macerebrity wanaoshi kwa mama/wazazi

macerebrity wanaoshi kwa mama/wazazi

Kwa nini unafikiri kumtoa mtu kwao ni kumsaidia wakati hata humjui mtu yukoje na mpango mzima wa kwao ukoje?
Kwa sababu kuishi kwa wazzi wakati una umri mkuwa si sawa.... EBU SOMA HII NA UICHUKE .........Over time, adult kids have stopped learning to solve problems and entertain themselves because adults/parents are quick to jump in and fix things for them. It’s done out of love and with the best of intentions, but over tim eadults/parents have gone from caring for their adult kids , to caretaking.
 
Unayoyaongea ni kweli.....
Hebu kumbuka wakifika wageni wakiume home, nani analala nao.... kama si wewe etc. Watu wanabisha lakini hawaishi kumsifia JAY kwa kujenga jumba lake...... Na hawaachi kujisifia wenyewe kwa kukusanya kodi toka kwenye majumba yao...

Unajuaje kwamba kila mtu anaruhusu wageni kwao?

Wengine wageni wanafikia hoteli. Au hawataki wageni kabisa kwa sababu zao

Ndo haya tunayokataa ya ku copy paste maisha yako kwa wenzako ukafikiri kila mtu anaishi au anataka kuishi kama unavyoishi wewe.
 
Kwa sababu kuishi kwa wazzi wakati una umri mkuwa si sawa.... EBU SOMA HII NA UICHUKE .........Over time, adult kids have stopped learning to solve problems and entertain themselves because adults/parents are quick to jump in and fix things for them. It's done out of love and with the best of intentions, but over tim eadults/parents have gone from caring for their adult kids , to caretaking.

Kama issue ni wazazi kuingilia maisha ya watoto, hata mtoto akiondoka nyumbani mzazi anaweza kumuingilia mtoto maisha yake wakati mtoto yupo kwake.

Kwa hiyo huja address issue bado.

Kukaa nyumbani kwa wazazi hakuna maana kwamba wazazi watakuingilia maisha.

Na kwenda kuishi kwako hakuna maana wazazi hawatakuingilia maisha.

Usitake majibu rahisi kwa maswali magumu.
 
Unajuaje kwamba kila mtu anaruhusu wageni kwao?

Wengine wageni wanafikia hoteli. Au hawataki wageni kabisa kwa sababu zao

Ndo haya tunayokataa ya ku copy paste maisha yako kwa wenzako ukafikiri kila mtu anaishi au anataka kuishi kama unavyoishi wewe.
We uwe mkweli..... Huko namanditi Songea, au Mkarakate Tunduru, AU kule Msalala baada ya kakola shinyanga kusiko na hoteli utawapeleka wapi? AU kutimka bongo ndo kunakufanya uone kila sehemu ya Tanzania ni mjini na ina hotel unazoziwazia?
 
Kama issue ni wazazi kuingilia maisha ya watoto, hata mtoto akiondoka nyumbani mzazi anaweza kumuingilia mtoto maisha yake wakati mtoto yupo kwake.

Kwa hiyo huja address issue bado.

Kukaa nyumbani kwa wazazi hakuna maana kwamba wazazi watakuingilia maisha.

Na kwenda kuishi kwako hakuna maana wazazi hawatakuingilia maisha.

Usitake majibu rahisi kwa maswali magumu.
Ni rahisi sana mzazi kuingilia maisha ya mtoto kama akiwa anaishi naye kwake kuliko kama mtoto anaishi nyumbani kwake.
 
We uwe mkweli..... Huko namanditi Songea, au Mkarakate Tunduru, AU kule Msalala baada ya kakola shinyanga kusiko na hoteli utawapeleka wapi? AU kutimka bongo ndo kunakufanya uone kila sehemu ya Tanzania ni mjini na ina hotel unazoziwazia?

Ndo wanakokaa ma celebrity huko? Ndo aliko P-Funk huko?

Ondoa hoteli, sio lazima kila mtu akubali wageni kwake, usifikiri kila mtu anataka kuishi kama unavyoishi wewe.
 
Ni rahisi sana mzazi kuingilia maisha ya mtoto kama akiwa anaishi naye kwake kuliko kama mtoto anaishi nyumbani kwake.

Ushafanya uchunguzi gani kuonyesha hilo? Rahisi kwa asilimia ngapi? Na kuingilia maisha kwa aina gani?

