Mabishano kati ya Wakili Kibatala na shahidi, kesi ya Boniface Jacob na Malisa

Mabishano kati ya Wakili Kibatala na shahidi, kesi ya Boniface Jacob na Malisa

Hujui kama unapotoa ushahidi unatoa exhibit zinarekodiwa?
Hii inaondoaje hoja kwamba,shahidi halazimishwi kujibu majibu anayoyapenda wakili na hakimu??
Na unajua majibu hayo yanajibiwa kwa mujibu wa sheria,
sheria inamtaka shahidi ajibu maswali ya kuthibitisha ushahidi,sio anayoyapenda wakili.
wewe tena unasema hakuna sheria😄😄😄 Yaan kwenye maneno kwamba ni dereva hakimu amenote kuwa ni porojo maana shahidi
hii kesi sio ya shahidi polisi,ni ya serikali kama ataandika hivyo kwa swala hilo polisi huyu atafungwa au atafukuzwa kazi??
ameshindwa kutoa exhibit au kesi hujawahi sikiliza ukajua zinaendaje?
bado utashindwa kueleza ameshindwaje kutoa exibit,ambayo haikuombwa na mahakama??hilo ni la kwake au la mahakama??
Enda fuatilia uone kesi zinavojibiwa kisheria na ndiyo maana hakimu alikuwa anamtaka shahidi kujibu kama anavoulizwa jibu ndiyo au hapana
Sio kila swali ni la ndio au hapana,swali kama una elimu gani,alitakiwa ajibu ndio,hapana au sijui???
.......na kwenye kufail kutoa exhibit pale panapotakiwa mahakamani huwezi kusema hukuulizwa yaani tayari ushashindwa na hapo sio kama unamjibu wakili unakuwa unatoa majibu kwa mahakama kwa vifungu vya sheria na
 
Hili taifa linapelekwa shimoni na hawa mbogamboga, Kuna siku watu watasema hapana tumechoka na huu ushetani
 
Hii inaondoaje hoja kwamba,shahidi halazimishwi kujibu majibu anayoyapenda wakili na hakimu??

sheria inamtaka shahidi ajibu maswali ya kuthibitisha ushahidi,sio anayoyapenda wakili.

hii kesi sio ya shahidi polisi,ni ya serikali kama ataandika hivyo kwa swala hilo polisi huyu atafungwa au atafukuzwa kazi??

bado utashindwa kueleza ameshindwaje kutoa exibit,ambayo haikuombwa na mahakama??hilo ni la kwake au la mahakama??

Sio kila swali ni la ndio au hapana,swali kama una elimu gani,alitakiwa ajibu ndio,hapana au sijui???
Basi kaa kimya kumbe hujui kesi zinaendaje, enda uliza kama hakimu atakuomba leta ushahidi😀😀😀 kwa faida yako tu unapotoa ushahidi mahakamani iwe unamshitaki mtu au unamtolea mtu ushahidi yaan pale unapotoa maelezo yako kama una kielelezo juu ya maelezo yako kuthibitisha unatoa hapo hapo, na maswali ya kuthibitisha ushahidi ndiyo hayo aliyomtwanga kibatala majibu yakawa ni hapana weee hadi hakimu akachoka.
Kwahiyo kesi ikiwa ya serikali na upande wa mashitaka haujatoa ushahidi wa kutosha ulitaka asiulizwe masawali au hakimu asiandike kile shahidi amesema? Vyote vinaandikwa na mapungufu yote yanaandikwa.
Kwenye kujibu wakili hakumwambia jibu ndiyo au hapana tu, umeona maswali yametofautiana suala la elimu ilikuwa ni kumjibu simple tu. Kitu nimeona watu wengi suala la ufahamu kuhusu kesi zinaendaje hatujui kituui uurrrurururuuu napiga nduru watu wakuje wakusaidie
 
Kesi ya jinai nambari 11805 Jamhuri dhidi ya Boniface Jacob na Godlisten Malisa ilisikilizwa juzi, Jumanne, Aprili 12, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Ifuatayo ni sehemu ya cross examination kati ya Wakili Msomi Peter Kibatala na Shahidi wa Jamhuri.

KIBATALA: Shahidi, ikumbushe Mahakamaa unaitwa nani?

SHAHIDI: Staff Sergeant Lugano (anataja Force number yake).

KIBATALA: Kazi yako?

SHAHIDI: Askari polisi.

KIBATALA: Kituo chako cha kazi?

SHAHIDI: ofisi ya ZCO kanda maalumu Dar.

