DOKEZO Madai ya Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kumlawiti Mwanafunzi, mama wa Mtoto aomba Serikali imsaidie

DOKEZO Madai ya Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kumlawiti Mwanafunzi, mama wa Mtoto aomba Serikali imsaidie

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kasema hajapewa ushirikiano na kanisa wakati ni fellow wa hapo sasa huoni ni ubaguzi wa kanisa kwenye matatizo binafsi tena yamesabibshwa na mliz wao ambaye analipwa kupitia sadaka zenu
Kwenye katiba ya Tanzania na sheria za jinai hakuna sehemu ambapo kunahitajika ushiriki wa kanisa kwenye kumkamata mtuhumiwa, kufuatilia, kupeleleza au kutoa hukumu. Kesi za mapadre kumwagiwa tindikali, makanisa kuchomwa na nyinginezo nazo huwa kanisa halihusiki pasipo mahala pake.

Kwenye kesi hii kanisa sio mshitaki wala mshtakiwa, wala sio shahidi. Ni muajiri tu. Sasa ukiajiliwa na Vodacom alafu ukaibia mtu ukiwa geti la ofisini umevaa sare za kazi, kampuni yako itahusika vipi mahakamani?
 
Baada ya member wa JamiiForums kuripoti madai kuwa kuna Mlinzi wa Kanisa Katoliki la Sinza kutuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wa kiume anayesoma Darasa la Tano katika Shule ya Msingi Sinza ya Jijini Dar es Salaam, kuna mwendelezo wa taarifa hiyo.

Andiko hilo la awali lipo hapa - Serikali imsaidie Mtoto huyu anayedaiwa kulawitiwa na Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza

Muda mfupi baada ya andiko hilo kwenda hewani Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima alitoa neno kwa kuweka ‘comment’ kuwa mama mzazi wa mtoto huyo amtafute ili kusaidia kushughulikia suala lake.
View attachment 2924113
Ujumbe wa Waziri Gwajima alioutoa kuhusu sakata hili

Mwendelezo wa simulizi huu hapa…
MAMA MTOTO ASIMULIA…
Siku ya tukio mwanangu alichelewa kurudi, hadi saa mbili kasoro usiku alikuwa hajarudi hali ambayo si kawaida yake, nikatoka kwenda kumtafuta, mara nyingi alikuwa akitoka shule au siku za wikiendi anaenda Kanisani.

Nilipokaribia kufika Kanisani nikaona kundi la watu limemzunguka mtu, nikasogea na kubaini kuwa aliyezunguka ni mwanangu.

Nilipohoji kulikoni nikaelezewa na mashuhuda kuwa wakati mtoto anatoka Kanisani aliingia chooni kujisaidia, ndipo huyo mlinzi akaingia na kumtishia kumpiga, akamtaka avue nguo, alipofanya hivyo akamgeuza na kuanza kumuingilia kinyume na maumbile.

Mwanangu alipopiga kelele kuna watu wakasikia hizo kelele wakiwemo watumishi wengine wa Kanisani hapo, wakaenda kutoa msaada, wakamkamata mtuhumiwa, ndipo nikakuta mvutano ukiendelea baadhi wakitaka suala hilo limalizike kienyeji kwa mazungumzo na wengine wakitaka lifike kwenye Vyombo vya Sheria.
View attachment 2924106
RB Namba ya shitaka hilo
View attachment 2924108
View attachment 2924109
Sehemu ya Ripoti ya Daktari
Yule mlinzi mtuhumiwa hakukimbia alikuwepo eneo la tukio akijaribu kunibembeleza kuwa yeye hana kosa, nilikuwa na hasira na sikutaka hata kumsikiliza, akaenda kuzungumza na Paroko ambaye alipokuja akasema yeye hawezi kutoa majibu bali anaachia Polisi walishughulikie.

Nikawapigia simu Askari Polisi ambao walifika na kumchukua mtuhumiwa ndipo hatua nyingine zikafuata.

MWENDELEZO WA MASHTAKA…
Mama mtu anasema Mtoto alifanyiwa vipimo Hospitali ya Palestina na majibu yakaonesha kweli kaingiliwa kinyume cha maumbile.

Nilienda wiki iliyopita (mwishoni mwa Februari 2024) pale Kituo cha Polisi Mabatini nikakutana na Mpelelezi nikajulishwa kuwa suala hilo lipo kwa Mwanasheria, lakini nimekuwa nikijibiwa hivyo kila ninapoenda.

Mpaka sasa unapita mwezi sijui chochote kinachoendelea, mwanangu ameshaanza kwenda shule lakini uongozi wa shule sijaujulisha chochote kwa sababu nahofia isije ikamuathiri zaidi kisaikolojia.

