Machinga wasilete siasa waondolewe haraka miji yote Tanzania

Mnaowaita WANYONGE wakiongea, mnasema wanafanya siasa!?
 
Usisahau Mmawia kaanzisha uzi wa kuwatetea
 
Hakuna bomu, watengewe maeneo yaliyo bora na watafanya biashara bila shida... tatizo siasa za JPM ndio zimesababisha wakae mabarabarani na kufanya misongamano isiyo na maana. Kuchafua miji.
 
Sawa, warudishieni kwanza fedha za vitambulisho! Wengine walilipia wakiamini serikali italinda biashara zao wasibughudhiwe !
 
umeambiwa usifanye kiki wewe ukakaidi basi utapigwa. ni kuda wa virungu sasa muda wote mji umesongamana kumbe wengi machinga
 
Hali ilikuwa mbaya sana, na waendelee hadi mikoani!
Barabara za mijini siku hizi zinajengwa na sehemu za watembea kwa miguu ili watu tusipate shida ya kupigwa na side-mirror za wenye magari, ajabu sehemu zote wamachinga wametandaza vitu vyao. Ujinga mtupu!!!
 
Yani naona wanapiga siasa tuuu, lazima wafuate utaratibu tuache kudanganyana. Kila lakheri Makala, usirudi nyuma, songa mbeleeeee
Mkuu, hao ndio wanarudi kitaa kutafuta pesa kwa ngeta!
Hivyo tukae mkao wa kutulia, tusubiri yajayo.

Nadhani kungekuwa na smooth transitiin ya maeneo wanayopaswa kufanyia biashara zao, na si kibabe kama ilivyokuwa leo vingunguti.
 
Mjini Kampala ukienda luwum street utaamini hili
Machinga wanajiunga wanne mpaka watano wanakodisha frame ila ndani ya fremu kila mtu anauza chake
Pia hapa Tanzania
ifike mahali machinga waungane wakodi fremu na sio kuhodhi brbr za watembea kwa miguu
Wapi tunafeli kuwapanga machinga kila wakati makundi ya machinga yanaongezeka
Tusitumie nguvu kubwa kuwapeleka kwenye masoko la hasha wapewe elimu ya namna ya kupanga frame kwa watu wanne watano ili nao walipe kodi
 
Dar ni kichafu jamani, embu tutembelee miji ya wenzetu tuone jinsi walivyo wasafi. Kwa hili naiunga mkono ya Mama yetu Rais Samia kuchukua hatua. Huu ujinga huwezi kuukuta hata kwa majiranj zetu hapo bondeni.
 
Ukiangalia machinga walivyojaa barabarani unajiuliza nchi hii tuna viongozi wa namna gani! Ikifika jioni barabara nyingine zinafungwa kabisa unakuta nyanya, vitunguu,viazi n.k ndio vimetandazwa chini barabara haipitiki! Halafu bado kuna watu wanatetea! Hivi miaka ya nyuma kulikuwa hamna machinga!??

Prime areas zote zimejaa vibanda, tuache siasa kwenye kila kitu machinga warudi walikokuwa Period.
 
Haya ni mawazo yako, hebu tuwasikie na wao huenda wana hoja zenye mashiko zaidi ya wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…