Machozi yamenitoka kusikia Bandari ya Bagamoyo itajengwa, tena na Wachina

Kinachofanyika sasa ktk nchi yetu ni unafiki wa hali ya juu sana kukebehi kazi za mzee Magu kumuona kama alikuwa hana akili kuiuza nchi yetu kwa wachina watufilisi kabisa watu wachache wawe mabilionea miungu watu wale pesa ya nchi vizazi na vizazi Mungu tu atusaidie
Lini huyo mungu wenu alikuwa na akili!!???
 
Uyo mungu wenu magufuli ndio ilitakiwa aweke mkataba azalani tungejua Kama nikweli ulikuwa haufai,aliishia kupiga kelele tu!!
Vipi mkataba wa ujenzi wa uwanja wa ndege chato ulionyeshwa?!
hata kuandika hujui,halafu mama anaamini kabisa anaungwa mkono na watz timamu[emoji38][emoji38]

hii nchi bana aaaaah.

azalani=hadharani.
 
Kwa kweli Mama Samia kama ataendeleza hii bandari bila kupitia kwa kina na kubadilisha mambo yaliyomo humo ndani, basi tujihesabie tumekufa tu bado kuzikwa. Ardhi ni yetu, huu mkataba hautufai watanzania kwani tunakurupuka nini na kwa tamaa zipi?
 
Hii movement ya kuweka wazi mikataba imeeleweka nabkukubalika sehemu nyingi.

Kuna jamaa mmoja nilikuwa nabishana naye, akawa qnqnibishia sana, alikuwa anasoma business Uingereza.

Tatizo alikuwa anaenda na usomi wa vitabuni, wa zamani. Hakuwa anaangalia zeitgeist, mqmbo yanavyobadilika sasa hivi.

Nikamuambia hayo mambo ya kuweka mikataba wazi yamekubalika sasa hivi hata World Bank wana initiative ya kuweka mikataba wazi.

Yani jamaa alinipinga sana, nilipompa link ya World Bank initiative akakubali mara moja. Point zike zike kazikataa kwangu, ika alivyoona zimeandikwa na World Bank akazikubali mara moja.

Kuweka mikataba wazi kunapunguza mianya ya rushwa na kunaongeza ushirikishwaji wa umma.

Hao wawekezaji wakiona hii mipango ya mikataba kuwekwa wazi inakubalika na kulazimishwa dunia nzima, itawabidi wakubali tu.

Kama kuna issue ya sensitive trade secrets kwa mfano, hizi zinaweza kuwa redacted kukiwa na reasonable cause, siyo kuficha mkataba mzima.

Mimi nakubaliana na Wewe issue ya kuweka mikataba wazi, sema by the time mnaingia mkataba makubaliano yalikuwaje? Na je Kama palikuwa na clause inayosema mikataba ni siri ikitokea upande mmoja una breach adhari zake ni nini?

Labda kwa mikataba tunayotaka kuingia from now ndio tunaweza kusema iwekwe wazi kwa wananchi baada ya kukamilika, na hii iwe kwa makubaliano ya pande zote mbili.
 
Kwanza kabisa, hakuna mkataba usioweza kurejewa na kubadilishwa kulingana na mabadiliko yanayotokea katika muda.

Magufuli alilalamikia mambo mengi sana ya msingi. Mimi si mshabiki wa Magufuli, nimempinga sana sana sana hapa, but even a broken clock is right twice a day.

Sasa basi, tuelezane.

1.Je, Magufuli alikuwa muongo na yale malalamiko yake hayana msingi?

2. Au, Magufuli hakuwa muongo, malalamiko yake yalikuwa na msingi, lakini yamefanyiwa kazi na kubadilishwa kutupa imani zaidi na mradi?

3. Au, Magufuli hakuwa muongo, malalamiko yake yalikuwa na msingi, na bado hayajafanyiwa kazi, lakini ndiyo mazungumzo yanaanza kuyafanyia kazi.

4. Au, Magufuli hakuwa muongo, malalamiko yake yalikuwa na msingi, na bado hayajafanyiwa kazi, ila tumekubali kupigwa hatutayajadili tena.

Yote manne haya ni vigumu kuyajadili kwa kina na kuyahakiki kama mikataba haijawekwa wazi. Kwa sababu utakuwa unajadili kitu cha kuhadithiwa bila kuangalia primary document mwenyewe.
 
Labda baada ya hayo malalamiko unayosema mengi si mikataba mingi ilejewa je iliwekwa wazi? Na je Kama haikuwekwa wazi nini kilizuia isiwekwe wazi?
 
Kihaki mikataba yote mikubwa inatakiwa kurejewa.Hata kama ni kwa kuangalia nani alipiga wapi tumuwajibishe au tujiweke sawa tusipigwe tena.

Unavyozidi kufanya mikataba iwe ya siri, ndivyo unavyozidisha mianya ya upigaji.

Mtu akijua hapa nachukua ten percent halafu mkataba unakuwa siri waandishi wa habari hawawezi kujua, anakuwa na ujasiri zaidi wa kuchukua hiyo ten percent, kuliko akijua kwamba, hapa nikichukua ten per cent kukubali mkataba mbaya, kesho mkataba utakuwa magazetini na waandishi wa habari watahoji na kujua kwa mkataba huu, aliyeupitisha hakuupitisha bure, tuangalie kama kachukua mlungula wa ten per cent hapa.

Mikataba ya awali haikuwekwa wazi kwa sababu sheria nyingi, mpaka leo, zinazuia mikataba kuwekwa wazi.Kwa kisingizio cha kulinda siri za kibiashara. Wakati unaweza kuweka mkataba wazi kwa namna ambayo bado italinda siri za kibiashara, una redact tu the most sensitive parts ambazo zina a justified and legitimate reason kuwekwa siri.

Kwa mfano, kama mkataba unashurutisha bandari nyingine zote za Tanzania zisiendelezwe ikiwa bandari ya Bagamoyo itajengwa, hili kuwekwa wazi ni jambo basic tu, linalo server interest ya wananchi kuliko ku invade trade secrets za muwekezaji. Hakuna sababu ya kuficha hili. Hili linatakiwa kuwekwa wazi, ili kesho, wananchi wa Mtwara wakiona bandari yao inadhoofika, wawe wanajua sababu. Siyo unaingia mkataba wa siri na Wachina leo, hujawaambia wananchi wa Mtwara kwamba bandari yao itatelekezwa kama sehemu ya makubaliano ya mkataba wa bandari ya Bagamoyo, halafu mbele kunakuja kuibuka mgogoro, kwa nini bandari ya Mtwara haiendelezwi.

Panatakiwa kuwepo na reasonable transparency. Sasa hivi hatuna transparency at all.

Lakini pia, umezungumzia nini kilifanya mikataba isiwekwe wazi. Jibu ni sheria za kizamani zinazowafanya wananchi kama watoto wadogo wasiojua nini kinawafaa, na viongozi ndio baba na mama wanaojua kuwachagulia watoto kitu kizuri.

Hizi sheria, hata kama zina nia nzuri -tuseme hazijawekwa kuendeleza ukiritimba na mianya ya rushwa, walioziweka waliamini kuwa wananchi wengi hawajui haya mambo-, inawezekana hizi sheria zilikuwa sahihi miaka ya 60 na 70 wakati watu wengi walikuwa hawana elimu. Sasa hivi wananchi wengi wameelimika na wanaweza kuhoji na kutoa mchango mzuri. Sasa sheria hizi zinainyima serikali nafasi ya kunufaika na vipaji vingi vya mjadala mkubwa zaidi wa wananchi. Ni rahisi kwa watumishi wa serikali ku miss vitu vikubwa, kwa kufanya kazi kwa mazoea. Lakini, mjadala mpana ukifanyika katika jamii, na watu wengi wakashiriki, kitu kikipitishwa, kinakuwa imara zaidi, kwa sababu kimepitia tanuru la moto wa mjadala wa jamii. Na kama kuna marekebisho ya muhimu, serikali itapata input ya jamii kabla ya ku commit kusaini mambo makubwa ambayo pengine kujitoa kuna kesi kubwa zenye gharama nyingi.

Sheria si sababu ya kutobadili kitu.Ndiyo maana tuna bunge, linarejea sheria za zamani na kutunga sheria mpya. Afrika Kusini walikuwa na sheria za kibaguzi, zikatupiliwa mbali.

Hizi sheria za kusema wanaoona mikataba ya mabilioni ya dola ni watu wachache tu wa juu, wengine hawajui, nao ni ubaguzi.Unawafanya wananchi kuwa kama watoto wasioweza kuchambua mambo, na maamuzi yote wanaachiwa watu wachache bila input ya wananchi.
 
Asante kwa Majibu Yako Mazuri Sana Ila Labda je Kama haikuwekwa wazi unaweza kulinganisha mikataba ya awali na iliyorejewa kama yote haipo for public consumption? Kwa maana utajuaje mkataba uliorejewa ni bora kuliko wa awali kama yote miwili huijui kwa undani? Maana inaweza ikawa bora katika baadhi ya viperenge na ikawa haifai katika vipengere vingine, na the same applies kwa mikataba iliyorejewa?
 
Mimi sisemi mikataba irejewe halafu ibaki kuwa ya siri.

Mimi nasema miaktaba iwekwe wazi yote, kisha irejewe kiujumla na kadamnasi yote (public review), kisha, tukishakubaliana kwa kiasi kikubwa kwenye vipengele vikubwa, kwa wananchi kujadili na kuongea na wawakilishi wao na mambo kujadiliwa bungeni, mipya ifuatishe makubaliano, na hiyo mipya iwekwe wazi.

Hapo utajua nani alipiga EPA, tumuwajibishe vipi, na tuweke vipengele gani kwenye mikataba mipya ili watu wasipige kwa style ile ile ya EPA.
 
Wewe ulikuwa segerea nn wkt wanasema vifungu vilivyomo kwenye mkataba? Kama huyo mama yenu ni mkweli na mwenye kutaka mema kwa watu wake apeleke Bungeni huo Mkataba ukachambuliwe

Bunge lipi wakati hata Spika toka mwanzo alitaka ijengwe?
 
Kwa njia moja ama nyingine wananchi watalipa.

Unategemea mu Oman akupe dola za Kimarekani bilioni 10 bila kuzilipa?

Hata kwa "opportunity cost" tu?

Unaelewa hata tax exemption tu nayo ni aina fulani ya kuwalipisha wananchi?

Unaelewa kuna vipengele vya compensation for any loss incurred vilipigiwa kelele, vipengele hivi maana yake project ikipata loss wananchi watalipa gharama?

Pia, kabla ya mkataba kuwekwa wazi, huwezi kusema hakuna hata senti mwananchi atatoa.

Ndiyo maana nasisitiza mkataba uwekwe wazi.
Ni kweli kabisa. Shida iko pale kwenye uwezo wetu wa kufanya negotiation. Kuna udhaifu hapo. Kama haijaridhiwa, ingekuwa busara tukaajiri independent relevant expert firm iliyowahi kufanya kazi ya kunegotiate similar contracts elsewhere na Wachina atupitishe kwenye project nzima akibainisha faida na hasara kwa sisi kuingia au kuacha.

Aidha, abainishe pia alternatives, ikiwemo kuchangia uwekezaji kwa some own sourced funds zinazoweza kupatikana kutoka kwa development partners na internal investors, zikiwemo benki zetu, in phases. Lengo ni kuwa duration ya Transfer iwe fupi katika Build Operate and Transfer framework of the PPP framework itakayotumika.

Hii ya kuwaacha wafanye kila kitu wenyewe, including financing yaweza isiwe 100% healthy. Naamini sana katika international advisory services on project negotiation. Si vyepesi kama tunavyofikiri.
 
Bandari itajengwa kwa mkataba gani?

Bandari kujengwa inawezekana si jambo baya, ila, kwa mkataba gani?

Kama mkataba haujawekwa wazi, hilo tu linahalalisha kusema hili jambo si zuri.

Fedha za wananchi zinatumika kujenga bandari kwa mkataba ambao wananchi hawaujui.
Transparency. Especially because we offer post presidential immunity. Accountability becomes secondary. [emoji2218]
 
Mama anajibu maswali ya waandishi wa habari kama Vladimir Putin huko.
 
We should not tolerate any belittling of our elected leadership, particularly the President.
 
Hii movement ya kuweka wazi mikataba imeeleweka nabkukubalika sehemu nyingi.

Kuna jamaa mmoja nilikuwa nabishana naye, akawa qnqnibishia sana, alikuwa anasoma business Uingereza.

Tatizo alikuwa anaenda na usomi wa vitabuni, wa zamani. Hakuwa anaangalia zeitgeist, mqmbo yanavyobadilika sasa hivi.

Nikamuambia hayo mambo ya kuweka mikataba wazi yamekubalika sasa hivi hata World Bank wana initiative ya kuweka mikataba wazi.

Yani jamaa alinipinga sana, nilipompa link ya World Bank initiative akakubali mara moja. Point zike zike kazikataa kwangu, ika alivyoona zimeandikwa na World Bank akazikubali mara moja.

Kuweka mikataba wazi kunapunguza mianya ya rushwa na kunaongeza ushirikishwaji wa umma.

Hao wawekezaji wakiona hii mipango ya mikataba kuwekwa wazi inakubalika na kulazimishwa dunia nzima, itawabidi wakubali tu.

Kama kuna issue ya sensitive trade secrets kwa mfano, hizi zinaweza kuwa redacted kukiwa na reasonable cause, siyo kuficha mkataba mzima.

Hata mikataba silaha?
 
Back
Top Bottom