Machache yanayonifanya niamini uwepo wa Mungu: Hatari ya kuamini hakuna Mungu

Machache yanayonifanya niamini uwepo wa Mungu: Hatari ya kuamini hakuna Mungu

Kutokuamini Mungu hakunifanyi nishindwe kujadili yaliyomo ndani yake kwa muktafha wa ku switch a side niweze kuelewana na mnao amini.

Naweza nikakusahihisha hadi kwenye habari iliyoandikwa katika kitabu cha darasa la tatu kumzungumzia pazi.

Ukisema Pazi alibebwa na kuku jike kichwa chini miguu juu, wakati habari yenyewe halisia imesema ni jogoo mi nitakupinga na kukusahihisha richa ya kwamba sikubaliani na uhalisia wa habari hiyo.

Mara ngapi humu umekuwa uki argue na wakristo kwenye imani ambayo we huiamini?

Ukisema Quran imetaja mbawa kwa maana hiyo ambayo wewe unaiandika hapa, mimi ili nikubaliane na hoja yako nataka hayo maelezo yatolewe na Quran yenyewe na sio mdomoni mwako.

Vinginevyo hiyo itakuwa ni conspiracy ya kuunga unga maneno ili kutafuta maana ambayo wewe umeikusudia na ndio chanzo cha dini nyingi kuwa na madhehebu mengi.

Mfano swala la Eva kuka tunda la mti wa kati, watu wameliwekea code wamelitengenezea conspiracy wengine wakidai kuwa tunda la kati ni sex, wengine wanasema ni sex ila ile ya kinyume na maumbile.

Lakini hayo maelezo hayatoki ndani ya vitabu ni watu tu kama wachambuzi wa mpira wanavyotofautiana kimtazamo ndivyo ilivyo hata kwa situation hii.

Hiyo hadithi ya Pazi inakushika wewe mwenyewe, mimi katika suala la kiti cha enzi cha Mungu (throne) sikuzungumzia juu ya usahihi wa habari ya hicho kiti bali nimezungumzia juu ya falsafa ya kiti chenyewe na nikasema hicho kiti maana yake ni utukufu, power nk za Mungu na sio kiti halisia kama viti vya kukalia wanadamu, huo mfano wako wa jogoo na Pazi unaunga mkono hicho ninachokisema kwamba hadithi hiyo ni metaphor/parable na inahitaji tafsiri ili upate maana yake kama jinsi utahitaji tafsiri kupata maana ya kiti cha enzi cha Mungu, kiti cha enzi kwa kizungu ni (throne) na mfalme au mtawala akiondolewa katika ufalme au utawala wake neno linalotumika ni (dethroned) hivyo utaona kiti cha enzi (throne) HASA kinawakilisha utawala, utukufu nk, kwani kiuhalisia hakuna kiti cha kawaida kinachoweza kumbeba Mungu jinsi isivyokuwa kawaida Jogoo kumbeba mtu, nashukuru kuleta hiyo hadithi ya Pazi.🤣🤣.

Unataka maelezo yangu uyapate kutoka kwenye Qur'an!!!, je ukiyapata ndipo utaamini uwepo wa Mungu??!!. ----Katika Qur'an Wapinzani wa mtume (saw) walimwambia mtume kwamba hawatamuamini hadi apande mbinguni na awaletee kitabu kutoka huko ili wakisome na sio hii Qur'an, Mungu akamwambia awaambie; "Mtukufu ni mola wangu mimi siye ila ni mtu na mtume"., hivyo madai yako ya kutaka maelezo yote yatoke ndani ya Qur'an ni madai yale yale ya Wapinzani na hata kama madai hayo yangetekelezwa bado ungetafuta madai mengine mapya. Kifupi ni kwamba; "Laa yumasuhu illa mutaharuun" yaani huwezi kushika/kupata maana za ndani za Qur'an bila kujitakasa, kutakasika au kuomba utakaswe.

Kumbuka akili zetu ndio nyenzo alizotupatia Mungu na usijisikie interior kujifunza kitu kipya chenye faida kutoka kwa mtu mnayepingana kimawazo.
 
Unafurahisha sana. Hivi unajua mwezi Ni kitu kilicho karibu Sana na dunia, alaf unazungumzia kwenda kuchunguza uwepo wa Mungu kwenye mwezi, are you serious? Alaf kama hujamuona Mungu kwenye mwezi ndio ukaconclude kuwa hakuna Mungu. Hivi unafahamu ukubwa wa hii universe. Ngoja nikuache Kwanza maana unaniletea utoto
Universe ni kubwa na still inazidi kutanuka na inatanuka kwa spidi ya mwanga... aya mungu yukowapi kwenye hii universe yote? Kuna viumbe kwenye sayari nyingine yyte mbali na dunia? Kama wapo, ni kwenye sayari gani? Kama hawapo ni kwanini, kwanini huyo mungu kaumba universe yote hii na kaweka kife duniani tu?Nataka kuona dini ikijibu maswali haya..
 
