara mbalimbali!!

Kwa watakaokuja kujenga viwanda, confidence yao itakuwa kubwa zaidi zaidi endapo manufacturers wataona SEZ ina huduma zote muhimu, including bandari!!

Na hata kama itakuwa haijakamilika, kwao wataona ni safe zaidi wakiona ujenzi umeshaanza!

REMEMBER, plan kwenye hiyo complex inahusisha viwanda vikubwa ambavyo vitahitaji sana kufanya export!
Unajua unaandika Maneno mengi yasio na mashiko nime kuwekea hiyo ya Sirilanka sijui kama umeisoma?

Tukirudi kwenye hadithi yako tutaona hiyo ya Sirilanka kwa sasa unatumia na india Kusafirisha magari ya Tata , sasa wewe huku Bagamoyo ujenge hiyo Bandari bila kuanza ku create demand for the port itakuwa ni ujinga uliopitiliza.
Na Sirilanka imekaja kwenye mkondo mzuri kwa mambo ya Usafiri. Kati ya Asia na europe na africa .
Hapa sikatai kwamba na sisi na geographical advantage, lakini kwa Sasa bado
Na tukisha stabilize na mambo ya production na railway kuwa tayari hivyo flow ya mizigo kuwa nzuri, tunaweza kuanza kujenga wenyewe kwa fedha zitakazokuwa zinatoka Bandari ya Mtwara, Tanga na Dar es salaam na mkopo kidogo
 
Ukiamua kujigubika uzandiki huwezo ona cha kujadili... aliwahi kuandika Marehemu Shaaban Robert "utu busara, ujinga hasara..." mapenzi yakikithiri moyoni hupofusha ubongo wa mpendaji... Mwalimu ambaye ndio baba wa Taifa mwenyewe alipata kukiri kukosea... iweje wengine? Unadhani alipoandika kitabu TUJISAHIHISHE alikuwa akilenga nini? Tuliandika mara kadhaa humu "Mwendazake alikuwa amezunguukwa na fisi na tai wenye uchu waliokuwa wakimpotosha kwa maslahi yao huku wakimsifu na kumpamba ili kujificha katika sura ya uzalendo..."
ukijivika usafihi na umbumbumbu hata kuvuka barabara tu huwezi jadili bali katisha tu midhali madereva wanakuona...

Tunawaita "wazalendo wachumia tumbo..."
Daah,!! Mkuu umekielewa sasa hata hicho ulichoandika mwenyewe

Ndiyo, JPM alizungukwa na wazandiki, lakini hoja ya msingi mbona unaacha Kwa maksudi kuijadili??

Mwandishi, amejitahidi kutuonyesha uzuri na faida za research aliyoifanya kuhusu mradi huu, ni Jambo jema na kiukweli, Kwa maelezo na umhimu wa mradi huu, ni mzuri na unavutia, lakini sasa, licha ya maelezo matamu yenye viambatanisho vingi Vya msingi, bado kunayo maswali ya kuuliza, na nadhani ameleta hii mada akifahamu fika, itajadiliwa Kwa namna tofauti, na utofauti ni kama huo unaouponda wewe badala ya kutoa maelezo sahaihi ya kile ameuliza

Binafsi, nachotaka kutoka kwenu, imma kwa Mleta mada au kwako ni hiki

JPM, alitudokeza Kwa ufupi kuhusu mapungufu makubwa yaliyo kwenye Mkataba wa mradi wa Bagamoyo, na hata kama ni uwongo!! Ninyi mnaotaka kutuaminisha kwamba haiko hivyo kama alivyodokeza JPM, basi nyinyi mlete huo Mkataba hapa, ama nukuu zenu za Uzi huu, zitawaliwe na nukuu kutoka Kwa Mkataba wenyewe, la sivyo, na nyinyi mnapaswa kutokuwa na mashaka kutoka kwa kina Kakonko

Pili, kuna mtu anaitwa Moasa Mao, ni mchina huyu, yeye, anakataa kila kilichosemwa na JPM kuonyesha jinsi Mkataba usivyo na manufaa kwetu kama nchi na Wala haambatanishi vipengele Vya Mkataba katika kupinga kwake dokezo la JPM kuhusu ubovu wa Mkataba na mashariti yasiyozingatia Uhuru wa nchi yetu na Sheria zetu,

Tunajiuliza, Ikiwa kina Mao ndio wanaotaka waje kuwekeza, nahisi pia huwenda alishiriki kuandaa mkaba ama anaufahamu vema Mkataba huo, Kwa nini asioneshe uwongo wa Kakonko na JPM Kwa kunukuu sehemu za mashariti ya Mkataba huo??

