Machinga wa Karume waitaka Serikali iwaachie wajenge soko lao lililoungua, Waziri Bashungwa aunda Tume ya Uchunguzi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa Tamisemi Mh Bashungwa ametoa siku 7 kwa tume ya uchunguzi kukamilisha kazi na kutoa taarifa ya chanzo cha moto soko la Karume.

Nao wamachinga wamemtaka RC Makalla awaruhusu wajenge soko lao wao wenyewe kwa gharama zao.

Source: East Africa tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Hizo tume kila siku zinaundwa wakati ripoti haisomwi kwa wananchi kuna maana gani kuendelea kuunda hizo tume?

Hawa jamaa waache kufanya kazi kwa mazoea, kama jambo limeshawashinda bora wakae kimya tu kuliko kuja na majibu yaleyale yaliyoshindwa kujibu mitihani iliyopita, wasichezee akili za watu.
 
Lilikua swala la kutoa amri tu kuwa Machinga warejee na kuchapa kazi.
 
Hiyo tume wawafuatishe na waandishi wa habari kwa kila hatua ya upelelezi uchwara huo ok
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…