Hapa nakupinga kidogo

Sayansi inafanya utafiti wa nature nikiwa na maana ya kwamba ulimwengu ambao unaweza ukautafiti.

Nature inahusisha vitu kama bacteria, maisha ya wanyama, bahari, mwezi, jua, sayari, viumbe hai na visivyo hai.

Sayansi haidili na Supernatural kwasabu ni vitu ambavyo vinakubalika katika misingi ya kiimani pekee.

Mafano majini, mapepo, nafsi, roho, wachawi, malaika, nyoka anayeongea, farasi mwenye mbawa anayepaa kwa kasi kuelekea mbinguni, mtu aliyelisha maelfu ya watu kwa mikate miwili ma samaki watano aliyo i extend kwa maombi nk.

Unafikiri sayansi itaanzia wapi hapo kufanya utafiti ili kuprove habari hizo?

Unatka Sayansi iingie porini kuthibitisha uchawi?

Kinachoitwa uchawi kisayansi hizo ni trics zinaweza kufundishwa na kuwa perfomed na mtu yeyote bila kuhusisha dhana ya super natural power.

Mfano mzuri ni mwanafizikia mmoja na mtu aliyekuwa mwana mazingaombwe (magician) aliitwa James Randi.

James Randi alikuwa mtu maarufu sana kwa ishu za kuperform hii miujiza mpaka watu wakawa wanamuona mchawi.

Lakini huwezi amini, Randi aliwahi kutoa dollar zaidi ya milion kwa yeyote atakayeweza kuthibitisha uchawi upo kwa kuperform bila kutumia tricks yani atumie super natural power lakini challenge ilichukua miaka zaidi ya 50 hakuna aliyewahi ku prove mpaka pale alipoamua ku terminate shindano.

Mkuu

Sayansi haihusiki na hayo mambo na yenyewe inafanya tafiti zake binafsi sio kwa ajili ya kuangalia vitabu vya dini vimesemaje.

Ila pale inapotokea kuna jambo ambalo lina telate na habari za vitabu vya dini ndio utaona hapo conspiracy zinavyoaanza.

Mfano kabla ya Sayansi kufanya utafiti wa bing bang, hakuna dini yeyote iliyowahi kutoa claims kuwa ulimwengu unatanuka na kwamba ulikuwa kwenye single point.

Ila mpaka pale ambapo sayansi ikaja na utafiti wake ndipo modern scholars wa hizi dini walipoibuka na hoja zao wakidai hizo habari zilielezwa kwenye vitabu vyao na wakionesha verse ambazo ni irrelevant na kile kilichoelezwa na Sayansi.

Watu hawa ndio wakawa wanasema Sayansi inatumia vitabu vyao kufanya tafiti.

Na saizi naona limetengenezwa hadi kundi la watu la kuhusianisha habari za Mungu na Sayansi vionekane ni vitu ambavyo vinaenda sambamba.

Kama umesikia theory ya intelligent design hiyo pia imetengenezwa na kundi hilo la watu ambapo wanadai hiyo intelligent design ni hoja ya kisayansi lakini hiyo ni pseudoscience.
Hapana bro, sijamaanisha kwamba sayansi ina project zinazolenga kumtafuta mungu. Bali kuna lile swali la "what's the origin of the universe?" Na hapa theory ya creation ILIKUA considered... ila kwa bahati mbaya tunazidi kupata sababu tu zaidi za kua hamna creator wa universe. Ndio maana sasaivi utasikia watu wanakwambia maandiko usiyachukulie literally [emoji23]
 
We jamaa hamna kitu kabisa, hivi unajua serikali kama ya USA, China, Russia nk zinapoteza kiasi gani cha pesa kuchunguza tu anga. Juzi tu hapa JWST imepiga picha kutoka sehemu ya mbali zaidi unaweza kuniambia zile picha zina faida gani na Wanapoteza a lot of money.

Sijui hata unazungumza Nini unavyosema Harry Potter na spider Man na wanahusika vip na kufanyiwa utafiti, labda Mimi sijui? Anyway labda Mimi mjinga wa hilo?

Acha kukaza shingo, sio kila inapozungumziwa miaka katika Bible basi inazungumziwa miaka ya namna fulani, be flexible kuna muda inatumika miaka ya kawaida na Kuna muda inatumika ambayo sio hii tulionayo. Nimetoa mfano mzuri tu kuwa ili kuwe na siku na hatimae wiki, mwezi na mwaka lazma rotation ya dunia katika axis yake itokee, Sasa kipindi dunia bado haipo je kulitumika kigezo gani kupata mwaka mmoja? Je, huo muda ukiuringanisha na miaka ya kawaida utapata miaka mingapi?