KIBATALA: Majukumu yako?

SHAHIDI: Mimi ni Mpelelzi lakini pia nafanya kazi kama dereva.

KIBATALA: Shahidi, hivi kuna tija yoyote kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?

SHAHIDI: Sijatoa ushahidi wa kutunga.

KIBATALA: Sijasema umetunga, nimekuuliza: hivi kuna tija yoyote mtu kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?

SHAHIDI: Nimekula kiapo, na kwenye kiapo hakuna kutunga.

KIBATALA: Sijakuuliza kama kwenye kiapo kuna kutunga au hakuna. Nimekuuliza: kuna tija yoyote mtu kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani? Jibu ndiyo au hapana.

SHAHIDI: Mimi sijatunga ushahidi.

HAKIMU: Shahidi, nakuonya. Jibu maswali kama unavyoulizwa.

KIBATALA: Shahidi, nakuuliza mara ya mwisho. Kuna tija yoyote kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?

SHAHIDI: Hakuna tija.

KIBATALA: Unajua ushahidi utakaoutoa utatumika kupima uwezo wako wa akili, hekima na uadilifu wako?

SHAHIDI: Nina akili timamu.

KIBATALA: Sijasema huna akili timamu. Nimesema: unajua kwamba ushahidi utakaoutoa utatumika kupima akili yako, hekima yako na uadilifu wako?

SHAHIDI: Nimekuja kutoa ushahidi nikiwa na akili timamu.

KIBATALA: Shahidi, acha kujitungia maswali. Jibu kama ninavyokuuliza.

SHAHIDI: Unanipimaje akili wakati nina akili timamu?

KIBATALA: Usiniulize maswali. Mimi ndiye natakiwa nikuulize wewe. Kazi yako ni kujibu.

HAKIMU: Shahidi, upo chini ya kiapo. Tafadhali Jibu kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Mheshimiwa, ananiuliza maswali kwa malengo yake.
KIBATALA: Ndiyo, ni kwa malengo yangu kama wakili. Kwa hiyo tuliza kichwa ujibu.

KIBATALA: Unajua kwamba ushahidi utakaoutoa utatumika kupima uwezo wako wa akili, hekima na uadilifu wako? Ndiyo ama hapana?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Umesema wewe ni dereva wa polisi?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Umeonesha leseni ili kuthibitisha kama kweli wewe ni dereva?

SHAHIDI: Sijaulizwa.

KIBATALA: Jibu swali, leseni umeonesha au hujaonesha?

SHAHIDI: Sijaulizwa.

KIBATALA: Shahidi, usijitungie maswali ambayo hujaulizwa, unaipotezea mahakama muda. Leseni umeonesha au hujaonesha?

SHAHIDI: Sijaulizwa.

KIBATALA: Unajifanya mjanja eeh? Tutakaa hadi saa 9 hapa.

SHAHIDI: Hata tukikaa hadi saa 10 hakuna shida. Ninao muda.

HAKIMU: Shahidi, nakuonya, jibu maswali kama unavyoulizwa.

KIBATALA: Leseni umeonesha au hujaonesha?

SHAHIDI: Sijaonesha.

KIBATALA: Umemwambia Mheshimiwa Hakimu kama ulishuhudia Boniface Jacob akipewa haki zake wakati anahojiwa?

SHAHIDI: Sio kazi yangu. Ni kazi ya mpelelezi.

KIBATALA: Hapa nakuhoji wewe sio mpelelezi.

SHAHIDI: Jukumu la kuhakikisha mtuhumiwa anapewa haki zake ni la mpelelezi.

KIBATALA: Shahidi, elewa swali. Umemwambia Hakimu kama ulishuhudia Boniface akipewa haki zake wakati anahojiwa?

SHAHIDI: Mimi nilikuta tayari ameshahojiwa.

HAKIMU: Shahidi, jibu swali kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, Wakili hanipi nafasi ya kutoa ufafanuzi.

HAKIMU: Wewe jibu kama anavyokuuliza, akitaka ufafanuzi atakuambia.

KIBATALA: Shahidi, ulimwambia Hakimu kama ulishuhudia mshtakiwa Boniface Jacob akipewa haki zake kwa mujibu wa sheria? Umemwambia au hujamwambia?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Sasa mbona ulikuwa unapoteza muda wa mahakama bure?

KIBATALA: Shahidi, una elimu gani?

SHAHIDI: Elimu yangu haikuhusu.

KIBATALA: Inanihusu.

