sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
kuna benki zina madirisha hadi 8 ila hali ipo hivi hivi
Yaani kwenye mabenki yetu haya uje kukuta madirisha yote yana tellers ni kama muujiza hivi, Nakumbuka zamani nikiwa chuoni nimetumiwa ada usiku niende kulipia asubuhi niliponea chupu chupu nisifanye mtihani isingekuwa huruma ya waliopanga foleni kuniruhusu nilipie ada niende kufanya pepa.
Hapa bongo watu wanakwepa sana uwajibikaji wa kukamilisha majukumu yao ya kwenye mikataba ya ajira, wengi wapo kusubiria mishahara tu na kuzuga zuga ofisini waonekane wapo, ukiwakuta wanawajibika basi kuna chances kubwa kwamba kuna mwanya wa upigaji hususani rushwa ama kuibia wateja pesa.
Ni bure kabisa hata elimu wanayosomea vyuoni haina msaada, Kwenye masomo kama operations research / Quantitative methods kuna somo la queuing linahusu haya mambo lakini unabaki kushangaa tu kanakwamba somo hilo ni kama pambo kwenye vyeti.