Wewe ushamaliza mambo yako yote mpaka ushikie bango ya wenzako yasiyokuhusu?

Burgeoning bubonic burlesk!
 
When a stupid man is doing something he is ashamed of, he always declares that it is his duty.
George Bernard Shaw 1856-1950
Irish dramatist & critic
The only true wisdom is in knowing you know nothing.”
― Socrates
 
akiwa hajamaliza na mm ndiye nae mlipia karo, nampa pesa za matumizi kama kunua nguo, viatu, chupi, mswaki n.k kisha nasimamia show nzima ya matibabu anapaswa kuendelea kuishi kwangu ila akimaliza tu masomo namfukuza aende nae akajitegemee ajifunze maisha.

Kama una machungu na mwanao anayeishi kwako, na hutaki hilo, mwambie.

Habari za kupayuka kwa maisha ya ma celebrity usiowajua wasiokujua ni embarassing to say the least.

You are insulting your intelligence.
 
Mwanaume wa kweli anaishi kwa kujitegemea na si kutegemea jasho la mtu mwingine.

Una hakika gani kuwa yeye msanii ndio mtegemezi na si kwamba ukaaji wake ni msaada kwa huyo mama yake?

Mimi nakushauri uache umbea na kupenda kushobokea maisha ya watu usiojua mipango yao. Mimi ninaishi na mama yangu na nitakupa mfano wangu.

Kati yangu na mama hakuna asiyeweza kujilisha wala kujivalisha. Nilipomaliza chuo nikaanza kazi, nilihamia kigamboni nikapanga huko na mama tukawa tunaonana mara moja au mbili kwa mwezi. Ndani ya miezi 9 nilikuja kubaini kuwa mama afya yake inadeteriorate rapidly japo alikuwa haumwi.

Nilichobaini ni upweke tu kwani baada ya mimi kuondoka hapo nyumbani alibaki peke yake. Ndio mke wangu akugundua tatizo na akashauri tukakae na mama na sasa hatumuoni akizeeka kwa kasi kama awali. Ile hali ya kukaa nje jioni peke yake haipo.. sasa akipatikana mwanamke mbea kama wewe atakachosema ni kwamba mimi siwezi kujilipia kodi ndio ninakaa nyumbani kwa mama. Mmbea wa namna hiyo hajui kama nimejenga au ninajenga, yeye atawahi tu kuzungumzia anayoona yanampatia riziki.

Acha umbea mwanaume, mtavishwa shanga msutwe
 
1. Kwake binafsi
Unajuwa unapokuwa wewe ndo wa mwisho na wa kutegemea kutatua jambo always you will put an extra effort. Ni kama baba nyumbani, kwa vile mupo basi wengine huwa wnarelax. Kitendo cha kuwa upo na mama, kuna ile hali ya kuwa ... MAMA YUPO ATAFANYA TU... inakufanya ushindwe kukua kiakili.

Kwenye football, kuna siku mchezaji maarufu anakuwa hayupo kwenye mudi nzuri ya kumwezesha kucheza vizuri, lakini kwa sababu ya historia yake, huwa anapangwa ili kuwaathiri wapinzania kisaikolojia. Kuna wengine wakishaona fulani yupo basi hata confidence inawashua

Hata kiswahili hujui kazi umbea na kufuatilia mambo ya watu, next time sema MPO sio MUPO.
Hapa ndio utashindana na mimi hadi asubuhi. Kwani nani alikwambia kuwa TID anamtegemea mama yake kwa chakula na kuamua mambo yake? What if mama ndio ananufaika na msaada wa TID hapo nyumbani, au umbea wako umekushughulisha mpk ukajua nyumba ile chakula na umeme analipa nani?

2. Kwa jamii

Mtu yeyote anayekaa kwa mama huwa anatazamwa na jamii kama mtoto. Na jamii zetu hizi kama unalishwa maana yake hata uwezo wa kufanya maamuzi yako binafsi unakuwa chini. Uwezo wako upo kwenye kuamua nguo gani uvae na lini ufue. Kwa hiyo kuna maswala jamii haitakuletea na wala hutashirikishwa kwa vile tu unaishi kwa wazazi.

Kuna jamii kama hujaoa/Hujaolewa basi kuna maeneo utatengwa.
Mimi nina mke na mtoto na ninakaa kwa mama. Hakuna jamii wala mwanamke yeyote wa dizain yako anayeweza kunifanya nimuache mama yangu peke yake kila siku anitumie mashtaka jirani kasogeza mpaka, bomba limepasuka maji hayafiki nyumbani, TANESCO wamekata umeme, n.k eti kisa jamii.

