You are falling into the same trap, being a tenant means the possession, you possess the land for your use and you have a right to that, which is recognized by law apart from ownership which you insist we do not have.Mwenye ardhi ni serikali tu. Hata wewe umepangishwa.
Waende machinga complexMakamu mwenyekiti wa Wamachinga nchini mh Lusinde amesema Rais Samia ameagiza wamachinga wapangwe vizuri katika maeneo waliyopo na siyo kuhamishwa kama inavyotafsiriwa na watendaji wa chini.
Source: ITV Malumbano ya Hoja
Watapangwaje barabarani?hao watolewe pembezoni mwa barabara wapelekwe sehem za wazi full stop,Upo sahihi kabisa ila wasifukuzwe wapangwe.
Kiswahili chake kigumu, hajasema hivyo ila yeye anamshangaa anayedai hivyo.Kwahiyo aliyekuwa mkurugenzi na mkuu wa mkoa walizidiwa na meya?
Ni matokeo ya Sera ambazo hazina tija tumekuwa tunazitumia Sera za majukwaani na kuendekeza unyumbu 'uncertainty policies and herding behaviour'Ila tukubaliaqne kuiwa hawa machinga;
Jambo hili halina afya hata kidogo na tuendako no hatari zaidi! Tuchukue hatua
- wameharibu kabisa mazingira ya miji yetu
- Kingo za barabara na mitaro ya maji imezibwa na vibanda jamabo ambalo ni hatari kabisa kwa kuundombinu husika.
- Njia za waenda kwa miguu zimezibwa na bidhaa zao hivyo waenda kwa miguu hutumia barabara za magari!
- Hata sehemu ambazo hazitakiwi kabisa kufanya biashara wao wamepanga bidhaa zao!
Kwa Mimi nilivoelewa ile kauli ya SSH nikwamba watafutiwe na wahamishiwe maeneo mengine ya kufanyia biashara,na sio kwamba wapangwe kwenye hayo maeneo waliopo ya barabarani (hii inamaanisha hawaitajiki maeneo ya barabara na kwenye hifadhi za barabara)Makamu mwenyekiti wa Wamachinga nchini mh Lusinde amesema Rais Samia ameagiza wamachinga wapangwe vizuri katika maeneo waliyopo na siyo kuhamishwa kama inavyotafsiriwa na watendaji wa chini.
Source: ITV Malumbano ya Hoja
Serikali hiyo hiyo iliwaacha wafanye biashara barabarani,maisha yao kwasasa yanategemea kukaa barabarani .Wameoa,wamekopa,wanajenga,wanasomesha wakiwa barabaraniWanapangwaje sasa kwenye barabara za waende kwa miguu? Wanapangwaje mbele ya maduka ya watu? Waondolewe katikati ya miji bwana! Wataenda kupangwa vizuri huko watakakopelekwa!
Eti wanyongeHawapangiki kabisa, solution ni kufukuza kabisa na vitambulisho vyao vya elfu 20.. nalipa kodi zaidi ya laki 6 kwa mwaka halafu machinga anapanga bidhaa mbele ya duka langu na anauza zaidi yangu
Wametuchafulia miji kila konaMakamu mwenyekiti wa Wamachinga nchini mh Lusinde amesema Rais Samia ameagiza wamachinga wapangwe vizuri katika maeneo waliyopo na siyo kuhamishwa kama inavyotafsiriwa na watendaji wa chini.
Source: ITV Malumbano ya Hoja
Kupangwa ni pamoja na kutafutiwa eneo mbadala ambalo watafanya shughuli zao bila kuwa kero au bughuza kwa Wafanyabiashara wengine na wapita njia (Magari na waendao kwa miguu).Makamu mwenyekiti wa Wamachinga nchini mh Lusinde amesema Rais Samia ameagiza wamachinga wapangwe vizuri katika maeneo waliyopo na siyo kuhamishwa kama inavyotafsiriwa na watendaji wa chini.
Source: ITV Malumbano ya Hoja
Nilishawahi ponea chupu chupu kuunguziwa gari mtaa WA Livingston hapa dar!!! Duh kuwepo na ustaarabu tu!! Uongozi wowote unapimwa kwa usimamizi bora WA taratibu na sheriaUkienda kariakoo kwa gari utajuta. Yaani hakuna nafasi kabisa. Njia za wapita kwa mguu zimejaa machinga. Hivyo watembea kwa mguu inabidi waje barabarani. Yaani ukigonga sasa. Hapo jua gari yako itapondwa na unaweza kata kupoteza maisha.
Kupangwa vizuri ndio kuhamishwa kwenyeweMakamu mwenyekiti wa Wamachinga nchini mh Lusinde amesema Rais Samia ameagiza wamachinga wapangwe vizuri katika maeneo waliyopo na siyo kuhamishwa kama inavyotafsiriwa na watendaji wa chini.
Source: ITV Malumbano ya Hoja
Tatizo ni kwamba Taratibu za Mipango Miji zinakataa kufanya kazi katika namna ya kuwafurahisha machingaHili jambo ni kweli kabisa maagizo yamepotoshwa na yanatekelezwa kwa mihemko!
Rais mwenyewe katambua kuwa Shida sio Machinga, Bali shida ni Machinga kukosa Management ilihali kila walipo pana DED, DC , RC, WEO na wengine wengi!
Uongozi ndio haujatekeleza wajibu wake ipasavyo, Uongozi ndi unaotakiwa kuwawekea mfumo wa kufanya hizo biashara zao katika mpangilio mzuri, lakini pia katika mazingira salama na wezeshi!
Kwa hiyo hapa Concept, sio kuwaondoa tu kama takataka, wapangwe upya na waendelee na shughuli zao muhimu za ujenzi wa familia zao na taifa kwa ujumla.
Nilitamani Mh. Rais atumbue RC mmoja au wawili kupitia sakata hili ili wengine wajifunze kutoka hapo!
Huwa Mungu anachukia Sana tunavyoshindwa kutunza mazingira!! Tunakuwa Kama tumelaaniwaNikimsikia kiongozi anahamasisha u-machinga huwa najiuliza kama anaelewa kuwa
1. anahamasisha ukwepaji Kodi,
2. Anashusha thamani ya shilingi,
3. Anaua viwanda vya ndani
4. matumizi mabaya ya nguvukazi ya vijana wa taifa
5. kutengeneza mazingira ya mripuko wa magonjwa
6.taswira mbaya ya nchi yenye mwonekano mchafu wakati miundombinu ni bora
Anayewatetea machinga ajibu hoja hizo bila jazba la sivyo u-machinga ukomeshwe kabisa biashara zifanyike kwa mujibu wa sheria na kwa ushindani wenye usawa.