Mabishano kati ya Wakili Kibatala na shahidi, kesi ya Boniface Jacob na Malisa

Mkuu mahakamani zinatumika sheria zilizotungwa na wanadamu na sio Mungu.
Sawa kabisa.ndio maana hatutizamii kama zinawezatumika kwa watu smart muda wote.
Wakili yupo sahihi.
Tena kibatala ni very smart person .
Kabisa.
Nia ya kibatala pamoja na kushinda kesi ni pamoja na kuwadhalilisha polisi kwani anajua wanatumika hovyo.
huu ni mtizamo wako ww,vipi hakimu anaposimama upande wa wakili anawadhalilisha polisi au anasimamia taaluma??
kibatala anachofanya ni kufanya kazi aliyopewa alipwe mambo ya kuwadhalilisha polisi ni hisia zako tu.
Unafikiria kwa nini dpp aliiondoa kesi ya mbowe mahakamani walijua kwamba wangekutana na maswali ya kudhalilisha sana kutoka kwa kibatala ambao yangeweza kuiacha uchi serikali hususani polisi.
polisi(kingai),hakimu,kibatala,wote walikuqa kazini kuhakikisha linafanyika lililofanyika.
nikuhakikishia,hakuna kesi ya kupandikizwa(mchongo)itapata muda mikononi kwa makundi yote hayo kama haina maagizo kutoka mamlaka za juu.
DPP aliiondoka pia kwa sababu muda wa kuiondoa ulifika.
hakuna kitu kinaitwa aibu kwenye mipango ya watu.
Ushauri ni kwamba Jeshi ka Polisi liache kutumika hovyo na wanasiasa manake wao ndio wanakwenda kutoa ushahidi mahakamani ambapo wanakuwa wanatunga uongo wanaoshindwa kuutete na hivyo kukuta wanadhalilishwa na kuaibika na maswali ya kibatala.
polisi wanakwenda pale wakiwa tayari wanajua wanachomwenda kukifanya,kwamba mwisho wa siku msio na kazi mtamcheka mkidhani anakwenda kujinyonga kwa aibu,wakati akitoka hapo either anapanda cheo au anaendelea na maisha yake ya kawaida.
Kibatala ni mwanasheria mzuri anajua hao mashahidi wote ni vilaza wanatumika na yeye anajua kuwaenyesha .
nadhani hizi ndio kesi zako za kwanza kuhudhuria mahakamani,kizimbani huwa kuna vita,wachana na huo utoto unaofanyika hapo kwenye makesi ya kuchonga hayo.
Nakumbuka kuna shahidi askari kwenye kesi aliomba poo alimwambia hakimu turbo linamuuma kumbe alitaka kukimbia maswali.
Hongera sana kwake kibatala anaitendea haki profession yake ya sheria
Watazamaji wakacheka sana kwamba polisi kakomeshwa,mwezi mmoja baadae akapandishwa cheo🤣🤣.
Msiwe serious sana na hayo madude watu wako kazini.
 
Nimependa battle ya wachangiaji ,huwa napenda sana watu wakipeana challenge

Nilimiss sana hizi mambo
 
Hakunaga kesi kama hiyo jombaa na ndiyo maana hakimu alikuwa anasimamia ya wakili ili mtuhumiwa ajibu kile alichoulizwa tu kama ni ndiyo ni ndiyo...no more explanations
Kama hapana ni hapana....
Anaingia next question
Sijui pia ni jibu mkuu kisheria
 
Kesi ya jinai nambari 11805 Jamhuri dhidi ya Boniface Jacob na Godlisten Malisa ilisikilizwa juzi, Jumanne, Aprili 12, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Ifuatayo ni sehemu ya cross examination kati ya Wakili Msomi Peter Kibatala na Shahidi wa Jamhuri.

KIBATALA: Shahidi, ikumbushe Mahakamaa unaitwa nani?

SHAHIDI: Staff Sergeant Lugano (anataja Force number yake).

KIBATALA: Kazi yako?

SHAHIDI: Askari polisi.

KIBATALA: Kituo chako cha kazi?

SHAHIDI: ofisi ya ZCO kanda maalumu Dar.

