Hili jambo ni kweli kabisa maagizo yamepotoshwa na yanatekelezwa kwa mihemko!
Rais mwenyewe katambua kuwa Shida sio Machinga, Bali shida ni Machinga kukosa Management ilihali kila walipo pana DED, DC , RC, WEO na wengine wengi!
Uongozi ndio haujatekeleza wajibu wake ipasavyo, Uongozi ndi unaotakiwa kuwawekea mfumo wa kufanya hizo biashara zao katika mpangilio mzuri, lakini pia katika mazingira salama na wezeshi!
Kwa hiyo hapa Concept, sio kuwaondoa tu kama takataka, wapangwe upya na waendelee na shughuli zao muhimu za ujenzi wa familia zao na taifa kwa ujumla.
Nilitamani Mh. Rais atumbue RC mmoja au wawili kupitia sakata hili ili wengine wajifunze kutoka hapo!