Machinga kuwashikashika wanawake inakera sana!

Machinga kuwashikashika wanawake inakera sana!

Mimi huwa nawakung'uta na hamna kitu wananifanya aisee, kuna siku nimeshuka mwenge machinga mmoja akawa ananing'ang'aniza kununua nguo kwake nikamwambia sihitaji nguo akaanza kunishika,kila nikijaribu kumkwepa naona ananizonga, niliweka mkoba begani vizuri nikageuka kama naondoka nikampa teke la nyuma, hajakaa vizuri nikampa side kick, anataka kunyanyuka nikamshika shati nikamnyanyua nikamwambia sasa wewe ulikua unanishika simama hapa unishike vizuri, ikabidi wenzie wamuamulie, nikawaambia msipende kuzoea watu sisi wengine ni waalimu wa taekwondo

Watu walijaa nikasepa zangu wakabaki wanamcheka
😂😂 kiboko ya wamachinga, darasa la taekwondo si lipo ntakuletea mwanafunzi mmoja.
 
Back
Top Bottom