Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabisa ndugu,Mungu yupo sema tu kushupaza shingo
Kwahiyo wewe unakiri MUNGU HAYUPO, sindio?Kama kila kitu sio lazima kiwe na chanzo basi hata ulimwengu hauna chanzo
Kama unakubali akili zetu haziwezi kufikiria kwa usahihi kwasababu ziko limited, utajuaje kuwa hata hilo wazo la kusema muumbaji wa ulimwengu ni Mungu sio muendelezo ule ule wa kufikiria majibu yasio sahihi?
Kabla ya kusema kumuamini Mungu hapo unakuwa umeruka vipengele baadhi ambavyo havijaonesha namna gani umefika hapo
Umejuaje kuna Mungu ambaye anapaswa kuaminiwa?
Ni akili ipi uliyoitumia kujua hilo?
Katika maswali yako uliyojiuliza kuhusu hatma ya ulimwengu nakujibu kwa kukupa maswali zaidi
Hapa nachukua upande wa dini ambao najua wengi ndio mnasimamia
Dini zimesema hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na ardhi
Kumbuka huo ni mwanzo, unaweza kujiuliza kabla ya mwanzo kulikuwaje?
Kama mwanzo umeanza na Mungu kuumba mbingu na ardhi, je huo sio mwanzo wa uwepo wa Mungu pia?
Kama Mungu alikuwepo kabla basi huo sio mwanzo
Lakini utajiuliza tena alikuwa akiishi wapi maana mbingu na ardhi kaviumba leo ambayo ndio mwanzo, na yeye wansema ni wamilele. Alikuwa akiishi wapi?
Haya huko pia alipokuwa akiishi kuliumbwa na nani?
Na kama kulikuwa kuna sehemu anaishi bado tu hii ya ulimwengu na ardhi itaendelea kuhesabika kama mwanzo?
Au tuseme ni mwanzo wa uumbaji na tukubaliane kwamba hakukuwa na uimbaji mwingine uliotangulia kabla ya huo?
Hapo kuna maswali mengi magumu naomba tupaache tuelekee section ya pili na huwezi kukuta pastor ana hubiri hoja tata kama hizo
Haya tujiulize mazingira ya uumbaji yalivyofanyika
Mfano leo hii ukitaka kuchimba shimo lazima utaanzia juu ya ardhi, nikiwa na maana kwamba utasimama ukiwa hapo na likikamilika utaweza kuingia ndani
Leo hii ukimkuta mtu yupo shimoni baada ya kuchimba shimo itakuwa ni rahisi kufikiria kuwa kabla ya kuingia shimoni kulikuwa na ardhi ambayo iko level ambapo hapo ndio alisimama akachimba mpaka kutengeneza shimo
Sasa Mungu aliumba ulimwengu akiwa wapi?
Huwezi kufikiria aliumba ulimwengu akiwa ndani ya ulimwengu kwasababu itaonekana hapo anaufanyia repair kwa maana ya kwamba ulikwisha jengwa
Wewe inabidi ueleweshwe, China kuotesha mmea angani sio issue ni kitu common sana ,science experiments nyingi zinakuwa na matokeo ya haraka na uhakika zikifanyika sehemu yenye gravity ndogo ndio maana wenzetu wana space station ambako kazi yake kubwa ni kufanya hizo experiments, space station ina cost billions of dollars kila mwaka unafikiri yale ni mapambo? vitu vingi sana kwenye agriculture, medicine, technology etc vimegunduliwa kutokana na hiyo space stationNilipongeze shirika la Anga la Russia kwa kufungua njia hao wengineo ni kama harusi hawakosekaniki wasindikizaji.
Katika tafiti zao wanafika mahala wanaamini yupo mwenye vyake.
China juzi kati kaotesha mimea huko angani kaja ipanda duniani tujiulize kwa nini aioteshee huko?
Kuna mahala nilisoma mti uloteremshwa na malaika wengi 99 ni mwarobaini.
