macerebrity wanaoshi kwa mama/wazazi

Kumbe wewe unawaongopea wenzio... I hate this kind of people. Yaani unatetea mtu kukaa kwa mama wakati mtetezi wao hukai kwa mama yako..??

Wapi nimetetea mtu kukaa kwa mama yake?

You totally miss my point.

Mie nasema usijihusishe na visivyokuhusu. Mtu celebrity hata hakujui wewe utatokaje povu kummind anakaa kwa mam yake?

Una muda mchafu kweli wewe.

What's next? Utataka kwenda hapo kwa mama yake ukague kwenye jaa lao kama wanakula dagaa au mayai?
 
Kama hizo chupi mbili nimenunua mwenyewe sioni tatizo, ila kama hizo hizo mbili ndo umepewa na mama hapo pana shida... etehe etehee
 

When a stupid man is doing something he is ashamed of, he always declares that it is his duty.
George Bernard Shaw 1856-1950
Irish dramatist & critic
 
Kwa nini usiwashauri cha kufanya, ambacho wewe ulipitia kuliko kuwatetea waendelee kukaa kwa mama?

Kwa nini nimshauri cha kufanya mtu ambaye sio tu hajaniomba ushauri, bali hajui hata kama nipo?

Wewe una uhakika ushamaliza ya kwako mpaka uanze kutoa ushauri usioombwa kwa watu wasiokujua?
 
Kama hizo chupi mbili nimenunua mwenyewe sioni tatizo, ila kama hizo hizo mbili ndo umepewa na mama hapo pana shida... etehe etehee

Huyo TID mlizaliwa wote? Unajua alipotoka? Unaifahamu mipango yake ya maisha?

Vipi ikiwa TID amedhamiria siku atakayoondoka nyumbani anataka akaingie kwenye nyumba yake anayojenga na si kwenda kupanga, hilo wewe linakuhusu vipi kama mwanaume mwenye shughuli zako za kufanya?

Hakuna maneno yeyote yanayojustify umbea kwa mwanaume. Kama wewe ni wa kike si haba, maumbile yanakuongoza, lkn kama ni wa kiume ndio nyinyi mnavishwaga khanga uswahilini
 
Kama huwezi ona aibu kuishi na wazazi mnapishana koridoni toka kwenye kunyoa ndevu basi wewe una tatizo. Kuna umri unafika ni lazima ukajitegemee... na kujitegemea kunaanzia mahala unapoishi na mengine mengi tu. Haya mambo ya kusema hatumjui wakati tunazijuwa historia zao unakosea. Hata kama unakula daga, kama uko kwako haina tabu.. Hebu rejea hotuba ya Nyerere... UKIWA NA CHAKO UNAKITUMIA KWA KIBURI, HAKUNA WA KUKUHANGAISHA
 
Wewe hapa ndo umezungumza point ehee? :clap2:

Ngoja nikuulize swali kama mwanaume kweli na ujibu: Nini ubaya wa mtu kukaa kwa mama yake?
1. Kwake binafsi
2. Kwa jamii
3. Kwa mama yake
 
Kwa nini nimshauri cha kufanya mtu ambaye sio tu hajaniomba ushauri, bali hajui hata kama nipo?

Wewe una uhakika ushamaliza ya kwako mpaka uanze kutoa ushauri usioombwa kwa watu wasiokujua?
Ndo nyie mnaosubiri mtu afe ndo mnakuja na michango ya majeneza ya bei mbaya. Wakati akiwa mzima hata hamuoneka. Kumsaidia mtu si mpaka akuombe. Situation yake ndo inatakiwa ikupe taarifa ya uhitaji huo
 
Mkuu nakubaliana na wewe kwa asilimia 100,Unajua wakati mwingine malezi yanachangia kwa kiasi kikubwa.Mimi tokea niko mdogo nilikua naandaliwa kuja kujitegemea kuna baadhi ya vitu vidogo nilikua navifanya kimasihara nikiwa mdogo kama kufua nguo zangu mwenyewe,kupiga pasi,kufagia uwanja asubuhi na kuosha vyombo tulipangiwa zamu,kujua muda sahihi wa kulala na kuamka asubuhi kwa ajili ya shule nk.Na kwetu uchagani kuna kile kitu kwamba ukishamaliza std 7 umekuwa kijana sasa vitu kama hivyo vinasaidia sana kumjenga mtu asiwe tegemezi.Vijana wengi sasa hivi wanaogopa kuhama nyumbani ili kuficha madhaifu yao mtu hata kutandika kitanda chake mwenyewe hajui achana na kufua PICHU,sahani yake mwenyewe ya kulia chakula hawezi osha akakae mwenyewe avunde??Amkeni vijana nchi ishauzwa hii,hamna kitu kizuri kwa kijana kama kujitegemea kwanza inakuongezea kujiamini na hata ndugu jamaa na marafiki wanakuheshimu kwa kweli.
 

Bottom line, huwezi kumpangia mtu mzima mwenzako namna ya kuishi.

Ukifikiri una weza wewe ndiye utakayekuwa una matatizo.
 
Ndo nyie mnaosubiri mtu afe ndo mnakuja na michango ya majeneza ya bei mbaya. Wakati akiwa mzima hata hamuoneka. Kumsaidia mtu si mpaka akuombe. Situation yake ndo inatakiwa ikupe taarifa ya uhitaji huo

Tatizo unafikiri unasaidia wakati unaotaka "kuwasaidia" hata hawajui kama una exist dunia hii.

Saidia familia yako.

Uzabizabina si msaada.
 
