CHOMBEZO....!!!
Kuna kisa braza yenu kimenikuta......unajua kutokana na maisha ya kutotulia kila siku safari basi shemeji yenu akawa anielewi.
Unajua sisi wasaka tonge mambo ya mapenzi na mahusiano hatuyapi kipaumbele sana.
Sasa shemeji yenu akanichana tuvunje ndoa sababu mimi situlii nyumbani na nimekua na maneno mengi kuliko vitendo.....akadai kua nimekua tapeli wa mjini hivyo kama nafikiria kuoa mke wa pili huko DRC bora tuachane.....nikawa na kibarua cha bure kumbembeleza MAMA MAWILI au nitafute njia mbadala ya kutikisa kiberiti ili atulie
IKUMBUKWE:
Huyu kipenzi changu MAMA WAWILI tulikutana mtaani na kwa upendo tukachukuana na kuanza maisha pamoja.
Kutokea maisha ya kula milo miwili kwa siku mpaka maisha ya kula milo nane kwa siku.
Kuanzia maisha ya kupanga chumba kimoja mpaka maisha ya nyumba ya vyumba sita na vigari vyetu used vya kijapani.
Sikatai mimi msela ila sio msela mavi....na mama wawili nampenda kindakindaki.
Fasta nikafanya yafuatayo ili kutingisha kiberiti nione hali ya hewa ipoje kwa ushauri wa braza yangu MUDI MUZUNGU
1: Nikatengeneza nakala feki ya urithi na mali zote nikaandika majina ya watu wengine..... zikabaki mali chache za kishikaji nilizoandika mapacha wangu
2:Nikajifanya nabadili dini na nimekua Rastafarian toka nimetoka DRC siendi kusali nae KKT kwa mchungaji Mwakasege tena.
Sasa nikaivujisha siri kimakusudi ili kutikisa kiberiti...na mashosti zake wakaenda wakamwambia.....kua mumeo ana mpango kazi a.k.a plan B.
Nimerudi kutoka kwenye harakati....WAJOMBA NIMEKIMBIZWA NA PANGA NA MWIKO🤣🤣....na nimepewa onyo nikitia tu mguu nyumbani nakatwa masikio😂😂😂😂 na huo urastafarian wangu niupeleke jamaica na sio kwake Bunju........na huyo mwanamke wa kimanyema kule Kivu kama ndio anaenipa kiburi atakiona cha mtema kuni.
Shemeji yenu kawafuata wanangu wote wa kariakoo anamuulizia MUDI MUZUNGU amtimue na mapanga,sababu anadai ndio kanipa haya maujanja ya kuandika majina ya watu wengine mali zangu na kunifanya siku hizi nimekua Rastafarian a.k.a ganja man.
Na kilichomuuma zaidi shemeji yenu ni kwamba kwenye waraka wa urithi nimeandika yeye anatakiwa kurithi vyombo vya ndani na nguo zangu...mali zote ni za mapacha 🤣🤣🤣 case closed.
Sasa toka last week huyu wife wa kimachame ananitafuta na mwiko anitoe manundu 🤣🤣🤣.
Nimepanga kesho niende na wazee tuyasuluishe...........maana hii imekua balaa... kila nikifika home nafukuzwa na mwiko na maneno makali juu.....mchaga wangu kakasirika anadai nimeoa mwanamke wa kimanyema kule Kivu nirudi huko.......Nimegundua kumbe ananipenda nimetikisa kiberiti nimepata majibu.Nikimalizana na mama wawili tutaendelea na simulizi.......!!!
**************************