Macho yangu yananidanganya?

Macho yangu yananidanganya?

Msiba wa Mobutu Sesesko kuku ngwendu wa Zabanga ulikuwa ni mzito kuliko huu

Madikteta wa kiafrika huogopwa hata wanapokufa
Wananchi wao wanajua wasipojiliza na kuhudhuria mazishi wanajua cha mtema kuni watakipata

Wako Wananchi wengine huwa wanalia tu hata kwenye misiba ya Redioni

Halafu kuna hii propaganda machine ya CCM ni hatari sana
unajaribu kukimbia ukweli bro,kubali utapona roho yako[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Msiba wa Mobutu Sesesko kuku ngwendu wa Zabanga ulikuwa ni mzito kuliko huu

Madikteta wa kiafrika huogopwa hata wanapokufa
Wananchi wao wanajua wasipojiliza na kuhudhuria mazishi wanajua cha mtema kuni watakipata

Wako Wananchi wengine huwa wanalia tu hata kwenye misiba ya Redioni

Halafu kuna hii propaganda machine ya CCM ni hatari sana
Msiba wa Mobutu? 🤣🤣🤣🤣

Hivi alifia wapi huyo jamaa? Na kazikwa wapi?
 
FIPA tulia,kilio na wewe ni ndugu wa damu,hakitakuacha hata baada ya kifo cha jpm,wewe ni wa kusokotwa tu.
Kama wewe ambaye umesha izoa korona ipo kwenye mfuko wako wa jeans umetoka nayo hapo uwanjani.

Very soon utaanza kutoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango
 
Magu anapendwa sana. Kuna tatizo moja kubwa sana la propaganda chafu ambazo zjnaendeshwa na kambi pinzani hasa kupitia mitandao ya kijamii. Lakini uhalisia kwa wananchi ni tofauti kabisa.

Tangu amefariki kambi pinzani wamefanya hate campaign kwa kasi kubwa zaidi. Na hata kudanganya dunia kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi mkuu. Angalia mtu kama Fatma Karume anachukua picha ya msafara sehemu ambayo hakuna makazi ya watu na kuzirusha eti watu wachache! na kuficha sehemu kubwa ambako kuna umati wa watu!

Yaani wanachuki iliyopitiliza na isiyo na sababu, kisha eti wanasema eti marehemu ndiyo alikuwa na chuki
 
Ngoja nikuongezee na hii ndugu ili hayo mafundo yawakabe kabisa na kufa[emoji116]
 
waambieni waume zenu,corona tumeipokea tz na tunaishi nayo.

[emoji23][emoji23][emoji23]sababu tuko na Mungu.

mbwa nyinyi.
Wewe unaonekana bado kijana mdogo huwezi kuona athari za Corona Wazee na Watu wenye Betrii kwenye Mioyo yao ndio wanaopukutika
 
Macho hayajadanganya.Ni kweli JPM alikuwa anapendwa hata tangu akiwa Waziri kwani alikuwa mtu wa matokeo hasa yanayoonekana.Kukariri kwake takwimu kulimfanya hata akiwa waziri wa ujenzi bajeti yake kupitwa bila mikwara yoyote.
Na ndio maana wengi tunabaki kujiuliza kwa kupendwa kule na huku kwa leo tunakokuona palikuwa na haja gani ya ,
  1. Kunyima uhuru wa vyama vingine vya siasa?
  2. Kuvuruga uchaguzi wa serikali za mitaa
  3. Kuvuruga uchaguzi mkuu?
Jambo moja ni wazi na limepata uthibitisho katika kipindi hiki ni kuwa "Watanzania ni wanafiki wa kupindukia"Sorry to say that!!!
 
Watu wanachanganya kati ya kumpenda Magufuli na kupenda maiti ya Magufuli.

Wengi tunapenda maiti yake, na ndicho kinatufanya tujae kwa wingi kuishangilia.

Hatuamini kama kweli kafa.

2719296_Ew5TiVsXIAMLyRh.jpeg
 
Uwingi wa watu, siyo ishara kamilifu ya kupendwa kwa kitu. Yapo mengi yanayowafanya watu kwenda barabarani kuona msafara wa maiti hii...

1. Unatangazwa sana karibu na vyombo vyote vya habari hapa nchini. TV zote na Redio zote 24hrs ni "promotion" ya kifo cha Jiwe tu...

2. Huyu alikuwa "Rais aliyekuwa ofisini, amefia ndani ya ofisi". Hili jipya kwa Watanzania. Lazima kwa kiasi kikubwa livute hisia za wengi. Ktk mazingira haya, si lazima uwe unampenda kwenda kuona maiti yake barabarani...

3. Huyu bwana, katika uhai wake na ktk staili na aina yake ya uongozi wake wa kipekee kuwahi kutokea Tanzania;

Yaani wa kibabe, kikatili, kujiona yeye hajawahi kukosea au hakosei kabisa kiasi cha watu wote hususani viongozi wenzake, wasaidizi wake kumuogopa kama " ki - mungu" fulani hivi...

Kufa kwake kunawashangaza wengi, kiasi cha kujiuliza; "...ala kumbe hata ka - mungu" kanaweza kufa siyo..?". Hebu ngoja tukaitazame maiti yake bararani inakopita na kuzungushwa...

4. Watu hawaamini kuwa kumbe hata Jiwe gumu linaweza kufa. Wanakwenda barabarani kushangaa na kujiridhisha..

5. Serikali iliyoko madarakani chini ya CCM lazima ikitumie kifo hiki kujitangaza kujaribu kujenga political popularity japo itakuwa ya muda tu. Kwa hiyo msiba wake unatumika kisiasa pia na ndiyo maana watu wanakamatwa mitaani eti kwa kusheherekea kifo cha jiwe...

6. Marehemu alitumia nguvu nyingi ikiwemo uongo, propaganda na utakatifu bandia kujihalalishia kuwa anapendwa sana huku ukweli ukiwa siyo. Ili ujue unakabalika au la, lazima uwe compared fairly na mtu mwingine. Kwa huyu hayati, haikuwa hivi. He was him alone huku wenzake akiwa amewa - pin wengine akiwasaka awafunge au awaue kabisa....

7. Hapo walipo wanatumia fedha na nguvu nyingi sana kujenga mazingira ya "anapendwa sana". Cheki tu, maiti anatembezwa nchi nzima eti, tena kwa gharama kubwa kupita kiasi.

Kwa hili lazima tujiulize iwapo tuna akili kweli. Fedha inayopaswa kutumika kumaliza baadhi ya matatizo ya walio HAI, inatumika kui - promote maiti barabarani na angani...!!

Tuna akili kweli sisi watanzania?
 
Watanzania ni wajamaa kwa asili. Linapotokea tatizo hua tuna desturi ya kuweka tofauti zetu pembeni na kujumuika kwa pamoja.
WaTz walishazoea manyanyaso toka majumbani mwao, walishazoea maisha magumu, toka huko walikokuzwa walishazoea kupigwa na kugombezwa hovyo hawakuwa wanaona shida yoyote juu ya uongozi wa JPM, isipokuwa wachache, wachache sana wanaojitambua, wanaotambua kiongozi anatakiwa aweje.

Hivyo ni kweli kuwa wanyonge hawajawahi kuwa na shida na JPM na wanampenda, hata akijibu shit utawaona wanavyocheka na kufurahi, Hivyo walikuwa wananampenda mtu wao.
 
Back
Top Bottom