KM ni hivo basi Ulimwengu woote!! including weye, wana sayansi, Rais wako, waalimu wako nk! ni wajinga kwa sababu wanaogopa siraha za USA/Russia!....km siyo Mujinga jaribu uone moto!!....Vitisho ni silaha ya mwisho ya mjinga
Tofauti ni kuwa yule mtoto anaye enda shule kwa kuogopa viboko bila kuhoji uhalali wa viboko, ni Mjinga, Muoga, mnafiki wa kesho, hafai, siyo mdadisi, viboko ni siraha ya kukuza udadisi wa mtoto, kitaaluma!.......Huna tofauti na mtoto anayeenda shule kwa hofu ya viboko.
amaepata nguvu za ziada kutoka kwa roho mtaka tifuUmesema akili ya kawaida haiwezi kutambua, vipi kama hata swala lako la kusema Mungu yupo sio majibu potofu ya akili yako?
Hiyo nguvu ameitambuaje na kujua ni roho mtakatifu na sio kama anapitia paranoia tu?amaepata nguvu za ziada kutoka kwa roho mtaka tifu
''Imani si mali ya kila Mtu!'' Paranoia ni jibu rahisi kwa swali tata! utazunguka weee! lkn hutapata jibu rahisi ivo!Hiyo nguvu ameitambuaje na kujua ni roho mtakatifu na sio kama anapitia paranoia tu?
Hayo manyota makubwa yazinidi kua formed mpaka leo... yani nyota zinazaliwa na kufa. Mfano hili jua letu (likiwa nalo ni nyota) linategemewa kufa baada ya miaka billion tano. Makadirio haya yanafanywa kwa kuangalia nyota nyingine zenye mfanano na jua. Mpaka sasa bado ziko nyota zinazidi kutengenezwa na bado ziko nyota zinazidi kufa.Dunia imebadilikia, utandawazi unatukutanisha na watu mbalimbali duniani. Fikra mpya, filosofia na elimu inatujuza mitazamo ya watu mbalimbali katika Historia na hata ulimwengu tulio nao.
Moja kwa moja niende kuelezea kwanini naamini uwepo wa Mungu kwa kutumia hoja za kisayansi zenye kufikirika na hoja za kiroho (kihisia)
HOJA ZA KIULIMWENGU
kwa kuuangalia ulimwengu jinsi ulivyoumbwa basi ni alama tosha ya kuthibisha uwepo wa Mungu.
Sayari, nyota, nebula, Galaksi, mashimo meusi (black holes), miezi, magimba na vyengine vingi.
Nikijaribu kusoma ulimwengu, basi nafsi yangu inaniambia kabisa kuwa Kuna muumba wa vitu vyote hivi. Hivi ni kweli nyota kubwa kubwa Kama Stephenson 2-18, Betelgause, Rigel, Sirius A na nyengine, Nebula kama Carina nebula, Orion nebula, Helix nebula na nyengine nyingi, havina mtengenezaji? Hivi ni kweli vitu vyote hivi vimetokea kwa bahati nasibu?
View attachment 2301621
View attachment 2301612
Ulimwengu ni mkubwa na umeumbwa kwa namna ya kushangaza sana. Mnapo tarehe 11 julai 2022, shirika la utafiti wa anga la Marekani NASA kwa kutumia darubini ya James Webb limeweza kupiga picha za mbali kabisa, wanasayansi wanahuita ukingo wa ulimwengu (edge of the observable universe). Kwakweli picha hizo ni zenye kupendeza sana. Kilichonistaajabisha sana ni kuwa kuna picha imechukuliwa kutoka umbali wa miaka ya mwanga bilioni 4.5 (4.5 billion light years). Umbali huu ni mrefu sana ambao mwanadamu hawezi akapata picha halisi. Lakini kwa tafsiri yenye kueleweka ni kuwa mwanga umesafiri kutoka huko katika ukingo wa ulimwengu hadi hapa duniani kwa miaka bilioni 4.5 iliyopita na hizo galaksi tunazoziona kwenye picha basi tunaziona jinsi nilivyokuwa miaka bilioni 4.5 iliyopita.
View attachment 2301572
View attachment 2301618
Wanasayansi wanathibitisha ya kuwa ulimwengu wenyekuonekana ni sehemu ndogo tu ya ulimwengu mzima, ni nukta tu ya ulimwengu mzima. Wapo wanaothibitisha ya kuwa Kuna ulimwengu zaidi ya mmoja (multiverse). Hivi kwa uumbaji huu ni kweli hakuna mwenye nguvu zisizo za kawaida ambae ndio katengeneza vyote hivyo?