Kwa mfano wa Nabii Musa ni rahisi sana kuwa huenda kuna namna ambayo iliwafanya kutumia muda huo kutembea. It is very simple. Ni Kama unavyowaona hawa wairak, wanyaturu au wamasai walivyotumia miaka mingi kufika Tanzania kutoka Western Asia. Hivi unajua Nabii musa alizitumia siku 40 kuomba mrimani. haikuwa ni kitembea tu ni Kama unavyoona wanavyofanya hawa normadic pastoralists, wanaweza kutumia muda wowote kutembea kwakua wanatembea na kuanzisha makazi then baada ya muda wanahama. Hivi unatumia Nini kufikirika? Utumbo Mpana?
Ona sasa... eti space exploration ni waste of money! Hapana, hii ndo inasaidia kujua mahala tulipo katika universe kuelewa muundo wa universe, na hata kupata idea universe iliundwaje, since... well ...we can't trust your gods.

Na pia siunaelewa kua jua lita ingia stage ya red giant in a few billion yrs to come? Hizi exploration zinasaidia kutafuta mbadala wa kuamisha colonization kwenye sayari ingine. Mdg mdg miaka maelfu ijayo huenda sayari habitable ikapatikana. Maybe or maybe not...
 
Subiri kidogo

"The heavens, We have built them with power. And verily, We are expanding it" Qur'an (51:47) {579-632}

Then Hubble in 1920s discovered that the universe is expanding
Kwahiyo heavens=universe? Anhaa sawa...
 
Kwanza hauwezi kuuza nafsi kwa shetani.

Kwasababu hauna hiyo nafsi, umeaminishwa tu kuwa ipo na we ukakubali bila ya hata kuhoji inapatikana eneo gani la mwili wako

Hilo swali hata pastor wako hawezi jibu.

Lakini kingine ambacho unakithibotisha hapa ni kuwa wanao amini Mungu wengi wana amini kwa utumwa

Hawako huru wanafanya hivyo kwasababu ya KUOGOPA.

Heshima inayokuja kwasababu ya mtu kuelewa nini thamani ya heshima ni tofauti na ile heshima inayokuja baada ya vitisho.

Hiyo ni heshima ya WOGA

Mimi siibi sio kwasbabu ya kuogopa polisi, siibi kwasbabu napenda naelewa nini maana ya empathy.

Sipendi kuibiwa, najiweka katika nafsi ya huyo mtu ambaye nataka kumuibia kufikiria ni kiasi gani anaweza kufadhaika na kumrudisha nyuma kimaendeleo najikuta nimeelewa kuwa hilo ni jambo baya na sina haja ya kukifanya.

Mpaka hapo nimeepuka kuiba sio kwasababu ya kuhofia polisi, ni empathy

Aiuwi watu sio kwasbabu nahofia kufungwa hapana ni kwasbabu mimi mwenyewe sipendi niuliwe au mtu yeyote nimpendaye sipendi niskie kauwawa.

Kama upendo wako kwa watu haujazingatia factor hizi basi ni wazi kwamba imani ya uwepo wa Mungu ndio kitu pekee kinachokuepesha usiwe rapist, serial killer, robber nk
Sasa huoni kwamba kuna wakati vitu kama hasira, malipizi ya visasi, chuki vinaweza kumfanya mwanadamu afikirie kuua ila hapohapo unakuta kinachomfanya asifanye hivyo ikawa woga wa kuingia matatizoni, Ila anyway kama ungekuta woga hautakiwi basi kwenye maandiko pasingekuwa na maneno kama "Ole wao" Haya umesema kuna kuheshimu na sio kuogopa Rais ni cheo cha kuheshimika hivyo basi kama tunapaswa kukiheshimu na heshima inafanya tushindwe kufanya baya juu yake basi ni kwanini anawekewa ulinzi.... Sasa ukitaka ujue tofauti ya heshima na woga kajaribu kumsogelea kiholela.... Huwezi kusema unaheshimu kitu bila kuogopa kuvunja heshima.
 
Dunia imebadilikia, utandawazi unatukutanisha na watu mbalimbali duniani. Fikra mpya, filosofia na elimu inatujuza mitazamo ya watu mbalimbali katika Historia na hata ulimwengu tulio nao.

Moja kwa moja niende kuelezea kwanini naamini uwepo wa Mungu kwa kutumia hoja za kisayansi zenye kufikirika na hoja za kiroho (kihisia)

HOJA ZA KIULIMWENGU
kwa kuuangalia ulimwengu jinsi ulivyoumbwa basi ni alama tosha ya kuthibisha uwepo wa Mungu.

