Mabingwa wa Afrika Wydad Casablanca watuma ofa Simba SC

Mabingwa wa Afrika Wydad Casablanca watuma ofa Simba SC

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Taarifa nilizozipata muda huu zinasema mabingwa wa Afrika, Wydad Casablanca, wametuma ofa ya dola laki nane za kimarekani [bilioni 1.8 za kitanzania] ili wamnase Pape O. Sakho raia wa Senegal.

Hali ya mambo inaonekana kuwavuruga mabosi wa Simba SC, huku wengine wakitaka asiuzwe, na wengine wakisema auzwe.

Wale wanaotaka asiuzwe wanakuja na hoja kwamba, kwa umri mdogo wa Sakho, miaka 25, bado ana muda wa kutosha kuongezewa mkataba na Simba SC, ili kama wakija kumuuza mbele ya safari wamuuze kwa bei kubwa zaidi.

Wengine wakisema, dili kama hili haliji kila wakati, hivyo wameishauri klabu ya Simba SC wasirembe, wabebe huo mzigo wa waarabu "faster" wakautumie kuimarisha kikosi kwenye maeneo mengine.

Vipi wewe mdau wa JF, Pape O. Sakho, mshindi wa goli bora la mwaka CAF, auzwe au asiuzwe?
 
Back
Top Bottom