Uwingi wa nyota, galaksi, nebula na vyengine vingi. Uwingi tu wa vitu hivyo unastaajabisha sana. Hizi vyota tumaziona ni nyota chache tu kati ya nyota nyingi katika galaksi yetu yaani milky way. Inakadiliwa kuwa Kuna nyota bilioni 100 hadi 400 katika galaksi yetu yaani milky way. Ni nyota nyingi ambazo kama ungeweza kuziangalia kutoka katika umbali fulani basi ungepata picha halisi. Sasa hii ni galaksi moja na wanasayansi wanakadiria pia kuwa kuna takribani galaksi bilioni 100 hadi 200 katika ulimwengu unaoonekana. Na huu ulimwengu wenyekuonekana ni sehemu tu ya ulimwengu mzima, je Kuna vitu vingapi katika ulimwengu usiooneka?
View attachment 2301578
View attachment 2301583
Mifumo ya kiulimwengu yenye kutulinda wanadamu. Nikiangalia jinsi tabaka la ozoni (ozone layer) inavyotulinda kutokana na mionzi ya UV, mzunguko wa jua na dunia, mwezi na sayari nyengine ambapo Kama vitaenda tofauti basi maisha ya mwanadamu yatakuwa hatarini. Ukitafakari mfumo wa uzungukaji wa maji (water cycle) unaweza ukapata taswira ya kivipi maisha yetu yanategemea huruma ya Mungu. Dunia ingeweza hata kuhama kutoka katika obiti yake. Lakini kuna mlizi wetu ambae halali, anaetupenda.
Kuna magimba makubwa yanayodondoka kila siku, kila saa na dakika, Lakini Mungu kaweka utaratibu wake, magimba hayo huyayuka kabla ya kutufikia binadamu katika uso wa dunia. Ni njia ya Mungu kutulinda binadamu kwani kuna sayari ngapi huangukiwa na magimba hayo.
View attachment 2301584
SABABU ZA KIROHO (KIHISIA)
Kutambua uwepo wa Mungu ni suala la asili ya mwanadamu na viumbe wengine. Tangu tunazaliwa, tunakuwa na utambuzi wa asili juu ya uwepo wa Mungu. Hakuna mtoto ambae haamini uwepo wa Mungu. Ingawa Mungu haonekani lakini mara zote watoto hutaja neno Mungu. Kiasili kila mtu ana schema ya kutambua uwepo wa Mungu lakini mazingira yanaweza yakambadilisha na kuamini kuwa hakuna Mungu.
Mapenzi ya mzazi kwa mtoto, upendo wa mzazi hasa wa mama ni alama ya uwepo wa Mungu. Ukitafakari kwa kina utagundua kuna alieweka mapenzi haya ambae ni Mungu. Na hii si kwa binadamu tu bali hata kwa wanyama pia. Mzazi yuko tayari kuhatarisha uhai wake ili awalinde watoto wake, ona kuku anavyowalinda vifaranga vyake dhidi ya mwewe, nyoka na wanyama wengine. .
Utofauti wa binadamu na wanyama wengine. Hapa najiuliza kwanini binadamu tunavaa nguo, tunasoma elimu mbalimbali, tuna majumba mazuri, teknolojia, usafiri wa anga na kila kitu kizuri, Kila leo binadamu hubadilika na kugundua vitu vipya, mitindo mipya ya mavazi, nyumba na magari hubadilika pia. Maisha ya viumbe wengine yapo hivyo hivyo miaka nenda, miaka rudi. Si ajabu kabisa kuku kumpanda mama yake, kujamiiana kwao huwa ni sehemu yoyote. Binadamu tunahifadhi hadi kinyesi chetu, lakini wanyama hawana utaratibu huo. Ni jambo gumu kwa binadamu kumla binadamu mwenzake lakini leo ukichinja kuku nyumbani kwako basi mabaki ya nyama hiyo unawatupia kuku wengine. Hivi binadamu kuwa na utambuzi, fikra, akili, uwezo kwa kupanga na kuamua umekuja kwa bahati nasibu au ni Mungu ndio kapanga iwe hivyo?