Sayari, nyota, nebula, Galaksi, mashimo meusi (black holes), miezi, magimba na vyengine vingi.
Nikijaribu kusoma ulimwengu, basi nafsi yangu inaniambia kabisa kuwa Kuna muumba wa vitu vyote hivi. Hivi ni kweli nyota kubwa kubwa Kama Stephenson 2-18, Betelgause, Rigel, Sirius A na nyengine, Nebula kama Carina nebula, Orion nebula, Helix nebula na nyengine nyingi, havina mtengenezaji? Hivi ni kweli vitu vyote hivi vimetokea kwa bahati nasibu?
View attachment 2301621
View attachment 2301612
Ulimwengu ni mkubwa na umeumbwa kwa namna ya kushangaza sana. Mnapo tarehe 11 julai 2022, shirika la utafiti wa anga la Marekani NASA kwa kutumia darubini ya James Webb limeweza kupiga picha za mbali kabisa, wanasayansi wanahuita ukingo wa ulimwengu (edge of the observable universe). Kwakweli picha hizo ni zenye kupendeza sana. Kilichonistaajabisha sana ni kuwa kuna picha imechukuliwa kutoka umbali wa miaka ya mwanga bilioni 4.5 (4.5 billion light years). Umbali huu ni mrefu sana ambao mwanadamu hawezi akapata picha halisi. Lakini kwa tafsiri yenye kueleweka ni kuwa mwanga umesafiri kutoka huko katika ukingo wa ulimwengu hadi hapa duniani kwa miaka bilioni 4.5 iliyopita na hizo galaksi tunazoziona kwenye picha basi tunaziona jinsi nilivyokuwa miaka bilioni 4.5 iliyopita.
View attachment 2301572
View attachment 2301618
Wanasayansi wanathibitisha ya kuwa ulimwengu wenyekuonekana ni sehemu ndogo tu ya ulimwengu mzima, ni nukta tu ya ulimwengu mzima. Wapo wanaothibitisha ya kuwa Kuna ulimwengu zaidi ya mmoja (multiverse). Hivi kwa uumbaji huu ni kweli hakuna mwenye nguvu zisizo za kawaida ambae ndio katengeneza vyote hivyo?

Uwingi wa nyota, galaksi, nebula na vyengine vingi. Uwingi tu wa vitu hivyo unastaajabisha sana. Hizi vyota tumaziona ni nyota chache tu kati ya nyota nyingi katika galaksi yetu yaani milky way. Inakadiliwa kuwa Kuna nyota bilioni 100 hadi 400 katika galaksi yetu yaani milky way. Ni nyota nyingi ambazo kama ungeweza kuziangalia kutoka katika umbali fulani basi ungepata picha halisi. Sasa hii ni galaksi moja na wanasayansi wanakadiria pia kuwa kuna takribani galaksi bilioni 100 hadi 200 katika ulimwengu unaoonekana. Na huu ulimwengu wenyekuonekana ni sehemu tu ya ulimwengu mzima, je Kuna vitu vingapi katika ulimwengu usiooneka?
View attachment 2301578
View attachment 2301583
Mifumo ya kiulimwengu yenye kutulinda wanadamu. Nikiangalia jinsi tabaka la ozoni (ozone layer) inavyotulinda kutokana na mionzi ya UV, mzunguko wa jua na dunia, mwezi na sayari nyengine ambapo Kama vitaenda tofauti basi maisha ya mwanadamu yatakuwa hatarini. Ukitafakari mfumo wa uzungukaji wa maji (water cycle) unaweza ukapata taswira ya kivipi maisha yetu yanategemea huruma ya Mungu. Dunia ingeweza hata kuhama kutoka katika obiti yake. Lakini kuna mlizi wetu ambae halali, anaetupenda.
Kuna magimba makubwa yanayodondoka kila siku, kila saa na dakika, Lakini Mungu kaweka utaratibu wake, magimba hayo huyayuka kabla ya kutufikia binadamu katika uso wa dunia. Ni njia ya Mungu kutulinda binadamu kwani kuna sayari ngapi huangukiwa na magimba hayo.
View attachment 2301584

SABABU ZA KIROHO (KIHISIA)
Kutambua uwepo wa Mungu ni suala la asili ya mwanadamu na viumbe wengine. Tangu tunazaliwa, tunakuwa na utambuzi wa asili juu ya uwepo wa Mungu. Hakuna mtoto ambae haamini uwepo wa Mungu. Ingawa Mungu haonekani lakini mara zote watoto hutaja neno Mungu. Kiasili kila mtu ana schema ya kutambua uwepo wa Mungu lakini mazingira yanaweza yakambadilisha na kuamini kuwa hakuna Mungu.

Mapenzi ya mzazi kwa mtoto, upendo wa mzazi hasa wa mama ni alama ya uwepo wa Mungu. Ukitafakari kwa kina utagundua kuna alieweka mapenzi haya ambae ni Mungu. Na hii si kwa binadamu tu bali hata kwa wanyama pia. Mzazi yuko tayari kuhatarisha uhai wake ili awalinde watoto wake, ona kuku anavyowalinda vifaranga vyake dhidi ya mwewe, nyoka na wanyama wengine. .