KIBATALA: Majukumu yako?

SHAHIDI: Mimi ni Mpelelzi lakini pia nafanya kazi kama dereva.

KIBATALA: Shahidi, hivi kuna tija yoyote kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?

SHAHIDI: Sijatoa ushahidi wa kutunga.

KIBATALA: Sijasema umetunga, nimekuuliza: hivi kuna tija yoyote mtu kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?

SHAHIDI: Nimekula kiapo, na kwenye kiapo hakuna kutunga.

KIBATALA: Sijakuuliza kama kwenye kiapo kuna kutunga au hakuna. Nimekuuliza: kuna tija yoyote mtu kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani? Jibu ndiyo au hapana.

SHAHIDI: Mimi sijatunga ushahidi.

HAKIMU: Shahidi, nakuonya. Jibu maswali kama unavyoulizwa.

KIBATALA: Shahidi, nakuuliza mara ya mwisho. Kuna tija yoyote kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?

SHAHIDI: Hakuna tija.

KIBATALA: Unajua ushahidi utakaoutoa utatumika kupima uwezo wako wa akili, hekima na uadilifu wako?

SHAHIDI: Nina akili timamu.

KIBATALA: Sijasema huna akili timamu. Nimesema: unajua kwamba ushahidi utakaoutoa utatumika kupima akili yako, hekima yako na uadilifu wako?

SHAHIDI: Nimekuja kutoa ushahidi nikiwa na akili timamu.

KIBATALA: Shahidi, acha kujitungia maswali. Jibu kama ninavyokuuliza.

SHAHIDI: Unanipimaje akili wakati nina akili timamu?

KIBATALA: Usiniulize maswali. Mimi ndiye natakiwa nikuulize wewe. Kazi yako ni kujibu.

HAKIMU: Shahidi, upo chini ya kiapo. Tafadhali Jibu kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Mheshimiwa, ananiuliza maswali kwa malengo yake.
KIBATALA: Ndiyo, ni kwa malengo yangu kama wakili. Kwa hiyo tuliza kichwa ujibu.

KIBATALA: Unajua kwamba ushahidi utakaoutoa utatumika kupima uwezo wako wa akili, hekima na uadilifu wako? Ndiyo ama hapana?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Umesema wewe ni dereva wa polisi?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Umeonesha leseni ili kuthibitisha kama kweli wewe ni dereva?

SHAHIDI: Sijaulizwa.

KIBATALA: Jibu swali, leseni umeonesha au hujaonesha?

SHAHIDI: Sijaulizwa.

KIBATALA: Shahidi, usijitungie maswali ambayo hujaulizwa, unaipotezea mahakama muda. Leseni umeonesha au hujaonesha?

SHAHIDI: Sijaulizwa.

KIBATALA: Unajifanya mjanja eeh? Tutakaa hadi saa 9 hapa.

SHAHIDI: Hata tukikaa hadi saa 10 hakuna shida. Ninao muda.

HAKIMU: Shahidi, nakuonya, jibu maswali kama unavyoulizwa.

KIBATALA: Leseni umeonesha au hujaonesha?

SHAHIDI: Sijaonesha.

KIBATALA: Umemwambia Mheshimiwa Hakimu kama ulishuhudia Boniface Jacob akipewa haki zake wakati anahojiwa?

SHAHIDI: Sio kazi yangu. Ni kazi ya mpelelezi.

KIBATALA: Hapa nakuhoji wewe sio mpelelezi.

SHAHIDI: Jukumu la kuhakikisha mtuhumiwa anapewa haki zake ni la mpelelezi.

KIBATALA: Shahidi, elewa swali. Umemwambia Hakimu kama ulishuhudia Boniface akipewa haki zake wakati anahojiwa?

SHAHIDI: Mimi nilikuta tayari ameshahojiwa.

HAKIMU: Shahidi, jibu swali kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, Wakili hanipi nafasi ya kutoa ufafanuzi.

HAKIMU: Wewe jibu kama anavyokuuliza, akitaka ufafanuzi atakuambia.