Mifumo ya mwili na jinsi inavyofanya kazi. Hakika binadamu na wanyama wengine wameumbwa katika namna tata sana. Ona Kuna mfumo wa chakula, mfumo wa hewa, mfumo wa utoaji taka mwili, mfumo wa Neva, mfumo wa mzunguko wa damu na mifumo mingine mingi. Mungu amempa Mwanaamu changamoto ya kuumba hata sisimizi na kamwe hataweza.
NI IPI HASARA YA KUTOAMINI MUNGU?
Mbali na hasara kuu ambayo mtu ataipata siku ya malipo kwa kutoamini kwakwe, pia kuna hasara nyingi ambazo zinaitesa dunia ya leo kutokana na upingaji huu.
Kutoamini Mungu kunaondoa utu, mtu ambae haamini Mungu anaweza akaingia katika matendo ambayo hayatamtofautisha yeye na mnyama. Kama tulivyoona awali kuwa mnyama na binadamu ni tofauti basi mtu ambae haamini uwepo wa Mungu anaweza akakaribiana kimatendo na mnyama.
Mambo yafuatayo yamesababishwa kwa kiasi kikubwa na kuto kuwa na imani ya Mungu
i. Filamu za ngono, matamasha ya kutembea utupu na mfano wa hayo.
Dunia leo inashuhudia kilele cha maovu ya mwanadamu. Kuna maelfu kwa malaki ya waigizaji wa filamu za ngono tena kwa namna tofauti.
ii. Kukua kwa matendo ya ushoga, usagaji na kuwekewa kampeni maalumu ili kukuza vitendo hivyo.
iii. Ujambazi, ukatili, mauwaji na maovu mengine. Jamii ambayo watu wake hawaamini Mungu basi ni rahisi sana kuangukia katika dunia yenye migogoro kuuwana na ukatili wa aina zote.
Ili tuijenge jamii yenye ustawi mzuri, maadili mema, ukuaji uchumi na hatimae maendeleo endelevu basi tusimsahau Mungu wetu.
ELIMU, KAZI NA SALA
Sayansi imejibu 10% tu ya maswali? Hapana... labda kama ni vinginevyo, dini ndo imejibu 10%, ambapo pia hata izo 10% zimethibitishwa kua sio ukweli, na kuna sababu za kwamba sio kweliKiyasansi Mungu hayupo. Lakini kwa elimu zingine zinathibitisha Mungu yupo.
Sayansi haina uwezo wa kujibu KILA kitu, hadi SAsa imejibu asilimia 10 tu ya mambo yaliyopo. 90 ya mambo imeshindwa yamejibiwa na elimu zingine.
1.Sayansi haina majibu kuhusu maisha ya ulimwengu usioonekana.Sayansi imejibu 10% tu ya maswali? Hapana... labda kama ni vinginevyo, dini ndo imejibu 10%, ambapo pia hata izo 10% zimethibitishwa kua sio ukweli, na kuna sababu za kwamba sio kweli
Baadhi ya maswali yaliojibiwa na elimu ya sayansi (na hayajajibiwa na elimu nyingine, kama unavosema);
1. Kwanini anga linaonekana lina rangu ya blue ukiwa ndani ya dunia
2. Kuna viumbw vya aina ngapi (at species level)
3. Namna sayari zinavotengenezeka
4. Kwanini ukiruka unarudi chini
5. Kwanini baadhi ya viumbe vilitoweka. Mfano tuseme, dinosaurs.
6. Nini kinafanya kuepo kuna usiku na mchana
7. Mvua inatokea wapi
8. Umbali wa mwezi kutoka dunian
9. Kwanini tunaugua, na dawa zinatibu vipi
10. Na hili la mwisho, popo ni mnyama au ndege? [emoji16]
Ukiangalia haya maswali yote, either kidini hayana majibu au yamejibiwa lakini ukienda kiuhalisia unaona kabisa tumepigwa...
