Machache yanayonifanya niamini uwepo wa Mungu: Hatari ya kuamini hakuna Mungu

Utakuwa una matatizo ya uelewa


Hivi ni mimi ndiye ninayo matatizo ya uelewa au ni wewe??.

Hebu angalia kwa makini; "kiti cha enzi", maneno hayo matatu yanawakilisha hadhi, wadhifa, utukufu, heshima, utawala nk wa mtu husika na kwa kiarabu ndio ARSHI na kwa kizungu ndio Throne, wewe unadai "kiti cha enzi" ni kiti HALISI, kiti halisi kwa kiarabu ni kursiyyu na kwa kimombo ni chair, sasa inatakiwa kuanzia leo ujue kuwa maneno; kiti cha enzi yanawakilisha sifa tajwa na hakuna kitu TANGIBLE kinaitwa "KITI CHA ENZI" katika muktadha huo.

Ajabu ni kwamba unajadili kitu cha mtu ulichokiunda physically mawazoni mwako "mtu"ambaye kwako wewe hayupo wala hajapata kuwepo, kwako ilikuwa ni just simple useme kwamba kwakuwa mtu huyo hayupo hata kujadili kitu kinachosemwa kuwa ni mali yake haijuzu kwakuwa mtu huyo hayupo wala hajapata kuwepo, yaani unajadili mbeleko ya mtoto "hewa" ambaye hata mimba haipo!!!, naam unayo haki ya kujadili lakini jadili katika context iliyokuwa sahihi kwamba kiti cha enzi sio kiti kama sofa, stool au mbuzi ya kukunia nazi tunazotumia katika shughuli zetu za kawaida. Ni kwamba wewe unadai kiti cha enzi ni physical chair na sio Throne ili tu ujipatie hoja ya kukanusha uwepo wa Mungu.

Sasa hapo ni nani mwenye uelewa hafifu??

Kumbuka "kiti cha enzi" pia ni jina la sifa na sio jina la kitu katika huo muktafha.
 
Hivi maana ya kuketi nini?

Refer hii #"ameketi kwenye kiti cha enzi"#
 
Hivi maana ya kuketi nini?

Refer hii #"ameketi kwenye kiti cha enzi"#


Hivi kutupa macho mbele ni nini??--- unaposema; nimetupa macho mbele, unamaanisha kitu gani??.

Ukipata jibu la swali hilo bila shaka utakuwa umepata jibu la swali lako.

NB; Misemo hiyo inaitwa thamathali za Lugha ( figure of speeches).
 
Hoja yangu haipo katika maneno hayo matatu "kiti cha enzi"

Hoja yangu ipo kwenye sentesi kamili "ameketi kwenye kiti cha enzi"

Lakini nimekuambia swala hilo ni kitendo cha kukaa kutokana na kwamba huyu Mungu ameelezwa sehemu tofauti tofauti zinazo thibitisha yuko physically

Mfano katika uumbaji, huyu Mungu alikuwa ana tamka kitu fulani kiwe na kina kuwa.

Hapo ni mdomo ulikuwa unatumika, hakuna namna unaweza kutafuta maneno ya kuunga useme haikumaanisha hivyo

Kwenye stori hiyo hiyo ya uumbaji alipofika hatua ya kumuumba mtu alichukua udongo kwa mikono yake mwenyewe kisha akaufinyanga na baada ya kukamilisha akaupulizia pumzi.

Hivyo vyote ni vitendo physically vinavyoonesha Mungu ana mdomo na mikono aliyotumia kufinyangia udongo.

Na ndio maana baada ya kukamilisha uumbaji wa mtu akasema amemuumba kwa mfano wake.
 

Unacho kiwaza mm niliwaza tu hii space nafas nan aliitengeneza na kama
Mungu yeye alikaa wapi kama nafasi haikuwepo kulipia kuna vitu gan
 

[emoji23][emoji23][emoji23] unachekesha mkristu akisema mungu wake ana mwana utampinga sana

Hii nafas au space iliumbwa na nan na b4 kulikua na nn wana sayansi wamesema chanzo cha haya mabara iyo big bang theory
Tuseme haya maisha yametokea tu bila mtu kutia mkono wake
 
Kiyasansi Mungu hayupo. Lakini kwa elimu zingine zinathibitisha Mungu yupo.
Sayansi haina uwezo wa kujibu KILA kitu, hadi SAsa imejibu asilimia 10 tu ya mambo yaliyopo. 90 ya mambo imeshindwa yamejibiwa na elimu zingine.

Mfano yapi 90% science haijajibu?
 

Scars we bro n genius aiSee tunaomba kitabu please sjawah kuwaza ilo jambo walivo sem sku saba alt jua wala mwez havikuwepo aisee
 
Kama Qur'an isingeandika baadhi ya aya zake katika muundo wa tamathali hiyo Qur'an nadhani ingekuwa na uzito wa zaidi ya tani kumi.

Thamathali makes a person use his/her mental power thus exercises his brain apart from gaining desired lessons.

[emoji43]‍[emoji94][emoji43]‍[emoji94][emoji43]‍[emoji94][emoji23][emoji23] tan kumi duuh
 


Usiingie kwenye mada mpya ya uumbaji wa Mungu na "mdomo" na "mikono" yake japo hata katika hilo hoja yako haina mashiko, kwanza tubaki kwenye "kuketi kwenye kiti cha enzi".

Hebu chukua msemo huu maarufu wa kiswahili; "Tupa macho mbele" je huu msemo maana yake ni angalia mbele au ng'oa macho yako kutoka hapo yalipo na uyatupe mbele yako??!-- bila shaka utakubaliana na mimi kwamba kutupa macho mbele ni kuangalia mbele, au mfano inaposemwa kiongozi fulani kasimikwa au katawazwa je maana yake kasimikwa ardhini kama mti au katawazwa kasafishwa mwili wake!!??--- kusimikwa au kutawazwa ni kupewa wadhifa au majukumu nk, ni hivyo hivyo kuketi kwenye kiti cha enzi maana yake ni "kuchukua mamlaka, madaraka, jukumu nk, kinyume chake ni kuondoshwa au kuondoka madarakani (dethroned), Vyovyote utakavyo yaweka hayo maneno maana yake ni hiyohiyo ya kupata madaraka, wadhifa, majukumu ya kiutawala nk, ama useme; kukaa juu ya kiti cha enzi, kukaa kwenye kiti cha enzi au kuketi katika kiti cha enzi yote hayo maneno yana maana moja, hebu chukua mfano huu hai wakati spika wa bunge letu mara kadhaa mbunge anapopingana naye yeye husema kumwambia mbunge: "mbona unabishana na kiti !!" Je inawezekana kidhahiri mbunge akabishana na kiti anachokalia spika??
hapa kubishana na kiti ni kubishana na mamlaka ya spika na si vinginevyo na hizo ndizo (figure of speeches).

Kumbuka Mungu ni spirit hivyo anayo staili yake ya kutupasha habari sisi physical beings.

Narudia tena, katika Qur'an kuna aya za aina mbili, kwanza zilizo straightforward katika maana na zile zilizo implicit katika maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…