KIBATALA: Shahidi, ulimwambia Hakimu kama ulishuhudia mshtakiwa Boniface Jacob akipewa haki zake kwa mujibu wa sheria? Umemwambia au hujamwambia?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Sasa mbona ulikuwa unapoteza muda wa mahakama bure?

KIBATALA: Shahidi, una elimu gani?

SHAHIDI: Elimu yangu haikuhusu.

KIBATALA: Inanihusu.

SHAHIDI: Haikuhusu.

KIBATALA: Unataka nikuoneshe kama inanihusu? (Anafungua nyaraka na kusoma vifungu, kabla hajamaliza Hakimu anaingilia kati).

HAKIMU: Shahidi, una wajibu kisheria wa kutaja elimu yako ikiwa Wakili atahitaji kufahamu.

SHAHIDI: Elimu yangu ni Form Four.

KIBATALA: Kumbe ndiyo maana ulikuwa unakataa kutaja? Sikuulizi ulipata division ngapi usije ukashindwa kuendelea na ushahidi.

MAHAKAMA: (Kicheko)

KIBATALA: Sheria inataka mtuhumiwa kabla hajapekuliwa, yeye awapekue kwanza askari. Je, ulimwambia Hakimu kama Boniface alipata nafasi ya kuwapekua askari?

KIBATALA: Shahidi, hapa umeletwa wewe au mpelelezi?

SHAHIDI: Mpelelezi atakuja utamuuliza.

KIBATALA: Kwa sasa mahakamani mpelelezi yupo?

SHAHIDI: Atakuja.

KIBATALA: Nakuuliza wewe, umemwambia Hakimu kama ulishuhudia Boniface akiwapekua askari kabla? Umemwambia, hujamwambia?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Sasa kwa nini unapoteza muda wa mahakama?

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, samahani, naomba kumuelimisha kidogo Wakili.

KIBATALA: Huwezi kunielimisha chochote. Hapa umekuja kujibu maswali, sio kuelimisha. Kama unataka kunielimisha subiri nikija kituo cha polisi, lakini hapa upo kwenye himaya yangu, na utajibu maswali kama navyokuuliza.

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, naomba kumuelimisha Wakili kuhusu taratibu za utendaji kazi za polisi.

HAKIMU: Jibu maswali kama anavyokuuliza. Akitaka kujua taratibu za kazi atakuuliza.

SHAHIDI: Sawa Mheshimiwa.

KIBATALA: Pole sana Shahidi, unajisikia vibaya?

SHAHIDI: Hapana.

MAHAKAMA: (Kicheko).

KIBATALA: Umesema wakati wa upekuzi nyumbani kwa Boniface kuna jirani aliitwa kushuhudia.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Anaitwa nani?

SHAHIDI: George Steven.

KIBATALA: Unajua kwamba hakuna jirani yeyote wa Boniface mwenye jina hilo?

SHAHIDI: Anaitwa George Steven.

KIBATALA: Unajua kwamba kati ya majirani wanaomzunguka Boniface ni mmoja tu mwenye jina Frank Steven. Na hata huyo si yeye aliyekuja kushuhudia upekuzi.

SHAHIDI: Mi sikumbuki.

KIBATALA: Jina la jirani aliyeshuhudia upekuzi lipo kwenye nyaraka zenu au halipo?

SHAHIDI: Lipo.

KIBATALA: Na nyaraka hizo umezipitia lini mara ya mwisho?

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, Wakili ananiuliza maswali bila kunipa nafasi ya ufafanuzi.

HAKIMU: Amekuambia anataka ufafanuzi?

SHAHIDI: (Kimya).

HAKIMU: We jibu kama anavyokuuliza, akitaka ufafanuzi atakuambia. Pia baadae una nafasi ya kutoa ufafanuzi kadri utakavyoongozwa na Wakili wa Jamhuri.

SHAHIDI: Sawa, Mheshimiwa.

KIBATALA: Unafahamu kuwa Bonny ni kiongozi wa kisiasa mwenye wafuasi wengi na anayefahamika ndani na nje ya nchi?

SHAHIDI: Labda anafahamika na familia yake.