Lengo la dini si kuelezea Mambo ya kisayansi, lengo kubwa la dini ni kumuelekeza binadamu namna ya kuishi na watu wengine. ingawa Kuna Mambo kadhaa ya kisayansi yapo katika vitabu vya dini ila wewe kwa kuwa mbali na dini ndio maana hata hufahamu.Sayansi imejibu 10% tu ya maswali? Hapana... labda kama ni vinginevyo, dini ndo imejibu 10%, ambapo pia hata izo 10% zimethibitishwa kua sio ukweli, na kuna sababu za kwamba sio kweli
Baadhi ya maswali yaliojibiwa na elimu ya sayansi (na hayajajibiwa na elimu nyingine, kama unavosema);
1. Kwanini anga linaonekana lina rangu ya blue ukiwa ndani ya dunia
2. Kuna viumbw vya aina ngapi (at species level)
3. Namna sayari zinavotengenezeka
4. Kwanini ukiruka unarudi chini
5. Kwanini baadhi ya viumbe vilitoweka. Mfano tuseme, dinosaurs.
6. Nini kinafanya kuepo kuna usiku na mchana
7. Mvua inatokea wapi
8. Umbali wa mwezi kutoka dunian
9. Kwanini tunaugua, na dawa zinatibu vipi
10. Na hili la mwisho, popo ni mnyama au ndege? [emoji16]
Ukiangalia haya maswali yote, either kidini hayana majibu au yamejibiwa lakini ukienda kiuhalisia unaona kabisa tumepigwa...
1.Sayansi haina majibu kuhusu maisha ya ulimwengu usioonekana.
2.Kuhusu Ndoto
3.Nguvu ya mawazo
4.Roho
5.Maisha baada ya kifo
6.Viumbe vilivyopo katika sayari zingine
7.Asili ya mwanadamu
8.Nini asili ya chuki, wivu, hasira, wema, upendo,
9.Sayansi haina majibu juu ya Mungu ni nani na Shetani ni nani plus viwango vyao vya kuzidiana nguvu
10.Sayansi haiwezi dhibiti uchawi
KILA tatizo ujibiwa kwa elimu yake
Bado sana naona umejifungia kwenye box la kutegemea only sayansi ya darasani ndio KILA kitu.1. Hakuna ushaidi wowote kuhusu ulimwengu usionekana wala huwezi kuleta ushahidi wowote ivo basi kisayansi hakuna kitu kama ulimwengu usioonekana.
2. Sayansi inamajibu kuhusu ndoto
3. "Nguvi ya mawazo" unamaana gani kusema ivo? Ukiwa na msongo wa mawazo unajirisk kupata matatizo ya akili...
4. Roho? Hakuna uwezekano wa kuprove existence ya roho, ivo hakuna kitu kama roho
5. Hakuna maisha baada ya kifo
6. Viumbe vilivo katika sayari nyingine havijagunduliwa. Kama vipo, vipi sayari gani? Itakua rahisi kuprove uwepo wao...
7. Asili ya mwanadamu, kuna theories nyingi zinazo suggest asili yetu. Uumbaji ikiwa far off from the truth...
8. Chuki, wivu, hasira, upendo? Hivi vitu vinategemea sana na jinsi mtu alivokizwa toka utotoni, mazingira aliopo na vitu kama ivo
9. Sayansi haiamini katika mungu, muumba wa ulimwengu wote. Inategemea unadefine vipi neno "mungu"
10. Kwenye uchawi tumepigwa, hamna kitu kama icho[emoji38]
Sayansi ina majibu. Sayansi ipo kwaajili ya kutafuta majibu. Ww ndio umejifungia kwenye box... nilishawahi kua muamini. Ila kwenye dini fix tu zimejaa. Nimesoma biblia yote, ninesoma baadhi ya aya za quran. Hamna kitu humo...Bado sana naona umejifungia kwenye box la kutegemea only sayansi ya darasani ndio KILA kitu.
Roho ndio inayoongoza MWILI inaongoza vipi sayansi haitokupa jibu
Hizo elimu zingine zimekuwepo kabla ya sayansi.Vipi kuhusu nguvu za asili mfano negative na positive energy na jinsi zinavyoathiri watu je sayansi inayo majibu?Sayansi ina majibu. Sayansi ipo kwaajili ya kutafuta majibu. Ww ndio umejifungia kwenye box... nilishawahi kua muamini. Ila kwenye dini fix tu zimejaa. Nimesoma biblia yote, ninesoma baadhi ya aya za quran. Hamna kitu humo...