Machozi yamenitoka kusikia Bandari ya Bagamoyo itajengwa, tena na Wachina

Machozi yamenitoka kusikia Bandari ya Bagamoyo itajengwa, tena na Wachina

Mkataba wa ununuzi wa ndege uliuona? Ulijiridhisha ulikuwa na maslahi kwa Watanzania?

Mkataba wa bwawa la Nyerere uliuona? Ulijiridhisha ulikuwa na maslahi kwa Watanzania?

Mkataba wa SGR (segments zote) uliuona? Ulijiridhisha ulikuwa na maslahi kwa Watanzania?

Usiwe bendera fuata mkumbo. Hii nchi mikataba haijawahi kuwa na ahueni. Mikataba yote huwa tunapigwa mjomba. Ishu huwa ni nani ananufaika na kupigwa kwetu, nakuhakikishia hata mikataba enzi za Jiwe ilikuwa tunapigwa mno!

Tuungane kudai katiba itakayotaka mikataba yote kuwekwa hadharani kabla haijasainiwa

NB
Sina maslahi na bandari ya Bagamoyo wala siungi mkono mkataba unless uwekwe wazi
 
Sikuwahi kudhani Tanzania tuna uhaba wa Port mpk tuwauzie wachina Bagamoyo tumekarabati Bandari ya Dsm na Bandari zingine kwa gharama kubwa kabisa lakini leo tunakwenda kuziua bandari zote....
Tulie wote vpi cia kweli hii ndo Tanzania ya wakina Nkobe
 
Hivi watu huwa wanasikiliza sababu au basi wao wanafuata maneno ya marehemu tu. Hakuna nchi duniani itakayoendelea bila kuwa na uwekezaji. Port ya Dar tumeshaambiwa mara alfu haina wala haitakuwa na uwezo wa kupokea meli kubwa za kisasa Bagamoyo ni perfect na itachochea sana ukuwaji wa kiuchumi nje ya Dar hasa Bagamoyo.

JK alisema Bagamoyo, JPM akasema hapana sio kwa kuwa mradi mbaya ila masharti, Mama anasema mradi mzuri na maongezi yafanyike kwa hapo majority wins. JPM kishaondoka na hata yako Nyerere aliyakataa lakini yakaja kufanyika sio kwamba kila alichokataa JPM ndio sawa yale yalikuwa maono yake na zama zake zimeisha.

Bagamoyo port naunga mkono 100% mwekezaji yoyote anafanya biashara haji kutoa sadaka. Mikopo mkipewa wa China ndugu zetu wakitaka biashara wa China wabaya.
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe....
Tumeingia mikataba mingi saana na hawa wachina, na tukienda mbele zaidi Dr.Magufuli aliwachukulia kama marafiki wa kweli tofauti na makaburu wa kizungu........Why tunaogopa tena kuhusu hili na hao marafiki wetu wa kweli?
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe...
Kuna vipengele vikirebishwa ni mradi mzuri:
1. Umiliki uwe wa pamoja kwa asilimia zisizoachana sana.

2. Faida tugawane baada ya kipindi kifupi, chini ya miaka 30.

3. Bandari zingine ziendelee kuboreshwa na kufanya kazi.

4. Mkopo uwe wa masharti nafuu.

5. Management isiwe ya wageni pekee.

6.nk nk
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe....
Ukisikia kelele nyingi kuhusu china,kwamba inazinyonya nchi za Afrika,unaweza ukadhani hao wanaozusha na kupiga hizo kelele,Kuna jema lolote waliloifsnyia Afrika.

Kelele na propaganda zinapigwa na USA,UK,Ulaya,Ufaransa,wao wanaona wivu,sie Afrika tukiomba msaada,wao wazungu wanaweka masharti magumu,haki za binadamu,utawala bora,haki za mashoga,lakini china,misaada yake Haina masharti,yeye haangalii kama nchi inaendeshwa kidikiteta,inakiuka haki za binadamu,mchina anatoa tu,hapo wazungu ndipo wanakereka wanaamua kuzusha propaganda.

Wazungu,ndio wametupitisha utumwani,kwenye ukoloni,hawana jema,Wala hawajawahi kuomba radhi kwa madhala waliyotufanyia,usiwasikilize sana.
 
Mzee unang'ang'ania kuonyeshwa mikataba,mikataba mingapi uliwahi kuonyeshwa??
Mpuuzi ww, Sasa kumbe unalalama mkataba haufai wakati hata kuona ujauona, mmekalilishwa na Magufuli tu, magufuli alikuwa na chuki iyo bandari isijengwe bagamoyo, alihisi itamnufahisha kikwete, alitamani ikajengwe chato
 
Endelea kulilia mkuu. Ni zamu yako. Sisi tulilia wakati fulani hapo nyuma hadi machozi yakatukauka. Ni wakati sasa wa kukusanya mengine na pengine kwa jinsi mama SSH anavyokwenda hatutegemei kulia tena kwa kilio kile cha miaka 5 iliyopita.
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi.

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.
 
Umeuona mkataba?! Haya tuambie una vipengele gani vibaya?? Au mnafuata mkumbo sababu dikteta alikuwa haupendi huo mradi kwa chuki zake binafsi na mkwere
Alikuwa na chuki na mkwere? Chuki kwa ajili ya nini?

Magufuli alitoa dondoo za kilichopo kwenye huo mkataba ndio maana alisitisha na watu wakamuunga mkono!

Vipi wewe unaetetea sababu ya chuki zako kwa Magufuli unaweza kutuwekea huo mktaba hapa?
 
The best thing Magufuli heavily succeeded is on "BRAINWASHING PROPAGANDA". You can name it from corona to uzalendo. I bet, this will cost the nation for a decades. Today, everything is equated to what Magu believed. We are sick nation ready for special healing.
Wewe ni mpumbavu!

Weka mkataba hapa ili tuona Magufuli alikuwa anafanya propaganda
 
Alikuwa na chuki na mkwere? Chuki kwa ajili ya nini?

Magufuli alitoa dondoo za kilichopo kwenye huo mkataba ndio maana alisitisha na watu wakamuunga mkono!

Vipi wewe unaetetea sababu ya chuki zako kwa Magufuli unaweza kutuwekea huo mktaba hapa?
Uyo mungu wenu magufuli ndio ilitakiwa aweke mkataba azalani tungejua Kama nikweli ulikuwa haufai,aliishia kupiga kelele tu!!
Vipi mkataba wa ujenzi wa uwanja wa ndege chato ulionyeshwa?!
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi.

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.
Reli ya uhuru yaani TAZARA walijenga Wachina mbona hatukuisha???
 
Back
Top Bottom