1. Kwake binafsi
Unajuwa unapokuwa wewe ndo wa mwisho na wa kutegemea kutatua jambo always you will put an extra effort. Ni kama baba nyumbani, kwa vile mupo basi wengine huwa wnarelax. Kitendo cha kuwa upo na mama, kuna ile hali ya kuwa ... MAMA YUPO ATAFANYA TU... inakufanya ushindwe kukua kiakili.
Kwenye football, kuna siku mchezaji maarufu anakuwa hayupo kwenye mudi nzuri ya kumwezesha kucheza vizuri, lakini kwa sababu ya historia yake, huwa anapangwa ili kuwaathiri wapinzania kisaikolojia. Kuna wengine wakishaona fulani yupo basi hata confidence inawashua
Hata kiswahili hujui kazi umbea na kufuatilia mambo ya watu, next time sema MPO sio MUPO.
Hapa ndio utashindana na mimi hadi asubuhi. Kwani nani alikwambia kuwa TID anamtegemea mama yake kwa chakula na kuamua mambo yake? What if mama ndio ananufaika na msaada wa TID hapo nyumbani, au umbea wako umekushughulisha mpk ukajua nyumba ile chakula na umeme analipa nani?
2. Kwa jamii
Mtu yeyote anayekaa kwa mama huwa anatazamwa na jamii kama mtoto. Na jamii zetu hizi kama unalishwa maana yake hata uwezo wa kufanya maamuzi yako binafsi unakuwa chini. Uwezo wako upo kwenye kuamua nguo gani uvae na lini ufue. Kwa hiyo kuna maswala jamii haitakuletea na wala hutashirikishwa kwa vile tu unaishi kwa wazazi.
Kuna jamii kama hujaoa/Hujaolewa basi kuna maeneo utatengwa.
Mimi nina mke na mtoto na ninakaa kwa mama. Hakuna jamii wala mwanamke yeyote wa dizain yako anayeweza kunifanya nimuache mama yangu peke yake kila siku anitumie mashtaka jirani kasogeza mpaka, bomba limepasuka maji hayafiki nyumbani, TANESCO wamekata umeme, n.k eti kisa jamii.
ANGALIZO: Wewe unayejifanya unakaa mwenyewe akili yako imekua ndio unaonekana kilaza hasa na hujiamini. Unaamini kuwa jamii ndio inakupangia la kufanya kwa hiyo unaishi kwa hofu ya fulani atanionaje. Fedha ambayo ungeitumia kumalizia nyumba uhamie kwako unaitumia kupanga kwa kuwa unaogopa jamii itakuonaje. Unaongozwa na jamii wewe, wala sio na akili yako.
3. Kwa mama yake
Hasara anaoipata mama ni kuwa anaandaa ombaomba wa baadaye. Yeye kwake anadhani anampenda sana mwanae, lakini siku akiondoka ndo inakuwa balaa. Si mmeshawahi kuona kuna wazee wengine wana mali nyingi tu, lakini akifa leo, kesho wanawe wanasambaratika , na hii ni kwa vile hawakuwajengea confidence ya kuishi wenyewe.
Kwa ujumla, kushi kwa wazazi ukiwa na umri mkubwa ni hasra zaidi kuliko tunavyodhani. Kuna jamii huwa wanawaita watoto wa mama....
Confidence haijengwi na kuishi kwa kuogopa jamii. Think what is right for you regardless what voyeurs are going to say. Kama wewe umehama kwa kuwa watu wanasema basi hiyo ni dalili kuwa unaongozwa na external facts na sio akili yako. Wangapi waliuza nyumba za urithi wakaendelea kuishi kwenye maghetto na kukaa kwao mtaani hakukuwasaidia?
Mwanamke atakayeolewa na mwanaume wa dizain yako ajue anaishi na mwanamke mwenzake. Haiwezekani mwanaume ukawa una swing kwa kila majirani watakalosema. Siku watakayosema unamdekeza mwanao basi kwa kuwa huna akili utampeleka boarding hata ya hovyo na ataishiwa kubakwa.
Wakati huu unaongea umbea hapa, hujui pengine TID au hao wengine uliowataja wanajenga mijengo yao ya hatari ila wewe unayeishi kwa mdomo na macho ya kutizama jirani anaishije unapanga na kujiita mjanja. Usipende kufuatilia maisha ya watu usiowajua. Haikusaidii maishani mwako na kamwe haikuongezei maksi mbele za wanaume wenye tabia za kiume.