KIBATALA: Familia yake haihusiki hapa. Nimekuuliza wewe.

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Unajua Bonny amewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo?

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Unajua Bonny ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani na alishinda akiwa gerezani?

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Unajifanya mjanja eeh? Sasa hao waliokutuma leo utaenda kuwaambia ulichokutana nacho mahakamani.

KIBATALA: Umemwambia Hakimu mlipoenda kumpekua Bonny mlichukua simu aina gani yenye IMEI number gani?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Umemwambia Hakimu kama Bonny alisaini hati ya upekuzi?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Ukiwa dereva wa gari la polisi lililoenda nyumbani kwa Bonny, ulimwambia Hakimu nani alifungua geti?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Ulipokuja hapa umeoneshwa hati ya upekuzi ili uitambue?

SHAHIDI: Hiyo ataoneshwa mpelelezi.

KIBATALA: Jibu swali, usijitungie maswali yako.

SHAHIDI: Utaratibu wa kazi haupo hivyo.

KIBATALA: Sijakuuliza utaratibu wa kazi zenu. Nimekuuliza umeoneshwa hati ya upekuzi au hujaoneshwa?

SHAHIDI: Sio kazi yangu.

HAKIMU: Shahidi nakuonya upo chini ya kiapo, jibu maswali kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Sijaoneshwa Mheshimiwa.

KIBATALA: Sasa kwa nini unatupotezea muda?

KIBATALA: Umemwambia Hakimu mlipotoka kwa Bonny mlielekea wapi?

SHAHIDI: Tulirudi ofisi ya ZCO.

KIBATALA: Elewa swali. Umemwambia Hakimu au hujamwambia?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Umemwambia Hakimu mliporudi kituoni mliripoti kwa nani?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Ni hayo tu Mheshimiwa.

HAKIMU: Jamhuri kuna re-examination?

JAMHURI: Hapana Mheshimiwa.

HAKIMU: Shahidi, tumemaliza unaweza kuondoka.

HAKIMU: Upande wa Jamhuri mmebakiza mashahidi wangapi?

JAMHURI: 10 Mheshimiwa.

HAKIMU: Kama mashahidi wenyewe ni kama huyu, nashauri mulete watatu watatu.

MAHAKAMA: (Kicheko).

HAKIMU: Namaanisha kama watatoa ushahidi mfupi kama huyu basi waje watatu watatu ili tumalize haraka.

JAMHURI: Sawa Mheshimiwa.

Credit😛age ya malisa fb
HAKIMU: Kesi imeahirishwa itasikilizwa mfululizo tarehe 05, 06 na 07 Mei 2025.
Kwa wanasheria hakuna cha maana kwenye mahojiano hayo kwrnye kuharibu jesi zaidi ya hoja za vichekesho
 
Tuliza akili unapojadiliana na Mimi. Hakuna sehemu nilipo nakishi kuhusu hapana, nimenakishi kuhusu sijui na usahihi wa maswali yanayo ulizwa bali na uendeshwaji.

Umesahau ya kuwa huko mmetuambia ya kuwa tayari Shahidi ameshatoa ushahidi, hapo anachofanya Wakili ni kuhakiki tu. Aisee, nyinyi ni vilaza sana. Hata kumbukumbu huna na umakini kadhalika.

Huu nao ni utoto mwingine, wingi kwetu sisi si hoja, hoja ni usahihi. Ndio maana Kuna baadhi ya wakati mtu mmoja huitwa "Umma/Uma" na wingi huwa ni WA jinsi ya Kike. Hapo ndio umethibitisha bila kificho kati yangu na wewe nani box.
Bure kabisa
 
nafasi ya ni ya wakiri kuuliza swali,hakuna sheria inamtaka mtuhumiwa au shahidi ajibu anavyopenda wakili.pale sio mjadala wa kibiashara ni mahakamani,ni either mtu apate haki au aipoteze.