Ngoja nikuulize swali kama mwanaume kweli na ujibu: Nini ubaya wa mtu kukaa kwa mama yake?
1. Kwake binafsi
2. Kwa jamii
3. Kwa mama yake

Mwanaume wa kweli anaishi kwa kujitegemea na si kutegemea jasho la mtu mwingine.
 
Ngoja nikuulize swali kama mwanaume kweli na ujibu: Nini ubaya wa mtu kukaa kwa mama yake?
1. Kwake binafsi
2. Kwa jamii
3. Kwa mama yake

1. Kwake binafsi
Unajuwa unapokuwa wewe ndo wa mwisho na wa kutegemea kutatua jambo always you will put an extra effort. Ni kama baba nyumbani, kwa vile mupo basi wengine huwa wnarelax. Kitendo cha kuwa upo na mama, kuna ile hali ya kuwa ... MAMA YUPO ATAFANYA TU... inakufanya ushindwe kukua kiakili.

Kwenye football, kuna siku mchezaji maarufu anakuwa hayupo kwenye mudi nzuri ya kumwezesha kucheza vizuri, lakini kwa sababu ya historia yake, huwa anapangwa ili kuwaathiri wapinzania kisaikolojia. Kuna wengine wakishaona fulani yupo basi hata confidence inawashua

2. Kwa jamii

Mtu yeyote anayekaa kwa mama huwa anatazamwa na jamii kama mtoto. Na jamii zetu hizi kama unalishwa maana yake hata uwezo wa kufanya maamuzi yako binafsi unakuwa chini. Uwezo wako upo kwenye kuamua nguo gani uvae na lini ufue. Kwa hiyo kuna maswala jamii haitakuletea na wala hutashirikishwa kwa vile tu unaishi kwa wazazi.

Kuna jamii kama hujaoa/Hujaolewa basi kuna maeneo utatengwa.

3. Kwa mama yake

Hasara anaoipata mama ni kuwa anaandaa ombaomba wa baadaye. Yeye kwake anadhani anampenda sana mwanae, lakini siku akiondoka ndo inakuwa balaa. Si mmeshawahi kuona kuna wazee wengine wana mali nyingi tu, lakini akifa leo, kesho wanawe wanasambaratika , na hii ni kwa vile hawakuwajengea confidence ya kuishi wenyewe.

Kwa ujumla, kushi kwa wazazi ukiwa na umri mkubwa ni hasra zaidi kuliko tunavyodhani. Kuna jamii huwa wanawaita watoto wa mama....
 
Tatizo unafikiri unasaidia wakati unaotaka "kuwasaidia" hata hawajui kama una exist dunia hii.

Saidia familia yako.

Uzabizabina si msaada.
Hata hiyo keyboard unayoitumia kujibizana nayo kuna mtu alikaa mwenyewe akaitengeneza.... Na huyo mtu hata hajui kama wewe una-exist. Kwa hiyo whether mtu anajuwa kuwa nae-exist, or not, is not a point to discuss. Issue ni namna ya kumsaidia mtu aondokane na kushi kwa wazazi akiwa na umri mkubwa... acheni kuwadanganya wenzenu.... Wewe mwenyewe umesema sijui nani ankulipa nini kwa kumpangisha kwenye mjengo wako, sasa kwa nini usiwasaidie na wengine nao wafikie huko?
 
Ukishafikia kuona kuishi kwa mama si tatizo, KWA WAKWE WE UNAWEZA UKAISHI NA USIONE NI TATIZO
 
Hizi mentality za kuishi kijima, kuwa ufanye kitu kwa sababu jamii inataka ndizo zinazopelekea umaskini.
 
Ngalikihinja, changamoto uliyonayo humu ni kwamba topic ni tight na katika transition period hii...wengi hawatakuunga mkono ingawa uliyoyaongea wanayajua na kuyaelewa! Nchi yetu imekua na changamoto kubwa sana za kiuchumi, ukosefu wa ajira, malezi duni ... vijana wengi wamekua ni watu wa kuchagua kazi na kulinganisha mishahara yao na ya wakongwe bila kujua kila siku anayozidi kukaa nyumbani anazidi anapoteza! Binafsi nakumbuka miongoni mwa vitu vilivyonifanya nikimbie home mapema ni kuletewa wadogo chumbani kwangu nilale nao, kitu ambacho nilikua sijazoea kabisa hali iliyopelekea kuamini heshima na usiri wangu utakua umeingiliwa....

Kwa wazazi, msiwape watoto uhuru mkubwa sana wa wao kujiona wanamiliki sehemu ya nyumba zenu ... kwa wale watoto wa kiume wenye ajira, kama vipi, hebu walazeni na watoto ama 'shamba-boy' kwa wiki moja tu muone matokeo!
 
Ukishafikia kuona kuishi kwa mama si tatizo, KWA WAKWE WE UNAWEZA UKAISHI NA USIONE NI TATIZO

Kila kitu na mazingira. Siwezi kumhukumu mtu anaekaa kwa wakwe zake. Kwa nini inikere?

Mimi binafsi ndio naweza kukaa kwa mkwe, sina tatizo hata dogo
 

Kwa nini unafikiri kumtoa mtu kwao ni kumsaidia wakati hata humjui mtu yukoje na mpango mzima wa kwao ukoje?

Tatizo your worldview is informed by a prejudiced one track mindedness inayo generalize kila kitu bila hata kujua specifics.
 
Unayoyaongea ni kweli.....
Hebu kumbuka wakifika wageni wakiume home, nani analala nao.... kama si wewe etc. Watu wanabisha lakini hawaishi kumsifia JAY kwa kujenga jumba lake...... Na hawaachi kujisifia wenyewe kwa kukusanya kodi toka kwenye majumba yao...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…