Utofauti wa binadamu na wanyama wengine. Hapa najiuliza kwanini binadamu tunavaa nguo, tunasoma elimu mbalimbali, tuna majumba mazuri, teknolojia, usafiri wa anga na kila kitu kizuri, Kila leo binadamu hubadilika na kugundua vitu vipya, mitindo mipya ya mavazi, nyumba na magari hubadilika pia. Maisha ya viumbe wengine yapo hivyo hivyo miaka nenda, miaka rudi. Si ajabu kabisa kuku kumpanda mama yake, kujamiiana kwao huwa ni sehemu yoyote. Binadamu tunahifadhi hadi kinyesi chetu, lakini wanyama hawana utaratibu huo. Ni jambo gumu kwa binadamu kumla binadamu mwenzake lakini leo ukichinja kuku nyumbani kwako basi mabaki ya nyama hiyo unawatupia kuku wengine. Hivi binadamu kuwa na utambuzi, fikra, akili, uwezo kwa kupanga na kuamua umekuja kwa bahati nasibu au ni Mungu ndio kapanga iwe hivyo?

Mifumo ya mwili na jinsi inavyofanya kazi. Hakika binadamu na wanyama wengine wameumbwa katika namna tata sana. Ona Kuna mfumo wa chakula, mfumo wa hewa, mfumo wa utoaji taka mwili, mfumo wa Neva, mfumo wa mzunguko wa damu na mifumo mingine mingi. Mungu amempa Mwanaamu changamoto ya kuumba hata sisimizi na kamwe hataweza.

NI IPI HASARA YA KUTOAMINI MUNGU?
Mbali na hasara kuu ambayo mtu ataipata siku ya malipo kwa kutoamini kwakwe, pia kuna hasara nyingi ambazo zinaitesa dunia ya leo kutokana na upingaji huu.
Kutoamini Mungu kunaondoa utu, mtu ambae haamini Mungu anaweza akaingia katika matendo ambayo hayatamtofautisha yeye na mnyama. Kama tulivyoona awali kuwa mnyama na binadamu ni tofauti basi mtu ambae haamini uwepo wa Mungu anaweza akakaribiana kimatendo na mnyama.
Mambo yafuatayo yamesababishwa kwa kiasi kikubwa na kuto kuwa na imani ya Mungu

i. Filamu za ngono, matamasha ya kutembea utupu na mfano wa hayo.
Dunia leo inashuhudia kilele cha maovu ya mwanadamu. Kuna maelfu kwa malaki ya waigizaji wa filamu za ngono tena kwa namna tofauti.

ii. Kukua kwa matendo ya ushoga, usagaji na kuwekewa kampeni maalumu ili kukuza vitendo hivyo.

iii. Ujambazi, ukatili, mauwaji na maovu mengine. Jamii ambayo watu wake hawaamini Mungu basi ni rahisi sana kuangukia katika dunia yenye migogoro kuuwana na ukatili wa aina zote.

Ili tuijenge jamii yenye ustawi mzuri, maadili mema, ukuaji uchumi na hatimae maendeleo endelevu basi tusimsahau Mungu wetu.
ELIMU, KAZI NA SALA
Uzi wako umeniongezea kasi ya kumuamini Mungu katika changamoto ninazopitia kwamba kama aliweza kuumba hayo yote basi anaweza kutatua mapito yangu.
 
Hiyo hadithi ya Pazi inakushika wewe mwenyewe, mimi katika suala la kiti cha enzi cha Mungu (throne) sikuzungumzia juu ya usahihi wa habari ya hicho kiti bali nimezungumzia juu ya falsafa ya kiti chenyewe na nikasema hicho kiti maana yake ni utukufu, power nk za Mungu na sio kiti halisia kama viti vya kukalia wanadamu, huo mfano wako wa jogoo na Pazi unaunga mkono hicho ninachokisema kwamba hadithi hiyo ni metaphor/parable na inahitaji tafsiri ili upate maana yake kama jinsi utahitaji tafsiri kupata maana ya kiti cha enzi cha Mungu, kiti cha enzi kwa kizungu ni (throne) na mfalme au mtawala akiondolewa katika ufalme au utawala wake neno linalotumika ni (dethroned) hivyo utaona kiti cha enzi (throne) HASA kinawakilisha utawala, utukufu nk, kwani kiuhalisia hakuna kiti cha kawaida kinachoweza kumbeba Mungu jinsi isivyokuwa kawaida Jogoo kumbeba mtu, nashukuru kuleta hiyo hadithi ya Pazi.🤣🤣.

Unataka maelezo yangu uyapate kutoka kwenye Qur'an!!!, je ukiyapata ndipo utaamini uwepo wa Mungu??!!. ----Katika Qur'an Wapinzani wa mtume (saw) walimwambia mtume kwamba hawatamuamini hadi apande mbinguni na awaletee kitabu kutoka huko ili wakisome na sio hii Qur'an, Mungu akamwambia awaambie; "Mtukufu ni mola wangu mimi siye ila ni mtu na mtume"., hivyo madai yako ya kutaka maelezo yote yatoke ndani ya Qur'an ni madai yale yale ya Wapinzani na hata kama madai hayo yangetekelezwa bado ungetafuta madai mengine mapya. Kifupi ni kwamba; "Laa yumasuhu illa mutaharuun" yaani huwezi kushika/kupata maana za ndani za Qur'an bila kujitakasa, kutakasika au kuomba utakaswe.

