Uwingi wa watu, siyo ishara kamilifu ya kupendwa kwa kitu. Yapo mengi yanayowafanya watu kwenda barabarani kuona msafara wa maiti hii...
1. Unatangazwa sana karibu na vyombo vyote vya habari hapa nchini. TV zote na Redio zote 24hrs ni "promotion" ya kifo cha Jiwe tu...
2. Huyu alikuwa "Rais aliyekuwa ofisini, amefia ndani ya ofisi". Hili jipya kwa Watanzania. Lazima kwa kiasi kikubwa livute hisia za wengi. Ktk mazingira haya, si lazima uwe unampenda kwenda kuona maiti yake barabarani...
3. Huyu bwana, katika uhai wake na ktk staili na aina yake ya uongozi wake wa kipekee kuwahi kutokea Tanzania;
Yaani wa kibabe, kikatili, kujiona yeye hajawahi kukosea au hakosei kabisa kiasi cha watu wote hususani viongozi wenzake, wasaidizi wake kumuogopa kama " ki - mungu" fulani hivi...
Kufa kwake kunawashangaza wengi, kiasi cha kujiuliza; "...ala kumbe hata ka - mungu" kanaweza kufa siyo..?". Hebu ngoja tukaitazame maiti yake bararani inakopita na kuzungushwa...
4. Watu hawaamini kuwa kumbe hata Jiwe gumu linaweza kufa. Wanakwenda barabarani kushangaa na kujiridhisha..
5. Serikali iliyoko madarakani chini ya CCM lazima ikitumie kifo hiki kujitangaza kujaribu kujenga political popularity japo itakuwa ya muda tu. Kwa hiyo msiba wake unatumika kisiasa pia na ndiyo maana watu wanakamatwa mitaani eti kwa kusheherekea kifo cha jiwe...
6. Marehemu alitumia nguvu nyingi ikiwemo uongo, propaganda na utakatifu bandia kujihalalishia kuwa anapendwa sana huku ukweli ukiwa siyo. Ili ujue unakabalika au la, lazima uwe compared fairly na mtu mwingine. Kwa huyu hayati, haikuwa hivi. He was him alone huku wenzake akiwa amewa - pin wengine akiwasaka awafunge au awaue kabisa....
7. Hapo walipo wanatumia fedha na nguvu nyingi sana kujenga mazingira ya "anapendwa sana". Cheki tu, maiti anatembezwa nchi nzima eti, tena kwa gharama kubwa kupita kiasi.
Kwa hili lazima tujiulize iwapo tuna akili kweli. Fedha inayopaswa kutumika kumaliza baadhi ya matatizo ya walio HAI, inatumika kui - promote maiti barabarani na angani...!!
Tuna akili kweli sisi watanzania?