Machinga kuwashikashika wanawake inakera sana!



Walaumiwe “watu” na sio jinsia zao.

Kama ambavyo kuna wanaume wasio wastaarabu na wasiojiheshimu, wapo wanawake pia wenye hizo hulka mbovu.

Suala la maadili kwa mazingira tuliyopo leo ni pana sana kiasi kwamba ni dhahiri hata wenye mamlaka na wajibu wa kuyasemea na kuyakemea hawajui wapi pa kuanzia na kibaya zaidi asilimia kubwa kati Yao ni washiriki wazuri pia wa uvunjifu wa hayo maadili yenyewe.


Makadirio ya Nguvu ya Uumbaji yataamua.

It’s a twisted & sad dilemma!
 
😁 ikawaje sasa
 
unaonekana hip hop kweli
 
Nenda na mwanaume, hawatathubutu kukushika, utaskia shemeji hii inakutosha kwa mbali sana na kwa adabu.
Huo ujinga maana unaenda kumtia aibu tu,ukivaa Kwa heshima hakuna lolote litatokea,akivaa hovyo hata uwe naye,miluzi na maneno ya kejeri ni aibu tu Kwa mwanaume
 
Wanawake wengi hawajielewi.
Mtu anavaa nguo inabana kichizi afu fupi anategemea nini?
Chupi hawavai siku hizi

Matako makubwa anayatetemesha makusudi afu ategemee kusamehewa kushikwa.

Wanawake wanajirahisisha wenyewe kuanzia kwenye kucha
Na akivaa hivyo wahuni wanamdanganya umependeza, kumbe wanamchora tu na kesho anazidisha kuvaa ovyo zaidi, yaani akiwa anasifiwa sifiwa kinafiki anadhani ni kweli........
 
Usikae kinyonge wapige vibao,
Mimi Wamachinga wa Kariakoo wananielewa vema nawabutua vibao au mateke na ukishamkong'ota mmoja wenzie wanakushangilia utasikia "sawa, sawa dada kazoea huyoooo"

Pia ukiwa sehemu kama hizo usitembee kwa madaha, usijivute vute na kubinua kiuno, kua mkakamavu, macho yawe mbele au kwenye bidhaa unazotaka kununua,

Angalia na mavazi ya kuvaa ukiwa unaenda sehemu kama hizo, umevaa kimini au kitight na kitop kazi utakua nayo, vaa suruali, tshirt na raba, au gauni au baibui kidogo inapunguza na hata ukimbutua huyo mshenzi anayejitoa ufahamu unakua na confidence zote.
 
Kuna wanawake hatuvai hovyo bado tunashikwa shikwa thaman yetu tunaishusha vipi?
Kwenye kucha ni wanawake wote wanaenda huko? Na hata wanaoenda huko kuna wanawake wanajiheshimu haruhusu kushikwa huko mapajani unaposema. Acheni kuwatetea vijana wa hovyo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akitokea mmoja akabutuliwa ya kichwa au mguuni ndo wataacha hiyo tabia chafu, inakera sana nchi imejaa wavuta bangi
 
Pole.Anayeshikwa ni Kwa kua hajui haki yake kisheria.Kutomaswa tomaswa bila ridhaa Yako ni kosa kisheria. Ni shambulio la aibu. Ukiwa na ushahidi unamfungulia mashtaka.
 
Wanawake 90% wanajishushia heshima, hizo 10% za nini... Wengi wape.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…