ANGALIZO: Wewe unayejifanya unakaa mwenyewe akili yako imekua ndio unaonekana kilaza hasa na hujiamini. Unaamini kuwa jamii ndio inakupangia la kufanya kwa hiyo unaishi kwa hofu ya fulani atanionaje. Fedha ambayo ungeitumia kumalizia nyumba uhamie kwako unaitumia kupanga kwa kuwa unaogopa jamii itakuonaje. Unaongozwa na jamii wewe, wala sio na akili yako.

3. Kwa mama yake

Hasara anaoipata mama ni kuwa anaandaa ombaomba wa baadaye. Yeye kwake anadhani anampenda sana mwanae, lakini siku akiondoka ndo inakuwa balaa. Si mmeshawahi kuona kuna wazee wengine wana mali nyingi tu, lakini akifa leo, kesho wanawe wanasambaratika , na hii ni kwa vile hawakuwajengea confidence ya kuishi wenyewe.

Kwa ujumla, kushi kwa wazazi ukiwa na umri mkubwa ni hasra zaidi kuliko tunavyodhani. Kuna jamii huwa wanawaita watoto wa mama....

Confidence haijengwi na kuishi kwa kuogopa jamii. Think what is right for you regardless what voyeurs are going to say. Kama wewe umehama kwa kuwa watu wanasema basi hiyo ni dalili kuwa unaongozwa na external facts na sio akili yako. Wangapi waliuza nyumba za urithi wakaendelea kuishi kwenye maghetto na kukaa kwao mtaani hakukuwasaidia?

Mwanamke atakayeolewa na mwanaume wa dizain yako ajue anaishi na mwanamke mwenzake. Haiwezekani mwanaume ukawa una swing kwa kila majirani watakalosema. Siku watakayosema unamdekeza mwanao basi kwa kuwa huna akili utampeleka boarding hata ya hovyo na ataishiwa kubakwa.

Wakati huu unaongea umbea hapa, hujui pengine TID au hao wengine uliowataja wanajenga mijengo yao ya hatari ila wewe unayeishi kwa mdomo na macho ya kutizama jirani anaishije unapanga na kujiita mjanja. Usipende kufuatilia maisha ya watu usiowajua. Haikusaidii maishani mwako na kamwe haikuongezei maksi mbele za wanaume wenye tabia za kiume.
 
ingekua vizuri hii mijadala watu wakawa wana declare interest,manake duuu!ngoja niendelee kujifunza kitu fulan
 
Pamoja na wana jf wote wanaoamini its ok kuendelea kuishi kwa wazazi with you hairy grown up arce! Heh! Mi mkaka anaeishi kwa mamake naomba asiquote wala.kujibizana na mimi hunu jamvini!

King'asti nipo nawe 100% and even more. Mom boys wote mje hapa! Kwani kutunza family ndio ukae kwenye nyumba ya mwanaume mwenzio ( babako) mpaka midevu kwenye ' mdhuti' laanakum mkubwa hama kwenu ukatengeneze kwako mkeo ajitambe sio kila muda mamako upo nae mpaka kwa show! !! Waweza kumhudumia remotely!
 
Kuna wakati huwa nawaza, kwa nini mtu ni maarufu halafu bado anaishi kwa wazazi? Kwa mfano, Mlelwa kwa umaarufu wako hustahili kuishi kwa mama, Baraka wa 69 records kwa nini bado upo kwa mama? TID, unaishi hananasifu kwa mama hivi kweli unachangia chakula na mama? Yaani mama akufungulie mlango ukitoka kwenye show? Msechu unaishi kwa mama mdogo? Mnanishangaza maceleb wetu...

Acha hizo habari mbofu mbofu
Ukiwa maarufu BONGO haimaanishi automatically unakuwa na kipato cha kukuwezesha kujitegemea, umaarufu unakuongezea mzigo tu wa matumizi ambayo maybe yange epukika ka usingekuwa maarufu
so kuondoka kwa bi mkubwa ni BAADAE SANAAA.
 
King'asti nipo nawe 100% and even more. Mom boys wote mje hapa! Kwani kutunza family ndio ukae kwenye nyumba ya mwanaume mwenzio ( babako) mpaka midevu kwenye ' mdhuti' laanakum mkubwa hama kwenu ukatengeneze kwako mkeo ajitambe sio kila muda mamako upo nae mpaka kwa show! !! Waweza kumhudumia remotely!