Kumbuka akili zetu ndio nyenzo alizotupatia Mungu na usijisikie interior kujifunza kitu kipya chenye faida kutoka kwa mtu mnayepingana kimawazo.
Kuna mambo ambayo hujayaelewa sijui ni kwa bahati mbaya au kusudi.

Kwanza mfano wa Pazi na jogoo niliuweka kuonesha uwezekano wa kujadili stori fulani kama ilivyoandikwa pasipo kukubaliana na uhalisia wake.

Ukiniambia Pazi alibebwa na kuku jike nitakupinga kwasababu umepotosha stori ya mwandishi. Kukupinga huko hakuna maana kwamba nakubaliana na uhalisia wa stori hiyo.

Nataka nijue hiyo falsafa ya kiti umeitoa ndani ya kitabu au ni interpretation yako tu?

Kuuliza kama ukinipa maelezo kutoka ndani ya kitabu yanayoelezea maana ya kiti cha enzi kwa jinsi ulivyodai wewe inakuwa hauna tofauti na mtu anayesema Pazi alibebwa na kuku jike nikamuomba anioneshe hayo maneno ndani ya kitabu afu ye akasema kwani nikikuonesha ndio utaamini kuwa Pazi aliwahi kubebwa kichwa chini miguu na kuku?
 
Sasa huoni kwamba kuna wakati vitu kama hasira, malipizi ya visasi, chuki vinaweza kumfanya mwanadamu afikirie kuua ila hapohapo unakuta kinachomfanya asifanye hivyo ikawa woga wa kuingia matatizoni, Ila anyway kama ungekuta woga hautakiwi basi kwenye maandiko pasingekuwa na maneno kama "Ole wao" Haya umesema kuna kuheshimu na sio kuogopa Rais ni cheo cha kuheshimika hivyo basi kama tunapaswa kukiheshimu na heshima inafanya tushindwe kufanya baya juu yake basi ni kwanini anawekewa ulinzi.... Sasa ukitaka ujue tofauti ya heshima na woga kajaribu kumsogelea kiholela.... Huwezi kusema unaheshimu kitu bila kuogopa kuvunja heshima.
Ngoja tujadili kwa namna ambayo we unataka

Kama woga ndio unaosababisha watu washindwe kufanya mabaya, mbona bado kuna mabaya?

impact ya huo uwoga iko wapi?

Unazungumzia mwanadamu kufikiria kuua halafu akaja kughairi kwa kuogopa Mungu atamuadhibu wakati vitabu vya dini vimesimulia namna mitume wenu walivyokuwa wakifanya mauaji bila woga

Na sio tu kwamba mtu ndio anafanya mabaya kwa kuhemkwa kushindwa kuzuia hisia zake, hata Mungu katajwa kufanya mauaji kwa wasio na hatia na ameshindwa kuzuia hisia zake.

Nakupa mfano wa ile hadithi ya Pharao na Mussa ambapo ili kumfanya Pharao awaruhusu waisrael waondoke ilibidi apigwe mapigo kumi

Hayo mapigo kumi hayakumlenga yeye, yalilenga watu wengine wasio kuwa na hatia.

Mungu alitoa agizo la kila nyumba kupaka damu ya kondoo juu ya milango yao na usiku roho mtakatifu alipita ku scan kila nyumba.

Nyumba ambayo haikupakwa damu juu ya milango yao iliadhibiwa kwa kuuwawa mtoto wa kwanza wa kiume.

Huyo mtoto wa kwanza wa kiume hajahusika kwa namna yeyote na dhambi ya pharao lakini pharao kaachwa, akaenda kuadhibiwa mwingine.

Mungu anayekuambia ole wako ufanye jambo fulani halafu yeye ambaye tunategemea kumuona kama mfano unamuona analifanya jambo hilo unafikiri inaleta picha gani?
 
Kuna mambo ambayo hujayaelewa sijui ni kwa bahati mbaya au kusudi.

Kwanza mfano wa Pazi na jogoo niliuweka kuonesha uwezekano wa kujadili stori fulani kama ilivyoandikwa pasipo kukubaliana na uhalisia wake.

Ukiniambia Pazi alibebwa na kuku jike nitakupinga kwasababu umepotosha stori ya mwandishi. Kukupinga huko hakuna maana kwamba nakubaliana na uhalisia wa stori hiyo.

Nataka nijue hiyo falsafa ya kiti umeitoa ndani ya kitabu au ni interpretation yako tu?

Kuuliza kama ukinipa maelezo kutoka ndani ya kitabu yanayoelezea maana ya kiti cha enzi kwa jinsi ulivyodai wewe inakuwa hauna tofauti na mtu anayesema Pazi alibebwa na kuku jike nikamuomba anioneshe hayo maneno ndani ya kitabu afu ye akasema kwani nikikuonesha ndio utaamini kuwa Pazi aliwahi kubebwa kichwa chini miguu na kuku?

