Mabraza wa Kariakoo na dili zao

Mabraza wa Kariakoo na dili zao

EXTRA:
Kabla sijaendelea ningependa kidogo niwajuze kitu...Unajua watu hasa watoto wa mama hawaelewi baadhi ya vitu wanachukulia maisha poa hasa wakiwaona mabraza na madogo wa DOWNTOWN.
1:WEWE KAMA MPAKA LEO WAZAZI WAPO SHUKURU MUNGU
2:WEWE KAMA HUJAWAHI KUA TEJA SHUKURU MUNGU
3: WEWE KAMA HUJAWAHI KWENDA JELA SHUKURU MUNGU
4: WEWE KAMA HUJAWAHI KULALA NJAA SHUKURU MUNGU.
5: WEWE KAMA UNA AFYA NJEMA SHUKURU MUNGU.
6:WEWE KAMA UNA MKE MWELEWA SHUKURU MUNGU
7: WEWE KAMA UNA WATOTO SHUKURU MUNGU.
Watoto wa downtown hatukupenda kua wezi au majambazi au vibaka au matapeli...Hatukupenda kila siku kukinzana na vyombo vya sheria.hatukupenda kua wahalifu au makahaba au malaya na hatuna excuse yoyote ile.
Lakini maisha wewe yasikie kwa mwenzio omba yasikukute.
Hatukuzaliwa familia bora hivyo ilitubidi tupambane kuanzia kwenye kusoma mpaka kutafuta chaneli za kutoka.
Hatukutokea familia zenye uwezo au wazazi wetu kua na ajira rasmi....tulitokea maisha ya watu wa daraja la chini.
UNAJUA KWANINI????
1: TULIUZA NGADA.
2: TULIUZA SIGARA PORI.
3: TULIKUA MARIOO.
4: DADA ZETU KUA MAESCORT NA MAKAHABA NA MAPROSTUTE UGHAIBUNI.
5: WADOGO ZETU KUKATAA SHULE ILI KUSAKA MAHELA WAKITUIGA SISI.
6:WAZAZI WETU KUTUKOMAZA KABLA YA WAKATI.
7: NA WALIMU WETU WA SEKONDARI KUTUSUSA TUJIFUNDISHE WENYEWE NA TULIFAULU KIBISHI.
Maisha wakuu na yalitufanya tupambane na ni Mungu tu ndio ametuweka hai mpaka leo""TULIKUA WADOGO NA TULIHITAJI UPENDO NA UANGALIZI ILA JAMII ILITUTENGA MABRAZA WAKACHUKUA JUKUMU LA KUTULEA KIMTAA MPAKA TUNAKOMAA NA MAISHA.
HAKUNA KIONGOZI WA SERIKALI KUANZIA NGAZI YA KITAIFA MPAKA MTAA ALIYEWAHI KUTUPA SAPOTI YA VITENDO ZAIDI YA MANENO......NI MUNGU TU ALITUONEA HURUMA.
1: TUSHAKABA.
2:TUSHADHULUMU.
3:TUSHATAPELI.
4:TUSHANUSURIKA KUFA ILA HATUKUWAHI KUTAKA KUUA SABABU YA PESA""DAMU NZITO.
5:TULITOKA MBALI MPAKA HUKO MBALI HATUPAKUMBUKI TENA.
6: TUSHAJIKANA UTU WETU KATIKA HARAKATI KWA KUWEKA REHANI ROHO KWA DILI HATARI ZA KWENYE BLACK MARKET'S WORLDWIDE.
7:TUSHAPOTEZA HISIA ZA KUKASIRIKA AU KUSUSA AU KUNYONGONYEA.
Mtaani unaamka asubuhi baba anakuangalia na mama anakuangalia na wadogo zako wanakutazama.,....utafanyaje na umetokea maisha ya tabaka la chini????
THAT'S WHY WE BECOME FIRST DOPE NIGGA,S IN (EA) ENZI HIZO ZA MID 1980,S AND 1990,S...!!USIPOTOKA MAISHA YANAKUTOKEA WEWE
Mabraza walitufundisha roho ngumu.....ya kwamba dili halali fanyia mwangani na haramu fanyia gizani....Hata ulaya tulikataa kwenda bila mipango maana tulikua na ndoto kubwa kuliko uhalisia wenyewe...!!!
Kutokana na ndoto kubwa kuliko uhalisia kitaani tuliwapoteza hawa wana.....maisha ni kujaribu bahati nasibu ni kama kamari...kuna kula au uliwe...!!
RIP : NGUZO YOSSO A.K.A BOSS
RIP : ORIGINAL MUBANDA A.K.A NYERERE
RIP : JEBBY YOSSO A.K.A MTIKILA
RIP : MEDDY YOSSO A.K.A MTEMVU
RIP : MUNDENDE YOSSO A.K.A SOKOINE
RIP : KITWANA YOSSO A.K.A SALMINI
RIP : AFIZI YOSSO A.K.A KARUME
RIP : KIPEPE YOSSO A.K.A MALICHELA
RIP :MALI YA MUNGU A.K.A KAMBONA.
Watoto wa downtown tulipambana wenyewe hatukupambaniwa na hata nyumba za urithi hatukuhesabiwa sababu koo zetu za kiafrika tunazijua wenyewe.
Tofauti na sasa enzi hizo pamoja na tofauti zetu ugomvi kuibiana na kudhulumiana ila mwisho wa siku tulipeana chaneli.....za aina zote na kizazi chetu kilikua mfano wa kuigwa.. !!!Unajua watu wengi waga wanachukulia watoto wa downtown kama watoto wa kishua ila asilimia 80% ni watoto wa watanzania wenye kipato cha chini.Hivyo ukiona watoto wa downtown wamefanikiwa waheshimu""WAMEPAMBANA""
KATI YETU KUNA WALIOPO JELA MPAKA LEO KAMA AKINA...!!!
MUBABA 27yrs.....anatoka 2032
NONDO Life sentence
KIBAKULI SR Life sentence
BAKULE 17 years,,,anatoka 2026
Y2K 9 years anatoka mwaka huu 2024.....Hao wote wapo jela za ughaibuni na kuna wengine walishatoka kama akina
LUNYAMILA alikaa jela miaka 9
MEJA alikaa jela miaka 6
SHOKISHUGI alikaa jela miaka 4....na wengine weengi nimeshawasahau...wote walipata majanga katika kutafuta maisha
Maisha yanaenda kwa kasi na uzee unakuja ila kumbukumbu ni kama jana tu......enzi hizo watu wachache downtown....leo hii downtown pekee watu karibia laki nne wanaingia na kutoka city center kila baada ya masaa mawili.
Kwahiyo ukiona wazee wa downtown wana maisha yao basi wape heshima....mjini bila akili ya kiroho na kimwili hauwezi kufanikiwa kwa lolote na chochote.
MWISHO WA EXTRA
TUTAENDELEA NA SIMULIZI.....!!!
SALUTE
 