Mpaka sasa Kwa maelezo haya, nadiriki kuwaita kina JPM na Kakonko ni wazalendo wa nchi yetu kwa hichi mnachokitetea, na kama hamtakuja kutuonyesha ukweli unaotoka kwenye Mkataba, muache kuwaita waongo kina Kakonko,

Tatu, Tanzania tumegawika katika sehemu mbili, kuna anayewashuku wenzake kwamba huwenda wamekula chenji ya mchina ili kuupigia Kampeni mradi huu, lkn kuna mwingine anaona ni kama watu hao wanakataa tu bila sababu,

Wanaokataa huu mradi Hadi wajiridhishe Kwa kuusoma Mkataba, mi naona wako Sawa kabisa, Kwa sababu, hili Jambo limeibuka Kwa nguvu na Kwa Kasi ya 4g baada Tu ya JPM kufariki, huoni kwamba kweli hata hizo nukuu za Mao huwenda zimetengenezwa Tu ili kuendelea kuwa sehemu ya Kampeni ya hao tunaodhani wamekula chenji ya mchina? Kampeni nzuri ni Ile inayoonyesha, Sera zako na namna ya kufanya, sasa nyinyi mnakuja hapa bila Sera, Ila mnatuonyesha tu jinsi itakavyokuwa, hii siyo Sawa!!

Mradi tunautaka, lakini Kwa sabb umeleta sintofahamu, basi Mkataba upelekwe bungeni Kwa uwazi usomwe, na hapo tutawapuuza vilivyo hao mnaotaka tuwapuuze!! Bila hivyo, basi tunaona ni kama na nyinyi mnataka kuingizwa kwenye shimo moja na speeker!!
 
NONSENSE! NONSENSE! NONSENSE! NONSENSE!
Badala ya kujadili hoja unajadili mtu... very stupid, and shallow minded!!
AIBU! AIBU! AIBU! AIBU!

Hakuna hoja bali ni udalali wa kuuza lango la nchi kwa wageni. Kina Zitto ni vibaraka.
 
Mkuu Chige , mkataba wa awali ambao mwendazake aliukataa akiuita wa unyonyaji,tunaruhusiwa kuuweka hapa?
Wewe umeelezea manufaa/faida na hasara za mradi wa Bagamoyo,tatizo watu hawajui tofauti baina ya manufaa/faida na mkataba "hewa" aliousema mwendazake.
Naamini ataamini kweli kama mkataba ulikuwa hivyo alivyokuwa anasema mwendazake,tungeonyeshwa.
Tumeaminishwa kuwa Wachina ndio "rafiki wa kweli", sasa kwa nini hao hao rafiki wa kweli watake kutupiga kwenye mradi huo!!??
Je,huko kwenye miradi mingine ya hao "rafiki wa kweli" Wachina hawatupigi!!?
Unajua nini?!

Hawa jamaa hapa JF wanatoka povu bure tu!! Kwanza, ambacho kilikuwepo wakati wa JK sio mkataba bali agreement ambayo ili-expire tangu 2017 kama sikosei!!

Kwenye agreement ile ambayo hata hivyo hatukuoneshwa, serikali na China Merchant walikubaliana iwe kama model, itakayowaongoza katika kufanya majadiliano rasmi, na hatimae kuwekeana mkataba rasmi!!

Majadiliano hayo yamefanyika wakati wa JPM, na vipengele vingi walikubaliana vikabaki vichache ambavyo hata hivyo waligoma kuviweka wazi!!

Hata hivyo, tulipata taarifa zisizo rasmi kwamba moja ya vipengele vilivyoleta taabu ni suala la ardhi ambapo Mchina anataka amilikishwe kwa miaka 99.

Lingine ni suala la kodi, ambalo ndo hilo nimelisema hapo juu kwamba Kakoko ameamua kutosema ukweli makusudi wakati uhalisia sio kwamba hatutaruhusiwa kukusanya kodi, bali Mchina ana kawaida ya kuomba msamaha wa income tax, na anataka msamaha huo uwe miaka 30.

Sasa kinachogomba hapa ni hiyo miaka 30!!

Na ingawaje nimesema sio taarifa rasmi lakini sio kwamba ni taarifa za kuokoteza barabarani! Ni taarifa kutoka watu wa ndani ambao walizitoa hizo informally, na bila kutaka kuacha evidence ambayo ingetumika kama reference!
 
