Madai kwamba Magufuli alimpiga Ben Saanane risasi pale Ikulu isichukiliwe kihisia; hizi hapa ni sababu za msingi kuamini kwamba ni ukweli

Hicho wapuuzi wanajifanya hawakijui..
 
WANAOTAKIWA KUJIBU NI SERIKALI , UONGOZI WA IKULU NA SIO FAMILIA
 
Kwanini usishauri apelekwe mahakamani akatoe ushahidi?
Unafahamu utaratibu wa kupublish kitabu?na ikitokea unayoongea ni uongo ufanywe nn?

Hilo swali hapo juu tunatakiwa tukuulize ww?,maana ndio unashida ya hilo swala
 
Wewe ni mtumish wa Mungu, sifa kuu ya watumishi wa Mungu ni kusema ukweli.
 
Kama mtaalam wa afya ya akili, ninasema pasi na shaka, ndugu Kabendera, anasumbuliwa sasa na Post traumatic stress disorder. Ndio maana, anapata relief kwa kuwasema wale anaodhani walikua sababu ya yeye kupitia aliyo yapitia.

Hata hivyo, kwa wale mliokaribu nae, msaidieni. Mpelekeni kwa psychiatrists na clinical psychologists wamsaidie. Ukisoma yale aliyoyaandika, unaona kabisa, hakuyaandika akiwa normal.
AHURUMIWE NA ASAIDIWE.
TUkiendelea kumsangilia tutakua hatumsaidii
 
Anayeamini huo ujinga wa kabendera ni kichaa na anatakiwa kupelekwa hospitali ya vichaa milembe Dodoma.
Tuanze na wewe unayepinga alichoandika kabendera wewe ndo umeandika ujinga unatakiwa kuwa na proof of evidence kuja kukataa hapa! Huwezi kutoka from no where unakuja kubeza hata wanaotaka kuchukua hatua lazima waje kimkakati kumbuka kitabu kimechafua taswira ya Taasisi ya Urais ambayo waligombe a wote na Rais aliyopo madarakani sasa hvi! Ile ni taasisi ya Urais siyo Personal as Magufuri inatakiwa mamlaka zitolee ufafanuzi na wasikimbilie dola au kukifungia kitabu!
 
Hebu soma maelezo yake katika haya mahojiano juu ya uandishi wa hiki kitabu halafu utuambie ana PTS.

View: https://youtu.be/HfQqupIGlKM?si=4QpdGYaV7b42UJjx

Labda wewe ndio una PTS kwa kumoteza Magufuli
 
Curious!!!! Kwa sababu tu Kabendera kaandika basi niamini, kama siamini nilete Ushahidi.
Nikuulize, umesikiliza alichosema Kabendera juu ya process ilivyokuwa hadi kitabu hiki kuchapishwa? Au unafikiri kaamka tu toka usingizini na kuandika Magufuli alimpiga risasi ya kichwa Ben Saanane? Sikiliza haya maelezokisha rudi utoe comments. Kimsing anauambia, kama kuna asiyeamini aende mahakamani nilete ushahidi

View: https://youtu.be/HfQqupIGlKM?si=4QpdGYaV7b42UJjx
 
Curious!!!! Kwa sababu tu Kabendera kaandika basi niamini, kama siamini nilete Ushahidi.
Mimi naamini kwasababi alikuwa na roho mbaya sana. Alafu kuna ule msemo usemao "ukitaka kujua tabia ya mtu, angalia rafiki zake" mfano Sabaya, Bashite nk nk.
 
Uandishi wa kitabu hauhitaji uweke ushahidi, kwa hiyo kusema Kabendera hajaweka ushahidi kwenye kitabu ni kutoielewa tasnia ya uandishi vitabu. Kama angeweka ushahidi kwa kila alichoandika, hicho kitabu kingekuwa kikubwa kiasi gani? Ile sio encyclopedia, ni memoir. Na amesema wazi, ushahidi upo na watu wa kuthibisha wapo, sasa ni jukumu lenu msiomuamini Kabendera kuchukua hatua ili atoe ushahidi. Hata wewe unaweza kwenda mahakamani kama mtu mwenye personal interest na Magufuli kwa kuwa alikuwa raisi wako.

Kuna mambo makubwa maishani mwenu mmeyakubali bila kupewa ushahidi, kama kumkubali mwanaume fulani kuwa baba yako, na hadi leo hamjawaambia mama zenu watoe ushahidi kwamba ni kweli, tukijua wengi wenu mmelelewa na baba ambao sio baba zenu kweli walibambikizwa mimba zenu. Sasa kwa nini hili mnashupalia Kabendera atoe ushahidi?
 
leaders who don't listen will eventually be surrounded by people who have nothing to say

A.S
 
Samahan naomba nikujibu tofauti na swali au hoja yako. Kuna vitu ushahidi haupo ila inaaminika ipo kama inavyosemekana kwa mfano uwepo wa malaika au YESU, kinachofanya usiamin magu kuuwa ni uwepo wa maofisa wa serikali au kukosekana kwa evidence ya picha mjongeo ?

Kama ni hv kwa vile hujawahi kuona video za lissu akipigwa risasi tuandike jamaa hakupigwa risasi ?, we unaamin kuna mjinga wa kuchezea camera za ulinzi eneo wanalokaa viongozi, nje na serikali ?
 
Well, “Kama kuna watu wanasema Kabendera ni muongo, wamshitaki…” Could you possibly be one of them?

Kama shida yako ni kujua mbinu na mbichi, kwa nini wewe usifanye hivyo?
Nakueleza principles tu.

Silence implies consent.

Ukituhumiwa, ukabaki kimya, hujakanusha tuhuma, hujamshitaki anayetuhuma, hulo linamaanisha umekubali tuhuma.

Mimi niko zangu Marekani nina kazi zangu kibao sina muda mchafu wa kukimbizana na Kabendera wala sina nia ya kufanya hivyo.

Nakufundisheni tu principles.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…