Mimi nimeongelea kiti cha enzi cha Mungu na wala sijaongelea kiti cha enzi cha Scars au jini nk, ningalikuwa nimeongelea kiti kingine kinyume na hicho basi ulikuwa unayo haki ya kutoa mfano wa hadithi ya Jogoo na kuku tembe na Pazi kwa maana hiyo huo mfano wako ni irrelevant katika case hii.

Kwa upande mwingine Ulipotoa huo mfano wa Pazi na jogoo ndipo na mimi nika take advantage wa kuhusisha mfano huo na kiti cha enzi cha Mungu kwamba habari zote hizo mbili zimekaa kimafumbo kwani haiingii akilini Kwamba ipo siku jogoo atamning'iniza mtu kichwa chini miguu juu halikadhali haitatokea Mungu aketi kwenye kiti au sofa akinywa soda akiangalia TV kama binadamu afanyavyo, hivyo ukisoma maandiko ni lazima uyapime kwani maandiko mengine ni tamathali za semi (figure of speech).

Umeshikilia tu nikuonyeshe ni wapi nimepata hiyo interpretation, nataka ujue kwamba aya za Qur'an (kwa mujibu wa Qur'an) zimegawanyika katika makundi mawili; ayat Muhakamat na ayat Mutashabihat, hizo za kwanza zinakupa maana ya moja kwa moja na hizo za pili zinakupa maana ya iliyojificha, aya ya Kiti cha enzi ni kundi la pili (mutashabihat) ambayo inahitaji ufafanuzi ili Kuelewa maana zake za ndani, kama nilivyokueleza Qur'an inasema; "laa yumasuhu illa almutaharuun", yaani mtu hashiki/hataelewa maana za ndani za Qur'an kama huyupo tohara kiroho, sasa wewe unapinga kuwepo kwa Mungu kwa Kibri je huyo Mungu anaweza atakase roho yako ili ujue undani wa maneno yake wakati umeweka kibri kama uzio !??--- ondoa hicho kibri na jaribu kunyenyekea na hapo Mungu atajitokeza kwako Miraculously.
 
Kuna point unai miss hapo, mfano wa Pazi nimeutoa kuonesha jinsi mtu anavyo weza kuingia mjadla kujadili stori yeyote bila kukubaliana na uhalisia wa stori hiyo.

Hapo nilikuwa nai refute hoja yako iliyokuwa unadai sipaswi kukosoa madai yako uliyoyatoa kinyume na ilivyoandikwa kwasbabu tu siamini Mungu yupo

Mkuu hiyo ya kusema tohara ya kiroho wote tunakubaliana ni propaganda za kidini zinazotumika kuzuia ukosolewaji na watu waliokinyume na dini husika

Hata wewe huwezi kuupinga ukristo maana nao wameweka defense ya namna hiyo kuwa kabla ya yote unatakiwa umpokee roho mtakatifu

Roho mtakatifu huanza kwa kumkiri Yesu kuwa bwana na mokozi wa maisha yako.

Ikifuatiwa na kubatizwa kwa ajili ya kuruhusu huyo Roho mtakatifu akuingie

Wanakuambia ukiwa na Roho mtakatifu huwezi ukaona dosari kwenye biblia, kama umeona dosari tafsiri yake ni kwamba hauna roho mtakatifu

Sasa mpaka hapo ukisema ufuate kanuni hiyo utaweza?
 
Kuna point unai miss hapo, mfano wa Pazi nimeutoa kuonesha jinsi mtu anavyo weza kuingia mjadla kujadili stori yeyote bila kukubaliana na uhalisia wa stori hiyo.

Hapo nilikuwa nai refute hoja yako iliyokuwa unadai sipaswi kukosoa madai yako uliyoyatoa kinyume na ilivyoandikwa kwasbabu tu siamini Mungu yupo

Mkuu, mimi points zako zote nizipata labda mimi naongea kwa falsafa ya juu sana kiadi kwamba unashindwa kunipata.

Ni hivi; Wewe unadai kwamba kiti cha enzi cha Mungu ni kiti halisia au unataka kuamini kwa mujibu wa hiyo habari kwamba kiti hicho ni halisia na hapo unapingana na mimi ninaposema kwamba kiti hicho ni metaphor, sasa unawezaje kujadili kitu cha mtu ambaye hayupo???---- eti nianze kujadili simu ya mtu anayeitwa Scars wakati mtu mwenyewe hajulikani wala siamini Kwamba aliwahi kuishi!!!, hekima inasema hivi; kwanza tuthibitishe huyo Scars yupo au aliwahi kuishi na halafu ndipo tujadili habari ya simu yake, mbaya zaidi unashadidia kwamba kiti hicho ni HALISI kana kwamba umeingia ndani ya fikra za mleta hadithi (katika Qur'an ni Mungu mwenyewe) au kana kwamba umewahi kukiona hicho kiti!!, hutaki kusikia kwamba sio aya zote za Qur'an zinayo direct interpretation na mojawapo ni hiyo ya kiti cha enzi.