SHAHIDI: Haikuhusu.

KIBATALA: Unataka nikuoneshe kama inanihusu? (Anafungua nyaraka na kusoma vifungu, kabla hajamaliza Hakimu anaingilia kati).

HAKIMU: Shahidi, una wajibu kisheria wa kutaja elimu yako ikiwa Wakili atahitaji kufahamu.

SHAHIDI: Elimu yangu ni Form Four.

KIBATALA: Kumbe ndiyo maana ulikuwa unakataa kutaja? Sikuulizi ulipata division ngapi usije ukashindwa kuendelea na ushahidi.

MAHAKAMA: (Kicheko)

KIBATALA: Sheria inataka mtuhumiwa kabla hajapekuliwa, yeye awapekue kwanza askari. Je, ulimwambia Hakimu kama Boniface alipata nafasi ya kuwapekua askari?

SHAHIDI: Sio kazi yangu. Ni kazi ya mpelelezi.

KIBATALA: Shahidi, hapa umeletwa wewe au mpelelezi?

SHAHIDI: Mpelelezi atakuja utamuuliza.

KIBATALA: Kwa sasa mahakamani mpelelezi yupo?

SHAHIDI: Atakuja.

KIBATALA: Nakuuliza wewe, umemwambia Hakimu kama ulishuhudia Boniface akiwapekua askari kabla? Umemwambia, hujamwambia?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Sasa kwa nini unapoteza muda wa mahakama?

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, samahani, naomba kumuelimisha kidogo Wakili.

KIBATALA: Huwezi kunielimisha chochote. Hapa umekuja kujibu maswali, sio kuelimisha. Kama unataka kunielimisha subiri nikija kituo cha polisi, lakini hapa upo kwenye himaya yangu, na utajibu maswali kama navyokuuliza.

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, naomba kumuelimisha Wakili kuhusu taratibu za utendaji kazi za polisi.

HAKIMU: Jibu maswali kama anavyokuuliza. Akitaka kujua taratibu za kazi atakuuliza.

SHAHIDI: Sawa Mheshimiwa.

KIBATALA: Pole sana Shahidi, unajisikia vibaya?

SHAHIDI: Hapana.

MAHAKAMA: (Kicheko).

KIBATALA: Umesema wakati wa upekuzi nyumbani kwa Boniface kuna jirani aliitwa kushuhudia.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Anaitwa nani?

SHAHIDI: George Steven.

KIBATALA: Unajua kwamba hakuna jirani yeyote wa Boniface mwenye jina hilo?

SHAHIDI: Anaitwa George Steven.

KIBATALA: Unajua kwamba kati ya majirani wanaomzunguka Boniface ni mmoja tu mwenye jina Frank Steven. Na hata huyo si yeye aliyekuja kushuhudia upekuzi.

SHAHIDI: Mi sikumbuki.

KIBATALA: Jina la jirani aliyeshuhudia upekuzi lipo kwenye nyaraka zenu au halipo?

SHAHIDI: Lipo.

KIBATALA: Na nyaraka hizo umezipitia lini mara ya mwisho?

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, Wakili ananiuliza maswali bila kunipa nafasi ya ufafanuzi.

HAKIMU: Amekuambia anataka ufafanuzi?

SHAHIDI: (Kimya).

HAKIMU: We jibu kama anavyokuuliza, akitaka ufafanuzi atakuambia. Pia baadae una nafasi ya kutoa ufafanuzi kadri utakavyoongozwa na Wakili wa Jamhuri.

SHAHIDI: Sawa, Mheshimiwa.

KIBATALA: Unafahamu kuwa Bonny ni kiongozi wa kisiasa mwenye wafuasi wengi na anayefahamika ndani na nje ya nchi?

SHAHIDI: Labda anafahamika na familia yake.

KIBATALA: Familia yake haihusiki hapa. Nimekuuliza wewe.

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Unajua Bonny amewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo?

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Unajua Bonny ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani na alishinda akiwa gerezani?

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Unajifanya mjanja eeh? Sasa hao waliokutuma leo utaenda kuwaambia ulichokutana nacho mahakamani.

KIBATALA: Umemwambia Hakimu mlipoenda kumpekua Bonny mlichukua simu aina gani yenye IMEI number gani?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Umemwambia Hakimu kama Bonny alisaini hati ya upekuzi?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Ukiwa dereva wa gari la polisi lililoenda nyumbani kwa Bonny, ulimwambia Hakimu nani alifungua geti?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Ulipokuja hapa umeoneshwa hati ya upekuzi ili uitambue?