Unaweza kumuondolea mtu upweke remotely?

Kwani kukaa na mama maana yake huna uwezo wa kukaa mwenyewe?

Vijana msiwe wenye kuchunguza maisha ya watu kwa namna ya ushabiki namna hii. Nani ajuaye mipango ya mwenzake mpk mumuhukumu kuwa analishwa?

If I have to declare interest, mimi nilikaa na baba yangu till 38. Alikuwa na nyumba kubwa lkn sikuona sahihi kwake kuishi all alone kwa kuwa tu mimi nina uwezo wa kupanga. Mimi na mke wangu tulikaa pale mpk baba alipofariki ndio tukahamia kwetu. Mom boys ni jina la kishambenga tu ambalo halimaanishi udhaifu in actual fact.

Kama unaishi peke yako lkn maisha yako yanatawaliwa na hofu ya nikifanya hivi majirani wataniona dhaifu, basi bado hujawa mwanaume. Jirani au jamii isiwe remote control ya kukufanya uishi usivyoweza mwishowe ukapotea
 
Kama wewe ulitoka nduki Bongo na kwa wazazi wako nasi tulipo huku ufipani tunawashangaa hao wanao ng'ang'ania kukaa kwa wazazi wao, unajisikiaje kupishana na taulo kwenye velandaa na mama ako mzazi na vyoo vya uswazi umebeba kopo la chooni unaenda kukata gogo mama ako yupo chooni unasubilia atoke wewe uingie! hii si heshima

Umenichekesha sana yaani hii ndo sababu ya kukufanya uhame kwenu kisa kupisha na mama yako mlango wa chooni si heshima? kuna ubaya gani ukikaa kwenu then ukasevu money ambayo ulikuwa ulipie pango? Sioni mantiki ya kupanga kama nyumbani kwenu ni pakubwa na unaweza kaa mpaka utakapokuwa na kwako!
Kuliko nilipe kodi ya nyumba more than 1,5Million TSH kwa mwaka bora nikae kwa mama na hiyo hela nisevu.....
 
Kuna wakati huwa nawaza, kwa nini mtu ni maarufu halafu bado anaishi kwa wazazi? Kwa mfano, Mlelwa kwa umaarufu wako hustahili kuishi kwa mama, Baraka wa 69 records kwa nini bado upo kwa mama? TID, unaishi hananasifu kwa mama hivi kweli unachangia chakula na mama? Yaani mama akufungulie mlango ukitoka kwenye show? Msechu unaishi kwa mama mdogo? Mnanishangaza maceleb wetu...

Mbona unajitaabisha sana kwa kutafuta sifa tu?

Hawa wote uliowataja si wewe mwenye kuwalisha wala kuwahudumia na pengine hujui ni nani huwakirimu mahitaji yao, ila umeona ni vyema tu kuweka maisha yao hadharani kwa ajili ya kujikweza kwako.

Sikia ushauri wangu ewe mwana usiye na akili ya kuwaza yaliyo yako: Maisha yako ni yako na kamwe yasiathiriwe na mijadala ya wapita njia. Hawajui ulipotoka, hawaifahamu njia uliyopitia hata unakokwenda hawakujui. Iweje leo mliokutana nao njiani wajivike umahiri wa kuyachambua maisha yako na kujifanya watabiri wa kesho yako? Ishi kwa kadiri ya mipango yako na si kwa jinsi watu wengine wanavyofikiri.

Kama mama yako hana nyumba au ni muhuni kiasi unaona aibu kukaa naye karibu, usiwachambe wenzio.
 
Kama umehama umri huo kwa nn unawatetea wanao subiri ugali wa kupikiwa na mama zao wakiwa na age za 30+?
Ndugu Tiqo, ujumbe umefika na umewakera watoto wa mama wengi. Ukitaka kujua hilo we hesabu wanatoa povu hapo juu. Wanaogopa kuruka kwa mbawa zao kwa visingizio lukuki. King'asti, endelea kuwapa somo, huenda wakabadili mawazo!
 
Last edited by a moderator:
Wabongo wengine kwa kushikia mabango maisha ya wenzenu ndo maana hatuendelei.

Nevertheless this thread reminded me of my ninja Bartholomew from "Don't Be A Menace..."

.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom