Labda baada ya hayo malalamiko unayosema mengi si mikataba mingi ilejewa je iliwekwa wazi? Na je Kama haikuwekwa wazi nini kilizuia isiwekwe wazi?
Kihaki mikataba yote mikubwa inatakiwa kurejewa.Hata kama ni kwa kuangalia nani alipiga wapi tumuwajibishe au tujiweke sawa tusipigwe tena.
Unavyozidi kufanya mikataba iwe ya siri, ndivyo unavyozidisha mianya ya upigaji.
Mtu akijua hapa nachukua ten percent halafu mkataba unakuwa siri waandishi wa habari hawawezi kujua, anakuwa na ujasiri zaidi wa kuchukua hiyo ten percent, kuliko akijua kwamba, hapa nikichukua ten per cent kukubali mkataba mbaya, kesho mkataba utakuwa magazetini na waandishi wa habari watahoji na kujua kwa mkataba huu, aliyeupitisha hakuupitisha bure, tuangalie kama kachukua mlungula wa ten per cent hapa.
Mikataba ya awali haikuwekwa wazi kwa sababu sheria nyingi, mpaka leo, zinazuia mikataba kuwekwa wazi.Kwa kisingizio cha kulinda siri za kibiashara. Wakati unaweza kuweka mkataba wazi kwa namna ambayo bado italinda siri za kibiashara, una redact tu the most sensitive parts ambazo zina a justified and legitimate reason kuwekwa siri.
Kwa mfano, kama mkataba unashurutisha bandari nyingine zote za Tanzania zisiendelezwe ikiwa bandari ya Bagamoyo itajengwa, hili kuwekwa wazi ni jambo basic tu, linalo server interest ya wananchi kuliko ku invade trade secrets za muwekezaji. Hakuna sababu ya kuficha hili. Hili linatakiwa kuwekwa wazi, ili kesho, wananchi wa Mtwara wakiona bandari yao inadhoofika, wawe wanajua sababu. Siyo unaingia mkataba wa siri na Wachina leo, hujawaambia wananchi wa Mtwara kwamba bandari yao itatelekezwa kama sehemu ya makubaliano ya mkataba wa bandari ya Bagamoyo, halafu mbele kunakuja kuibuka mgogoro, kwa nini bandari ya Mtwara haiendelezwi.
Panatakiwa kuwepo na reasonable transparency. Sasa hivi hatuna transparency at all.
Lakini pia, umezungumzia nini kilifanya mikataba isiwekwe wazi. Jibu ni sheria za kizamani zinazowafanya wananchi kama watoto wadogo wasiojua nini kinawafaa, na viongozi ndio baba na mama wanaojua kuwachagulia watoto kitu kizuri.
Hizi sheria, hata kama zina nia nzuri -tuseme hazijawekwa kuendeleza ukiritimba na mianya ya rushwa, walioziweka waliamini kuwa wananchi wengi hawajui haya mambo-, inawezekana hizi sheria zilikuwa sahihi miaka ya 60 na 70 wakati watu wengi walikuwa hawana elimu. Sasa hivi wananchi wengi wameelimika na wanaweza kuhoji na kutoa mchango mzuri. Sasa sheria hizi zinainyima serikali nafasi ya kunufaika na vipaji vingi vya mjadala mkubwa zaidi wa wananchi. Ni rahisi kwa watumishi wa serikali ku miss vitu vikubwa, kwa kufanya kazi kwa mazoea. Lakini, mjadala mpana ukifanyika katika jamii, na watu wengi wakashiriki, kitu kikipitishwa, kinakuwa imara zaidi, kwa sababu kimepitia tanuru la moto wa mjadala wa jamii. Na kama kuna marekebisho ya muhimu, serikali itapata input ya jamii kabla ya ku commit kusaini mambo makubwa ambayo pengine kujitoa kuna kesi kubwa zenye gharama nyingi.
Sheria si sababu ya kutobadili kitu.Ndiyo maana tuna bunge, linarejea sheria za zamani na kutunga sheria mpya. Afrika Kusini walikuwa na sheria za kibaguzi, zikatupiliwa mbali.
Hizi sheria za kusema wanaoona mikataba ya mabilioni ya dola ni watu wachache tu wa juu, wengine hawajui, nao ni ubaguzi.Unawafanya wananchi kuwa kama watoto wasioweza kuchambua mambo, na maamuzi yote wanaachiwa watu wachache bila input ya wananchi.