Machinga: Rais Samia amesema tupangwe vizuri hajasema tuhamishwe kama inavyotafsiriwa na watendaji!

Machinga: Rais Samia amesema tupangwe vizuri hajasema tuhamishwe kama inavyotafsiriwa na watendaji!

Makamu mwenyekiti wa Wamachinga nchini mh Lusinde amesema Rais Samia ameagiza wamachinga wapangwe vizuri katika maeneo waliyopo na siyo kuhamishwa kama inavyotafsiriwa na watendaji wa chini.

Source: ITV Malumbano ya Hoja
Waende machinga complex
 
😁😁😁
AMK5Se.png
 
Hawa watu hawapangiki kwa sababu hata akili zao hazipangiwi, haiwezekani hata unajua njia za biashara VIPi alafu ukaziba njia zote wateja wasipite.yaani cha muhimu warudi maeneo yaliyotengwa kwa ajiri yao wafanyabiashara wenye dhamana waliokodi wapate aki zao
 
Ila tukubaliaqne kuiwa hawa machinga;
  1. wameharibu kabisa mazingira ya miji yetu
  2. Kingo za barabara na mitaro ya maji imezibwa na vibanda jamabo ambalo ni hatari kabisa kwa kuundombinu husika.
  3. Njia za waenda kwa miguu zimezibwa na bidhaa zao hivyo waenda kwa miguu hutumia barabara za magari!
  4. Hata sehemu ambazo hazitakiwi kabisa kufanya biashara wao wamepanga bidhaa zao!
Jambo hili halina afya hata kidogo na tuendako no hatari zaidi! Tuchukue hatua
Ni matokeo ya Sera ambazo hazina tija tumekuwa tunazitumia Sera za majukwaani na kuendekeza unyumbu 'uncertainty policies and herding behaviour'
 
Hakuna lugha ya kumpanga mmachinga inayoeleweka, kiukweli wamachinga wanaogopwa, cha msingi wakajipange wenyewe, ila maeneo yanayotakiwa wasiwepo waondoke, bila kujali kitatokea nini, mnawaogopa nini, madarakani ni kwendo wa kujitangaza bila kujali umepata kura au la! Tunahitaji miji iwe safi hata kama madarakani mmeingia kwa mnavyojua wenyewe!
 
Makamu mwenyekiti wa Wamachinga nchini mh Lusinde amesema Rais Samia ameagiza wamachinga wapangwe vizuri katika maeneo waliyopo na siyo kuhamishwa kama inavyotafsiriwa na watendaji wa chini.

Source: ITV Malumbano ya Hoja
Kwa Mimi nilivoelewa ile kauli ya SSH nikwamba watafutiwe na wahamishiwe maeneo mengine ya kufanyia biashara,na sio kwamba wapangwe kwenye hayo maeneo waliopo ya barabarani (hii inamaanisha hawaitajiki maeneo ya barabara na kwenye hifadhi za barabara)
 
Wanapangwaje sasa kwenye barabara za waende kwa miguu? Wanapangwaje mbele ya maduka ya watu? Waondolewe katikati ya miji bwana! Wataenda kupangwa vizuri huko watakakopelekwa!
Serikali hiyo hiyo iliwaacha wafanye biashara barabarani,maisha yao kwasasa yanategemea kukaa barabarani .Wameoa,wamekopa,wanajenga,wanasomesha wakiwa barabarani
 
Hawapangiki kabisa, solution ni kufukuza kabisa na vitambulisho vyao vya elfu 20.. nalipa kodi zaidi ya laki 6 kwa mwaka halafu machinga anapanga bidhaa mbele ya duka langu na anauza zaidi yangu
Eti wanyonge
 
Makamu mwenyekiti wa Wamachinga nchini mh Lusinde amesema Rais Samia ameagiza wamachinga wapangwe vizuri katika maeneo waliyopo na siyo kuhamishwa kama inavyotafsiriwa na watendaji wa chini.

Source: ITV Malumbano ya Hoja
Wametuchafulia miji kila kona
 
Makamu mwenyekiti wa Wamachinga nchini mh Lusinde amesema Rais Samia ameagiza wamachinga wapangwe vizuri katika maeneo waliyopo na siyo kuhamishwa kama inavyotafsiriwa na watendaji wa chini.

