Machache yaliyoonekana Simba ikiibuka na ushindi dhidi ya Singida Big Stars

Machache yaliyoonekana Simba ikiibuka na ushindi dhidi ya Singida Big Stars

1. Leo tumeshuhudia mechi nyingine tafu kwa Simba, ukubwa wa Simba umeamua mechi.

2. Singida waliingiia na maneno ya nje ya uwanja kuwa marefa wako upande wa Simba, hii iliwatoa mchezoni mapema.

3. Huenda Jean Charles Ahoua ameanza kuizoea ligi, anacheza kikubwa mno ( nilikua nikiuponda uchezaji wake wa nyuma).

4. Kibu Denis ni msaada mkubwa mno kwa Simba, anashambulia na kukaba.

5. Kumtoa Mohamed Hussein kuliifanya Simba icheze defensive game badala ya offensive, Fadlu asingeepuka lawama kama Singida wangepata goli maana ile sub iliwakaribisha Singida langoni kwa Simba.

6. Metacha Mnata ni moja kati ya magolikipa bora wazawa, sielewi kwanini Yanga walimuacha.

7. Mechi ya leo imedefine Simba inataka nini msimu huu, kuna uwezekano Simba ikatwaa ubingwa wa NBC.

Simba nguvu moja.
8 refa lawi alikuwa upande wa simba.
9 ande koffi ni bonge moja ya fullback
10 kennedy juma leo kazima fresh sana
11 simba bado wapo weak kwente transition....makosa yaliyo sababisha 5-1 bado yapo. Kocha ayafanyie kazi.
 
Hapana Marefa wanaharibu Sana mpira, Inawaharia ata kupata nafasi za kuchezesha mechi za Mashindano makubwa.
Hawa jamaa wanavyocheza kwa kutegemea marefa na ushindi wao wa goli Moja Moja natamani sana mechi yao na yanga ifike ata wao na Azam utakuja kuona makosa yao vizuri,,hizo mechi kwa uchezaji wao huu awatotoboa kwa maana wanafanya pressing kukabia juu wakati huo awako vizuri kwenye defence line yao,,angalia nafasi 2 alizopata Rupia akashindwa kuzitumia ilitokana na wao kujaa juu na kuacha nafasi eneo lao la ulinzi,,pia angalia aina ya magori yao,,wamefunga magori 5 kwenye mechi tofauti ndani ya kipindi cha kwanza na kipindi cha pili wanakuwa pumzi imekata,,sasa uwezi kucheza na yanga kwa au Azam ya sasa kwa dizaini iyo maana awatokupa nafasi kuanzia dk ya kwanza mpaka sekunde ya mwisho na yale magori ya papatu papatu utoweza kupata hizo nafasi!
 
Ni Tanzania pekee timu inaongoza Ligi uku marefa wanao chezesha mechi zake wakitoka na aibu na kudhallika kwa upendeleo.
Maguvu yote ayo mnayotumia si mngewekeza kwenye usajili wa wachezaji wazuri!!
Sasa marefa wanadhalilika na Ubingwa hamchukui si inakua kazi Bure.😄😄
 
8 refa lawi alikuwa upande wa simba.
9 ande koffi ni bonge moja ya fullback
10 kennedy juma leo kazima fresh sana
11 simba bado wapo weak kwente transition....makosa yaliyo sababisha 5-1 bado yapo. Kocha ayafanyie kazi.
Ni timu gani imeibuka na ushindi?
 
Back
Top Bottom