Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

Rais Samia aliwaomba mabalozi wakaulize nchi walioendelea walitumia uchawi gani...

Anauliza hilo wakati ripoti ya CAG kaifungia kabatini
 
Tukisema bandar akabiziwe DPW watu wanaona sisi sio wazalendo ngoja tuone octbr sio mbali
Mkuu punguza mawenge.
Bandari ni yetu. Tutaingia ubia na siyo kuitoa kwa hao jamaa wanaotaka kujimilikisha
 
Hizi ni blah blah tupu. hiyo IGA ya DPW inaongelea juu ya kupandisha uwezo wa wafanyakazi wa sekta nzima ya usafiri wa majini, maana yake ni kwamba nguvu kazi yetu ya bandari bado ina uwezo mdogo na hili ni tatizo la afrika nzima.

Tunakuwa na ufundi mwingi wa kuongea lakini ile output yetu inakuwa ni sifuri kabisa.
 
Ni utamaduni wa serikali yetu kulinda wezi kwa kuwapa more chances kwa kuwahamisha hamisha
 
Hiyo ni IGA ambayo ni kifupisho cha mradi mzima kwa ufupi utakuwa vipi, project contracts zinazoandikwa muda huu ndio pana zenye kuhusisha kila kitu. IGA ina kurasa 32 lakini hizo consession na lease plan zinakuwa na kurasa mpaka 200.
Soma article 2 ya huu mkataba
Objective is to set legally set of framework to
1: develop
2: Improve
3: Manage
Ports in ocean and Lakes
Chawa mkibanwa kufafanua hii objective mnakimbilia oooh IGA mbona hili kusudi hamlisemi
 
Kinachoniuma ni kwa nini tunaangalia kampuni za nje. Kuna matajiri watanzania wanaweza wakapewa tenda na wakasimamia vizuri. Hii ishu ya bandari ilibidi wapewe watanzania. Unampa mkataba mwarabu yeye mchango wake ni kukupa faida. Lakini ukimpa mtanzania atakupa faida na pesa ataiwekeza hapa nyumbani. Vilevile Mtanzania akiharibu ni rahisi kumkamata maana yupo hapa hapa nyumbani. Serikali yetu ina ulimbukeni unampa mchongo mhindi au mwarabu, anajua hapa sio nyumbani. Akipata hela anapeleka kwao, mwisho wa siku tunapungukiwa dola. Nimefanya biashara na wahindi na waarabu wao wanaishi kwa kujibana sana ili wawwekeze kwao.
 
Bajeti inakata vipi wakati wanauwezo wa kukusanya fedha za kutosha. Naona mnapima upepo humu. Shubamit [emoji3]
 
Hiko kipengele siyo kibaya.

Eneo tata ni muda wa mkataba, status ya eneo la uwekezaji, fao la kujitoa na mkataba unasoma Tanzania lakini utekelezaji ni upande mmoja wa Muungano
 
Hacha kupotosha, ni sehemu ipo ya mkataba onaonesha hivyo
 
HHil

Hili suala siyo la kumuachia Mungu kwani lipo NDANI ya uwezo wetu
Tunafanyaje mkuu.

Kwa sasa tunakosoa huku tumeficha majina yetu. Tumeona kilichowapata waliotumia majukwaa kukosoa.

Wale wanaounga mkono huu uzwazwa wanaweka mabandiko huku wameambatanisha namba zao za simu🤣
 
Vipengele vya mkataba boss. Wengi tunaunga mkono uwekezaji ila mkataba uboreshwe
Hii ndio point ya msingi watu tunazungumzia vipengele vyenye utata wajinga wamekazana kutuletea faida za huo mkataba sasa kama mkataba hauna ukomo hizo faida tutazipataje tutampimaje muwekezaji
 
Hii ndio point ya msingi watu tunazungumzia vipengele vyenye utata wajinga wamekazana kutuletea faida za huo mkataba sasa kama mkataba hauna ukomo hizo faida tutazipataje tutampimaje muwekezaji
Huu utata umekuwa ukifafanuliwa zaidi ya mara elfu moja. Tumepotoshwa kwa kulishwa kwa kina suala la mwarabu kutaka kututawala tena miaka hii ya 2020!, na wasomi wetu wamedanganyika na kuuingia huo mkenge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…