Wakiri:ulionyesha leseni mahakamani??
Shahidi:sikuulizwa/sikutakwa kuionyesha.

wakili,hakimu sukari zinapanda"shahidi jibu kama ulivyoulizwa"

Ningerudia jibu hili hili mpaka aombe mwongozo,na kuifafanulia mahakama kwanini anadhani sikumjibu kama alivyouliza!!!
Hujui kama unapotoa ushahidi unatoa exhibit zinarekodiwa? Na unajua majibu hayo yanajibiwa kwa mujibu wa sheria, wewe tena unasema hakuna sheria😄😄😄 Yaan kwenye maneno kwamba ni dereva hakimu amenote kuwa ni porojo maana shahidi ameshindwa kutoa exhibit au kesi hujawahi sikiliza ukajua zinaendaje? Enda fuatilia uone kesi zinavojibiwa kisheria na ndiyo maana hakimu alikuwa anamtaka shahidi kujibu kama anavoulizwa jibu ndiyo au hapana.......na kwenye kufail kutoa exhibit pale panapotakiwa mahakamani huwezi kusema hukuulizwa yaani tayari ushashindwa na hapo sio kama unamjibu wakili unakuwa unatoa majibu kwa mahakama kwa vifungu vya sheria na sio kama unafikiri wewe.
 
Mkuu mahakamani zinatumika sheria zilizotungwa na wanadamu na sio Mungu.
Wakili yupo sahihi.
Tena kibatala ni very smart person .
Nia ya kibatala pamoja na kushinda kesi ni pamoja na kuwadhalilisha polisi kwani anajua wanatumika hovyo.
Unafikiria kwa nini dpp aliiondoa kesi ya mbowe mahakamani walijua kwamba wangekutana na maswali ya kudhalilisha sana kutoka kwa kibatala ambao yangeweza kuiacha uchi serikali hususani polisi.
Ushauri ni kwamba Jeshi ka Polisi liache kutumika hovyo na wanasiasa manake wao ndio wanakwenda kutoa ushahidi mahakamani ambapo wanakuwa wanatunga uongo wanaoshindwa kuutete na hivyo kukuta wanadhalilishwa na kuaibika na maswali ya kibatala.
Kibatala ni mwanasheria mzuri anajua hao mashahidi wote ni vilaza wanatumika na yeye anajua kuwaenyesha .
Nakumbuka kuna shahidi askari kwenye kesi aliomba poo alimwambia hakimu turbo linamuuma kumbe alitaka kukimbia maswali.
Hongera sana kwake kibatala anaitendea haki profession yake ya sheria
Tayari walikutana nayo na wakawa wanajibu kama watoto yaani ikawa kama hawajui kwanini wamemkamata
 
Tuliza akili unapojadiliana na Mimi. Hakuna sehemu nilipo nakishi kuhusu hapana, nimenakishi kuhusu sijui na usahihi wa maswali yanayo ulizwa bali na uendeshwaji.

Umesahau ya kuwa huko mmetuambia ya kuwa tayari Shahidi ameshatoa ushahidi, hapo anachofanya Wakili ni kuhakiki tu. Aisee, nyinyi ni vilaza sana. Hata kumbukumbu huna na umakini kadhalika.

Huu nao ni utoto mwingine, wingi kwetu sisi si hoja, hoja ni usahihi. Ndio maana Kuna baadhi ya wakati mtu mmoja huitwa "Umma/Uma" na wingi huwa ni WA jinsi ya Kike. Hapo ndio umethibitisha bila kificho kati yangu na wewe nani box.
Kumbe kwenye kuhakiki kwenye kesi zenu mawakili mnafanyaje? Tufundishe na sisi tujue
 
Naendesha kwa uadilifu na maarifa, zenu zimekosa uadilifu lakini wakili akiuliza anataka mtu awe Muadilifu wakati yeye sio Muadilifu.
Kesi zako unaedesha chumbani na mkeo au chooni na dodoki?
 
Unatakiwa ujibu swali jinsi ulivyoulizwa .
Kama hujui unasema sijui ,
Huwezi kurekebisha swali uliloulizwa.
Swali linapokosewa kuulizwa unatakiwa ujibu jambo ambalo swali lake sio sahihi ? Unaelewa maana ya swali kukosewa ?

Swali, linapokosewa kuulizwa, unatakiwa ulikosoe ili utoe majibu sahihi.

