Kuna mfumo wa wizi, ubadhirifu na uhujumu uchumi. Ni mfumo, tena ulioasisiwa kabisa toka "god-knows-where"
Usifikiri watawala hawajui, sema wao ni sehemu ya yote yanayotendeka.
Mwafrika na ustaarabu ni mbingu na dunia!!
Huwa nausema sana humu mfumo huo waitwa Kleptokrasia.
Suluhisho pekee lilobaki ni kuzipa manispaa uwezo wa kupanga na kujenga njia za mabasi, na baadae kupanua njia mbalimbali za usafiri kwa wakazi wa kila manispaa.
Hivyo waziri wa usafirishaji atakuja na mpango wa kuelekeza fedha (resource allocations) kwa miaka tuseme mitatu kwenda kwenye manispaa hizo na kuziweka manispaa hizo chini ya uangalizi maalum hadi mipango hiyo ikamilike.
Hivyo ndani ya miaka mitatu ujenzi wa njia za reli, mabasi na miundombinu ingine inakuwa umekamilika.
itakuwa ni usumbufu na vurugu ndani ya miaka hiyo mitatu lakini usimamizi chini ya timu maalum ya watu maalum manispaa hizo zitahakikisha kunakuwepo miundombinu ilokusudiwa na wakti huohuo kiwanda cha kuunda mabasi kipo chaunda mabasi ya kuanza kazi ya kutoa huduma kwa wakazi wa manispaa hizo.
Tanzania lazima nayo ifuate nchi kama Uganda ambazo sasa zaunda mabasi ya kutoa huduma ya usafiri na pia kuwepo viwanda kadhaa vya kutengeneza vipuri vya mabasi hayo vilivyothibitishwa na wizara ya uchukuzi na usafirishaji.
Sambamba na hilo ili kuzuia tatizo la wizi katika uuzaji wa tiketi, itailazimu serikali ianzishe tiketi za kidijitali kwa wasafiri kununua tiketi za kidijitali kutoka katika tovuti maalum na kuwa wakifanya scanning ya tiketi hiyo kwenye vituo vya mabasi hayo.
Udhibiti wa wizi wa Tiketi na kwenye karakana za mabasi.
Udhibiti huu utawezekana endapo tu wizara itawekeza katika ulinzi na ufuatiliaji kwa kutumia vifaa kama CCTV, ukaguzi wa wafanyakazi wanapotoka kwenda majumbani, ukaguzi katika mageti wakati wa kuingia na kutoka na kuwepo kwa mfumo wa Access Control khasa katika bohari ya vifaa.
Ukiwa na hii Access Control utagundua ni nani aliingia bohari fulani kwa kutumia kadi maalum na wakati gani pamoja na kuwepo kwa CCTV kwenye eneo hilo.
Nasisitiza hili ni zoezi zito lakini lenye faida kubwa kwa miaka mingi ijayo na lahitaji fedha nyingi kuligharamia kwa hapa twazungumzia kibadili kabisa tabia na wizi na watu kutokuwa waaminifu.
Cha msingi iwepo nia thabiti na ari ya kuondoa tatizo la usafiri na miundombinu, kuondoa wizi na kudhibiti hali hizo.