Mabraza mliofanikiwa, tupeni michongo ya madili makubwa

Mabraza mliofanikiwa, tupeni michongo ya madili makubwa

Mimi nataka mtu mmoja alete mchongo wakupata japo milion 4 tu kwa mwezi kama faida 🤣 manaa tunaoishi laki mbili ni wengi🥹
 
Mimi nataka mtu mmoja alete mchongo wakupata japo milion 4 tu kwa mwezi kama faida [emoji1787] manaa tunaoishi laki mbili ni wengi🥹
Michongo ipo ila Lazima uwe na nyundo mkononi ndo utapigilia msumari
 
unaweza kujitoa kwamtu bilamalipo ya uhakika huku ukijijenga kwa kuona mambo yanavyofanyika?

mana mafanikio yanakuja kwakuona wakubwazako wanafanya nini na utulie wakufundishe mbinu kabambe

wengi mnafeli hapo hamjifunzi kwa wababe
Sasa hivi hata kujitolea ni sawa na kuomba kazi. Kama una ofisi tangaza nafasi za kujitolea uone umati wa vijana utakaokuja
 
Kanuni ni hizi hapa.
1. Badili mtazamo wako.
2. Badili baadhi ya tabia zako ambazo hazitumiki kukuingizia hela badala yake zinatumia hata kile unachopata.
3. Hakikisha unaiweka afya yako katika kipaumbele namba moja cha utajiri.
4. Soma vitabu utapata madini mengi sana kutoka kwenye vitabu.
5. Mwisho acha maisha ya flow yenyewe, ukipata umepata, ukikosa ni kama umepata pia maana pengine ukizipata itakuwa maangamizi yako. Ukinyimwa umeepushiwa janga au kuna wanaoepushiwa majanga kupitia kupata kwako, ukipata muda wako umefika. Tafuta password..........
Hizi motivational speech tayari zishazoeleka sana.

Wewe kama umetoboa toa code. Mfano unapiga mishe za madini, sema mimi napiga mishe za madini nilianzia hapa nikiwa na hiki mpaka nimefika nilipo. Ndio lengo la uzi
 
Tupeni ushauri wa mishe zinazoweza kumtoa mtu angalau faida milion 3 kwa mwezi tujifunze sisi tuliokomea huku chini🤣 mimi huwa naheshimh sana mtu anayeweza kutafuta pesa mwenyewe , mtu mwenye uwezo wakutafuta kuanzia milion 500 mwenyewe nimtu wa kuheshimu sana . Tupeni mawazo niasisi tupatepo
Biashara nzuri hutokana na kutatua tatizo kililokuwepo.

Sehemu yeyote unayofanya kazi, kuna tatizo linasumbua - kifaa kisichopatikana, spare za bei ghali, software ambayo ni ngumu kuitumia au haifanyi kazi inavyotakuwa, bidhaa inayoadimika mara kwa mara etc.

Wewe unatafuta namna ya kutatua mfano, tafuta supplier wa kitu hiko au kakichongeshe uwauzie, tengeneza software mpya, kama ni tatizo la usafirishaji angalia namna ya kukitengeneza kitu hapa Tanzania upunguze uadimikaji n.k

Tatizo la wabongo mtu anaishi sehemu yenye shida kubwa ya maji, badala ya kutumia mtaji kuchimba kisima auze maji, anaenda kufungua duka la nguo!!

Huku ndo kukosa elimu ya ujasiriamali
 
Ila kuona fursa sio mchezo. Ukicheki mazingira yako kila unachokifikiria kipo, sasa hapo ufanye kwa namna tofauti au uje na kitu kipya kabisa ambacho hakipo sokoni. Sio suala dogo.

Itoshe tu kusema ubunifu wa kibiashara ni kipawa cha mtu. Kwenye hiyo nyanja binadamu hatupo sawa kama ambavyo tunataka kuaminishana
 
Matajiri hawatoagi code za kutoboa!! Ukweli ni kuwa mpaka mtu anatoboa mara nyingi lazima apige mchongo yaani biashara haramu ikiwemo kukwepa kodi halali za TRA, kupiga mzigo wa wizi, machimboni huko kudhamini wizi wa mifuko ya udongo kwenye mgodi unaotema ratio kubwa, kuhonga na kupata tenda zenye faida kubwa( ku inflate bei ya mauzo). Wachache sana wanafanikiwa kwa njia nyoofu. Bado wazee wa misukule!! ni hatari. Ni ngumu sana tajiri kukupa code za mafanikio cha msingi pambana tu ipo siku nawewe unaweza kutana na fursa huku ukiwa tayari kuitumia hapo sasa ndo huja mafanikio.
Hii ndo akili inayofanya watu wasifanikiwe.

Wewe toka uneamka asubuhi umewapa watu wangapi pesa?

Umepiga mswaki - umempa pesa aliyetengeneza dawa ya meno, umeoga - mtengeneza sabuni, unachat na simu yako - muuza simu, umetoa hela ya mafuta au nauli - mwenye sheli au mwenye daladala, umekula - mkulima/hoteli/ mama lishe, umenunua vocha - mitandao ya simu/mawakala.

Yani umegawa hela kwa watu zaidi ya 20 kila siku kwa wafanya biashara biashara halali halafu unasema kuwa huwezi kufanikiwa bila kuingia kwenye uharamia?

Imekaa sawa hiyo?
 
Ila kuona fursa sio mchezo. Ukicheki mazingira yako kila unachokifikiria kipo, sasa hapo ufanye kwa namna tofauti au uje na kitu kipya kabisa ambacho hakipo sokoni. Sio suala dogo.

Itoshe tu kusema ubunifu wa kibiashara ni kipawa cha mtu. Kwenye hiyo nyanja binadamu hatupo sawa kama ambavyo tunataka kuaminishana
Nimetembea nchi nyingi lakini hakuna nchi yenye fursa kama Tanzania.

Ukisema fursa hamna maana yake hakuna shida yeyote wala hakuna maendeleo yanayohitajika maana kutatua shida ndo fursa zenyewe.

Kila kitu kilichokuzunguka hapo ulipo kimenunuliwa sehemu, zungusha kichwa chako hapo ulipo, karibu kila kitu kilitolewa pesa ili kiwepo hapo mpaka lami unayokanyaga kuna mtu kaiuza hiyo ili imwagwe hapo.

Opportunities ni nyingi mno kutafakari tu na kuanza na step ya mwanzo
 
Duh
 
Ingekua rahisi hivyo biashara zingekua hazifi, kila mmoja angekua tajiri. Fursa zipo lakini suala la kuziona na implementation yake tumetofautiana sana. Ndio maana nikasema ni kipawa. Kama ikivyo tu mambo mengine, mfano soka hata watu wote tupewe jezi, njumu na kila kitu halafu twende uwanjani haiwezekani wote tukawa mahiri kama Pacome
 
Sasa hivi hata kujitolea ni sawa na kuomba kazi. Kama una ofisi tangaza nafasi za kujitolea uone umati wa vijana utakaokuja
mimi natafuta sana vijana wadogo siwapati hawa wakubwa niwezi tu. hawaliziki na unacho wapa wanaweza kumuibia ndio shida hiyo ila ningewaajiri sana tu
 
mm nimenyoka niajiri Boss coz natafut fursa mtaan nakwama nipe hyo sehem ya kuanzia au nikufuate Pm
Waaminifu madogo wapo mkuu ninao kama 3 hiv nishawatest kwa mitego kadhaa wamwnyooka...ukihitaji vijana na ukawa siriaz nipm
 
Back
Top Bottom