SHAHIDI: Hiyo ataoneshwa mpelelezi.

KIBATALA: Jibu swali, usijitungie maswali yako.

SHAHIDI: Utaratibu wa kazi haupo hivyo.

KIBATALA: Sijakuuliza utaratibu wa kazi zenu. Nimekuuliza umeoneshwa hati ya upekuzi au hujaoneshwa?

SHAHIDI: Sio kazi yangu.

HAKIMU: Shahidi nakuonya upo chini ya kiapo, jibu maswali kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Sijaoneshwa Mheshimiwa.

KIBATALA: Sasa kwa nini unatupotezea muda?

KIBATALA: Umemwambia Hakimu mlipotoka kwa Bonny mlielekea wapi?

SHAHIDI: Tulirudi ofisi ya ZCO.

KIBATALA: Elewa swali. Umemwambia Hakimu au hujamwambia?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Umemwambia Hakimu mliporudi kituoni mliripoti kwa nani?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Ni hayo tu Mheshimiwa.

HAKIMU: Jamhuri kuna re-examination?

JAMHURI: Hapana Mheshimiwa.

HAKIMU: Shahidi, tumemaliza unaweza kuondoka.

HAKIMU: Upande wa Jamhuri mmebakiza mashahidi wangapi?

JAMHURI: 10 Mheshimiwa.

HAKIMU: Kama mashahidi wenyewe ni kama huyu, nashauri mulete watatu watatu.

MAHAKAMA: (Kicheko).

HAKIMU: Namaanisha kama watatoa ushahidi mfupi kama huyu basi waje watatu watatu ili tumalize haraka.

JAMHURI: Sawa Mheshimiwa.

Credit😛age ya malisa fb
HAKIMU: Kesi imeahirishwa itasikilizwa mfululizo tarehe 05, 06 na 07 Mei 2025.
Naomba kuuliza…

Huwa inaruhusiwa kuingia mahakamani kusikikiza tu kesi?
Si ndugu,jamaa au rafiki bse ina public interest
 
Nimeandika nukuu yangu ya kwanza kwako.
Ninguliza elimu ipi unaulizia??
Unaulizaje swali sasa na wakati amekuuliza tu level ya elimu kama ni degree utasema nina degree, km masters degree utaitaja kama ni form four utasema form four full stop.
 
Naomba kuuliza…

Huwa inaruhusiwa kuingia mahakamani kusikikiza tu kesi?
Si ndugu,jamaa au rafiki bse ina public interest
Wanaingia wengi tu kusikiliza cha muhimu usikivu wako na kuna vingi utajifunza
 
Huwa napenda sana vitu kama hivi sijui kwanini .

Nakumbuka kwenye kesi ya mbowe nilikuwa nafurahi sana aise yani polisi walivyokuwa wanqdharirishwa hadi wanabanwa na haja ndogo na kubwa.

Ombi langu wadau mimi shuka chini naomba kesi ya LISSU ikianza apatikane mtu atuletee moja kwa moja maelezo ya kesi kutoka mahakamani itapendeza sana .


Peter kibatala kwa upande wako nakukubali sana polisi nadhani wakikuona huwa wanakasirika sana maana unajua kuwavua nguo hadharani.


"Eti sitakuuliza ulipata division gani mwisho ushindwe kutoa ushahidi."🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Basi kaa kimya kumbe hujui kesi zinaendaje,
mbona mipasho??nikae kimya tena!!!au ndio ushaathirika na mentality ya wakili msomi😂
enda uliza kama hakimu atakuomba leta ushahidi😀😀😀 kwa faida yako tu unapotoa ushahidi mahakamani iwe unamshitaki mtu au unamtolea mtu ushahidi yaan pale unapotoa maelezo yako kama una kielelezo juu ya maelezo yako kuthibitisha unatoa hapo hapo,
unaelewa kwanini shahidi alijibu sikuombwa??au unatiririka tu kwa sababu umeshiba🤣🤣.
maana yake kama anataka reseni anayo hapo anaweza itoa.
na maswali ya kuthibitisha ushahidi ndiyo hayo aliyomtwanga kibatala majibu yakawa ni hapana weee hadi hakimu akachoka.
hapo lazima hakimu achoke sababu alimtaka shahidi ajibu kama alivyoulizwa,mpaka akiulizwa umri wake kazini ajibu sijui,ndio au hapana😂😂😂.
Kwahiyo kesi ikiwa ya serikali na upande wa mashitaka haujatoa ushahidi wa kutosha ulitaka asiulizwe masawali au hakimu asiandike kile shahidi amesema?
sasa kwani alishindwa nini kuandika alichosema shahidi au aliona ni kirefu atamuacha??
Vyote vinaandikwa na mapungufu yote yanaandikwa.
ndio alitakiwa aaandike anachojibu shahidi.
Kwenye kujibu wakili hakumwambia jibu ndiyo au hapana tu,
si ni jibu kama alivyoukizwa??embu waambie kumbi kumbi wengine hapa,shahidi anajibu swali hata kamaanahitaji lifafanuliwe kwanza??
umeona maswali yametofautiana suala la elimu ilikuwa ni kumjibu simple tu
hakuna jibu simple mahakamani,wewe ni mgeni wa kesi,jibu kichwa kichwa uone dkk 3 mbele nini kinafata.
. Kitu nimeona watu wengi suala la ufahamu kuhusu kesi zinaendaje hatujui kituui uurrrurururuuu napiga nduru watu wakuje wakusaidie
Ndio tunamsoma kibatala na shahidi hapa,tujue mengi.
 
