Mabraza wa Kariakoo na dili zao

SALUTE
 
Jamaa muda sana hajawepo au ndio kusema M23 wamefanya yao
 

Attachments

  • IMG_20240606_122510.jpg
    16.1 KB · Views: 9
Tutaendelea baada ya mda kidogo......!!!
Njaa mbaya sana hapa katikati nikapata dili la kuingia DRC kutazama fursa tena...ndio maana nikapotea.
Ila tutaendelea na simulizi yetu......lakini kwa sasa niwape story mpya fupi.
NILIVYONUSURIKA KUA MSUKULE MAHALI.
Ebwana wadau uchawi upo na DRC ndio wanaongoza kwa kupenda mambo hayo...!!!!
Hasa majimbo ya manyema na tanganyika......!!
Kule kuna sehemu utamaduni wao
ndio huo.
Sasa katika utafutaji tunakutana na mengi.......siku moja si nikakutana na mganga wa kienyeji akadai nyota yangu kali sana anipe hela au madini nimfanyie kazi yake moja hivi.
Nikamuambia mimi nimekuja kimagumashi napiga dili zangu fasta narudi kigoma.
Kumbe mdau kafanya yake nisivuke ziwa nizame aniweke ndichi.
Sasa katika kampani yangu kuna dogo mbilikimo anaitwa kwa jina la utani FERRE GOLA ila jina lake kamili ni MAYENGE...ndio akinichana na kunipa dawa za kujikinga......la sivyo yule mbangu bangu alipanga anilosotishe ila sasa akazidiwa uchawi na dogo niiyekua nae.Wadau mkienda DRC muwe mnawatafuta mbilikimo wawape maujanja...maana wao ndio wanamiliki njia zote za kupata mawe kirahisi...lakini kuwapata nao sio mchezo....!!!!!
Mbilikimo wanajua michezo yotemichafu ya kutafuta mawe......usiende kichwa kichwa utaishia kupoteza hela zako zote.
Pia wadau mkienda DRC muwe mnaaga nyumbani kabisa kwa wazee wenu afu mkubali kua uchawi upo msijifanye wajuaji
Nitaleta uzi kamili baadae au ndani ya week hii.
Namshukuru Mungu nimerejea salama ila ndio hivyo pesa ngumu wadau na sio bongo tu...hata DRC mpaka waasi wanalia hela ngumu,afu wanawamaindi kichizi wanajeshi wa Tanzania sababu wakiwaotea wanawapa kichapo kweli.
Wameniambia kua wanajeshi wa Tanzania wapo very trained na wapo dedicated kwenye majukumu yao tofauti na wanajeshi wa FARDIC.
ILA WABONGO TUNAWACHUKULIA POA VIJANA WETU AMBAO SIFA ZAO NI KUBWA MNO UKANDA HUU WA SADC..
HATA MAKOMANDOO WA SPECIAL ELITE UNIT ZA JESHI LA JWTZ WANA SIFA KUBWA SANA KWA WELEDI WAO NA MISHENI ZAO WANAZOZIKAMILISHA KWA ASIKIMIA MPAKA 97%.
Wadau tutaendelea na uzi wetu...cha msingi mpiganaji nimerudi salama kidogo kilichopatikana sio haba namshukuru Mungu mwingi wa rehema......!!!
Nipo zangu kariakoo nakunywa juisi ya alovera...nikimaliza nitulie niendelee kuwamwagia uzi za utafutaji na tukipeana moyo wanaume wapambanaji.
USHAURI WA BURE
USIKUBALI MWANAMKE AKUFANYE WEWE KUA NGAZI YAKE YA MAFANIKIO...
MAPENZI NI MTEGO INGIA KWA AKILI NA SIO HISIA.
TUTAENDELEA.............WADAU!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…