Inakuwaje mathalani, unapoulizwa swali ambalo jibu sahihi ni "Sijui", na muulizaji anataka ujibu "Ndiyo" au "Hapana" ? Hii ni kwa upande wa uhuru wa majibuji swali.

Lakini Kuna makosa ya Kilugha, haya mayo ujibu kama ulivyo ulizwa ?
 
Yupo sahihi kwa kuuliza maswali yakipuuzi na yasiyo kuwa na maana ?
Angekuwa nje ya mada hakimu angempa muongozo na ndiyo maana hakimu alikuwa anahitaji shahidi kujibu kilichoulizwa wanaongozwa na vifungu sio hisia
 
Kesi ya jinai nambari 11805 Jamhuri dhidi ya Boniface Jacob na Godlisten Malisa ilisikilizwa juzi, Jumanne, Aprili 12, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Ifuatayo ni sehemu ya cross examination kati ya Wakili Msomi Peter Kibatala na Shahidi wa Jamhuri.

KIBATALA: Shahidi, ikumbushe Mahakamaa unaitwa nani?

SHAHIDI: Staff Sergeant Lugano (anataja Force number yake).

KIBATALA: Kazi yako?

SHAHIDI: Askari polisi.

KIBATALA: Kituo chako cha kazi?

SHAHIDI: ofisi ya ZCO kanda maalumu Dar.

KIBATALA: Majukumu yako?

SHAHIDI: Mimi ni Mpelelzi lakini pia nafanya kazi kama dereva.

KIBATALA: Shahidi, hivi kuna tija yoyote kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?

SHAHIDI: Sijatoa ushahidi wa kutunga.

KIBATALA: Sijasema umetunga, nimekuuliza: hivi kuna tija yoyote mtu kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?

SHAHIDI: Nimekula kiapo, na kwenye kiapo hakuna kutunga.

KIBATALA: Sijakuuliza kama kwenye kiapo kuna kutunga au hakuna. Nimekuuliza: kuna tija yoyote mtu kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani? Jibu ndiyo au hapana.

SHAHIDI: Mimi sijatunga ushahidi.

HAKIMU: Shahidi, nakuonya. Jibu maswali kama unavyoulizwa.

KIBATALA: Shahidi, nakuuliza mara ya mwisho. Kuna tija yoyote kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?

SHAHIDI: Hakuna tija.

KIBATALA: Unajua ushahidi utakaoutoa utatumika kupima uwezo wako wa akili, hekima na uadilifu wako?

SHAHIDI: Nina akili timamu.

KIBATALA: Sijasema huna akili timamu. Nimesema: unajua kwamba ushahidi utakaoutoa utatumika kupima akili yako, hekima yako na uadilifu wako?

SHAHIDI: Nimekuja kutoa ushahidi nikiwa na akili timamu.

KIBATALA: Shahidi, acha kujitungia maswali. Jibu kama ninavyokuuliza.

SHAHIDI: Unanipimaje akili wakati nina akili timamu?

KIBATALA: Usiniulize maswali. Mimi ndiye natakiwa nikuulize wewe. Kazi yako ni kujibu.

HAKIMU: Shahidi, upo chini ya kiapo. Tafadhali Jibu kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Mheshimiwa, ananiuliza maswali kwa malengo yake.
KIBATALA: Ndiyo, ni kwa malengo yangu kama wakili. Kwa hiyo tuliza kichwa ujibu.

KIBATALA: Unajua kwamba ushahidi utakaoutoa utatumika kupima uwezo wako wa akili, hekima na uadilifu wako? Ndiyo ama hapana?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Umesema wewe ni dereva wa polisi?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Umeonesha leseni ili kuthibitisha kama kweli wewe ni dereva?

SHAHIDI: Sijaulizwa.

KIBATALA: Jibu swali, leseni umeonesha au hujaonesha?

SHAHIDI: Sijaulizwa.

KIBATALA: Shahidi, usijitungie maswali ambayo hujaulizwa, unaipotezea mahakama muda. Leseni umeonesha au hujaonesha?

SHAHIDI: Sijaulizwa.