Nlichokiona kiujumla watu wengi wanajifanya wajuaji na wanahisi wanaweza kuenenda kwa fikra zao kwenye kesi ila kumbe hawajui kuna sheria zinasimamia yote hayo.
mkorinto , Kisai Rudini mjifunze hata kwa kuwauliza uliza wanasheria watawapa abc juu ya kesi zinavyoendeshwa mahakamani.
Mahakani haujibu kwa mihememko tu kwakuwa unajua kiswahili.
Na kingine mjue tu unapotoa ushahidi maelezo yoyote yanayohitaji exhibit toa hapohapo hakimu anazirecord hakunaga excuse za kusema sijaombwa exhibit mahakamani haijalishi unajua au hujui failing to do so hakimu anaandika hakuna kielelezo chochote kilichotolewa kuthibitisha maelezo ya shahidi inakuwa imetoka hiyo😀
 
Unaulizaje swali sasa na wakati amekuuliza tu level ya elimu kama ni degree utasema nina degree, km masters degree utaitaja kama ni form four utasema form four full stop.
hapa unataka jibu uliloliandaa ama ulilolitarajia.

Elimu ziko nyingi,na mahakamani tobo dogo tu linaweza geuza mwelekeo mzima wa mwenendo wa mashtaka,mbeleni akija kudai ana elimu ya juu ya uchawi utakataa jibu???
 
Nlichokiona kiujumla watu wengi wanajifanya wajuaji na wanahisi wanaweza kuenenda kwa fikra zao kwenye kesi ila kumbe hawajui kuna sheria zinasimamia yote hayo.
mkorinto , Kisai Rudini mjifunze hata kwa kuwauliza uliza wanasheria watawapa abc juu ya kesi zinavyoendeshwa mahakamani.
Mahakani haujibu kwa mihememko tu kwakuwa unajua kiswahili.
Na kingine mjue tu unapotoa ushahidi maelezo yoyote yanayohitaji exhibit toa hapohapo hakimu anazirecord hakunaga excuse za kusema sijaombwa exhibit mahakamani haijalishi unajua au hujui failing to do so hakimu anaandika hakuna kielelezo chochote kilichotolewa kuthibitisha maelezo ya shahidi inakuwa imetoka hiyo😀
Wakili sio Mungu,nayeye ni mtu,anaweza kosolewa vile vile.
Labda hujapenda tumkosoe kwamba anauliza mswali ya kipuuzi.
 
mbona mipasho??nikae kimya tena!!!au ndio ushaathirika na mentality ya wakili msomi😂

unaelewa kwanini shahidi alijibu sikuombwa??au unatiririka tu kwa sababu umeshiba🤣🤣.
maana yake kama anataka reseni anayo hapo anaweza itoa.


hapo lazima hakimu achoke sababu alimtaka shahidi ajibu kama alivyoulizwa,mpaka akiulizwa umri wake kazini ajibu sijui,ndio au hapana😂😂😂.

sasa kwani alishindwa nini kuandika alichosema shahidi au aliona ni kirefu atamuacha??

ndio alitakiwa aaandike anachojibu shahidi.

si ni jibu kama alivyoukizwa??embu waambie kumbi kumbi wengine hapa,shahidi anajibu swali hata kamaanahitaji lifafanuliwe kwanza??

hakuna jibu simple mahakamani,wewe ni mgeni wa kesi,jibu kichwa kichwa uone dkk 3 mbele nini kinafata.

