Machache yaliyoonekana Simba ikiibuka na ushindi dhidi ya Singida Big Stars

kalisheshe

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2020
Posts
2,064
Reaction score
4,056
1. Leo tumeshuhudia mechi nyingine tafu kwa Simba, ukubwa wa Simba umeamua mechi.

2. Singida waliingiia na maneno ya nje ya uwanja kuwa marefa wako upande wa Simba, hii iliwatoa mchezoni mapema.

3. Huenda Jean Charles Ahoua ameanza kuizoea ligi, anacheza kikubwa mno ( nilikua nikiuponda uchezaji wake wa nyuma).

4. Kibu Denis ni msaada mkubwa mno kwa Simba, anashambulia na kukaba.

5. Kumtoa Mohamed Hussein kuliifanya Simba icheze defensive game badala ya offensive, Fadlu asingeepuka lawama kama Singida wangepata goli maana ile sub iliwakaribisha Singida langoni kwa Simba.

6. Metacha Mnata ni moja kati ya magolikipa bora wazawa, sielewi kwanini Yanga walimuacha.

7. Mechi ya leo imedefine Simba inataka nini msimu huu, kuna uwezekano Simba ikatwaa ubingwa wa NBC.

Simba nguvu moja.
 
Umechambua vema mkuu! Ila soka letu bado linasafari ndefu sana kuwapata marefari wanaojiamini, kuchezesha fear na kujiamini hasa wanapochezesha timu hizi kubwa za Simba na ama Yanga
 
Umechambua vema mkuu! Ila soka letu bado linasafari ndefu sana kuwapata marefari wanaojiamini, kuchezesha fear na kujiamini hasa wanapochezesha timu hizi kubwa za Simba na ama Yanga
Presha ni kubwa mno kwa marefa wetu
Ila tutafika
 
Labda ubingwa wa kuzawadiwa vinginevyo awatofua dafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…