MADA: Fahamu zaidi kuhusu mbinu za kilimo cha tikitimaji, faida na changamoto zake

MADA: Fahamu zaidi kuhusu mbinu za kilimo cha tikitimaji, faida na changamoto zake

MJINI CHAI,
Mkuu kama perception yako ndivyo ilivyo, basi kamwe hutoweza kuja kuthubutu na utaendelea kukaa na utegemezi wako na kazi za kitumwa... kwa kukosa utashi wakusoma nyakati.

Kilimo kinahitaji timing, lazima ujue soko linataka nini na kwa muda gani ndio ulime ilo zao utakalo,

Ata kama utakuwa na mtaji leo, maji na kila kitu lakini sokoni iyo bidhaa imeja, hapo utakua umefanya kazi ya kanisa tuu.

Kilimo cha biashara sio kuingia shambani muda wowote na kulima tuu, bali kilimo cha biashara ni timing ya soko, muda na hali nzuri kwaajili ya ustawi wa mazao.

Hivyo jitathimini tena angalia ulikosea wapi urekebishe..

Kila la kheri
 
Kulima heka moja tsh, 30000 ?

Huko raha sana, kwa sisi wa huku dar-mwasonga,
Trekta ni 60000/=
Ng’ombe ni 50000/=
Mmwagiliaji 300k hapo bado hata hujapalilia, huja panda wala huja kupiga dawa au kuweka mbolea,

Kwa mtu anaetaka kulima nakushauri uangalie na eneo pia maana zinatofautiana sana, mwingine ni ghali sana

Huku kwa huyu dada kidogo amebahatika kuwa na nafuu,

Bila ivyo lazima yakulize, matikiti yana changamoto sana, japo mtoa mada hajaziweka hapo
 
MJINI CHAI,
Acha kuwa negative na kukatisha watu tamaa.
Changamoto zipo kwenye kila aina ya ujasiria mali, hata wenye daladala na mabasi makubwa kuna kipindi inawapiga, waulize wenye maroli ya mizigo safari ndefu utasikia changamoto kibao.
Cha msingi ni kuwa jasiri na kuwekeza.
 
Mmewahi Kulima.......??? au Mnakunywa CHAI Mjini tuu.....? Mwaka wa Kwanza nililima CHOROKO Soko likadorora.....mwaka wa Pili nikaenda Mbinga nililima TANGAWIZI nilipata gunia 200 Soko likawa hakuna mpaka nikaweka Uzi humu JF......!!!! Nikageukia kulima MBAAZI Tuliambiwa zitakuwa na Soko Kg 1 itakuwa Tsh 3500/= Looooo imekula Kwangu kilo Tsh 150/= wanunuzi hakuna.......Nimerudi Town naangalia Upepo kwanza.................KILIMO siyo Mchezo kulima kwenye Makaratasi aaaaaaaaaaaaaaa mbona Powa sana na Faida utapata na utasema KAZI ndiyo hii..........!!!!!
Mimi ni mkulima wa mboga mboga.
Nina green house kadhaa moshono Arusha.
Watu kama wewe hamtufai. Ni wakatisha tamaa sana.
Kama kilimo kimekushinda kuna mahali unakosea.
Pata ushauri wa kitaalam na jitahidi sana kutumia kilimo cha kisasa kadri iwezekanavyo...pia lisome soko.
Ukitumia utaalam utazalisha kipindi ambacho sio cha msimu na soko la mazao yako litakuwa safi tu.
 
Back
Top Bottom