Machinga: Rais Samia amesema tupangwe vizuri hajasema tuhamishwe kama inavyotafsiriwa na watendaji!

Makamu mwen
Sasa barabarani utawapangaje upya, machinga ni kero tupu!!zamu hii wakuu wa mikoa wana baraka tosha toka kwa rais, ndio maana unaona mambo yanaenda kisayansi, nenda mitaa ya posta/zanaki wenyewe wana bomoa mabanda yao , nguvu itatumika kwa wale manunda tu watakao jifanya hawataki kutii!!chanzo cha fujo hii ni awamu ya tano kuwatumia machinga kama mtaji wa kisiasa, hao ma RC, DED, DC, mbele ya rais wangefanya nini?
 
Makamu mwenyekiti wa Wamachinga nchini mh Lusinde amesema Rais Samia ameagiza wamachinga wapangwe vizuri katika maeneo waliyopo na siyo kuhamishwa kama inavyotafsiriwa na watendaji wa chini.

Source: ITV Malumbano ya Hoja
Ukiona manyoya yake hata usiulize, ujue kisha chinjwa huyo! Kupangwa upya ndio kuhamishwa kwenyewe huko [emoji124][emoji125][emoji1739]
 
Makamu mwenyekiti wa Wamachinga nchini mh Lusinde amesema Rais Samia ameagiza wamachinga wapangwe vizuri katika maeneo waliyopo na siyo kuhamishwa kama inavyotafsiriwa na watendaji wa chini.

Source: ITV Malumbano ya Hoja
Huyo Mwenyekiti naye asilete za kuleta, wewe uko kwenye NJIA YA WAENDA KWA MIGUU, UMEZIBA NJIA, wakitaka kukupanga wakupeleke wapi kama siyo KUKUONDOA hapo kwenye service road? Aaache siasa za kwenye TV!
 
Waende walikotoka, Nani kawaleta mjini. Kila ardhi ina mwenyewe,wewe unatoka kijijini kuja mjini umeshàwahi kujiuliza unakwenda kukalia ardhi ya Nani?
Mbona wewe unaishi Mabwepande badala ya kijijini kwenu huko ushoro Machame?!
 
Huyu katibu wa hao wamachinga Rais Samia amempigia simu au kukutana naye na kuelezwa hivyo?
 
nilichojifunza ni kwamba Machinga wa nchi hii ni mtu muhimu saana. Hawana document yoyote ya kisheria ya kufanya biashara ila analindwa vby mno.... afu watu wanategemea ati taifa lisonge mbele.

Taifa la wachuuzi ni lini likaendelea.
Meya wa jiji la Dar es salaam aliyetokea Chadema ndio aliwaruhusu!
 
Hili swala la machinga kiukweli kabisa ni swala gumu sana kulitatua,wanasiasa ndio wanaowapa nguvu ya kukaa katika maeneo yasiyoruhusiwa......Hapa viongozi wanaongea tu lakini ifikapo karibia na uchaguzi hao wamachinga wanakuwa marafiki zao
 
Sasa wewe gari lako moja lina thamani gani kuliko riziki ya wananchi 50?

Kama Wamachinga ni adha ya wewe kutodrive basi tembea kwa mguu. bora wewe usiendeshe gari lakini watanzania 50 wapate hela ya kula!
Tatizo lisipotatuliwa leo litaendelea kuwepo tu. Kulionea haya/huruma siyo kulimaliza.

Duniani kote wanafanyaJe swala la wachuuzi ?!. Gari langu moja linawakilisha magari yote yanayotumia barabara na ni haki yetu. Tunalipa kodi kupitia mafuta na ndiyo hiyo inayojenga ma barabara . So ondoa ujinga
 
Watu wafuate sheria na taratibu tulizojiwekea kama Taifa ipasavyo, vinginevyo ni kuendekeza UPUMBAVU.
kuna sheria ya wamachinga kulipa 20000 kisha wasisumbuliwe. Hii sheria iheshimiwe
Tatizo litatuliwe, siyo kuliahirisha kwa kufukuza wmachinga
 
Waende walikotoka, Nani kawaleta mjini. Kila ardhi ina mwenyewe,wewe unatoka kijijini kuja mjini umeshàwahi kujiuliza unakwenda kukalia ardhi ya Nani?
Mwenye ardhi ni serikali tu. Hata wewe umepangishwa.
 
Hawapangiki kabisa, solution ni kufukuza kabisa na vitambulisho vyao vya elfu 20.. nalipa kodi zaidi ya laki 6 kwa mwaka halafu machinga anapanga bidhaa mbele ya duka langu na anauza zaidi yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…