Jamaa muda sana hajawepo au ndio kusema M23 wamefanya yao
 

Attachments

  • IMG_20240606_122510.jpg
    IMG_20240606_122510.jpg
    16.1 KB · Views: 9
Tutaendelea baada ya mda kidogo......!!!
Njaa mbaya sana hapa katikati nikapata dili la kuingia DRC kutazama fursa tena...ndio maana nikapotea.
Ila tutaendelea na simulizi yetu......lakini kwa sasa niwape story mpya fupi.
NILIVYONUSURIKA KUA MSUKULE MAHALI.
Ebwana wadau uchawi upo na DRC ndio wanaongoza kwa kupenda mambo hayo...!!!!
Hasa majimbo ya manyema na tanganyika......!!
Kule kuna sehemu utamaduni wao
ndio huo.
Sasa katika utafutaji tunakutana na mengi.......siku moja si nikakutana na mganga wa kienyeji akadai nyota yangu kali sana anipe hela au madini nimfanyie kazi yake moja hivi.
Nikamuambia mimi nimekuja kimagumashi napiga dili zangu fasta narudi kigoma.
Kumbe mdau kafanya yake nisivuke ziwa nizame aniweke ndichi.
Sasa katika kampani yangu kuna dogo mbilikimo anaitwa kwa jina la utani FERRE GOLA ila jina lake kamili ni MAYENGE...ndio akinichana na kunipa dawa za kujikinga......la sivyo yule mbangu bangu alipanga anilosotishe ila sasa akazidiwa uchawi na dogo niiyekua nae.Wadau mkienda DRC muwe mnawatafuta mbilikimo wawape maujanja...maana wao ndio wanamiliki njia zote za kupata mawe kirahisi...lakini kuwapata nao sio mchezo....!!!!!
Mbilikimo wanajua michezo yotemichafu ya kutafuta mawe......usiende kichwa kichwa utaishia kupoteza hela zako zote.
Pia wadau mkienda DRC muwe mnaaga nyumbani kabisa kwa wazee wenu afu mkubali kua uchawi upo msijifanye wajuaji
Nitaleta uzi kamili baadae au ndani ya week hii.
Namshukuru Mungu nimerejea salama ila ndio hivyo pesa ngumu wadau na sio bongo tu...hata DRC mpaka waasi wanalia hela ngumu,afu wanawamaindi kichizi wanajeshi wa Tanzania sababu wakiwaotea wanawapa kichapo kweli.
Wameniambia kua wanajeshi wa Tanzania wapo very trained na wapo dedicated kwenye majukumu yao tofauti na wanajeshi wa FARDIC.
ILA WABONGO TUNAWACHUKULIA POA VIJANA WETU AMBAO SIFA ZAO NI KUBWA MNO UKANDA HUU WA SADC..
HATA MAKOMANDOO WA SPECIAL ELITE UNIT ZA JESHI LA JWTZ WANA SIFA KUBWA SANA KWA WELEDI WAO NA MISHENI ZAO WANAZOZIKAMILISHA KWA ASIKIMIA MPAKA 97%.
Wadau tutaendelea na uzi wetu...cha msingi mpiganaji nimerudi salama kidogo kilichopatikana sio haba namshukuru Mungu mwingi wa rehema......!!!
Nipo zangu kariakoo nakunywa juisi ya alovera...nikimaliza nitulie niendelee kuwamwagia uzi za utafutaji na tukipeana moyo wanaume wapambanaji.
USHAURI WA BURE
USIKUBALI MWANAMKE AKUFANYE WEWE KUA NGAZI YAKE YA MAFANIKIO...
MAPENZI NI MTEGO INGIA KWA AKILI NA SIO HISIA.
TUTAENDELEA.............WADAU!!!!!
 
Back
Top Bottom