Machimbo mazuri ya kupata bidhaa mbalimbali Kariakoo kwa bei nafuu
Unatafuta bidhaa bei nafuu na jumla Kariakoo? Hapa nakupa machimbo bure ufanye biashara,

Save hiii post kwanza itakusaidia baadae.

Kwa nguo za ndani (chupi) ukimaliza kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, kwenye upande wa vitu vya make up kuna mtaa mmoja unaingia yapo maduka mengi dozen za cotton Ni Bei nafuu.

Make up _ kituo cha mwendokasi ukiachana na huu upande ilipo msimbazi polisi ule mwingine unaingia ndanindani.

Maduka ya jumla kwa vitambaa vya Masofa, yanapitakana mtaa wa kipata, anza na kipata na msimbazi mpaka kipata na swahili yapo ya kutosha.

Vifaa vya umeme nenda Mtaa wa Narung'ombe.

Spear za pikipiki Nenda mtaa wa swahili na k/koo hapo kuna maduka mengi.

Mtaa wa congo na narung'ombe underground ya Tanzanite kule chini kuna mtaa mzima unaingia unatembea chini kwa chini kuna t-shirts za bei nafuu.

Vifaa vya plastiki Nenda Duka la cello kariakoo .

Rasta bei ya jumla ziko upande wa pili wa kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, mtaa yanapopaki magari ya makumbusho gerezani yanayopitia Sinza.

vitambaa vya vijora ni Msimbazi Kwa nyuma.

Chimbo la dawa muhimu za binadamu kwa kariakooo linapatikana mtaa wa Kipata na nyamwezi street.

Bidhaa za simu, cover, charger, housing Kwa bei Chee ziko Upande wa kushoto ukiwa unashuka chini kuelelekea fire kabla hujafika kituo Cha Mwendokasi Cha Msimbazi B unazama Kwa ndani

Vifaa vya ujenzi ni Mtaa wa livingstone kuna Duka Linaitwa Bahdela bei poa vyote utapata.

Vifaa vya stationaries ni mtaa wa Kipata ( maduka ya wasomali ndo bei nzuri )

Shati ni mtaa wa Agrey/congo au mchikichi/Congo

Mashine mbalimbali kama za miwa, kusaga nk nenda Mtaa wa SIDO

Narudia Vitenge ni pale mnazi mmoja ile njia ya kuingia posta. Wale wahindi watakuuzia vitenge vizuri bei nafuu. (ukipata connection ya Uganda utatisha)

Maduka ya wachina wanaouza viatu vya kike ni mtaa wa congo.
Mkuu elezea vzr hapo kweny vitambaa vya vijora
 
Ukifika kituo cha mwendokas B kuna chochoro njia ya Narung'ombe st ingia hio njia upande wako wa kushoto kabla hujafika congo st kuna maduka meng sana ya viatu vya kiume unashuka vingazi ndan maduka yapo meng na mengine yapo juu hiv
Wahuni tu ,duka cheap nmesahau ni wap ila mtaa wa msimbazi Kuna jamaa Yuko poa Bei zake ziko gud raba Original na imara
 
Shuka vingazi Airforce black/kijivu watakwambia 70k wakat ni 35k
 
Je maduka ya jumla ya vifungashio kwa kariakoo yapo sehemu gani
Msaada tafadhali[emoji120]
 
Napajua ila sijui mtaa unaitwaje
Lakini ni meneo ya shimoni panapojengwa soko jipya walipozungumza mabati nafikiri ni sikukuu mtaa ule ukiuliza utaonyesha
 
Uzi poa sana

Kabisa msaada jamani na wanapouza Mikoba handbags za kina dada aina tofauti tofauti pamoja na belts za nje zakina dada na Accessories kwa bei ya jumla na nzuri Heleni vikuku cheni na mikufu blaclet pamoja na viatu mchanganyiko hills na slippers nzur zinazo trend kwa bei nzuri ya jumla yaan bei ya mfanyabiashara anae nunua ili nae akauze mkoani kwake apate kitu Heshima yenu wakubwa[emoji120]
 
Accessories wacheki prestigeaccessories tz insta

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Wakuu chimbo la bales za mikoba ya mtumba na nguo za wadada za mtumba ni wapi, msaada please [emoji120]
 
Unatafuta bidhaa bei nafuu na jumla Kariakoo? Hapa nakupa machimbo bure ufanye biashara,

Save hiii post kwanza itakusaidia baadae.

Kwa nguo za ndani (chupi) ukimaliza kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, kwenye upande wa vitu vya make up kuna mtaa mmoja unaingia yapo maduka mengi dozen za cotton Ni Bei nafuu.

Make up _ kituo cha mwendokasi ukiachana na huu upande ilipo msimbazi polisi ule mwingine unaingia ndanindani.

Maduka ya jumla kwa vitambaa vya Masofa, yanapitakana mtaa wa kipata, anza na kipata na msimbazi mpaka kipata na swahili yapo ya kutosha.

Vifaa vya umeme nenda Mtaa wa Narung'ombe.

Spear za pikipiki Nenda mtaa wa swahili na k/koo hapo kuna maduka mengi.

Mtaa wa congo na narung'ombe underground ya Tanzanite kule chini kuna mtaa mzima unaingia unatembea chini kwa chini kuna t-shirts za bei nafuu.

Vifaa vya plastiki Nenda Duka la cello kariakoo .

Rasta bei ya jumla ziko upande wa pili wa kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, mtaa yanapopaki magari ya makumbusho gerezani yanayopitia Sinza.

vitambaa vya vijora ni Msimbazi Kwa nyuma.

Chimbo la dawa muhimu za binadamu kwa kariakooo linapatikana mtaa wa Kipata na nyamwezi street.

Bidhaa za simu, cover, charger, housing Kwa bei Chee ziko Upande wa kushoto ukiwa unashuka chini kuelelekea fire kabla hujafika kituo Cha Mwendokasi Cha Msimbazi B unazama Kwa ndani

Vifaa vya ujenzi ni Mtaa wa livingstone kuna Duka Linaitwa Bahdela bei poa vyote utapata.

Vifaa vya stationaries ni mtaa wa Kipata ( maduka ya wasomali ndo bei nzuri )

Shati ni mtaa wa Agrey/congo au mchikichi/Congo

Mashine mbalimbali kama za miwa, kusaga nk nenda Mtaa wa SIDO

Narudia Vitenge ni pale mnazi mmoja ile njia ya kuingia posta. Wale wahindi watakuuzia vitenge vizuri bei nafuu. (ukipata connection ya Uganda utatisha)

Maduka ya wachina wanaouza viatu vya kike ni mtaa wa congo.
Weka ramani ya Kariakoo inayoonyesha mitaa
 
Vifaa vya stationaries ni mtaa wa Kipata ( maduka ya wasomali ndo bei nzuri )
Asante kwa koneksheni hii mkuu. Hivi vifaa vya stationers wanauza kwa bei nafuu kuliko Masumin Printway and Sataioners Limited (Mtaa wa Kitumbini)?
 
Naomba msaada waungwana sehemu wanapouza kwa jumla haya mazulia ya mlangoni
IMG-20221128-WA0017.jpg
 
Back
Top Bottom