Mabingwa wa Kuharibu: Toka Mabasi 140 hadi 30

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,256
Reaction score
44,597
Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa kampuni ya UDART (mwendokasi) ilianza ikiwa na mabasi 140 lakini hadi kufikia hiyo juzi yalibakia mabasi 30!!! Yaani wameshindwa kutengeneza mabasi zaidi ya 110!!

CAG alitakiwa kufanya uchunguzi maalum na TAKUKURU wangekuwa na cha kufanya...yaani wameharibu vyetu ili walete vya kwao
 
mangekimambi80-20251002-0001.jpg
 
Barabara yao njia nzima hakuna daladala nyingine,hakuna foleni abiria uhakika (uhakika wa pesa ni mkubwa) unafeli vipi huu mradi.

Wakata tiketi ni wezi vibaya mno.
Kuna mfumo wa wizi, ubadhirifu na uhujumu uchumi. Ni mfumo, tena ulioasisiwa kabisa toka "god-knows-where"
Usifikiri watawala hawajui, sema wao ni sehemu ya yote yanayotendeka.

Mwafrika na ustaarabu ni mbingu na dunia!!
 
Barabara yao njia nzima hakuna daladala nyingine,hakuna foleni abiria uhakika (uhakika wa pesa ni mkubwa) unafeli vipi huu mradi.

Wakata tiketi ni wezi vibaya mno.
Kusema wakata tiketi ni wezi ni kutojua tatizo liko wapi. Lakini kwanza elewa: sipingi kuwa ni wezi. Infact watanzania wengi ndivyo tulivyo. Kiini cha tatizo: uongozi wa CCM. CCM ime-fail kabisa. Viongozi wake wengi ni wezi na mafisadi ukianzia kwa top wao Samia. Usitegemee wafanyakazi wa chini waache kuiba wakati juu ndiyo kumeoza. Kama mkuu wa majeshi, kama mkuu wa usalama, kama mkuu wa polisi, kama mkuu wa nchi na mawaziri wengi ni wezi, kwa nini wafanyakazi wa chini wenye kipato kidogo kuliko hao viongozi mara milioni moja wasiibe?
 
Yaani ununue mabasi ambayo kampuni nyingine; imeyauza at residual value. Halafu wewe ukafanyie biashara, serikali inayo ruhusu upuuzi huo elewa haipo serious.

Sasa kwanini huyo anaekuuzia yeye, anabadili.

Worst watu wameshajadibu kuwaeleza why it won’t work.

Akili za viongozi wa Tanzania zinawatosha wenyewe.
 
Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa kampuni ya UDART (mwendokasi) ilianza ikiwa na mabasi 140 lakini hadi kufikia hiyo juzi yalibakia mabasi 30!!! Yaani wameshindwa kutengeneza mabasi zaidi ya 110!!

CAG alitakiwa kufanya uchunguzi maalum na TAKUKURU wangekuwa na cha kufanya...yaani wameharibu vyetu ili walete vya kwao
Tatizo la UDART ni wrong business model wanayo operate. Kutokana na mahesabu ya miradi UDART za 2013, gharama ya tiketi ya Mbezi- Kivukoni - Mbezi (round trip) ilipaswa kuwa Tsh 3,000 au Tsh 1,500 kwa saffari ya kwenda tu.

Hiyo ndiyo bei inayoweza kulipa ghharama za uwekezaji, gharama za uendeshaji na riba za Benki.

Mradi ulipoanza ulianza kwa Serikali kuingiza Siasa ndipo UDART wakaambiwa wa charge Tsh 1,300 kwa round trip au Tsh 650/= kwa trip ya kwenda tu.

Gharama kubwa sana ya kuendesha UDART iko kwenye Workshop (Karakana). Karakana siyo revenue centre kama yalivyo mabasi, instead yenyewe ni cost centre. Inakula tu na haizalishi.

Hiyo tofauti ya Tsh 3,000 ya kwenye upembuzi yakinifu na ile Tsh 1,300 ya Serikali ambayo imelazimisha ni Tsh 1,700.
Kwa hiyo kila abiria wa Mwendokasi anakokwenda Kariakoo na kurudi anatengeneza hasara ya Tsh 1,700.

TUSITAFUTE MCHAWI, SERIKALI NDIYO CHANZO CHA KUDORORA KWA UDART
 
Hivi ni kwa nini serikali inapenda kujiingiza kwenye hizi biashara kwenye hii dunia ya ubepari? Hivi walishindwa nini kujenga miundombinu, halafu wakawapangisha wafanyabiashara wenye uwezo wa kuendesha huo mradi na wenyewe wabakie tu kukusanya kodi itokanayo na pango ya majengo/ofisi zao, nk?

Mbona kuna makampuni mengi ya mabasi mfano Shabiby yanafanya hii biashara kitaalam kuliko serikali! Kwa nini msiwape tenda waendeshe miradi ya aina hii kwenye Majiji yote nchini? Serikali ingejikita kwenye ujenzi wa miundombinu tu! Mfano kuwajengea barabara zao maalum, kuwajengea ofisi, nk. Halafu wanakusanya kodi baada ya kuwapangisha.
 
