Machache yanayonifanya niamini uwepo wa Mungu: Hatari ya kuamini hakuna Mungu

Mfano yapi 90% science haijajibu?
Mengi Sana mfano
1.Maisha baada ya kifo
2.Nguvu ya Imani
3.Viumbe visiovyoonekana
5.Kuhusu Roho,Nafsi
6.Laana na baraka
7.Ndoto
8.Mawazo
9.Mawasiliano ya ROHO kwa roho
10.chanzo cha tabia na dawa ya tabia mfano ulevi, uzinzi, ushoga, uteja, hasira,chuki, ubinafsi nk
11.Magonjwa ya kiroho
12.Kifo
13.Mungu na shetani
14.viumbe vilivyopo katika sayari zingine
15.uhusiano uliopo katika ya wanadamu na viumbe visiovyoonekana
16.nk
Yapo mengi zaidi tutakesha
 

Bro... hayo maswali yote mbona yana majibu

1. Maisha baada ya kufo? Hakuna maisha baada ya kifo, ukifa una decompose
2. Nguvu ya imani? Imani which? Imani what?
3. Viumbe visivyoonekana -unamaanisha viruses na bacterias? Hao wanaonekana kwa microscopes
4. ..??
5. Tupe proof ya kwamba roho au nafsi vinaexist..
6. Laana au baraka? Wtf is that crap, hakuna kitu kama mtu anakulaani au kukubariki.
7. Ndoto? Hii kwa urahisi, ni replay ya mawazo yako mwenyewe... ndiomaana huwezi kuota kitu ambacho hujawahi kukiona au kitu hujawahi kukiimagine
8. Mawazo? Ukikaa idle lazima uwe na mawazo
9. Mawasiliano ya roho kwa roho, hakuna kitu kama icho... ni sawa na watu wanaoamini mambo ya utabiri wa nyota
10. Tiba ya tabia zipo, ndiomaana kuna rehabilitation centers
11. Mgonjwa wa kiroho? Soma namba 9 hapo juu
12. Kifo, kila kiumbe kitakufa... ispokua species kadhaa za jelly fish. Wao wana biological immortality, watakufa tu ukiwaua. Usipowaua wanaishi milele... au unataka explanation gan kuhusu kifo?
13. Mungu na shetan. Hawapo, hakuna namna ya kuprove existence yao
14. Aliens. So far hatujagundua aina yyte... ingawa kuna sayari zinaonesha uwezekano wakuwepo au kuanzisha maisha kama yalio duniani.
15. Refer to point number 9
16.... ?
 
1.Mwili ndio unaokoma baada ya kifo lakini Roho na nafsi uendelea
2.Mwili wa binadamu uendeshwa na roho na nafsi vikitoka uhai ukoma.
3.Ndoto inaweza kuwa ni reflection ya Yale uliyofanya, au ujumbe fulani toka outer universe, au nafsi inakuwa imesafiri eneo halisi usilolijua nafsi Ina uwezo wa kusafiri kwa kasi ya sekunde moja hadi bara jingine, thus umeshawahi ota vingi ambavyo ukuwahi kutana navyo maisha mwako.
4.Sayansi haiwezi tibu ubinafsi, uzinzi, wizi na tabia zisizo na maadili
 

Huwezi kuota kitu ambacho hujawahi kukiwaza. Kuna study zinaonesha kua hata baadhi wanyama wanauwezo wa kuota (if they're intelligent enough). mfano, mbwa

Uzinzi kwa pov ya sayansi sio ugonjwa, tabia zisizo na maadili (mfano wizi, uuwaji, kutumia madawa) unaweza ukaacha mwenyewe tu ukiamua, au ukiwa motivated kuacha. Vingine vinawezakua vinakupa addiction, ivo vinatibika kwa rehabilitation, sayansi.
 
"Tupa macho kule" kwanza hiyo sio sentensi sahihi

Lakini hata tukiipa uhalali tukisema tuijadili bado utaona kuna materials body vimehusika

Namna ulivyoweka huu mfano na jinsi ulivyoutolea maelezo umeshindwa kufanya relation na habari ya "kuketi kiti cha enzi"

Kwasababu hapo macho yaliyozungumziwa ni kitu halisia na sio code name

Kwenye ishu ya Mungu kiti ulisema ni code name

Kwenye ishu ya "Mungu kuketi katika kiti cha enzi" hakuna jambo lolote unalokubali kuwa linahusiana na physically

"Tupa macho kule"

Hapo kuna macho: Kiungo cha mwili au ogani iliyopo mwilini mwa huyo mtu anayeambiwa

Kule: Hiyo ni direction ambayo kaelekezwa huyo mtu eidha kwa kidole au kwa ishara nyingine.

Vyote hivyo viwili "macho na eneo" ni physically matter

Wakati kwenye "kiti na kuketi" hivyo vyote wewe unesema ni code names zinazo maanisha "cheo"
 
Aliyeumba ni CHANZO HALISI, alikuwa peke yake MAHALI PAKE na hakuna anayepajua ila yeye Mika 1:3 "Kwa maana, angalieni, Bwana anakuja akitoka MAHALI PAKE, naye atashuka, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka."

Hata atheist anayeamini muumba wa vyote, yote na wote hayupo huwa wanakitu wanakiabudu either kwa Siri ama kwa wazi, mfano mtu anaweza akawa haamini uwepo wa aliyeumba ila akaamini (science,nature,ushirikina,hela n.k) icho ndo kitu anachoabudu
 
Mungu wala hatuaminishi chochote, wala hahitaji chochote kutoka kwetu...sisi wanadamu ndo tunakuwa na chokochoko ya kutaka kujua na kumjua..Design zetu (Kimwili na kiroho) tayari ni limits tosha ambazo zinakurudisha kule kule kwa Mungu.
Hivyo mtu yoyote hata ambaye hajawahi gusa biblia au quran..tayari ndani mwake anajua kuna nguvu inamuendesha....

Wewe unamdiscuss Mungu na kumpa uwezo wa kibinadamu...which is fine sababu ni binadamu na uwezo wetu uko limited..lkn Mungu hana hizo physical boundaries unazosema...Hana mwanzo hana Mwisho, hana sehemu maalumu-yuko mahali pote...nguvu iko mahali pote....
Kila kitu kina chanzo na Mungu ndo chanzo chenyewe...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…