Sasa naanza kukuelewa, na kama madai yetu yako hivyo, basi kweli kulikuwepo Shida ya kimkataba

Nashukuru JPM hujamshambulia, basi Kwa maelezo yako haya, JPM Apewe japo heshima Kwa kuweza kuwa ngangali ktk Hilo akitetea vitukuu vyetu vijavyo Ikiwa ingelikuwa sharti la miaka 99 Kwa Aridhi ya Bagamoyo kuwa Chini ya mwekezaji

Barikiwa JPM huko uliko
 
Unajua unaandika Maneno mengi yasio na mashiko nime kuwekea hiyo ya Sirilanka sijui kama umeisoma?
Sri-Lanka imefanya nini wakati nimeshailezea kwenye thread?
Tukirudi kwenye hadithi yako tutaona hiyo ya Sirilanka kwa sasa unatumia na india Kusafirisha magari ya Tata , sasa wewe huku Bagamoyo ujenge hiyo Bandari bila kuanza ku create demand for the port itakuwa ni ujinga uliopitiliza.
Dah... we jamaa wewe! Hivi umesoma nilichoandika, au umekurupuka tu kuchangia?!

Ungesoma ungeona nimesema Hambantota ilikuwa ni loss-making port! Hizo tata unazosema wewe hazikuwa biashara mpya kwa Sri Lanka! Ambacho walifanya, meli ambazo hapo kabla zilikuwa zinashusha magari Colombo, baada zikawa zinapelekwa Hambantota ili kuipa unafuu!

Still ikaendelea kuwa loss making huku deni likiongezeka na ndipo walipoamua kuibinafsisha!

Hoja ya kwamba eti ni ujinga kujenga B'moyo bila kuanza ku-create demand for port, nimeshaisema sana, kwenye posts hadi kwenye thread!

Lakini kwavile umekimbilia ku-argue bila kusoma, ndo matatizo yote haya!
Na Sirilanka imekaja kwenye mkondo mzuri kwa mambo ya Usafiri. Kati ya Asia na europe na africa .
Hapa sikatai kwamba na sisi na geographical advantage, lakini kwa Sasa bado
Na tukisha stabilize na mambo ya production na railway kuwa tayari hivyo flow ya mizigo kuwa nzuri, tunaweza kuanza kujenga wenyewe kwa fedha zitakazokuwa zinatoka Bandari ya Mtwara, Tanga na Dar es salaam na mkopo kidogo
Narudia, YOTE HAYO NIMEYAJADILI! The problem thread ni ndefu na watu mmeona uvivu kusoma!!
 
Sasa naanza kukuelewa, na kama madai yetu yako hivyo, basi kweli kulikuwepo Shida ya kimkataba

Nashukuru JPM hujamshambulia, basi Kwa maelezo yako haya, JPM Apewe japo heshima Kwa kuweza kuwa ngangali ktk Hilo akitetea vitukuu vyetu vijavyo Ikiwa ingelikuwa sharti la miaka 99 Kwa Aridhi ya Bagamoyo kuwa Chini ya mwekezaji

Barikiwa JPM huko uliko
Shida ya vipi wakati nimekuambia hapo kabla hapakuwa na mkataba as mkataba bali makubaliano tu?! Yale makubaliano yalikuwa ya mpito na yalikuwa yana 1 year expiration period!

Kimsingi ilikuwa ni kama proposal tu ambayo baada ya huo mwaka 1 kupita, ndipo Merchant Group na Serikali wangekaa pamoja kujadiliana yale ambayo kila mmoja anaona yanamfaa kwake!!!

Hivi ingekuwa mkataba ulishasainiwa, mngekosa kusikia kwamba "serikali yavunja mkataba na China"! Umeshawahi kusikia jambo kama hilo zaidi ya kusikia mazungumzo yanaendelea?

Tatizo lenu nyie watu ni moja! Allegiance yenu ipo kwa JPM na sio kwa taifa! Matokeo yake, mkiona jambo lolote mnalohisi linalenga kumsemanga JPM, basi mtakuja juu!!
 
Hii ndio JF hasa. Hata kama hatubaliani, lakini angalau kuwe na debates za hoja na sio ushabiki tu. Makala kama hizi ndio hasa zinaweza kusaidia hata wafanya maamuzi na wakaanza kuipa JF heshima yake.

Asante sana mkuu Chige
 
Back
Top Bottom