KIBATALA: Unajifanya mjanja eeh? Tutakaa hadi saa 9 hapa.

SHAHIDI: Hata tukikaa hadi saa 10 hakuna shida. Ninao muda.

HAKIMU: Shahidi, nakuonya, jibu maswali kama unavyoulizwa.

KIBATALA: Leseni umeonesha au hujaonesha?

SHAHIDI: Sijaonesha.

KIBATALA: Umemwambia Mheshimiwa Hakimu kama ulishuhudia Boniface Jacob akipewa haki zake wakati anahojiwa?

SHAHIDI: Sio kazi yangu. Ni kazi ya mpelelezi.

KIBATALA: Hapa nakuhoji wewe sio mpelelezi.

SHAHIDI: Jukumu la kuhakikisha mtuhumiwa anapewa haki zake ni la mpelelezi.

KIBATALA: Shahidi, elewa swali. Umemwambia Hakimu kama ulishuhudia Boniface akipewa haki zake wakati anahojiwa?

SHAHIDI: Mimi nilikuta tayari ameshahojiwa.

HAKIMU: Shahidi, jibu swali kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, Wakili hanipi nafasi ya kutoa ufafanuzi.

HAKIMU: Wewe jibu kama anavyokuuliza, akitaka ufafanuzi atakuambia.

KIBATALA: Shahidi, ulimwambia Hakimu kama ulishuhudia mshtakiwa Boniface Jacob akipewa haki zake kwa mujibu wa sheria? Umemwambia au hujamwambia?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Sasa mbona ulikuwa unapoteza muda wa mahakama bure?

KIBATALA: Shahidi, una elimu gani?

SHAHIDI: Elimu yangu haikuhusu.

KIBATALA: Inanihusu.

SHAHIDI: Haikuhusu.

KIBATALA: Unataka nikuoneshe kama inanihusu? (Anafungua nyaraka na kusoma vifungu, kabla hajamaliza Hakimu anaingilia kati).

HAKIMU: Shahidi, una wajibu kisheria wa kutaja elimu yako ikiwa Wakili atahitaji kufahamu.

SHAHIDI: Elimu yangu ni Form Four.

KIBATALA: Kumbe ndiyo maana ulikuwa unakataa kutaja? Sikuulizi ulipata division ngapi usije ukashindwa kuendelea na ushahidi.

MAHAKAMA: (Kicheko)

KIBATALA: Sheria inataka mtuhumiwa kabla hajapekuliwa, yeye awapekue kwanza askari. Je, ulimwambia Hakimu kama Boniface alipata nafasi ya kuwapekua askari?

SHAHIDI: Sio kazi yangu. Ni kazi ya mpelelezi.

KIBATALA: Shahidi, hapa umeletwa wewe au mpelelezi?

SHAHIDI: Mpelelezi atakuja utamuuliza.

KIBATALA: Kwa sasa mahakamani mpelelezi yupo?

SHAHIDI: Atakuja.

KIBATALA: Nakuuliza wewe, umemwambia Hakimu kama ulishuhudia Boniface akiwapekua askari kabla? Umemwambia, hujamwambia?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Sasa kwa nini unapoteza muda wa mahakama?

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, samahani, naomba kumuelimisha kidogo Wakili.

KIBATALA: Huwezi kunielimisha chochote. Hapa umekuja kujibu maswali, sio kuelimisha. Kama unataka kunielimisha subiri nikija kituo cha polisi, lakini hapa upo kwenye himaya yangu, na utajibu maswali kama navyokuuliza.

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, naomba kumuelimisha Wakili kuhusu taratibu za utendaji kazi za polisi.

HAKIMU: Jibu maswali kama anavyokuuliza. Akitaka kujua taratibu za kazi atakuuliza.

SHAHIDI: Sawa Mheshimiwa.

KIBATALA: Pole sana Shahidi, unajisikia vibaya?

SHAHIDI: Hapana.

MAHAKAMA: (Kicheko).

KIBATALA: Umesema wakati wa upekuzi nyumbani kwa Boniface kuna jirani aliitwa kushuhudia.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Anaitwa nani?