Source: ITV Malumbano ya Hoja
Kupangwa ni pamoja na kutafutiwa eneo mbadala ambalo watafanya shughuli zao bila kuwa kero au bughuza kwa Wafanyabiashara wengine na wapita njia (Magari na waendao kwa miguu).
 
Vile vibasikeli vya chinga viliishia wapi? Mimi naona wangeomba kuruhusiwa kutembea mitaani na hizo duka linalotembea kuliko kulazimisha kukaa barabarani na kufukuzwa.
 
Nikimsikia kiongozi anahamasisha u-machinga huwa najiuliza kama anaelewa kuwa
1. anahamasisha ukwepaji Kodi,
2. Anashusha thamani ya shilingi,
3. Anaua viwanda vya ndani
4. matumizi mabaya ya nguvukazi ya vijana wa taifa
5. kutengeneza mazingira ya mripuko wa magonjwa
6.taswira mbaya ya nchi yenye mwonekano mchafu wakati miundombinu ni bora

Anayewatetea machinga ajibu hoja hizo bila jazba la sivyo u-machinga ukomeshwe kabisa biashara zifanyike kwa mujibu wa sheria na kwa ushindani wenye usawa.
 
Ukienda kariakoo kwa gari utajuta. Yaani hakuna nafasi kabisa. Njia za wapita kwa mguu zimejaa machinga. Hivyo watembea kwa mguu inabidi waje barabarani. Yaani ukigonga sasa. Hapo jua gari yako itapondwa na unaweza kata kupoteza maisha.
Nilishawahi ponea chupu chupu kuunguziwa gari mtaa WA Livingston hapa dar!!! Duh kuwepo na ustaarabu tu!! Uongozi wowote unapimwa kwa usimamizi bora WA taratibu na sheria
 
Makamu mwenyekiti wa Wamachinga nchini mh Lusinde amesema Rais Samia ameagiza wamachinga wapangwe vizuri katika maeneo waliyopo na siyo kuhamishwa kama inavyotafsiriwa na watendaji wa chini.

Source: ITV Malumbano ya Hoja
Kupangwa vizuri ndio kuhamishwa kwenyewe
 
Hili jambo ni kweli kabisa maagizo yamepotoshwa na yanatekelezwa kwa mihemko!
Rais mwenyewe katambua kuwa Shida sio Machinga, Bali shida ni Machinga kukosa Management ilihali kila walipo pana DED, DC , RC, WEO na wengine wengi!
Uongozi ndio haujatekeleza wajibu wake ipasavyo, Uongozi ndi unaotakiwa kuwawekea mfumo wa kufanya hizo biashara zao katika mpangilio mzuri, lakini pia katika mazingira salama na wezeshi!
Kwa hiyo hapa Concept, sio kuwaondoa tu kama takataka, wapangwe upya na waendelee na shughuli zao muhimu za ujenzi wa familia zao na taifa kwa ujumla.
Nilitamani Mh. Rais atumbue RC mmoja au wawili kupitia sakata hili ili wengine wajifunze kutoka hapo!
Tatizo ni kwamba Taratibu za Mipango Miji zinakataa kufanya kazi katika namna ya kuwafurahisha machinga

Sidhani kama kutumbua watu ni suluhu
Badilisheni sheria
Viongozi hao wanasimamia sheria
Shida JPM hakujali sheria na haya ndio matunda yake

Machinga kwa usalama wao wajiunge wakodi fremu waendelee na kazi
Barabarani hawatasalimika
Hawana haki hiyo kisheria
 
Nikimsikia kiongozi anahamasisha u-machinga huwa najiuliza kama anaelewa kuwa
1. anahamasisha ukwepaji Kodi,
2. Anashusha thamani ya shilingi,
3. Anaua viwanda vya ndani
4. matumizi mabaya ya nguvukazi ya vijana wa taifa
5. kutengeneza mazingira ya mripuko wa magonjwa
6.taswira mbaya ya nchi yenye mwonekano mchafu wakati miundombinu ni bora

Anayewatetea machinga ajibu hoja hizo bila jazba la sivyo u-machinga ukomeshwe kabisa biashara zifanyike kwa mujibu wa sheria na kwa ushindani wenye usawa.
Huwa Mungu anachukia Sana tunavyoshindwa kutunza mazingira!! Tunakuwa Kama tumelaaniwa
 
Back
Top Bottom