Ulipotoa mfano wa Jogoo na Pazi kwa kutoa hoja kwamba hukubaliani kwamba Jogoo anaweza kumning'iniza mtu kidhahiri lakini unayo haki ya kujadili kitu hicho japokuwa hukiamini na mimi pia naungana na wewe siamini kama jambo hilo linaweza kutendeka kidhahiri na ndio maana mimi nimetumia fursa hiyo kukuambia kuwa suala hilo na suala la kiti cha enzi cha Mungu ni metaphors yatupasa tujifunze kama tamathali za semi, kwani katika hiyo hadithi ya pazi na jogoo hakukuwa na fundisho?? au ilikuwa ni hadithi tu bila lessons and morals??-- na ndivyo hivyohivyo kwenye kiti cha enzi tunapata lessons and morals.
 
Prolly it is really beyond my grasp, can't deny that

Ni kweli nadai kiti cha enzi ni halisia kama ilivyoelezwa kwenye kitabu na sio code name.

Lakini hili nalijadili katika muktadha wa maandiko namna yalivyo andikwa na sio swala la mimi kukubaliana na hadithi hiyo.

Hata wewe unaweza kujadili habari za biblia ambazo hukubaliani nazo kwa kupoint vifungu vya biblia lakini haimaanishi kwamba unakubaliana nayo.

Kwasababu sio mara moja Mungu ameelezewa kwenge hivi vitabu akiwa na sifa zinazomtambulisha kuwa yupo physically

Kitabu chenu kimeandika Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake, ukiangalia hicho hicho kitaja kimetaja muonekano wa Mungu, Mungu huyu ana macho, anasikia, ana mdomo, hadi jinsia yake inafahamika, kuna maelezo mengi yanayopambanua muonekano wake yanayothibitisha kuwa ana mwili.

Na ndio maana napotaka utetee hoja yako uweke maneno yaliyoandikwa kwenye kitabu hicho yanayokanusha na sio kuweka mawazo yako
 
Kama Qur'an isingeandika baadhi ya aya zake katika muundo wa tamathali hiyo Qur'an nadhani ingekuwa na uzito wa zaidi ya tani kumi.

Thamathali makes a person use his/her mental power thus exercises his brain apart from gaining desired lessons.
 
Mungu ni Roho na shetani pia ni roho lakini uonekana kupitia matendo ya wanadamu. Mwanadamu anaweza akawa shetani au MUNGU. Neno mtu means Mungu you ndani ya mtu, ubinanadamu means uwepo wa Mungu. Shetani ni mtu mwenye matendo yasiyo ya kiutu
 
Kama Qur'an isingeandika baadhi ya aya zake katika muundo wa tamathali hiyo Qur'an nadhani ingekuwa na uzito wa zaidi ya tani kumi.

Thamathali makes a person use his/her mental power thus exercises his brain apart from gaining desired lessons.
Kila dini ina kauli mbiu kama hiyo
 
Ngoja tujadili kwa namna ambayo we unataka

Kama woga ndio unaosababisha watu washindwe kufanya mabaya, mbona bado kuna mabaya?

impact ya huo uwoga iko wapi?

Unazungumzia mwanadamu kufikiria kuua halafu akaja kughairi kwa kuogopa Mungu atamuadhibu wakati vitabu vya dini vimesimulia namna mitume wenu walivyokuwa wakifanya mauaji bila woga

Na sio tu kwamba mtu ndio anafanya mabaya kwa kuhemkwa kushindwa kuzuia hisia zake, hata Mungu katajwa kufanya mauaji kwa wasio na hatia na ameshindwa kuzuia hisia zake.

Nakupa mfano wa ile hadithi ya Pharao na Mussa ambapo ili kumfanya Pharao awaruhusu waisrael waondoke ilibidi apigwe mapigo kumi

Hayo mapigo kumi hayakumlenga yeye, yalilenga watu wengine wasio kuwa na hatia.

Mungu alitoa agizo la kila nyumba kupaka damu ya kondoo juu ya milango yao na usiku roho mtakatifu alipita ku scan kila nyumba.

Nyumba ambayo haikupakwa damu juu ya milango yao iliadhibiwa kwa kuuwawa mtoto wa kwanza wa kiume.

Huyo mtoto wa kwanza wa kiume hajahusika kwa namna yeyote na dhambi ya pharao lakini pharao kaachwa, akaenda kuadhibiwa mwingine.

Mungu anayekuambia ole wako ufanye jambo fulani halafu yeye ambaye tunategemea kumuona kama mfano unamuona analifanya jambo hilo unafikiri inaleta picha gani?
ebu tufupishe suala, Kwahiyo wewe unamuogopa Mungu au Umuogopi? Au huamini pia kama kuna Mungu.
 
Back
Top Bottom