Sawa Erick Kabendera ameandika kwamba raisi Magufuli alimpiga risasi ya kichwa Ben Saanane pale Ikulu Dar es Salaam.
Sasa ukitaka kujua umbumbumbu wa watu, ni pale mtu anaibuka tu na kusema Kabendera mwongo! Watu hata hawataki kuhoji taarifa hii Kabendera kaitoa wapi - japo ametaja wazi kuwa source yake inatia watu walioko serikalini. Wengine hata wanadiriki kusema Kabendera akamatwe na kutiwa ndani kwa kuandika jambo hili!
Watu wote wanaopinga hii taarifa ya Kabendera wanapaswa kutambua yafuatayo;
- ikiwa unashupalia Kabendera ni muongo, basi wewe unapaswa kujua ukweli juu ya kupotea kwa Ben Saanane au yuko wapi kama yupo hai, au unamjua aliemuua. Kama una akili sawasawa, huwezi kubisha alichosema Kabendera bila wewe kuwa na taarifa kamili tofauti na aliyosema Kabendera
- kwamba Kabendera hawezi hata siku moja kufumuka tu na kuandika kitu kama hicho kwenye kitabu. Ni wazi ana uhakika na anachokisema, na kwamba ana ushahidi zaidi na serikali haitamchukulia hatua kwa sababu wakimpeleka mahakamani watakuwa wamempa ukumbi wa kumwaga ukweli wa jambo hili na serikali ya CCM haitaki kabisa hilo litokee (sawa na Marekani waliposema Makonda ni muuaji, ulisikia serikali ikipinga au kuishutumu Marekani? Unafikiri kwa nini serikali iliufyata?)
- Magufuli kama raisi angeweza kumpiga mtu yeyote risasi na kumuua bila kushitakiwa au kufanywa lolote kwa sababu Katiba yetu inampa uhuru raisi kumuua mtu na raisi asifanywe lolote! Hata Raisi Samia leo akifanya hivyo hutamfanya chochote na ataendelea kuwa raisi
- kwamba Magufuli alipompiga risasi Ben Saanane kuna watu walikuwapo na walishuhudia hilo na hawa ndio waliompa taarifa Kabendera, wao hawawezi kuzitoa hadharani, na huenda wengine waliolina hilo tukio "walishapotezewa"
- kwamba Magufuli alikuwa na tabia ya kutembea na bastora akiwa tayari kuua mtu, hata pale alipokuwa akikagua miradi yake alishikilia bastora mkononi. Kuua mtu kwa bastora ni rahisi mno, hasa kwa mtu mwenye kuchukia wapinzani kama Magufuli. Hivyo kumuua Ben Saanane kuna-fit attitude profile ya Magufuli
- kwamba kwa wanaomfahamu Magufuli watakuambia wazi alikuwa hayuko sawa kichwani na kuua mtu kwa risasi ingewezekana kabisa kwake. Huiyu ni Magufuli ambae alimpiga sana mtoto wake karibu kumuua kwa kosa la kufeli mitihani tu, na huyu ni Magufuli aliekuwa akimpiga mkewe hadi hatua ya kukaribia kufa na kulazwa hospitali, sasa sembuse Ben Saanane ambae alikuwa sio ndugu yake na alikuwa na hasira nae ya kukosolewa?
- kama Marekani walikuwa na ushahidi juu ya Makonda kuua watu waliopinga serikali, ni wazi alifanya hivyo kwa kibali cha Magufuli, na kama Magufuli alimruhusu Makonda kuua watu basi kwa nini yeye binafsi asindwe kumuua mmojawapo wa aiana ya watu aliomruhusu Makonda kuwaua?
- kigugumizi cha polisi katika kupeleleza na kukamata watu waliopotea au kuuwawa, hasa wapinzani wa serikali, ni wazi kwamba vifo hivi ninahusisha watu wakubwa walioko serikalini, kutia ndani mtu kama Magufuli, au kwamba viliidhinishwa na Magufuli, pamoja na jaribio la kumuua Tundu Lisu