Barabara yao njia nzima hakuna daladala nyingine,hakuna foleni abiria uhakika (uhakika wa pesa ni mkubwa) unafeli vipi huu mradi.

Wakata tiketi ni wezi vibaya mno.
Mimi niko kwenye rekodi, ni mmoja ya watu waliopinga sana huu ujinga wanaoita eti ''mwendo kasi''. Ni njia za kuiba tu. Kwa nini hawakujenga barabara halafu watoe specification za mabasi yanayopaswa ku-operate hizo njia na watu binafsi waweke daladala zao? Tangu lini serikali ya Tanzania ilianzisha mradi ukafanikiwa?
 
Na wakati yanaharibika yanafikia 100, 90, 80, 70, 60 mpaka hayo 30 yeye na wenzake walikuwa hawajagundua tu ? Nadhani ifike wakati tuwalazimishe hawa wafanyakazi wa UMMA watumie Usafiri wa UMMA sababu inaonekana wapo out of touch.....

Yaani maji yalishamwagika kitambo unakuja kutuambia leo ? Huenda tatizo ni hao waliopo juu ya Chain majizi wanajua hili ni shamba la bibi kwahio wanajichukulia (ingawa huenda na wao ndio wanufaika wakuu wa huo mparaganyiko alafu wanajifanya kushangaa)
 
Tatizo la UDART ni wrong business model wanayo operate. Kutokana na mahesabu ya miradi UDART za 2013, gharama ya tiketi ya Mbezi- Kivukoni - Mbezi (round trip) ilipaswa kuwa Tsh 3,000 au Tsh 1,500 kwa saffari ya kwenda tu.

Hiyo ndiyo bei inayoweza kulipa ghharama za uwekezaji, gharama za uendeshaji na riba za Benki.

Mradi ulipoanza ulianza kwa Serikali kuingiza Siasa ndipo UDART wakaambiwa wa charge Tsh 1,300 kwa round trip au Tsh 650/= kwa trip ya kwenda tu.

Gharama kubwa sana ya kuendesha UDART iko kwenye Workshop (Karakana). Karakana siyo revenue centre kama yalivyo mabasi, instead yenyewe ni cost centre. Inakula tu na haizalishi.

Hiyo tofauti ya Tsh 3,000 ya kwenye upembuzi yakinifu na ile Tsh 1,300 ya Serikali ambayo imelazimisha ni Tsh 1,700.
Kwa hiyo kila abiria wa Mwendokasi anakokwenda Kariakoo na kurudi anatengeneza hasara ya Tsh 1,700.

TUSITAFUTE MCHAWI, SERIKALI NDIYO CHANZO CHA KUDORORA KWA UDART
Huwezi kujiandikia ujinga tu kama huu.

Biashara zina hesabu, si ajabu nauli ya serikali zikawa sahihi kuliko zako.

Halafu serikali ina jukumu la kumlinda mlaji katika mambo kama haya; nauli upanga wao au uthibitisha fairness kwa kuzingatia gharama za mwendeshaji.

Huwezi kusema serikali haiko sahihi bila ya justifications.
 
Ni mradi gani uliwahi kuanzishwa/kusimamiwa na gavoo ukafanikiwa 100% ? Tunawaonea bure
 
Tatizo la UDART ni wrong business model wanayo operate. Kutokana na mahesabu ya miradi UDART za 2013, gharama ya tiketi ya Mbezi- Kivukoni - Mbezi (round trip) ilipaswa kuwa Tsh 3,000 au Tsh 1,500 kwa saffari ya kwenda tu.

Hiyo ndiyo bei inayoweza kulipa ghharama za uwekezaji, gharama za uendeshaji na riba za Benki.

Mradi ulipoanza ulianza kwa Serikali kuingiza Siasa ndipo UDART wakaambiwa wa charge Tsh 1,300 kwa round trip au Tsh 650/= kwa trip ya kwenda tu.

Gharama kubwa sana ya kuendesha UDART iko kwenye Workshop (Karakana). Karakana siyo revenue centre kama yalivyo mabasi, instead yenyewe ni cost centre. Inakula tu na haizalishi.

Hiyo tofauti ya Tsh 3,000 ya kwenye upembuzi yakinifu na ile Tsh 1,300 ya Serikali ambayo imelazimisha ni Tsh 1,700.
Kwa hiyo kila abiria wa Mwendokasi anakokwenda Kariakoo na kurudi anatengeneza hasara ya Tsh 1,700.

TUSITAFUTE MCHAWI, SERIKALI NDIYO CHANZO CHA KUDORORA KWA UDART
Public insfrasttructures kama public transport huwa haziingizi faida duniani kote, nenda china fast train zao haziingizi faida, ukienda marekani postal service zao haziingizi faida. Hii ni miradi inayokuwa funded na serikali kwa lengo la kumsaidia mwananchi maisha yake kuwa rahisi na sio kutengeneza faida.
 
Back
Top Bottom