Ndio tunamsoma kibatala na shahidi hapa,tujue mengi.
Yaani hujui kitu, kwenye Cross examination husemi sikuombwa 😀😀😀 sio kazi ya hakimu kukwambia toa exhibit unapotoa maelezo toa, hakunaga kesi imeendeshwa kwenye Cross examination ukasema sikuombwa ila hii hapa😀😀😀 yaani wewe unahisi njia zako mwenyewe za kuendesha kesi. Sio kwa kibatala tu jifunze kuingia mahakama zozote hata za mwanzo palipo na kesi zinazosimamiwa na mawakili ndiyo utaelewa hapa unahisi ni majibu ya mwalimu na mwanafunzi.
Kwenye simplicity ya swali la elimu nlimaanisha angemwambia level ya elimu tu ikaishia hapo.
Hujui kitu bwana enda sikiliza kesi mbili tatu mahakama yoyote achana na ya kibatala maana unahisi kibatala anajiendesha kwa vile ni wakili maarufu.
Napoteza muda na akati hujawahi kusimama hata mahakama ya mwanzo unahisi kesi zinaendeshwa kwa ujuaji wa kujua kiswahili
 
@mkorinto ENDA MAHAKAMA YOYOTE HATA ZIWE TOFAUTI TOFAUTI FUATILIA KESI MBILI AU ZAIDI YA HAPO AFU URUDI HAPA.
MAANA UNAHISI MAHAKAMANI UNAJIBU KWA MIHEMKO NA SI SHERIA INAKUELEKEZA, KUBALI TU NI VINGI HUJUI DEAR TUJIFUNZE KWA PAMOJA.
WEWE UNAONEKANA HAKUNA KESI UMEWAHI SIKILIZA HATA MOJA.
 
Yaani hujui kitu, kwenye Cross examination husemi sikuombwa 😀😀😀
Embu nipe majibu ya moja kwa moja ya cross examination wewe mjuaji.
sio kazi ya hakimu kukwambia toa exhibit unapotoa maelezo toa,
Wapi nimeandika haya???nimesema hakimu alipaswa kuandika shahidi alichojibu.
hakunaga kesi imeendeshwa kwenye Cross examination ukasema sikuombwa ila hii hapa😀😀😀 yaani wewe unahisi njia zako mwenyewe za kuendesha kesi.
Ndio maana nikaomba majibu yanayotakiwa hatua hii inaonekana majibu ni matatu tu na wengine ambao hatuhidhurii mahakamani hatuyajui.
Sio kwa kibatala tu jifunze kuingia mahakama zozote hata za mwanzo palipo na kesi zinazosimamiwa na mawakili ndiyo utaelewa hapa unahisi ni majibu ya mwalimu na mwanafunzi.
wewe ndio unaona haya ni maswali ya mwalimu na mwanamfunzi wake,ndio maana unaotea majibu.
Nakukumbusha kwamba hayo ni maswali ya wakili upande wa utetezi na shahidi upande wa mashtaka,hakuna kucheka na kima hapo.
Kwenye simplicity ya swali la elimu nlimaanisha angemwambia level ya elimu tu ikaishia hapo.
Unakariri,hiyo sio mahakama itakuwa ni majibu ya table 1-12.
Hujui kitu bwana enda sikiliza kesi mbili tatu mahakama yoyote achana na ya kibatala maana unahisi kibatala anajiendesha kwa vile ni wakili maarufu.
Neno hujui kitu unalirudia kila nukuu yako😂😂,sijui wapi nimesema najua,mbona inaonekana una matatizo mengi sana??
Napoteza muda na akati hujawahi kusimama hata mahakama ya mwanzo unahisi kesi zinaendeshwa kwa ujuaji wa kujua kiswahili
Wewe huyu umeshasimamia mahakama ya mwanzo😂😂😂😂.
Eh,kazi ipo.
 
Huyo shahidi kapaniki tu, lakini ni maswali easy na yanajibika
Huyo shahidi, inaonyesha alishasikia sifa za Kibatala, hivyo alijiandaa kupambana naye! Bila kujua huko Mahakamani, kuna utaratibu unaofuatwa, na sio mambo ya kihuni kihuni, au ujuaji wa mitaani, unajijibia tu unavyotaka, au haulazimishwi kujibu swali ambalo hautaki kulijibu!
 
Alooo kam askari polis aliend coz yuko hv sasa c raia tutawez jibu maswali ki wakil
 
Back
Top Bottom