Nilipoona JamiiForums mmeandika na Waziri Gwajima akasema mama mwenye mtoto amtafute, nilifanya hivyo, siku chache baadaye kuna maafisa wa Serikali walinitafuta na kuniunganisha na Afisa Ustawi wa Jamii wa Sinza anaitwa Grace.

Nilipoenda kuonana naye akaniambia nimuelezee ilivyokuwa nikamuelezea kila kitu akasema atashughulikia na kufikisha suala hilo kwa wakubwa.

Kinachonipa shaka na kuniuma ni kuwa kumekuwa na ukimya, nasikia mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana, uongozi wa Kanisa pia haujanishirikisha wala kuzungumza nami kwa lolote na wala hawajanipa ushirikiano wowote.

Sijarejea kusali tena pale (Kanisani) ila kwenye Jumuia ya Kanisa naenda na huko nako hawajazungumza chochote kuhusu suala langu.

Mtuhumiwa namfahamu kwa jina moja tu anaitwa Baraka, sikuwa namjua kwa jina kabla.

Naomba Serikali inisaidie haki ipatikane kwa kuwa mwanangu wakati anakua alipata changamoto kidogo ya kuchelewa kuanza kuongea, hivyo mpaka leo yupo darasa la tano bado kidogo uwezo wake wa kujieleza sio mkubwa kama ilivyo Watoto wengine, inawezeka mlinzi aliona atumie udhaifu huo kumfanyia mwanangu ukatili.

AFISA USTAWI WA JAMII
Grace Ludovic ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii wa Sinza, anaelezea: Nilizungumza na mama mtoto akaniambia suala lake linaendelea na upelelezi kwa kuwa suala kama hilo lazima lifike kwa DPP.

Leo hii (Machi 4, 2024) ninatarajia kwenda Kituo cha Polisi Mabatini kujua kinachoendelea.

Kuhusu mtuhumiwa hatujazungumza naye, nilienda Kanisani sikufanikiwa kukutana na uongozi niliwakuta walinzi, hivyo nikashindwa kumhoji.

Mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana, Polisi wanasema ni haki yake Kisheria, anaishi wapi? Hilo sijui kwa sasa.

KAMANDA WA POLISI KINONDONI…
Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mtatiro Kitinkwi amesema “Faili la kesi lilipelekwa Ofisi ya Wakili wa Serikali kwa Hatua za mashtaka, linafanyiwa kazi, kuanzia sasa hatua zinaenda kuchukuliwa, isichukuliwe kuwa kuna kitu kinakwamisha.”
KANISA KATOLIKI kutoingilia suala hili ina maana tayari maagizo YA PAPA-PAPAI yameshaanza kufanyiwa kazi bila shaka!!!!.....mtasikia PAROKO wa hilo PAROKIA anapewa UASKOFU!!!...WAKATOLIKI noma sana MAN!! da!!!
 
Kasema hajapewa ushirikiano na kanisa wakati ni fellow wa hapo sasa huoni ni ubaguzi wa kanisa kwenye matatizo binafsi tena yamesabibshwa na mliz wao ambaye analipwa kupitia sadaka zenu
Sasa kanisa lifanye Nini wakati kesi ipo polisi chini ya uchunguzi wa DPP?
Hapo ni kumsaidia mtoto kisaikolojia tu akae sawa wakati wakisubiri kesi ianze mahakamani.
 
Si mitag waziri wa jinsia na watoto si yuko humu

Ova
 
Hate huu umaku kanisa linamtetea mbakaji daaah uyoo alitakiwa apigwe mawe live kwenye ibada
Walinzi wa makanisani huaga sio waumini wa hapo and hence kanisa halina uhusiano nae wa moja kwa moja, kuna sababu yeyote ya kumtetea? Nonsense
Halafu Sinza?😉🙃 pale si kuna hadi mademu wa buku buku? Pumbafu kabisa huyo mlinzi
 
Kwenye katiba ya Tanzania na sheria za jinai hakuna sehemu ambapo kunahitajika ushiriki wa kanisa kwenye kumkamata mtuhumiwa, kufuatilia, kupeleleza au kutoa hukumu. Kesi za mapadre kumwagiwa tindikali, makanisa kuchomwa na nyinginezo nazo huwa kanisa halihusiki pasipo mahala pake.

Kwenye kesi hii kanisa sio mshitaki wala mshtakiwa, wala sio shahidi. Ni muajiri tu. Sasa ukiajiliwa na Vodacom alafu ukaibia mtu ukiwa geti la ofisini umevaa sare za kazi, kampuni yako itahusika vipi mahakamani?
Mama mtoto anasema Toka tukio litokee sio kwenye jumuiya ama kanisan kwenyewe amewahi kuitwa walau kupewa pole na kutiwa moyo wakati ni muumini mzuri tu, hapa ndipo ninapoina usanii wa hizi dini.
 
Back
Top Bottom