SHAHIDI: George Steven.

KIBATALA: Unajua kwamba hakuna jirani yeyote wa Boniface mwenye jina hilo?

SHAHIDI: Anaitwa George Steven.

KIBATALA: Unajua kwamba kati ya majirani wanaomzunguka Boniface ni mmoja tu mwenye jina Frank Steven. Na hata huyo si yeye aliyekuja kushuhudia upekuzi.

SHAHIDI: Mi sikumbuki.

KIBATALA: Jina la jirani aliyeshuhudia upekuzi lipo kwenye nyaraka zenu au halipo?

SHAHIDI: Lipo.

KIBATALA: Na nyaraka hizo umezipitia lini mara ya mwisho?

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, Wakili ananiuliza maswali bila kunipa nafasi ya ufafanuzi.

HAKIMU: Amekuambia anataka ufafanuzi?

SHAHIDI: (Kimya).

HAKIMU: We jibu kama anavyokuuliza, akitaka ufafanuzi atakuambia. Pia baadae una nafasi ya kutoa ufafanuzi kadri utakavyoongozwa na Wakili wa Jamhuri.

SHAHIDI: Sawa, Mheshimiwa.

KIBATALA: Unafahamu kuwa Bonny ni kiongozi wa kisiasa mwenye wafuasi wengi na anayefahamika ndani na nje ya nchi?

SHAHIDI: Labda anafahamika na familia yake.

KIBATALA: Familia yake haihusiki hapa. Nimekuuliza wewe.

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Unajua Bonny amewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo?

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Unajua Bonny ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani na alishinda akiwa gerezani?

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Unajifanya mjanja eeh? Sasa hao waliokutuma leo utaenda kuwaambia ulichokutana nacho mahakamani.

KIBATALA: Umemwambia Hakimu mlipoenda kumpekua Bonny mlichukua simu aina gani yenye IMEI number gani?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Umemwambia Hakimu kama Bonny alisaini hati ya upekuzi?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Ukiwa dereva wa gari la polisi lililoenda nyumbani kwa Bonny, ulimwambia Hakimu nani alifungua geti?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Ulipokuja hapa umeoneshwa hati ya upekuzi ili uitambue?

SHAHIDI: Hiyo ataoneshwa mpelelezi.

KIBATALA: Jibu swali, usijitungie maswali yako.

SHAHIDI: Utaratibu wa kazi haupo hivyo.

KIBATALA: Sijakuuliza utaratibu wa kazi zenu. Nimekuuliza umeoneshwa hati ya upekuzi au hujaoneshwa?

SHAHIDI: Sio kazi yangu.

HAKIMU: Shahidi nakuonya upo chini ya kiapo, jibu maswali kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Sijaoneshwa Mheshimiwa.

KIBATALA: Sasa kwa nini unatupotezea muda?

KIBATALA: Umemwambia Hakimu mlipotoka kwa Bonny mlielekea wapi?

SHAHIDI: Tulirudi ofisi ya ZCO.

KIBATALA: Elewa swali. Umemwambia Hakimu au hujamwambia?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Umemwambia Hakimu mliporudi kituoni mliripoti kwa nani?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Ni hayo tu Mheshimiwa.

HAKIMU: Jamhuri kuna re-examination?

JAMHURI: Hapana Mheshimiwa.

HAKIMU: Shahidi, tumemaliza unaweza kuondoka.

HAKIMU: Upande wa Jamhuri mmebakiza mashahidi wangapi?

JAMHURI: 10 Mheshimiwa.

HAKIMU: Kama mashahidi wenyewe ni kama huyu, nashauri mulete watatu watatu.

MAHAKAMA: (Kicheko).

HAKIMU: Namaanisha kama watatoa ushahidi mfupi kama huyu basi waje watatu watatu ili tumalize haraka.

JAMHURI: Sawa Mheshimiwa.

Credit😛age ya malisa fb
HAKIMU: Kesi imeahirishwa itasikilizwa mfululizo tarehe 05, 06 na 07 Mei 2025.
Aisee natamani niende mahakamani nikashuhudie huu uhondo😀
 
Back
Top Bottom